MIMEA YA SPIRULINA

spirulina

Yawezekana kwa wengi ikawa ni mara yako ya kwanza kusikia kuusu mimea hii adimu ya spirulina. Mmea ambayo inapatikana nchi chache sana hapa Africa ikiwemo Chad. Mimea hii pia inalimwa sana huko Asia nchi kama China, Thailand na Maekani ndo zinaongoza kulima na kusambaza mimea hii.

Basi fuatana nami uweze kupata maarifa haya ambayo yanweza kukusaidia kuimarisha Afya yako na kuzuia kuugua magonjwa ya utandawazi hku ukiwa na Kinga nzuri ya mwili na mwenye nguvu.

HISTORIA YA MMEA WA SPIRULINA

Spirulina ni mimea jamii ya Algae ya blue, jina lake limetokana na lugha ya kilatini “helix” Hii ni kutokana na shape yake kama spiringi ambayo hupatikana katika bahari na baadhi ya maziwa yasiyo ya chumvi (Alkaline lakes)  katika baadhi ya nchi za Africa, Mexico, na America ya kusini.  Rekodi za kihstoria zinaonesha kwamba mimea hii ilivunwa na kuuzwa kama keki.

Mimea hii huota kama kamba ambazo huwa ni fupi kiasi cha milimita moja. hapo zamani watu wa kale walipenda kutumia mimea hii kama chakula kwa kuikausha na kutengeneza keki. Katika karne ya 20 mimea hii ya Spirulina plantensis ilianza kupata umaarufu mkubwa baada ya

Wataalamu kufanya utafiti na kugundua kuwa mmea huu una viini lishe vingi sana vinavyoweza kuimarisha Afya ya mwili kwa kuongeza vitamins, nguvu mwilini, na madini ya chuma. Katika miaka ya 1970,s ndipo makamuni makubwa kutoka ufaransa yalianza uzalishaji wa kiwango kikubwa wa mimea ya Spiriluna Platensis.

Baada ya miaka michache Nchi zingine kama Japan na Marekani zikaanza uzalishaji pia kwa kiasi kikubwa. Mimea hii kiasili huweza kulimwa na kuvunwa bila kutumia viiua vijidudu hii inaifanya kuhifadhi ubora wake.

Leo mimea hii yenye viini lishe vingi inatumika dunia nzima katika kusaidia kutibu matatzo mbalimbali ya kiafya na pia ni mimea ambayo inazungumzwa kuwa ndio inaweza kumaliza tatizo sugu la njaa linalozikumba baadhi ya nchi hapa Duniani.

Kwanini tunasema Spirulina inaweza kumaliza tatizo sugu la njaa??

Kama nilivyokwambia mpenzi msomaji wa makala hii kwamba mimea hii ina lishe zote muhimu ambazo zinatakiwa na mwili, na mwili unahitaji mlo kamili ili afya iwe bora. Hvo ni lazima mwili upate wanga, mafuta,vitamin na protini kwa kiwango cha kawaida na mimea ya spiriluna ina uwezo wa kutoa lishe zote hapo.

NINI BASI KINAFANYA MIMEA HII YA SPIRILUNA KUJULIKANA KWAMBA NI NUTRITIONAL SUPERSTAR(SUPASTAA WA VIINI LISHE) AMA KINARA WA VIINI LISHE

Moja ya sifa kubwa ya mimea ya spiriluna ni ule wingi wake wa protini, zaidi ya asilimia 70 mpaka 80 ya uzito wa mmea huu umetengenezwa   kwa protini, hvo utagundua mpenzi msomaji kwa jinsi gani mimea hii ina kiwango cha juu sana cha protini ukilinganisha na nyama ambayo inabeba asilimia 27 tu ya protini ndio maaana hutumika katika kuepusha utapiamlo kwa watu wa rika zote. Pia mimea hii ina vitamin muhimu katika afya ya mwili kama vitamin B na vitamin K, madini muhimu kama calcium kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno, madini ya chuma, magnesium ambayo husaidia ufanyaji kazi wa vimengenya chakula (enzymes), manganese potasiumu na zinc pia.

  • Protini iliyopo ndani ya spiriluna ni rahisi zaidi kuweza kuvunjwavunjwa, hvo kuongeza kiasi cha protini ambacho kitatumika na mwili/net protein utilization (NPU).
  • Spirulina ina idadi kubwa ya madini ya calcium, phosphorus na magnesium sawa na kiasi cha madini haya yaliyopo kwenye maziwa, hivo utaona kwamba badala ya kunywa maziwa ulipata kirutubisho cha spiriluna basi unakuwa umefidia kiasi kikubwa cha madini.
  1. HUONGEZA KINGA YA MWILI,KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA MAAMBUKZI, NA PIA KUPIGANA NA MAGONJWA SUGU

Tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonesha kwamba mimea ya spiriluna ina uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili, hvo krutubisho chake kinawafaa sana kundi la watu wenye kinga ndogo ya mwili mfano, wenye magonjwa ya fangasi, ukimwi, wanaougua mara kwa mara, wenye matatzo ya pumu, na pia wazee walioenda umri.

  1. KUBALANSI SHINIKIZO LA DAMU( BALANCE BLOOD PRESSURE)

Shinikizo kubwa la damu (hypertention) ni tatzo sugu na hatari kwa sasa kwani linasababisha vifo vingi kwa sasa. Hivo wenye shinikizo la damu wapo katika hatari ya kupoteza maisha ghafla kutokana na shambulizi la moyo (heart attack), au stroke. Habari nzuri ni kwamba endapo ukifata matumizi mazuri ya lishe na ukawa na nidhamu ya matumizi ya vyakula bora, kupata mazoezi ya mwili, na kuchagua mwenendo mzuri wa maisha usio na msongo wa mawazo na ukapata kirutubisho cha spiriluna basi itasaidia kuweka shinikizo lako la damu katika hali ya kawaida.

  1. SPIRILUNA KATIKA KUPUNGUZA MAFUTA MABAYA MWILINI

Je wewe ni mmoja wa wahanga katika kupunguza uzito??, umehudhuria gimme lakini bado uzito ni mkubwa, umemeza vidonge mbalimbali mpaka umekata tama lakini bado uzito unakusumbua, basi napenda kukwambia kuwa suluhisho lipo jikoni na  katika matumizi ya vitu asili ikiwemo unga ama kiruubisho cha spiriluna .na cyo dawa za kiphamasia ambazo zinaleta madhara makubwa sana ndani ya mwili ikiwemo, kupungua kwa uwezo kwenye  tendo la ndoa, upungufu wa damu mwilini,kupungua kwa kinga ya mwilini, matatizo ya ini na kongosho kutoakana na kwamba dawa hizi huambatana na sumu nyingi sana, pia dawa hizi za kiphamasia za kuounguza uzito zinaongeza hatari ya kuugua saratani . mpenzi msomaji wa makala hii unapotaka kupungua uzitoni lazima ujue chanzo cha tatizo ni nini, vinginevyo utakua unatwanga maji kwenye kinu. Kupunuza matumizi ya wanga na sukari ndio msingi wa kupungua uzito kiasili kabisa, lakini mmea wa spiriluna pia utakusaidia kwa kiasi kikubwa hivi jaribu kuagiza dawa hii nje ya nchi uone maajabu yake.

  1. SPIRILUNA INAVYOPUNGUZA HATARI YA KUUGUA SARATANI AMA KANSA

Mbali na ugonjwa wa kisukari saratani ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo vingi vya watu chini ya umri wa miaka 70, katika nchi yetu, na matibabu yake yanagharimu mpaka mamilioni ya pesa, utagundua ni jinsi gani gharam za kujikinga ni ndogo sana ukilinganisha na gharama za kutibu tatizo hili, USHAURI wangu wa kwanza katika kupunguza hatari ya kuugua saratani ni kujiepusha na matumizi ya sukari wala vinywaji vilivyosindikwa vyenye sukari, punguza vyakula vya wanga. Vionjo kama fructose vinavyowekwa kwenye soda na juisi zilizosindikwa ni mbolea nzuri kwa ajili ya ukuaji wa seli za kansa, pia napendekeza wlau kila siku upate joto la jua ili uapate vitamin D ambayo inasaidia kupunguza hatari ya kuugua saratani kwa zaidi ya nusu. Madini ya selenium yaliyopo kwenye spiriluna husaidia pia kuzuia ukuaji wa seli za kansa.

UTAFITI ULIOFANYIKA JUU YA FAIDA ZA MMEA WA SPIRILUNA

Sasa mpenzi msomaji baada kuona historian apicha ya jumla yam mea wa spiriluna, napenda tuangalie upande mwingine wa mmea huu wa spiriluna jinsi ambavyo unaweza kufanya mapinduzi makubwa katika afya yako. Tafiti nyingi sana zimeshawahi kufanywa juu ya faida za mmea huu kiasi kwamba ni ngumu kuziandika zote, lakini nimechukua zile muhimu ili nawe msomaji upate mwanga ili unapougua basi usikimbilie kumeza vidonge vyeney kemikali badala yake tumia njia za asili.

  1. SPIRILUNA NA UFANYAJI KAZI WA MACHO

Kadiri umri unavoenda basi uwezo wa kuona hupungua taratibu, kwenye macho kuna pigmenti ndogo ambazo huitwa carotenoid ambazo kazi yake ni kulinda macho kuathirika kutokana na mionzi mibaya ya jua pia kusaidia kuepusha ukungu kwenye macho, kiasi kidogo cha spiriluna gramu 3 kina pigmenti 3750 mpaka 6000 za carotenoid hivo utaona ni kwa kiasi gani mmea huu una maajabu makubwa kutokana na virutubsho vingi vilivyomo ndani yake.

  1. SPIRILUNA NA SUKARI AINA YA PILI(TYPE 2 DIABETES)

Kisukari ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vingi kwa sasa hapa nchini kwetu, kwa utafiti niliofanya kutoka kwa wagonjwa ambao nimewahi kuwahudumia spiriluna imeonesha mafanikio makubwa katika kutibu tatizo la kisukari,endapo ikiambatanishwa na virutubisho vingine kama basalm na zinc.

  1. SPIRILUNA NA AFYA YA MOYO NA MIRIJA YA DAMU.

Ugonjwa wa kisukari pamoja na matatzo ya moyo ni vitu vinavyofuatana, hapa naomba uelewe kuwa endapo ukiwa na kisukari basi upo kwenye hatari kubwa ya kuugua magonjwa ya moyo pia. Hivo isikushangaze kuwa Spiriluna inaonesha uwezo mkubwa kwa wagonjwa wenye matatzo ya moyo, ikiwemo shinikizo kubwa la damu na mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu kwa kurekebisha utanukaji wa mishipa ya damu

  1. SPIRILUNA NA INI

Mkusanyiko wa mafuta mabaya kwenye ini inahusishwa na matatzo ya kiafya yanayoweza kukupelekeza kuongezeka kwa hatari ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo. Nimekuwa nikihudumia wagonjwa wenye matatzo ya ini na wameleta matokeo mazuri sana baada ya kutumia kirutubisho huki cha spiriluna, kutokana na sifa yake kama kiondoa sumu hvo (antioxidant)  kusaidia uondoaji wa taka kama nitric oxide ambazo huzalishwa kwenye ini. . Zaidi ya hapo spiriluna inasaidia kupunguza maambukizi kwenye ini, na kulinda ini dhidi ya metali nzito kama lead na mercury.

  1. SPIRILUNA NA AFYA YA UBONGO

Mwisho kabisa tuangalie faida za mmea wa spiriluna na afya ya ubongo. Kwa sasa tatzo ambao linafata kwa kusababisha vifo vingi ni tatzo la stroke. Vyakula ambavyo vina sifa ya kuwa viondoa sumu kama kabeji, vitunguu saumu, na Spiriluna hupunguza kwa kiasi kikubwa cha kupata stroke.

HITIMISHO

Kama tulivyoona utafiti wa kisayansi umeinesha matokeo mazuri ya spiriluna kwenye afya yako. Jaribu kuagiza nje ya nchi uweze kujionea maajabu yam mea huu, ili upunguze gharama za kuja kutibu magonjwa yakishatokea ambapo itakugharimu mamilioni ya pesa. Kumbuka kinga ni rahisi kuliko tiba.unaweza kufika pia ofsini kwetu hapa Mwembechai dar ukapata virutubisho hivi kwa gharama nafuu ya 75,000/=

Kwa maoni naushauri usisite kutuandikia kwenye namba zetu. Whatsapp 0678626254. Usisite kushare na wenzako makala hii wajifunze zaidi.. health is wealth

Share and Enjoy !

Shares
Shares