Categories
Dondoo za afya

Kwanini Unanuka mdomo

Leo nataka kushea na wewe njia zangu rahisi jinsi gani uweze kutibu tatizo la kunuka mdomo, ikiwemo lishe na virutubisho vya kutumia katika program yako.

Kunuka mdomo ni hali ambayo kila mtu haipendi na moja ya matatizo ambayo watu huona aibu sana kuelezea. Lakini nataka nikwambie rafiki yangu unaesoma makala hii kwamba ukitaka kutibu tatizo la kunuka mdomo  inahitajika kufahamu chanzo cha tatizo hili.

Kikawaida kunuka mdomo kunasababishwa na kumea kwa bakteria wabaya kwenye mwili wako. Lkini kunuka mdomo ambako ni sugu na imekuwa ni hali ya muda mrefu husababishwa ukuaji kupita kiasi wa fangasi aina ya Candida kwenye mwili. Baadhi ya vyakula kama kitunguu saumu vinaweza kukupa ahueni ya muda mfupi . Nependa ufahamu kwamba kunuka mdomo si tu kwamba inaleta karaha bali pia ni kiashiria kwamba una tatizo kubwa la kiafya

Sababu Za Kunuka Mdomo

Karibu kila mmoja wetu hupata tatizo la kunuka mdomo katika muda fulani kwenye maisha yake. Wakati mwingine kisababisho kinaweza kuwa ni chakula ulichokula au aina ya bacteria wanaopatikana kwenye mdomo wako.

Harufu mabaya kwenye mdomo hutokea nyuma ya ulimi, kwenye koo na kwenye tonsils. Huku ndiko bacteria wabaya wanakozailiana na kutoa kemikali za Sulphur ambazo ndizo huleta harufu mbaya. Kwahiyo harufu mbaya mdomoni inaweza kusababishwa na ulaji wa vyakula vyenye Sulphur kwa wingi.

Ambapo kikawaida harufu hii huisha baada ya chakula kuchakatwa. Harufu mbaya mdomoni ya muda mrefu ni kiashiria cha uwepo wa tatizo la kiafya ambapo yaweza kuwa ni

 • Kutofanya usafi wa mdomo kwa makini
 • Lishe duni isiyo na virutubisho vya kutosha
 • Magonjwa ya fizi
 • Kuoza kwa meno na
 • Mataizo mengine ya kiafya kama kisukari au magonjwa ya ini

Ulaji wa vyakula hivi inaweza kuwa sababu ya kunuka mdomo kutokana na kwamba vizalisha kemikali nyingi ya Sulphur, vyakula hivi ni kama

 • Kitunguu maji na  kitunguu saumu: vyakula hivi huleta harufu kali zaidi hizo unatakiwa kuvitumia kwa tahadhari.
 • Vyakula vya sukari: sukari hupelekea kuoza kwa meno na kupelekea harufu mbaya mdomoni
 • Vinywaji vilivyosindikwa kama soda.

Hatua Tano za Kutibu tatizo la Harufu Mbaya Mdomoni

 1. Epuka kutumia vyakula vya sukari kwa wingi na nafaka kupita kiasi: hii ni ahtua ya kwanza katika kuelekea kuondoa harufu mbaya mdomoni, ambapo tunalenga katika kufata lishe ambayo ina kiwango kidogo cha sukari na nafaka. Vyakula hivi ni kama mikate, wali na bidhaa zingine za ngano. Hivo unapokula zaidi wanga fahamu kwamba unaenda kuvunjwa vunjwa na kubadilishwa kuwa katika mfumo wa sukari kitu ambacho ni mbolea kwa ukuaji wa fangasi na bacteria wabaya kwenye mwili wako
 2. Tumia vyakula vya mafuta zaidi(healthy fats) : badala ya kula wanga na sukari basi hakikisha unakula zaidi vyakula mafuta mazuri, mfano wa vyakula hivi ni kama parachichi, nazi, nyama , mayai na karanga. Mafuta ya nazi ya nazi yana lauric na Capric acid ambazo ni ni antibacterial yaani zinaua bacteria wabaya.kama una matatizo ini, mfuko wa bandama na figo.
 3. Tumia virutubisho zaidi. Unaweza kutembelea katika stoo yetu kwa kubonyeza hapa
 4. Tumia zaidi limau: limau na maji husaidia kwa kiasi kikubwa katika kuondoa harufu mbaya mdomoni. Unaweza kukata limau kisha ukanyonya maji yake, au ukaminya maji ya limau kwenye glass yenye maji kisha kunywa maji haya na yabaki mdomoni kwa muda wa dakika 10 kisha tema.

Kunywa maji ya kutosha: mdomo unapokuwa mkavu basi huongeza hatari ya kutoa harufu mbaya, kutokana na kwamba ukavu wa mdomo unapelekea kuzaliana kwa bacteria wabaya.

Coconut Oil Pulling

coconut oil pulling

Coconut oil pulling ni mja ya njia murua kabisa ya kusafisha bacteria wabaya mdomoni mwako na kukuacha na harufu nzuri ya kinywa sikuzote. ni njia salama na ya asili isiyohitaji matumizi ya kemikali mbaya wala dawa ambazo zina madhara makubwa.

Nimekuwa nikishauri mamia ya watu na wamefanikiwa kuondoa adha hii ya kunuka mdomo kupitia Coconut oili pulling, wewe pia unaweza kuwa mmoja wa mashuhuda wetu kama tu utazingatia kwa makini step za kufuata.

Uchafu na Vimelea Hutolewa Nje kupitia mafuta

Coconut oil pulling kama jina lake lilivyo ni kitendo cha kuvuta uchafu na bacteria ka vile sabauni inavyonyonya uchafu kwenye nguo wakati wa kufua nguo. Lakini kwenye upande wa kinywa unanyonya bacteria na uchafu kwenye meno kwa kutumia mafuta ya kupikia ya nazi.
Wenzetu wachina na nchi zingine kama India wamekuwa wakitumia njia hii tangu enzi za zamani katika kutibu matatizo kama

Kuoza kwa meno, kuondoa harufu mbaya kwenye kinywa, kuponya fizi zinazotoa damu, kuzuia magonjwa ya moyo, Kupunguza mcharuko mwilini (inflammation), Kusafisha meno kuwa meupe, Kuzuia magonjwa ya fizi, Kutibu lips kavu, Kuimarisha fizi na Kuondoa chunusi

Hatua 5 za Kufanya Coconut Oil Pulling

 1.  Hakikisha unafanya oil pulling asubuhi unapoamka kabla ya kula na kunywa kitu chochote
 2. Chukua kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya kupikia ya nazi kisha weka mdomoni, anza kuzungusha ulimi na kuyasambaza mdomo wote taratibu kwa dakika 10 mpaka 20
 3. Baada ya muda huu tema uchafu wote bila kumeza hata kidogo kisha safisha mdomo na maji, unaweza kutumia maji yenye chumvi ili kuondoa mafuta yote. na hakikish usiteme kwenye sink tema nje ili kuzuia kuziba kwa mafuta kwenye sinki
 4. Brush meno yako kama kawaida
 5. Rudia kitendo hiki mara 3 mpaka 5 kwa week kupata matokeo mazuri zaidi.

Tiba Kupitia mafuta ya Peppermint

Mafuta ya mnanaa ama peppermint yanapatikana kupitia majani ya mmea wa mnanaa (Mentha piperita). Mmea huu hutumika hasa majumbani kama tiba asili ya matatizo ya tumbo.

Mafuta ya peppermint ni tiba asili na salama kwa changamoto ya kunuka mdomo na mezo kuoza. Huhitaji tena kuagiza nje ya nchi, tumekuletea mafuta salama yasiyochakachuliwa. Anza leo kutumia urudishe furaha yako.

Gharama ya Mafuta ya Peppermint ni Tsh 40,000/= Tuandikie kwa whatsapp no 0678626254

Share and Enjoy !

Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shares