Mwanake kutokwa Damu baada ya Tendo la Ndoa

kuvuja damu baada ya tendo la ndoa
damu

Wanawake wengi hukutana na tatizo la kutokwa damu baada ya kumaliza kufanya mapenzi. Ukweli ni kwamba karibu asilimia 63 ya wanawake waliokoma hedhi hukumbana na matatizo ya ukavu kwenye uke na kutokwa damu baada ya tendo la ndoa.

Kinachosababisha Kutokwa damu baada ya Tendo la Ndoa.

Kutokwa damu baada ya tendo la ndoa inaweza kutokea kwa mwanamke wa umri wowote. Kwa wanawake wadogo ambao bado hawajafikia kukoma hedhi chanzo kikubwa cha tatizo ni kwenye mlango wa kizazi (cervix). Wanawake walikoma hedhi, chanzo cha tatizo hutofautiana yaweza kuwa kwenye

 • Mlango wa kizazi
 • Kizazi
 • Kwenye mashavu ya uke na kwenye
 • Njia ya mkojo.

Maambukizi.

Maambukizi kwenye njia ya uzazi au mkojo yanaweza kupelekea kutokwa damu baada ya tendo la ndoa. Maambukizi haya ni kama

 • PID
 • Magonjwa ya zinaa
 • Maambukizi kwenye uke na
 • Maambukizi kwenye mlango wa kizazi.

Genito-urinary Syndrome of Menopause (GSM)

Tatizo hili kwa kifupi GSM hutokea zaidi kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi, wale waliokoma hedhi na wanawake waliokwisha kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mifuko ya mayai (ovari).
Wanawake wanapofikia ama kukaribia kukoma hedhi, kiwango cha homoni ya estrogen hupungua. Estrogen inavopungua, baadhi ya dalili hutokea kwenye uke wako.

Mwili huanza kuzalisha kiwango kidogo na maji maji yanayolainisha uke, na hivo kupelekea uke kuwa mkavu na kuvimba wakati mwingine. Kiwango kidogo cha estrogen hupelekea pia kupungua kwa hali ya kuvutika ya uke. Tishu za uke zinakuwa nyembamba na kusinyaa. Hali hii hupelekea maumivu kwenye tendo la ndoa, kukosa uhuru na pia kutokwa damu.

Ukavu kwenye Uke.

Uke kuwa mkavu ni sababu ingine ya kutokwa damu baada ya tendo la ndoa kwa mwanamke. Uke mkavu unaweza kusababishwa ana vitu hivi.
Kunyonyesha

 • Upasuaji wa kuondoa mifuko ya mayai
 • Matumizi ya dawa mfano za pumu, dawa za kupunguza athari ya msongo wa mawazo.
 • Chemotherapy na radiotherapy
 • Kufanya ngono bila kuandaliwa
 • Matumizi ya kemikali na sabuni kwenye kuosha uke

Kulegea kwa Uke

Uke unaweza kulegea na kupata majeraha hasa mwanamke akifanya ngono kupita kiasi pasipo mpangilio (rough sex). Majeraha hutokea zaidi pale mwanmke anapokuwa amekoma hedhi au siku chache baada ya kujifungua.

Saratani

Kutokwa damu kusiko na mpangilio, hasa baada ya tendo la ndoa ni moja ya dalili ya saratani ya shingo ya kizazi. Ni muhimu kuwahi kufika hospitali kama tatizo litaendelea kuwa la muda mrefu.
Saratani ya shingo ya kizazi nuwapata zaidi wanawake wenye umri zaidi ya miaka 50 au waliokoma hedhi. sababu zingine hatarishi ukiachilia mbali umri ni pamoja na uzito mkubwa, matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi, na maambukizi ya virusi wa papiloma.

Maelezo ya mwisho

Kumbuka unahitaji kumwona daktari endapo unaona dalili kama

 • Muwasho ukeni au hali ya kuungua
 • Hali ya kuungua ukeni wakati wa kukojoa
 • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
 • Hedhi nzito yenye mabongemabonge
 • Maumivu ya mgongo wa chini
 • Maumivu makali ya tumbo
 • Kutapika na kichefuchefu
 • Kutokwa na uchafu ukeni kusiko kawaida

Athari za Kutokwa Damu baada ya Tendo la Ndoa.

Upungufu wa damu (Anemia)

Kutokwa damu kwa muda mrefu hupelekea mwanamke kuishiwa damu. Kutokana na kupoteza chembechembe nyingi nyekundu za damu. Upungufu wa damu huambatana na dalili hizi

 • Mwili kukosa nguvu na ganzi
 • Uchovu mara kwa mara
 • Kupata hali ya kusinzia muda mwingine
 • Maumivu ya kichwa na
 • Kubadilika rangi ya ngozi

Wasiliana nasi kupitia whatsapp namba 0678626254.

Share and Enjoy !

Shares
Shares