Homa ya mapafu/Pneumonia au nimonia ni  kitu gani?

Homa ya mapafu au nimonia ni ugonjwa mmoja unaosababisha vifo vingi vya watoto wadogo kuliko ugonjwa mwingine duniani kote. Inakadiriwa kwamba watoto zaidi ya 2500 wanafariki kila siku kutokana na nimonia. Kwa taarifa za uhakika kutoka kweye kitengo kinachoshugulikia magonjwa ya mapafu nchini marekani  kinasema kuna kuna visababishi zaidi ya 30 vya nimonia.

homa ya mapafu

Pneumonia  ni athari zinazotokea katika mapafu. Athari hizi zinaweza kusababishwa na bacteria, virusi au fangasi. Homa ya mapafu husababisha mcharuko na kututumka kwa vifuko vya hewa (alveolis) kwenye mapafu na kufanya mapafu kujaa maji na kupelekea ugumu katika upumuaji. Endelea kusoma zaidi makala yeru ili kujua namna gani ya kujikinga na kutibu pneumonia.

Dalili Za Homa Ya Mapafu (Pneumonia)

Dalili za pneumonia zinaweza kuwa za kawaida na pia dalili kali sana ambazo zinaweza kuhatarisha maisha kama ifuatavyo

 • Kikohozi kikali na kupata makohozi yenye mithili ya kamasi
 • Kupata homa kali na mwili kutoka jasho jingi
 • Kupata ugumu katika upumuaji
 • Maumivu ya kifua
 • Watoto chini ya miaka mitano hupumua haraka haraka
 • Watoto pia wenye pneumonia huweza kutapika, kuishiwa nguvu, na kupata shida ya kula na kunywa
 • Wagonjwa wazee na wenye umri mkubwa, joto hushuka sana kuliko joto la kawaida la mwil.

Aina Za Homa Ya Mapafu (Pneumonia)

Nimonia inaweza kugawanya katika makundi mbalimbali, mgawanyo wa kwanza ni kutokana na vimelea waliosababisha kutokea kwa ugonjwa.

 • Nimonia ya virusi: vimelea wanaosabaisha aina hii ya homa ya mapafu ni virusi na mara nyingi ni virusi kwenye mfumo wa hewa. Aina hii ya homa ya mapafu huwapata zaidi watoto na wazee. Aina hii ya homa ya mapafu huisha haraka ikilinganishwa na ile inayosababishwa bna bacteria.
 • Nimonia ya bacteria: bacteria wanaosababisha aina hii ya homa ya mapafu huitwa Streptococcus pneumoniae, Chlamydophil pneumoniae ma Legionella pneumophila.
 • Nimonia ya fangasi: fangasi kutoka kwenye udongo ama kupitia kwa viumbe kama ndege wanaweza kusabaisha nimonia, kama hewa ya manyoya ikivutwa. Watu wenye kinga ndogo na wenye magonjwa sugu wapo kwenye hatari zaidi ya kupatwa na nimonia ya fangasi.

Aina Za Nimonia (Homa Ya Mapafu) Kutokana Mahali.

 1. Nimonia ya kuambukizwa hospitali-hospital acquired pneumonia (HAP) : aina hii ya nimonia hupatikana kutokana na maambukizi hosputali wakati unapata tiba. Aina hii ya nimonia yaweza kuwa hatari zaidi kwani vimelea wanakuwa sugu na hawasikii dawa.
 2. Nimonia ya kuambukizwa kwenye jumuiya-community acquired pneumonia): hii ni aina ya homa ya mapafu ambayo huambukizwa nje ya kituo cha afya.
Je nimonia inaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine kwa kugusana?

Nimonia ya bacteria na ile ya virusi zote kwa pamoja zaweza kuambukizwa kwa kuvuta hewa yenye vimelea kutoka kwenye mafua ama kikohozi.nimonia ya fangasi haiwezi kuambikizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine.

Makundi Yaliyo Kwenye Hatari Zaidi Ya Kupata Nimonia.

Japo kila mtu anaweza kuugua homa ya ini lakini kuna baadhi ya makundi wapo kwenye hatari zaidi pengine kutokana na kutoimarika kwa kinga zao, mitindo ya maisha, hali zao za kiafya ama mazingira wanakoishi, makundi haya ni

 1. Waototo chini ya miaka miwili na watu wazima zaidi ya miaka 65
 2. Watu wenye matatizo katika kumeza na waliowahi kuugua kiharusi
 3. Wenye kinga hafifu kutokana na eidha kuugua sana magonjwa ama matumizi ya dawa kwa muda mrefu kama dawa za saratani.
 4. Wavutaji wa sigara, wanywaji wa pombe na watumiaji wa dawa za kulevya
 5. Wagonjwa wenye matatizo sugu kama vile matatizo ya moyo, pumu, kisukari na matatizo mengine ya mfumo wa upumuaji.
HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUJIKINGA KUPATA HOMA YA MAPAFU
 1. Hakikisha unapata chanjo ya homa ya mapafu: chanzo hizi hupatikana mahospitalini. Kabla hujapata chanjo ongea na Dactari wako akupe ushauri.
 2. Hakikisha watoto wanapata chanjo ya homa ya mapafu: madactari wanashauri watoto wenye umri wa chini ya miaka miwili na wenye umri wa miaka miwili mapak mitano kupata chanjo kutegemeana na mazingira hatarishi ya kupata homa ya ini.
 3. Weka mazingira ya kuishi katika hali ya usafi: hii itakusaidia kuzuia maambukzizi ya njia ya hewa ambayo huletekeza homa ya mapafu, osha mikono yako kila mara kwa sabuni na maji ya moto.
 4. Usivute sigara: uvutaji wa sigara unaharibu tishu za mapafu na hivo kuzorotesha kinga ya mwili.

Tahadhari za kuchukua pale unapotibu nimonia

Kama umeona una dalili za nimonia basi onana na dactari haraka ili kufanya vipimo na kupata uhakika, hasahasa kama uliugua mafua makali, ama umri wako ni zaidi ya miaka 65. Watoto wadogo na wale wachanga wanatakiwa kufanyiwa vipimo kwa haraka ili kupata uhakikisho kuwa wanaumwa nimonia kutokana na kwamba wapo kwenye hatari zaidi ya kufa kwa ugonjwa huu kuliko watu wazima.kama unajisikia dalili zifuatazo basi wahi hospitali ili kuzuia tatizo la nimonia lisiwe kubwa zaidi

 • Kupata damu kwenye mkojo
 • Kukosa nguvu na kudondoka mara kwa mara
 • Kukosa uwezo wa kupumua kwa ghafla
 • Viashiria vya kukusanyika kwa maji kwenye mapafu
 • Homa kali ambayo inapandisha joto la mwili mpaka 104 degree
 • Kuharisha na kutapika mfululizo.

Maelezo ya hitimisho kwa ugonjwa wa nimonia

 • Pneumonia ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kugusana na mgonjw na pia huleta athari mbaya sana kwenye mapafu, mambukizi haya yakiwa ni ya bacteria, virusi na vimelea wengine.
 • Jinsi ya kuzuia pneumonia ni pamoja , kuimarisha kinga ya mwili, kula chakula safi na bora, kunyonyesha watoto mda mrefu, kutibu alegi na matatizo yote ya mfumo wa hewa na kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Tiba asili kwa Nimonia Kupitia Vidonge vya Propolis

Vidonge vya propolis vimethibitika kutibu nimonia inayoanza na ile sugu pia. Itakufanya uondokane na dalili mbaya za maumivu ya kifua, kukohoa, homa kali, kushindwa kupumua vizuri na kuishiwa nguvu. Ndani ya week 1 ukianza kutumia dawa hii utaanza kupata matokeo.
Gharama ya dawa ni Tsh 90,000/= tu

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai.

Tupigie kwa namba 0762336530 au

Share and Enjoy !

0Shares
0 0