kizazi kupanuka husababishwa na nini?

kizazi kupanuka (adenomyosis)
kizazi

Kupanuka kwa mfuko wa mimba(uterus) au wengi huita kizazi kupanuka ni tatizo linaloathiri wanawake wengi sana wenye umri wa kuanzia miaka 40 na 50. Hali hii hutokea baada ya tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba zinazoitwa endometrial tissue kuanza kukua kuelekea kwenye tishu za ndani za mfuko wa mimba.

Tatizo hili kitaalamu huitwa Adenomyosis, linaweza kusababisha maumivu makali wakati wa hedhi. Habari njema ni kwamba kuna tiba mbadala nyingi ambazo unaweza kutumia ukiwa nyumbani kwako kupunguza makali ya maumivu haya.

Adenomyosis ni kitu gani?

Mayo clinic wanaeleza Adenomyosis ni kupanuka kwa mfuko wa mimba ambako husababishwa na kukua kwa tishu za ukuta wa mfuko wa mimba kuelekea kwenye tishu na misuli ya ndani ya mfuko wa mimba. Kutokana na kwamba dalili za tatizo hili halijioneshi mapema hivo imekuwa ngumu kwa wataalamu wa afya kujua ukubwa wa tatizo hili.

Lakini kwa makadirio ni kwamba tatizo hili huwakuta zaidi wanawake waliowahi kujifungua, wenye umri kuanzia miaka 40s na 50s.

Kizazi kupanuka na Homoni ya Estrogen

Adenomyosis hutegemea na kiasi cha homoni ya estrogen kwenye mwili wa mwanamke. Pale kiasi cha estrogen kinapokuwa chini mfano katika kipindi cha hedhi ama baada ya upasuaji wa kutoa kizazi chote, tatizo hili huwa lipo chini. NB kwa msaada homoni za estrogen hutolewa kwa mwanamke ili kuhusika katika kujenga sifa za mwanamke kama kuota matiti, kupata hedhi na kuandaa mfuko wa mimba kwa ajili ya kupokea ujauzito.

Tofauti kati ya Adenomyosis na Endometriosis

Tumeona hapo juu kwamba adenomyosis ni kukua kwa seli ama tishu za ukuta wa mfuko wa mimba kuelekea ndani kwenye misuli ya mfuko wa mimba. Lakini endometriosis ni pale tishu laini za mfuko wa mimba zinapokua kuelekea maeneo mengine ya uzazi wa mwanamke. Mfano kuelekea kwenye tumbo la chini, nyonga na mirija ya uzazi.

Matatizo haya mawili huwa na dalili zinazofanana na wakati mwingine madaktari hushindwa kutofautisha mpaka pale wanapofanya upasuaji. Upasuaji kujua kama seli zimeanza kukua kuelekea mahali tofauti au mpaka pale wanapoondoa kizazi chote.

Je ni hatari ya kwa kizazi Kupanuka?

Kwa ujumla  kizazi kupanuka siyo hatari. Lakini angalizo kwa wanawake ambao tatizo limekuwa kubwa na hivo kupelekea kuvuja damu nyingi sana wakati wa hedhi. Tatizo ambalo linaweza kuleta upungufu wa damu mwilini. Kuvuja sana kwa damu hupelekea wanawake wengi kushindwa kufanya kazi zao kiufasaha, kushindwa kushirikiana na marafiki na pia msongo wa mawazo.

Je Adenomyosis ni Saratani?

Jibu ni hapana, kupanuka huku kwa kizazi siyo aina ya saratani. Japo tatizo hili linaweza kusababisha mkusanyiko wa tishu ambazo huitwa adenomyoma. Huu ni uvimbe  wa kawaida usio saratani. Baadhi ya wanawake hupata hofu kwamba kuna uhusiano kati ya adenomyosis na saratani ya mfuko wa kizazi. Lakini utafiti unasema hakuna uhusiano wa moja kwa moja, japo baadhi ya wanawake wenye adenomyosis wanaweza kupata saratani pia.

Je kupanuka Kizazi kunaweza kusababisha ugumba?

Inawezekana kabisa kizazi kupanuka kutokana na adenomyosis kusababisha ugumba, kama itatokea kwa wanawake wenye umri mdogo. Hii ni kutokana na kuharibika kwa mazingira ya mfuko wa mimba. Kushindwa kushika ujauzito pia kunaweza kusababishwa na mabadiliko katika ukuta wa uterus.

Dalili na viashiria kwamba Kizazi chako Kimepanuka.

Je Kizazi Kupanuka yaweza Kusababisha Kukosa choo au upate choo kwa shida?

Jibu ni ndio, kwa ujumla badhi ya dalili zingine zinazoweza kusababishwa na kupanuka kwa kizazi ni pamoja na

Nini husababisha Kupanuka kwa kizazi na Vihatarishi

Mpaka sasa bado hakuna sababu ya moja kwa moja kuhusu kinachosababisha tishu hizi kukua lakini baadhi ya nadharia zinatoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha tatizo hili ni kama ifuatavyo

  • Kuvamiwa kwa mfuko wa mimba na tishu za ukuta wa mfuko wa mimba
  • Nadharia ingine inasema kwamba tishu hizi huwepo tangu mtoto anapoafanyika tumbo mwa mama
  • Kututumka kwa tishu za mfuko wa mimba wakati wa kujifungua hupelekea kulegea kwa ukuta mwembemba unaotenganisha ukuta wa nje wa mfuko wa mimba na eneo la ndani la misuli ya uterus.
  • Seli za uroto (bone marrow) kuingia kwenye tishu za kizazi na hivo kusababisha ukuaji huu wa tishu.

Makundi ya Wanawake waliopo kwenye Hatari ya kupata Adenomyosis

  • Wenye umri wa miaka 40s na 50s
  • Waliowahi kujifungua zaidi ya mara moja
  • Waliowahi kutoa mimba au kufanyiwa upasuaji wa uterus
  • Waliopo kwenye dozi za saratani ya matiti.

Njia hizi tano Zitakusaidia Kupunguza Makali Ya Kizazi kupanuka

1.Tumia kitu cha moto kukanda sehemu ya tumbo : Mfano chupa ya plastic yenye maji ikiwekwa kwenye tumbo la chini husaidia kupunguza maumivu makali.

2.Fanya masaji kwa kutumia mafuta ya lavender (mrujuani)

3.Jaribu kutumia tiba asili na virutubisho: Kuna aina nyingi za tiba asili ambazo zimeonesha matokeo makubwa katika kutatua changamoto za hedhi. Mimea hii ni kama Valerian, Rhubarb na Tiba asili za china( Chinese traditional medicine). Virutubisho ni kama Vitamin B1 na Vitamin E, madini ya Magnesim na mafuta ya Omega 3. Unaweza kupata virutubisho hivi kwenye store yetu.

4.Badili lishe yako kupitia kwa; Kuongeza vyakula vyenye omega 3 kwa wingi ka samaki, mayai, walnuts na flaxseed. Tumia vyakula vyenye nyuzinyuzi/kambakamba kwa wingi mfano mboga za majani, jamii za karanga. Epuka kula vyakula vilivosindikwa kama mikate na mandazi, usitumie vinywaji vyenye caffeine kama pombe na kahawa, na hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku.

5.Fanya mazoezi ya kutosha: mfano Yoga.

Muhimu kwa wagonjwa wa Kizazi kupanuka

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya kizazi kupanuka na vimbe kwenye kizazi, kabla hajafikiria kufanyiwa upasuaji, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na mirija. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge vi4 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama kukosa hedhi, vimbe ndogo, harufu mbaya ukeni, maambukizi ya fangasi na bacteria, kupanuka kwa kizazi, PID na kuziba kwa mirija ya uzazi.

ucp
UCP

Vidonge hivi vinatumika kwa wiki mbili Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika siku 2,unaweka tena kidonge kingine.

Gharama ni sh 100,000/=

Angalizo unapotumia Uterus Cleasing Pill’s

Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi, ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata Huduma

Share and Enjoy !

Shares
Shares