Aleji husababishwa na nini

aleji au mzio

Tatizo la aleji au mzio ni kubwa sana na mara nyingi husababisha vifo kwa waathirika. Mpaka sasa bado hakuna dawa ya kutibu mzio au aleji lakini kuna dawa za kupunguza na kutibu madhara ya aleji na kupunguza tatizo.

Dawa hizi hupunguza mpambano kati ya kinga ya mwili na kitu kilichoingia ndani ya mwili ambacho hukusababishia mzio. Habari njema ni kwamba kuna vyakula asili na virutubisho ambavyo vinaweza kutumika kutibu aleji kwa kiasi kikikubwa sana. Hii ndio njia tunayotumia katika kituo chetu cha ushauri wa lishe katika kuwasaidia wagonjwa wa matatizo ya mzio na pumu.

Aleji Ya Chakula inatokeaje

Ndani ya seli za mwili kuna kemikali zinazoitwa histamine. Kazi ya histamine ni kuiruhusu kinga ya mwili kupambana na kitu chochote kigeni ambacho kimeleta athari kwenye tishu zako. Kinga ya mwili inaweza kupambana na kitu chochote ambacho kinaleta shida kwenye mwili mfano vimelea vya ugonjwa, hewa chafu, virusi, bacteria, baadhi ya vyakula nk.

Kwahiyo tunaelewa sasa kwamba histamine husababisha aleji juu ya chakula fulani. Maana yake umekula lakini mwili unaonesha kukikataa chakula hicho kwasababu mwili umeona kinaweza kuleta madhara makubwa. Kemikali hii ya histamine ndio inaleta matokeo kama kutapika, kukohoa au kujikuna. Hivyo basi unapotumia mara nyingine kitu au chakula husika mwili utakumbuka kwamba kiliwahi kuleta madhara ndipo haitaruusu kiingine ndani ya mwili tena.

Dalili Zinazoletekezwa na Aleji

Viashiria kwamba una aleji ya chakula hujionesha mapema zaidi, ndani ya dakika au masaa kadhaa baada ya kula chakula husika. Dalili hizi tunaziita allergic reactions ni kama

 • Malengelenge yanayowasha kweye ngozi.
 • Mdomo kuvimba, kutetemeka na kuwasha
 • Ulimi kuvimba, koo na uso
 • Kutapika
 • Kuharisha
 • Maumivu ya tumbo
 • Kukohoa sana na mafua makali
 • Mwili kuchoka sana na kujiskia uvivu
 • Kupata ugumu kupumua ama pumzi kukata
 • Kupoteza fahamu

Food allergy na Food intolerance

Wakati mwingine ni vigumu sana kwa madaktari kugundua chanzo cha aleji yako. Hii ni kutokana na kwamba kuna vitu viwili, aleji ya chakula(food allergy) na mwili kutovumilia uwepo wa chakula fulani(food intolerance). Tofauti na aleji ya chakula ambayo ni matokeo ya kinga kupambana na kitu kinachoingia.

Mwili kutovumilia chakula fulani ni kwa sababu aina ya chakula haiwezi kumng’enywa na mwili, mfano kwa watu wengi miili yao haiwezi kumeng’enya vyakula vya ngano na maziwa, vyakula vilivyoongezwa ladha na rangi .

Watu wanaopata aleji juu ya chakula fulani ni muhimu kuacha kutumia aina hiyo ya chakula mapema iwezekanavyo. Baadhi ya madhara ya kiafya ambayo mtu mwenye aleji na chakula anaweza kuyapata kama tatizo litakuwa ni la muda mrefu ni kama

 • Kupata maumivu ya viungo yasioisha
 • Tatizo la pumu
 • Upungufu wa virutubisho kwenye mwili
 • Magonjwa ya Ngozi
 • Magonjwa yanayotokana na mpambano kati ya kinga ya mwili na tishu za mwili (autoimmune diseases)
 • Matatizo ya kumbukumbu
 • Kukosa usingizi
 • Kuongezeka uzito
 • Kupata kizunguzungu
 • Matatizo ya figo na bandama

Hatua 6 Za Kutibu Aleji Ya Chakula Na Kupunguza Madhara Yake

Kutokana na kwamba aleji ya chakula inaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya Napendekeza wewe na watu wote wanaokuzunguka wenye tatizo hili kufutilia kwa makini na kufanya kwa vitendo hatua hizi hapa chini

Epuka kutumia hivi vyote ­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­

Chakula na lishe ifuatayo inaongeza mpambano ndani ya mwli, kuzorotesha kinga ya mwili na kisha kuleta matatizo kwenye umeng’enyaji wa chakula.

Vyakula vyote vilivyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye vifungashio visiharibike:

Vyakula vilivyosindikwa vimeongezwa kemikali, rangi na ladha vitu ambavyo vinaweza kusababisha aleji na mwili kushindwa kuvimeng’enya. Kwahivo ni muhimu sana kwa mtu mwenye aleji kuwa makini na uchaguzi wa vyakula na vinywaji vya kutumia ili kupunguza athari ya tatizo.

Sukari

Sukari husababisha ukuaji wa bateria wabaya kwenye mfumo wa chakula, na hivo kuzorotesha kinga yako ya mwili. Kinga inapokuwa chini huongeza hatari ya mwili kushindwa kuchakata baadhi ya vyakula, na kisha kuleta aleji ya vyakula.

Vyakula vya ngano

Utafiti unaonesha kwamba watu wengi wenye matatizo kwenye mfumo wa chakula na matatizo ya aleji hupata nafuu kubwa na afya zao kuimarika pale wanapoacha kutumia vyakula vya ngano. Tafiiti pia zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya watu wazima wamelalamika kuhusu kuongezeka kwa dalili mbaya za mzio/laji pale wanapotumia vyakula vya ngano.

Usitumie vyakula vinavyoleta mzio/aleji kama

Maziwa ya ng’ombe: Aleji kutokana  na maziwa ya ng’ombe ni tatizo kubwa sana kwa watoto wadogo. Kwa watu wazima ni mara chache sana wengi wao ni tatizo la mwili kushindwa kumen’genya viini lishe vilivyopo kwenye maziwa (lactogen intolerance).

Mayai:  Mayai huleta mzio/aleji kutokana na uwepo wa kiini lishe kinachoitwa ovomucoid.

Mazao na vyakula vyote vya  soy, karanga na samaki

Tumia kwa wingi vyakula hivi ambavyo havileti mpambano (allergic reaction)

Katika safari yako ya kupambana na aleji, fahamu kwamba kuna baadhi ya vyakula ambavyo havileti mpambano kati ya tishu za mwili na kinga ya mwili. Vyakula hivi ni kama

Mbogamboga za kijani: Mboga hizi ni kama spinach ambazo zinakuwa na vitamin, madini, viondoa sumu, na viambata ambavyo husaidia umeng’enyaji wa chakua  kwa wingi sana. Hakikisha unaongeza mbogamboga za kijani kwenye mlo wako zitasaidia kuimarisha kinga na kutoa sumu mwilini.

Maziwa ya nazi na nazi: Mbadala mzuri wa maziwa ya ng’ombe ni kutumia maziwa ya nazi. Maziwa haya kwa lugha rahisi ni tui la nazi. Hivo unaweza kutengeneza nyumbani kwako na ukaongeza viungo kama limau na tangawizi ukafurahia kinywaji chako.

Mbegu: Mbegu kama za maboga na mbegu za alizeti ni nzuri kwa mgonjwa wa aleji, huongeza madini ya zinc na mafuta ya Omega 3. Sawa na karanga, lakini uzuri wake ni kwamba hazisababishi mpambano (allergic reaction) ambayo huleta aleji au mzio.

Maziwa ya mama:  Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba kunyonyesha mtoto kwa miezi sita ya mwanzo bila kula kitu chochote na  kuendelea kunyonyesha kwa miaka miwili husaidia kupunguza hatari ya mtoto kupata pumu, matatizo ya ngozi na aleji mbalimbali. 

Tiba kupitia Mafuta ya Eucalyptus

mafuta ya mkaratusi
mafuta ya eucalyptus

Mafuta haya husaidia kulainisha koo la hewa na mfumo wa chakula na hivo kupunguza mpambano (inflammation) hivo kuzuia kutokea kwa athari za mzio au aleji. Mafuta haya pia husaidia kutibu baadhi ya madhara ya mzio kama kuumwa kichwa na mwili kuwasha.

Eucalyptus husaidia kufungua njia za hewa hasa kwa wagonjwa wa pumu na hivo kurahisisha usafrishaji wa hewa na upumuaji kwa ujumla. Huhitaji kuagiza nje ya nchi tumefanya utafiti na kukuletea mafuta asili yasiyochakachuliwa.

Gharama ya mafuta ni Tsh 40,000/=

Ofisi zetu zipo Mwembechai, Magomeni Tuandikie kwa whatsapp no 0746672914 kupata mafuta tiba

Share and Enjoy !

Shares
Shares