Kuona damu kwenye haja kubwa si jambo la utani. Hasa kama ni kinyesi cha kwako mwenyewe siyo cha mtu mwingine. Kwa kiasi kikubwa inaweza kuashiria uwepo wa tatizo kubwa la kiafya kwa hiyo usipuuze kabisa unapoona hali hii.
Watu wengi hawafahamu kwamba wakati mwingine kinyesi kinaweza kuwa cheusi lakini kikawa na damu. Siyo mpaka uone kinyesi chekundu. Cha msingi ni kutazama choo chako kwa uangalifu usiwahi kuflash na kutoka nje. Angalia shape, ukubwa na rangi ya kinyesi chako. Uwepo wa damu kwenye kinyesi inaweza kuashiria saratani ya eneo la juu ya mkundu (rectum) ama kuashiria kuvuja kwa damu kwenye eneo la ndani ya mkundu.
Wagonjwa wengine huvuja damu kupita kiasi na kupelekea damu kupungua mpaka kuhitaji kuongezewa damu. Kama wewe ni muhanga wa tatizo hili basi usiwe na wasiwasi. Fahamu kwamba kuna njia za asili na zisizo na madhara ambazo unaweza kuzitumia ukiwa nyumbani kwako ukapunguza athari ya tatizo na kulitibu kabisa.
Kinyesi/haja kubwa yenye Dam inakuwaje
Kupata kinyesi chenye damu kwa lugha ya kitaalamu tunaita hematochezia. Kikawaida rangi ya kinyesi inatakiwa kuwa brown au mpauko. Uwepo wa damu kwenye haja kubwa inaweza kusababishwa cha kuvuja kwa damu kwenye mishipa ya eneo la ndani ya utumbo mpana.
Kinyesi chenye damu huwa na rangi nyekundu na nyeusi. Kitu ninachotaka nikwambie kuona damu kwenye kinyesi siyo kitu cha kawaida. Siyo kwamba nakutisha lakini ni muhimu kutazama kwa makini na kufika hospitali kufanya vipimo.
Dalili na Viashiria kwamba Unapata Haja Kubwa yenye Damu
Kiashiria kikubwa kama tulivokwisha kusoma pale juu ni uwepo wa chembechembe za damu kwenye kinyesi. Utagundua tu kwa kuona mabadiliko ya kinyesi chako cha kawaida ulichozoea.
Wakati mwingine uwepo wa damu kwenye kinyesi inaweza kuwa ngumu kugundua. Lakini ikaambatana na dalili zingine kama maumivu ya tumbo, mwili kuishiwa nguvu na kuchoka sana. Kupata shida kwenye kupumua, kutapika, kubadilika badilika kwa mapigo ya moyo, kuharisha damu, na kupunguza uzito kwa kasi.
Dalili za mgonjwa hutegemea na chanzo cha uwepo wa damu kwenye haja kubwa na imechukua muda gani kwa halii hii pia kiasi cha damu ambacho mgonjwa amekwisha poteza kupitia hajakubwa.
Vipi kuhusu choo chenye kamasi?
Najua unajiuliza swali kama hili bila majibu. Kuwa na kinyesi chenye kamasi ni hali ya kawaida na nzuri kiafya. Kamasi hii inakusaidia kutoa hajakubwa kwa ulaini pasipo kujikaza. Lakini kamasi lisiwe jingi sana. Ukianza kuona kamasi nyingi basi kuna tatizo kubwa la kiafya na unatakiwa umwone daktari mapema iwezekanavyo.
Tabia na Mazingira Hatarishi Yanayokufanya Upatee Damu kwenye haja kubwa.
Damu kwenye haja kubwa inaweza kuanzia sehemu yoyote kwenye mfumo wa chakula. Kumaanisha kwamba lazima kuwe na mahali ndani ya mfumo wa chakula panapovuja damu kuanzia kwenye eneo la juu ya tumbo, tumbo lenyewe, utumbo mkubwa na mdogo. Kuvuja huku kwa damu inaweza kusababishwa na
- Kukua kupita kiasi kwa mishipa ya damu
- Kulegea kwa eneo la juu ya tumbo kutokana na kutapika sana
- Damu kutofikia baadhi ya maeneo ya utumbo mdogo
- Kuumia kihisia na msongo mkubwa wa mawazo
- Kuvimba na kututumka kwa ukuta wa tumbo na hivo kuanza kuvuja damu
- Kutanuka kwa mishipa ya damu iliyopo tumbomi
- Majeraha kwenye eneo la mkundu
- Tatizo la bawasiri ambapo ni kutokana na kuvimba kwa mishipa midogo ya damu kwenye eneo la mkundu.
- Saratani ya utumbo mpana
Hatua Tano za Kutibu Tatizo la Damu kwenye Haja Kubwa
Unapotaka kutibu tatizo lako basi hakikisha unatazama chanzo cha tatizo na siyo kutibu dalili. Hapa chini ni njia asili unazoweza kufanya pale unapoona kuna damu kwenye kinyesi kama tatizo linasababishwa na
Vidonda vya Tumbo
Kama vidonda vyako tumboni vinavuja damu basi unaweza kupata dalili kama kutapika damu. Vidonda hivi ni mareraha tumboni yanayotokana na kuliwa kwa ukuta wa tumbo na tindikali. Mara nyingi huambatana na maumivu makali ya tumbo.
Kutibu tatizo hili anza kwa kuepuka baaadhi ya vyakula ambavyo vinaongeza ukubwa wa tatizo. Vyakula kama vya ngano, pombe, sukari iliyochakatwa sana, kahawa na vinywaji vya soda. Badala yake kula zaidi vyakula vyenye kambakamba ambavyo havijakobolewa, mboga za majani, nazi na mafuta ya nazi. Tafiti zinasema kwamba matumizi ya juisi ya kabeji kila siku husaidia kuponya vidonda vya tumbo.
Gastritis
Gastritis ni tatizo la kiafya ambalo hutokana na kuvimba na kututumka kwa tishu za ukuta wa ndani wa tumbo. Dalili za gastritis hufanana sana na zile za vidonda vya tumbo. Hakikisha unatumia vyakua vyenye kambakamba kwa wingi, Vitamin B12 na mafuta ya omega 3. Na kisha uepuke vyakula vyenye tindikali kwa wingi kama machungwa na nyanya.
Diverticulitis
Diverticulitis ni hali ya kuvimba kwa sehemu ya ndani ya utumbo mpana. Supu ya mifupa na protein powder husaidia katika kumeng’enya chakula vizuri. Kula vyakula vyenye kambakamba (fibers) kwa wingi ni muhimu.
Rudisha viiini lishe vilivyopotea
kwenye mwili kama madini na Vitamins kwa kununua Virutubisho vyenye ubora wa hali ya juu ambavyo vimeshaandaliwa. Hakikisha unapata chanzo kizuri ili kuepuka bidhaa isiyo bora. Unaweza kutembelea stoo yetu kufanya manunuzi ya bidhaa hizi.
Kula Mbogamboga za kijani.
Licha ya kuwa na kambakamba nyingi kwenye mboga za kijani, pia kuna madini mengi ya magnesium ambayo tumeona hapo juu husaidia katika ufanyaji kazi mzuri wa misuli na hivo kupunguza tatizo la kukosa choo ama kupata choo kigumu.