Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Kulegea kwa uke

Je Inawezekana Kutibu Kulegea Kwa Uke?

kulegea kwa uke

Kulegea kwa uke ni moja ya mada inayowakuna sana wakina mama na wakina dada . Wengi hupendelea zaidi kuwa na uke uliobana ili kuwafurahisha wenza wao. Kuna nadharia dhana potofu nyingi sana kuhusu suala la uke wengine huamini kwamba uke unatakiwa kupoteza hali ya kutanuka na kusinyaa na kuwa mkubwa miaka yote.

Uke ni kiungo chenye lastiki, maana yake kinaweza kunanuka ili kuruhusu kutoka mfano mtoto na vitu kuingia yani uume. Lakini haitachukua muda mrefu kwa uke kusinyaa na kurudi katika hali ya kawaida.

Misuli ya uke

Uke hutanuka, kulegelea  na kuongezeka ukubwa kiasi fulani kadiri umri unavoongezeka na unavozaa zaidi. Sasa endelea kusoma makala yetu hii ili ufahamu vyema uke wako pamoja na fikra potofu kuhusu uke.

Nataka nikwambie kulegea kwa uke ni dhana mbaya ambayo inatumika kuwadhalilisha wanawake. Inawatokea zaidi hasa pale wanapoachana na wanaume zao. Wanaume hutumia hiki kama kigezo na silaha ya kuwadhalilisha wanawake kwamba wana uke mpana na wenye maji (bwawa) kitendo ambacho siyo kizuri.

Dhana potofu ni kwamba mwanamke mwenye kulegea kwa uke amekutana kimapenzi na wanaume wengi. Ukweli ni kwamba haijalishi umekutana na wanaume wangapi uke ni lastiki unaweza kutanuka na kusinyaa na ukaendelea kuwa kwenye ubora wake kama kawaida.

Uke mkavu yaweza kushiria ugonjwa

Ni muhimu kufahamu kwamba kuwa na uke uliokaza sana inaweza kuashiria una tatizo la kiafya. Hasa pale unapoingiliwa na kupata maumivu makali pamoja na kwamba mwenza wako amekuandaa vizuri. Mwili wa mwanamke unaposisimka misuli ya uke inalegea ili kuruhusu uume kupenya vizuri.

Kama misuli ya uke bado imekaza basi itakufanya upate maumivu makali sana na hutofurahia na kumaliza tendo la ndoa. Kama tatizo la maumivu ya uke yataendelea basi weka apointment na daktari wa magonjwa ya wanawake ili upate vipimo na ushauri zaidi maana unaweza kuwa na matatizo yafuatayo.

Hujaandaliwa vizuri na uke wako haujalainika inavotakiwa

Mwili wa mwanamke unaposisimuliwa basi huweza kutoa majimaji ya asili ambayo hulaishisha uke. Hivo hakikisha mwenza wako anakuaanda vizuri kabla ya kukuingilia. Kama una tatizo la kupata majimaji kidogo haijalishi umeandaliwa kiasi gani basi bofya hapa kutembelea stoo yetu kuagiza virutubisho ili ufurahie tendo la ndoa.

Maambukizi au ugonjwa

Maambukizi hasa ya kupitia ngono ni chanzo cha kupata maumivu wakati wa tendo. Maambukizi haya yanaweza kuwa ya fangasi au bakteria

Ajali na Msongo wa mawazo kupita kiasi.

Ajali kwenye maeneo ya nyonga na mfumo wa uzazi kwa ujumla inaweza kusababisha maumivu makali wakati wa tendo la ndoa na kukaza kwa uke. Hivo hakikisha umepona vizuri kabla hujaanza kushiriki ngono

Tatizo la Viginismus

Vaginismus ni tatizo la uke ambapo misuli ya uke inaweza kukaza pasipo hiyari ya mwanamke na hivo kuzuia uume kupenya. Wanawake wachache sana hukubwa na tatizo hili yaweza kuwa mmoja kati ya wanawake 500. Tatizo hili linaweza kuletekezwa na hofu na msongo wa mawazo. Dactari anaweza kutumia tiba zaidi ya moja katika kutatua shida hii ikiwemo kuongea na mgonjwa na kumshauri ama kutumia vifaa vya kutanua uke.

Ubora wa Uke Unabadilika Kadiri ya Muda na Umri

Fahamu kwamba vitu viwili vikubwa vinavyoathiri ubora na uwezo wa kunanuka na kusinyaa kwa uke ni umri na mara ngapi umezaa watoto. Kufanya ngono mara kwa mara na kubadilisha wanaume siyo tatizo na haviathiri uke wako.

Kadiri unavozaa zaidi ndivyo misuli ya uke huchoka na kulegea. Wanawake waliozaa zaidi ya mara moja huchoka zaidi. Umri pia kadiri unavosonga ndivyo uke huchoka zaidi hatakama uliwahi kujifunguaama laa.

Kulegea Kwa Uke Kutokana na Umri

Unapofikia umri kuanzia miaka ya 40 utaanza kuona mabadiliko. Hii ni kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen pale unapokaribia kukoma hedhi (menopause). Utaanza kupata dalili kama

  • Uke kusinyaa na  kuwa mdogo
  • Kukauka kwa uke
  • Kupungua kwa tindikali kwenye uke
  • Uwezo wa kutanuka kupungua

Kulegea kwa Uke Kutokana na Kuzaa

Ni kawaida kwa uke kulegea na kupungua ubora wake baada ya kujifungua. Hii inatokana na misuli ya uke kunanuka sana ili kuruhusu mtoto kupita. Baada ya kujifungua utagundua kwamba uke umebadilika kuliko ulivyokuwa mwanzo. Usipate shaka maana hii ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke lakini isichukue muda mrefu.

Maana uke unatakiwa urudi katika ubora wake baada ya miezi kadhaa. Japo haitarudi 100% kama shape ya mwanzo. Kama umejifungua mara nyingi zaidi basi uke utakuwa umetanuka zaidi na kupoteza lastiki yake kwa kiasi kikubwa. Najua hii ni habari mbaya kwa wengi lakini usipate shaka nitakuelekeza mazoezi ya kufanya pamoja na virutubisho vya kutumia ili kukaza uke na   kurudi kama zamani.

Jinsi ya Kukaza Misuli ya Uke Iliyolegea Kupitia Mazoezi ya Nyonga

Mazoezi ya nyonga ni njia nzuri na salama ya kukaza misuli ya uke inayoitwa(pelvic floor muscles). Misuli hii inasaidia kuweka sapoti kwenye

  • Kibofu cha mkojo
  • Kwenye eneo la haja kubwa
  • Utumbo mdogo na
  • Mfuko wa mimba (uterus)

Misuli ya pelvic floor inapolegea kutokana na umri kwenda ama kuzaa: basi utaanza kupata dalili kama

  • Kuponyoka kwa mkojo pasipo na hiyari yako
  • Kujiskia hali ya kukojoa mara kwa mara
  • Kupata maumivu ya nyonga na
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa

Mazoezi ya pelvic floor yanaweza kukusaidia kwa kesi za kurudisha ubora wa uke, lakini kama unashindwa kudhibiti mkojo mara kwa mara na kuvuja basi hakikisha unapata vipimo maana yaweza kuwa una shida ingine kubwa ya kiafya. Najua sasa unahamu ya kusikia kuhusu mazoezi haya basi na tuanze kuyachambua

Kegel Exercise

Kwanza unatakiwa kufahamu kuhusu misuli inayohusika katika kukusaidia kwenye safari yako ya kukaza uke. Fanya zoezi hili wakati unakojoa bana mkojo katikati.Ukifanikiwa zoezi hili basi tayari umetambua misuli yako ya kuitumia katika zoezi linalofuata, malizia kutoa mkojo iliobaki baada ya hapo fuata maelekezo haya

  1. Tafuta mahali pazuri pa kufanyia zoezi ukiwa nyumbani kwako, sehemu ambayo unaweza kulala chali ili tuanze zoezi
  2. Kumbuka misuli uliyokaza pale ulipokuwa unakojoa, basi tumia misuli hiyo hiyo.
  3. Kaza misuli yako kwa sekunde 5, kisha relax kwa sekunde 5 zingine
  4. Rudia zoezi hili mpaka awamu 5 kwa wakati mmoja unakaza unaachia

Kadiri unavoendelea na kulizoea zoezi hil basi ongeza muda wa kufanya zoezi hadi sekunde 10 kutoka sekunde 5 za awali. Hakikisha usitumie misuli ya tako, tumia misuli ya ndani ya uke na nyonga (pelvic floor muscles). Kwa matokeo mazuri zaidi fanya seti 3 za mazoezi ya kegel mara 5 mpaka 10 kwa siku.

Pelvic Tilt Exercise

Mazoezi ya kegel

Kukaza uke kwa kutumia zoezi hili fuata maelekezo haya

  1.  Lala chali kwenye floo  kisha mikono inyooshe chini
  2. Vuta tumbo kuelekea ndani kwa kubinuka kuelekea juu, unapofanya hivi sehemu ya mgongo itakuwa flati
  3. Endelea kukaza tumbo lako kwa sekende 4 bila kuachia
  4. Rudia hili zoezi mara 10 kwa kukaza na kuachia kila baada ya sekunde 4, ndani ya muda mmoja na urudie seti 5 ndani ya siku moja.

Jaribu Green health Uterus Cleansing Package Yetu.

Ni muunganiko wa virutubisho vya asili aina mbili zilizohifadhiwa katika mfumo wa vidonge 60. Vitakusaidia

  1. Kubalansi homoni za kike na kuimarisha ufanyaji kazi wa ovari
  2. Kuimarisha misuli ya uke na kujenga kuta za uke
  3. Kulainisha ngozi na kupunguza kasi ya uzee
  4. Kuzuia kutokea kwa saratani ya matiti
  5. Kuua bacteria wabaya na fangas (candidiasis) na kuimarisha kinga ya mwiliVirtubisho hivi vinawafaa zaidi wanawake
  • Wenye ute mdogo ukeni
  • Waliokoma hedhi
  • Wenye matatizo ya uke kusinyaa na kulegea
  • Wawagumba kutokana na kuvurugika kwa homoni na
  • Wanawake wanaotaka kuboresha afya zao

Muhimu kwa Wanawake wa tatizo la Kulegea kwa Uke

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya kulegea kwa uke na maambukizi ya bacteria ukeni tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na kuimarisha misuli ya uke. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama, kulegea kwa misuli ya uke, harufu mbaya ukeni, muwasho, fangasi na PID.

vidonge vya kusafisha kizazi na kuimarisha uke

Vidonge hivi vinatumika kwa siku 7. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika siku 1,unaweka tena kidonge kingine

Angalizo Wakati Unatumia Uterus cleansing Pills.

UCP haifai kutumiwa na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi na pia ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

Ofisi yetu ipo Mwembechai, Magomeni Dar eslaam.

Bei ya Ucp ni Tsh 50,000/ kwa dozi moja.Tunashauri utumie dozi mbili.
Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

Share and Enjoy !

Shares
Shares