Hatua za Kupanga Jinsia ya Mtoto

kupanga jinsia ya mtoto

Kwa miaka mingi watu wamakuwa wakitafuta njia kama inawezekana kupanga jinsia ya mtoto kabla mwanamke hajashika ujauzito. Ni kama ilivo kawaida tu pale mwanamke anapojifungua ndugu na jamaa hutaka kujua kama ni mwanamke au mwanaume.

Najua unajiuliza mnawezaje wewe na mpenzi wako mkawa na mchango katika kuchagua jinsia ya mtoto. Kama hii ni kiu yako ya muda mrefu basi makala hii itaweza kukata kiu yako endelea kusoma

Mbegu za Mwanaume

Kikawaida mwanaume huzalisha aina mbili za mbegu. Mbegu ya kike yani (X) na mbegu ya kiume yani (Y), na mwanamke yeye anakuwa na mayai ya kike tu yani X. Ili mtoto awe wa kiume inabidi mbegu Y ya mwanaume ikutane ya yai lenye X ili kufanya (XY) na ili mtoto wa kike afanyike inabidi mbegu ya kike (X) kutoka kwa Mume ikuta na X ya mke kufanya XX.

Tafiti za kisayansi zinasema kwamba mbegu ya kiume-Y ni ndogo, dhaifu lakini zenye spidi zaidi ya kuogelea kuliko mbegu ya kike X ambayo ni kubwa, yenye nguvu lakini iko taratibu katika kuogelea. Kutokana na sababu hizi kuna vitu wewe na mwenza wako mnaweza kufanya ili kupelekea mtoto wa kiume au wa kike.

1.Kujua vizuri Mzunguko wa Medhi kwa Mwanamke

Ni muhimu mke na mume kujua vizuri mzunguko unachukua siku ngapi, na ni mzunguko mfupi wa sku 28 ama mrefu wa kuanzia siku 31. Fahamu pia ni siku gani yai linatolewa kwenye mfuko wa mayai ama kwa kifupi siku ya hatari.

Utajuaje hii ndio Siku ya Hatari?

Njia ya kwanza ni kuhesabu mpangilio wako wa hedhi kuanzia siku ya kwanza kupata hedhi kwenye mwezi husika. Tumia kalenga kufatilia siku zako. Angalia mzunguko wako kama unachukua siku 28 basi yai hutolewa siku ya 14.

Kumbuka siyo kila mwanamke anapata yai siku ya 14, wengine huwa na mzunguko mrefu zaidi. Kwa mzunguko mrefu angalia dalili zingine za kutolewa kwa yai kama hizi

Mabadiliko ya mwili kwenye siku za hatari

Kubadilika kwa ute: ute huwa mzito na mweupe kama eneo jeupe la yai.
Kupanda kwa joto la mwili (Basal body temperature): Joto la mwili huongezeka taratibu baada ya ovulation. Unaweza kupima mabadiliko ya joto la mwili kwa kutumia kipima joto asubuhi baada tu ya kutoka kitandani.

Ili kujipa uhakika wa siku ya ovulation fatilia mizunguko mingi ya hedhi upate siku sahihi ambayo yai hutolewa. Unaweza kutembelea phamacy kupata vifaa ambavyo hupima mkojo kujua mabadiliko ya homoni.

Siku ya 14 na mtoto wa Kiume

Sasa turudi kwenye mada yetu husika: unapofanya ngono karibu na siku ya yai kutolewa(yani siku ya 14, kuna uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kiume. Hii ni kwasababu mbegu za kiume zina spidi sana ya kuogelea kwahivo zinawahi kufika kwenye yai la kike na kulirutubisha.

Kama utashiriki mapenzi siku 3 au zaidi kabla ya yai kutolewa ama ukashiriki tendo siku ile ile ya 14, chansi ya kupata mtoto wa kike ni kubwa kwa sababu mbegu za Y ni dhaifu na zinakufa mapema. Kumbuka mbegu kutoka kwa mwanaume huweza kukaa kwenye tumbo la uzazi kwa siku mpaka 5 zikisubiri yai litolewe ili lirutubishwe.

2.Mazingira ya ndani ya Uke

Mazingira ya ndani ya uke huchangia zaidi katika jinsia ya mtoto. Kama mazingira yana utindikali kwa wingi, chansi ya kupata mtoto wa kike ni kubwa kwani hali hii ya utundikali inaua mbegu dhaifu za kiume na kuziacha mbegu za kike (X).

Kwa upande mwingine kama uke una alkali kwa wingi basi chansi ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa. Kwahivo kwa kesi hii ili kutengeneza mazingira ya alakali osha uke mpaka ndani kwa maji yenye baking soda kabla ya tendo la ndoa ili kupata mtoto wa kiume. Kwa upande wa pili osha uke kwa maji yenye vinegar ya apple ili kushika mimba ya mtoto wa kike.

3.Staili ya Kufanya Mapenzi

Aina ya mkao wakati mnafanya ngono pamoja na kiasi gani uume umepenya kwenye uke vinachangia katika kuchagua jinsia ya mtoto. Hapa ifaamike kwamba eneo la mwanzo la uke linakuwa na utindikali kwa mwingi ukilinganisha na eneo la ndani la uke ambalo lina alkali kwa wingi.

Uume unaopenya zaidi unazipa mbegu za kiume muda mfupi wa kuogelea kuelekea kwenye yai na kulirutubisha. Wakati upande mwingine mbegu zinapotua eneo la mwanzo la uke ambapo pana utidikali kwa wingi inazipa mbegu za kike mazingira mazuri kwani zina nguvu ya kuongelea kwa muda mrefu na katika mazingira ya tindikali.
Tunashauri staili ya mbuzi kagoma (chuma mboga) ili kupata mtoto wa kiume na staili ya kifo cha mende kwa mtoto wa kike.

4.Mwanamke kufika kileleni

Kufika kileleni kwa mwanamke kunaathiri utindikali kwenye uke. Mwanamke anapofika kileleni mwili hutoa kemikali ambazo hupunguza utindikali ukeni na kuongeza alkali kwahivo kuongeza chansi ya kupata mtoto wa kiume. Kwa upande mwingine ili kupata mtoto wa kike basi mwanamke asifike kileleni.

5.Wingi wa Mbegu za Kiume

Wingi wa mbegu ni muhimu katika akupata mtoto wa jinsia yoyote. Mbegu kidogo hupelekea mwanamke asishike kabisa mimba. Mwanaume anapokuwa na mbegu nyingi zaidi, chansi ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa. Kama mwanaume ana changamoto ya mbegu muhimu atumie kwanza virutubishi hivi hapa.

Ushauri zaidi ili kuchagua jinsia ya mtoto

  • Unapojaribu kutafuna mvulana usifanye ngono kwa siku 3 mpaka 4 kabla ya siku ya hatari(ovolation day). Kupata msichana fanya ngono kila siku kwa siku 3 na pumzika kufanya ngono siku tatu kabla ya siku ya hatari.
  • Kwa mwanaume avae nguo pana za ndani zisizo za kubana kwa muda wa week moja kabla ya siku ya 14 ambapo atakukutana mwenza wake. Kuvaa nguo pana husaidia mbegu za kiume (Y) kustahimili na kuwa nyingi.
  • Ili kupata msichana mwanaume anashauriwa kuoga maji ya vuguvugu kabla ya kushiriki tendo la ndoa hii ni kupunguza mazingira mazuri kwa mbegu za kiume na hivo kutoa mazingira mazuri kwa mbegu za kike.

Mwisho kabisa

Nashauri kama unajaribu kupata mtoto mvulana, mwanaume atumie kikombe cha kahawa nusu saa kabla ya kufanya ngono.

Kumbuka kama utafatilia vizuri sheria na maelekezo kwenye makala yangu, uhakika wa kupata jinsia ya mtoto unayotaka ni asilimia 70 mpaka 75. Tunashauri pia kufatilia mpangilio wa hedhi kwa ukaribu zaidi kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne ili kufanya timing vizuri.

Njia salama za kusafisha kizazi ili kushika mimba haraka

Share and Enjoy !

Shares
Shares