Hatua 4 za Kushika Ujauzito Haraka.

kushika ujauzito haraka
mjamzito

Pale unapotaka kushika ujauzito haraka utagundua kwamba kufanya tendo la ndoa ni zaidi ya kufurahia na kukidhi matamanio ya mwili. Utagundua kwamba unahitaji kufanya vizuri kitandani ili kuongeza chansi ya kushika ujauzito. Kumbuka kwamba hakuna njia ambazo ni sahihi asilimia 100, lakini kujua wakati gani ushiriki tendo na katika staili ipi ni muhimu.

Lini Ushiriki Tendo la Ndoa ili Kuongeza Uwezekano wa Kushika Ujauzito haraka?

Siku nzuri kwa mwanamke kushirki tendo la ndoa ili uongeze uwezekano wa kushika ujauzito ni katika siku za hatari (window period). Siku hizi zinajumuisha siku tano kabla ya siku ya 14 ambapo yai hutolewa,na siku moja baada ya siku ya 14.

Kitendo cha yai kutolewa huitwa ovulation. Kumbuka ili kupata siku ya 14 unahesabu kuanzia pale ulipopata hedhi. Siku ya 14 ni siku ambapo yai hutolewa kwenye ovari na kwenda kusubiri mbegu kwenye mirija ya uzazi.

Siku mbili kabla ya siku ya 14 ni siku zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kushika ujauzito. Kwahivo hakikisha unafanya ngono zaidi kwenye kipindi hiki. Yai linapotolewa kwenye ovari linaweza kusubiri kwa masaa 48, lakini mbegu ya kiume inaweza kukaa kwenye kizazi kwa siku mpaka tano kusbiri yai litolewe.

Utajuaje Kama Yai Limetolewa kwenye Mfuko wa Mayai?

Lengo ni mbegu ya kiume ikutane na yai la mwanamke ili urutubishaji ufanyike na mimba itungwe.

Utajuaje kama yai limetolewa kwenye mfuko wa mayai?

Njia ya kwanza ni kuhesabu mpangilio wako wa hedhi kuanzia siku ya kwanza kupata hedhi kwenye mwezi husika. Tumia kalenda kufatilia siku zako. Angalia mzunguko wako kama unachukua siku 28 basi yai hutolewa siku ya 14.

Kumbuka siyo kila mwanamke anapata yai siku ya 14, wengine huwa na mzunguko mrefu zaidi. Kwa kesi hiyo angalia dalili zingine za kutolewa kwa yai kama hizi

  • Kubadilika kwa ute: ute huwa mzito na mweupe kama eneo jeupe la yai.
  • Kupanda kwa joto la mwili (Basal body temperature): Joto la mwili huongezeka taratibu baada ya ovulation. Unaweza kupima mabadiliko ya joto la mwili kwa kutumia kipima joto asubuhi baada tu ya kutoka kitandani. Ili kujipa uhakika fatilia mizunguko mingi ya hedhi upate siku sahihi ambayo yai hutolewa.
  • Ovulation kit: unaweza kutembelea duka la dawa kupata vifaa ambavyo hupima mkojo kujua mabadiliko ya homoni kwenye kipindi hiki cha ovulation.

Staili gani ni Nzuri ili Kushika Ujauzito haraka?

Kumbuka lengo ni kufanikisha mbegu nyingi ziingie kwenye uke na zifikie yai ili mimba iweze kutungwa. Baadhi ya mikao ya kufanya ngono huongeza wingi wa mbegu zinazoingia kwenye uke kuelekea kwenye yai.

Mikao kama kuchuma mboga (mwanaume kukaa kwa nyuma) na kifo cha mende (mwanaume kukaa juu) husaidia uume kupenya zaidi kiurahisi na hivo kurahisisha mbegu kufika kwenye mlango wa kizazi.

Mbegu za kiume ni waogeleaji wazuri, zinaweza kuogelea mpaka kwenye mlango wa kizazi ndani ya dakika 15. Kuweka mto chini ya mgongo wakati huo unafanya tendo husaidia mbegu kuogelea kwenda kwenye uelekeo sahihi.

Mara ngapi Ufanye Tendo la Ndoa ili Kushika Ujauzito Haraka?

Pengine umewahi kuuoma kwamba kufanya ngono kila mara inapunguza wingi wa mbegu na ubora wa mbegu. Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba mbegu huwa na ubora zaidi kama mwanamume akijizuia kufaya ngono kwa siku mbili mpaka tatu.

Tafiti pia zinaonesha kwamba wanawake hushika zaidi ujauzito wanapofanya ngono kila baada ya siku moja ama mbili.
Kufanya tendo kila siku kwenye siku za hatari itaongeza uwezekano wa mwanamke kushika mimba. Pumzika siku zingine kisha shiriki tendo kwenye siku tano za hatari.

Je Vilainishi vinaweza Kuathiri Uwezekano wako wa Kushika Ujauzito?

Karibu theluthi mbili ya wanawake hutumia vilainishi wakati wa tendo la ndoa ili kupunguza maumivu wakati wa msuguano. Maswali mengi ni je vilainishi hivi vina madhara kwenye mbegu za kiume?. Tafiti zinaonesha kwamba vilainishi hupunguza uwezo wa mbegu kuogelea kwa asilimia 40.

Dondoo zingine muhimu ili Kuongeza Uwezekano wa Kushika Ujauzito haraka.

  • Kufika kileleni: kwa mwanaume kumwaga mbegu ni muhimu ili kumpa ujauzito mwanamke. Kwa upande mwingine mwanamke siyo lazima afike kileleni ndipo ashike mimba japo mkao wake baada ya kufika kileleni husaidia mbegu kuogelea kiurahisi.
  • Rekebisha uzito wako: Uzito mkubwa na kitambi ama kuwa mwembamba sana kunapunguza uwezekano wa kushika mimba. Tembelea hapa kupata ushauri na virutubisho ili kupunguza uzito
  • Acha uvutaji wa sigara: Uvutaji sigara kwa mwanaume hupunguza idadi ya mbegu na pia kuongeza hatari ya mimba kuharibika kwa upande wa mwanamke.
  • Punguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenya caffeine mfano kahawa. Zaidi ya vikombe vitano kwa siku hupunguza ubora wa mbegu.

Ni lini Unatakiwa kumwona Daktari.

Endapo umekuwa ukijaribu kutafuta ujauzito kwa muda mrefu bila mafaniko zaidi ya mwaka. Pamoja na kujaribu njia hizi nilizolekeza hapo juu hakikisha unamwona daktari mtaalamu wa magonjwa ya wanawake ili kufanya vipimo kujua chanzo cha tatizo.

Wenza wasilaumiane kwani tatizo linaweza kuwepo kwa kila mmoja.
Wanawake chini ya umri wa miaka 30 wanatakiwa kusubiri walau kwa mwaka mmoja ndipo kumwona daktari. Kama una zaidi ya miaka 30 na unatafuta mtoto bila mafaniko kwa miezi 6 mfululizo hakikisha unamwona daktari haraka.

Kama pia una matatizo haya ya kiafya nenda hospitali haraka iwezekanavyo ufanye vipimo.

Daktari atafatilia historia ya tatizo lako na kukuanzishia huduma ya dawa.

Kipindi unaendelea na tiba ya hospitali hakikisha pia unapata virutubisho kutoka kwenye ofisi yetu iliyopo Dar es salaam, Magomeni Mwembechai, Jengo la Mwembechai Plaza. Vitakusaidia kuongeza chansi ya kushika ujauzito na kuimarisha mbegu kwa mwanaume.

Virutubisho hivi Huongeza Chansi ya Kushika Mimba.

Soy-power

Husaidia kuimarisha uzalishaji na upevushaji wa mayai na kurekebisha homoni hasa kwa waliowahi kutumia uzazi wa mpango, wanaokaribia kukoma hedhi na kuimarisha afya ya mifupa.

Soy power Tsh 90,000

Zinc

Husaidia upevushaji na utolewaji wa mayai kutoka kwenye mfuko wa mayai na kurekebisha homoni

kirutubisho cha zinc Tsh 65,000/=

Vidonge vya kusafisha kizazi vya UCP

UCP

UCP inajumuisha vidonge 2 vyenye mwonekano hapo juu vya kuweka ukeni. Husaidia kusafisha kizazi, na kuwafaa wenye matatizo ya PID, mirija kuziba, UTI na matatizo ya uke

Gharama ya UCP ni sh 50,000/=

Muhimu: Muhudumu atapendekeza aina ya dawa na virutubisho kwa kuendana na chanzo cha tatizo lako, kwahivo ni muhimu kujieleza kwa kina unapochati na daktari. Lakini pia kwa wanawake wote waliokosa mimba kwa muda mrefu tunawashauri kusafisha kwanza kizazi kwa dawa hii ya UCP kabla hawajaanza dawa zingine.

Ushuhuda wa mgonjwa wa uzazi Kabla ya kutumia dawa na Baada ya Kutumia

angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 kupata Tiba ili nawe uwe miongoni mwa mashuhuda wetu.

Makala inayofuata: Je inachukua muda gani kushika mimba

Share and Enjoy !

Shares
Shares