Hatua 7 za Kupunguza Makali ya Menopause.
Kukoma hedhi au menopause huanza katika ya umri wa miaka 40 mpaka 50. Wakati wa kipindi hiki wanawake hupata dalili zisizo za kawaida ambazo hazikuwepo awali. Dalili hizi ni pamoja na joto la mwili kuongezeka, kupata jasho jingi hasa wakati wa usiku, kujiskia vibaya na uchovu, kukosa hamu ya tendo na maumivu wakati wa tendo.
Kwa kuongezea ni kwamba wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya mifupa kama kumomonyoka kwa mifupa, kuongezeka uzito, magonjwa ya moyo na kisukari.
Tambua kwamba Menopasue/kukoma hedhi siyo ugonjwa
Kama tulivoona hapo juu pale mwili wa mwanamke unapokoma kutengeneza homoni za estrogen na progesterone ndipo hedhi yako itakoma. Wanasayansi huenda mbali zaidi na kuwaanzishia wahanga wa tatizo hili program ya kurudisha homoni hizi kwa kuwawekea homoni zilizotengenezwa maabara.
Kitendo hiki hufahamika zaidi kama hormone replacement therapy. Njia hii inatazama ishu ya kukoma hedhi kama ugonjwa wakati ni suala la kawaida kabisa linalomkuta kila mwanamke. Ukweli ni kwamba kitu chochote kilichotengenezwa kwa mkono wa binadamu hakitafanya kazi sawa na kitu kilitengenezwa halisi kwa ajili ya kazi fulani kwenye mwili. Ndio maana madhara ya kuwekewa homoni hizi ni makubwa zaidi.
Njia 7 asili za kutumia kupunguza makali ya menopause.
1.Kutumia vyakula vyenye madini ya Calcium na Vitamin D kwa wingi
Mabadiliko ya homoni wakati wa menopause huweza kusababisha kudhoofika kwa mifupa. Madini ya Calcium na vitamin D husaidia kuimarisha mifupa na kupunguza hatari ya kuchanika kwa nyonga. Unaweza kupata madini ya Calcium kwa kutumia vyakula kama maziwa. Mboga kama spinach na maharage.
Mwanga wa jua ni chanzo kizuri cha Vitamin D, hivo hakikisha kila siku unapata walau nusu saa ya kukaa juani. Kama huna muda wa kukaa juani au kukosa muda mzuri wa kuandaa chakula chako pengine kutokana na aina ya shuguli unayofanya basi hakikisha unatumia virutubishi ambavyo vipo kwenye mfumo wa vidonge ili kuongeza Madini ya Calcium na Vitamin D.
2.Kurekebisha uzito wako
Kuongezeka uzito ni changamoto inayowapata wanawake wengi wanapokoma hedhi. Hii ni kutokana na mabadiliko ya homoni, uzee na mabadiliko ya vinasaba.
Kuongezeka kwa mafuta hasa eneo la tumbo inaongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kisukari. Kwa kuongezea ni kwamba wanawake wenye uzito mkubwa dalili za menopause zinakuwa kali zaidi ukilinganisha na wale wenye uzito mdogo.
3.Epuka vyakula vinavyoongeza hatari kama
Vyakula vilivyosindikwa: vyakula vingi vilivyosindikwa kiwandani huongezwa sukari, vionjo vya kuongeza ladha na kemikali nyingine kulinda kisiharibike (preservatives). Pia vyakula vingi vya namna hii vimejaa wanga ambayo ni adui kwa mwanmke aliyekoma hedhi.
Mafuta ya kula yaliyosafishwa kama mafuta ya kupikia ya alizeti badala yake tumia mafuta ya nazi au olive kupikia. Pombe: ambayo huongeza hatari ya kuongezeka uzito na Vinywaji kama soda ambavyo huchangia katika kudhoofisha mifupa, na matatizo ya meno.
4.Punguza na udhibiti msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo usipodhibitwa ni chanzo cha kuvurugika kwa homoni na hivo kukufanya uwe mlevi wa vyakula vya sukari na wanga. Kukosa usingizi na kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa. Baadhi ya njia nzuri za kudhibiti msongo wa mawazo ni kama mazoezi, aromatherapy (kuvuta hewa ya mafuta mfano mafuta ya lavender), kutumia muda mwingi kwenye maeneo yaliyotulia, kuongea na uwapendao na kusali.
5.Weka ratiba ya kufanya mazoezi
Maozezi ni muhimu sana kwa mwanamke kama unataka kupunguza dalili mbaya zinazojitokeza wakati wa kukoma hedhi. Baadhi ya dalili hizi ambazo utadhibiti kwa mazoezi ni kama kuongezeka uzito, kukosa usingizi, misuli kupungua na msongo wa mawazo. Napendekeza kutumia walau dakika 10 mpaka 30 kwa siku kufanya mazoezi .
6.Pata muda mrefu wa kulala
Tafiti zinasema kwamba msongo wa mawazo pamoja na kukosa usingizi ni chanzo cha kupungua kwa kinga ya mwili, kupungua kwa ufanisi kwenye shughuli zako na kuongezeka uzito na kitambi. Ili kuruhusu mwili wako kurekebika kutokana na mawazo hakikisha unapata muda wa masaa 7 mapak 9 ya kulala kila usiku.
7.Jenga mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka
Tengeneza mtandao wa marafiki wazuri ambao utashauriana nao mambo ya kujenga na siyo mambo mabaya. Mahusiano mazuri yatakufanya mwili uwe mtumivu na kuepuka msongo wa mawazo
Soy power ni Muhimu kutumika kwa Wanawake waliokoma hedhi ana wanaokaribia kukoma.
Faida za soy power
- Kuongeza uzalishaji wa uteute ukeni ili ufurahie tendo
- Kuimarisha hamu ya tendo la ndoa
- Kuondoa dalili mbaya kama uchovu na kutokwa jasho jingi usiku
- Kuimrisha afya ya mifupa na usingizi mnono pamoja na
- Kuimarisha ngozi yako
Soy power ni Tsh 90,000/= tu. Itakufanya ufurahie tendo kama vile ulipokuwa binti.
Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai.