Chembe moyo husababishwa na nini

chembe moyo
maumivu ya chembe ya moyo

Chembe moyo au kwa kitaalamu stable angina au angina pectoris. Ni aina ya maumivu ya kifua yanayatokea baada ya kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye moyo. Kupungua kwa mzunguko wa damu husababisha kukosa hewa safi ya oksijeni kwenye moyo.

Maumivu hutokea baada ya mwili kufanya kazi flani ama pale unapopata msongo wa mawazo.
Mumivu haya ya chembe moyo husababisha mtu kukosa raha, kuhisi kama kifua kimejaa na kubana kwa kifua eneo la katikati.

Chembe Moyo Hutokea Wakati gani?

Chembe ya moyo hutokea pale misuli ya moyo inapohitaji damu ya kutosha zaidi kuliko kawaida. Mfano wakati unafanya mazoezi, au unapokuwa na msongo wa mawazo. Unapokua umetulia mfano umekaa kwenye kitu kiwango cha hewa ya oksijeni kinachohitajika ni kidogo. Lakini unapokuwa kwenye shughuli kama kupanda mlima au kukimbia moyo unahitaji kiwango kikubwa cha hewa na ndio matokeo ya chembe moyo.

Dalili za Chembe Moyo

 • Pamoja na maumivu na kubana kwa kifua dalili zingine za chembe ya moyo ni kama
 • Kushindwa kupumua vizuri
 • Kupata kichefuchefu
 • Mwili kukosa nguvu na kupata ganzi
 • Kutokwa na jasho na
 • Msongo wa mawazo

Mazingira na tabia Hatarishi Zinazopelekea kupata Chembe moyo

 • Kuwa na uzito mkubwa na kitambi
 • Kuwa na historia ya kugua magonjwa ya moyo
 • Kuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol au shinikizo la damu kuwa juu
 • Mgonjwa wa kisukari
 • Uvutaji wa sigara
 • Kutofanya mazoezi au kushugulisha mwili
 • Kula mlo mkubwa na
 • Mazingira ya joto kali au baridi kali

Vipimo kwa ajili ya chembe ya moyo

Kabla ya kufanyiwa vipimo daktari aatakuuliza kuhusu historia ya tatizo lakona kisha kufanya vipimo hivi
Electrocardiogram: kipimo hichi hufatilia umeme ndani ya moyo na kuchambua uwiano.
Angiography: Kipimo cha x-ray ambacho huchunguza mishipa ya damu na kupima mzunguko wa damu kwenye moyo.

Vipimo hivi vinasaidia kujua kama moyo unafanya kazi vizuri na kama mishipa ya damu inapitisha damu vizuri.

Matibabu ya Mgonjwa wa Chembe moyo

Matibabu kwa ajili ya chembe moyo yanahusisha, kubadili mtindo wa maisha, dawa na wakati mwingine upasuaji. Hakikisha unafatilia ni kipindi gani unapata maumivu, punguza mazoezi makali sana. Jaribu kuongea na daktari wako kuhusu swala la lishe na mazoezi ili kupunguza kutokewa kwa chembe ya moyo.

Mtindo wa maisha

Mabadiliko ya mtindo wa maisha husaidia kupunguza hatari ya kupata chembe moyo. Mabadiliko haya yanahusisha kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara, kula lishe nzuri, na kuacha kuvuta sigara.
Mabadiliko haya ya mtindo wa maisha yatakusaidia pia kuepuka magonjwa mengine kama kisukari, shinikizo kubwa la damu, na kuondoa cholesterol mbaya.

Dawa

Daktari anaweza kukuanzishia dawa ili kupunguza maumivu ya chembe moyo. Pia kutokana na kisababishi chako cha chembe moyo kama shinikizo kubwa la damu, cholesterol au kisukari, daktari atakuanzishia dawa ili kutibu chanzo cha tatizo.

Upasuaji

Upausaji (angioplasty) mara nyingi hutumika kwa wagonjwa wa chembe moyo. Upasuaji hulenga kutanua njia ya damu kweye mshipa ili kuruusu damu kupita.

Ushauri kwa Mgonjwa

Wagonjwa wengi huchanganya chembe moyo kutokana na shida ya moyo, na maumivu ya kifua kutokana na gesi tumboni. Gesi ambayo inaweza kupanda mpaka juu kwenye kifua na kuleta maumivu makali sana. Hakikisha umepima na kujua chanzo cha maumivu yako ni moyo au mfumo wa chakula yaani gesi.

Kama unapata dalili mbaya mara kwa mara, weka muda wa kwenda hospitali ufanye vipimo kujua chanzo cha tatizo lako. Kama tayari umefanya vipimo pamoja na dawa ulizopatiwa hospitali, nashauri tupigie simu upate dawa yetu iliyotengenezwa kwa mimea ili kuondoa mafuta mabaya,kusafisha mishipa ya damu na kuimarisha mzunguko wa damu kuelekea kwenye moyo ili utibu chembe moyo. Kama chanzo cha chembe ni kwenye mfumo wa damu na moyo, tutakupa dawa namba 1 ya supercoenzyme.

Endapo tatizo lako la chembe linatokana na hitilafu kwenye mfumo wa chakula mfano kuwa na gesi nyingi sana, tutakupatia dawa namba mbili ya Clear ambayo utatumia week mbili tu na kupona. Gharama ya dawa ni Tsh 100,000/=

Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 uanze tiba mapema

Share and Enjoy !

Shares
Shares