Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni 300 wanaishi na ugonjwa wa homa ya ini duniani kote. Mwaka 2015 pekee zaidi ya watu 887,000 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa zinaweza zisijioneshe mapema pale mtu anapopata maambukizi. Lakini ni moja ya magonjwa hatari sana unaoweza kuleta makovu na hata kusababisha saratani kwenye ini. Homa ya ini ni hatari zaidi kuliko ukimwi kwani huathiri ini kwa haraka zaidi.
Aina za Homa ya ini
Kuna aina nyingi za homa ya ini(hepatitis) lakini ambazo ni kubwa ni hepatitis A,B na C. Katika makala yetu tutajikita zaidi kuangalia hepatitis B kwani inaathiri watu wengi zaidi ukilinganisha na aina zingine. Mpaka sasa bado hakuna dawa kabisa ya Hepatitis B, lakini kuna virutubisho ambavyo vitakusaidia kuimarisha kinga yako na kutibu dalili za aina hii ya ugonjwa.
Nini Maana Ya Hepatitis B.
Homa ya ini (hepatitis B) ni ugonjwa wa virusi unaotishia uhai wa mtu kwa kuathiri ini lake. Ugonjwa unaweza kuleta athari ya muda mfupi kwenye ini (acute) au ikasababisha athari za muda mrefu(chronic) na hata kifo. Jambo la hatari ni kwamba madhara ya muda mfupi yanaweza kusababisha madhara ya muda mrefu na saratani ya ini.
Dalili za Homa Ya ini (hepatitis B)
Kundi kubwa la watu wenye athari za muda mfupi (acute hepatitis B) huwa hawaoni dalili za kuwepo kwa maambukizi. Dalili huanza kujionesha miezi miwili mpaka mitano. Dalili kuu za homa ya ini ni kama zifuatazo
- kupata homa kali
- kizunguzungu na kichefuchefu
- kutapika
- mwili kuchoka sana
- maumivu ya tumbo hasa upande wa juu kulia
- kukosa hamu ya kula
- maumivu ya joints
- kupata mkojo wenye weusi
- maumivu ya misuli
- ngozi na macho kuwa ya njano(jaundice)
Dalili huchukua muda gani Kuisha
Kwa watu wengi dalili za homa ya ini hupotea baada ya wiki kadhaa. Wagonjwa wenye athari za muda mrefu huchukua mpaka miezi 6 kumalizika.
Watu wenye mambukizi sugu/chronic huwa ni ngumu kutibu virusi wote wakaisha mwilini. Watu hawa huendelea kujisikia dalili kwa muda mrefu. Uwezekano wa ugonjwa kuwa sugu unategemea na umri wa mgonjwa , mfano watoto wanaopata maambukizi katika umri wa chini ya miaka 6 wana uwezekano mkubwa kwa tatizo lao kuwa sugu na la muda mrefu.
Mazingira Hatarishi Na Visababishi Vya Homa Ya Ini(Hepatitis B)
Homa ya ini (hepatitis B) inasababishwa na virusi. Virusi hawa wanaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu kwa siku 7 bila kufa. Ndani ya muda huu sasa hawa virusi wanaweza kumuathiri mtu yeyote endapo tu vitamuingia kwenye mwili wake.
Kikawaida baada ya virusi kumwingia mtu vinaweza kugundulika ndani ya siku 30 mpaka 60 baada ya kuambukizwa. Ugonjwa unaweza kusambazwa kwa njia zifuatazo
- Mama kwa mtoto: ni njia kubwa zaidi ambapo mama mwenye ugonjwa anaweza kumwambukiza mwanae wakati wa kujifungua.
- Kugusa damu iliyoathirika: hii yaweza kufanyika kwa matumizi ya vitu vyenye ncha kali kama viwembe na sindano na miswaki, kama damu yenye virusi ikagusana na jerha la mtu mzima basi anaweza kupata maambukizi kiurahisi.
- Maambikizi kupitia ngono: virusi wa homa ya ini wanaweza kusambazwa pale majimaji ya ukeni au mbegu za mtu aliyeathirika zinapomuingia mtu mzima. Watu wenye wapenzi wengi ama michepuko wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua ugonjwa huu kupitia njia ya ngono
- Kuchangia sindano: matumizi ya sindano kwa mtu zaidi ya mmoja husambazwa ugonjwa wa hoama ya ini kutoka kwa mgonjwa mpaka kwa mtu mzima, hii yaweza kutokea kwenye vituo vya afya, au kwa walevi wa madawa ya kujidunga. Ugonjwa unaweza kusambazwa pia kwa kutumia vifaa vya kuchora Ngozi(tatooing) na kwenye upasuaji hospitali.
Kumbuka kila mtu anaweza kupata homa ya ini, lakini makundi yafuatayo wapo kwenye hatari zaidi ukilinganisha na wengine. Makundi haya yanajumuisha
- Wenye wapenzi wengi/michepuko
- Wanaojidunga madawa ya kulevya na kuchangia sindano
- Kuishi ama kushirikiana kwa ukaribu na mtu mwenye homa ya ini
- Waliotumia muda mrefu gerezani na sehemu zenye mikusanyiko mikubwa
- Watumishi wa afya wanaofanya kazi mazingira yenye wagonjwa wa homa ya ini
- Wanaosafiri kwenye nchi zenye waathirika wengi zaidi wa homa ya ini
Tiba ya Hospitali kwa Homa ya ini
Kama tulivosoma dalili za homa ya ini zinafanana na dalili za magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi. Kwahiyo uchunguzi wake hufanyika kwa kuchukua sampuli ya damu na kuipeleka maabara.
Mpaka sasa bado hakuna dawa ya kutibu kabisa homa ya ini. Lakini kwa watu wenye ugonjwa sugu basi hupewa dawa za kupambana na virusi ili kupunguza makali ya ugonjwa na hivo kupunguza athari kwenye ini.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO), chanjo inaweza kutumika kuzuia maambukizi ya mwanzo ya hepatitis B. Kinga inaweza kufanya kazi kwa miaka 20 na zaidi.
Hatua Tano Za Kutibu Na Kupambana Na Dalili Za Homa Ya Ini
Kula mlo kamili na wenye afya na virutubisho kwa afya ya ini
Hii ni silaha kubwa katika kupambana na dalili za homa ya ini. Ulaji wa vyakula vyenye chrolophyl kwa wingi husaidia kupunguza utengenezwaji wa radikali huru ambazo ni sumu mwilini na hivo kupunguza athari kwenye ini. Baadhi ya vyakula vya kusafisha ini lako ni pamoja na
- mboga za kijani kama spinach na lettuce,
- matunda kama zabibu na machungwa
- mboga kwenye kundi la cruciferous kama broccoli, cabbage na cauliflower,
- mboga za mizizi kama karoti, beets na karanga
- mimea tiba kama tangawizi
- nyama kutoka kwa wanyama waliolishwa majani na maini ya kuku na
- mafuta yasiyosindikwa kama mafuta ya nazi na mafuta ya mizeituni
Epuka vyakula na vinywaji vinavyoongeza mcharuko wa mwili(inflammation)
Kuepuka vyakula na vinywaji hivi itasaidia kuzuia kusambaa haraka kwa virusi wa hepatitis. Vyakula hivi inajumuisha sukari, mafuta yaliyosindikwa na kusafishwa kiwandani, nafaka iliyokobolewa, maziwa yaliyosindikwa kiwandani na kuongezwa ladha na kemikali. Epuka pia matumizi ya pombe maana huongeza athari ya ugonjwa.
Muda wote hakikisha unakunywa maji ya kutosha
Kutokana na kwamba moja ya dalili ya homa ya ini ni kutapika ambako hupelekea kupoteza maji mengi, basi tunashauri kunywa maji ya kutosha ili kufidia maji yanayopotea. Unaweza kutumia juisi ya matunda halisi, maziwa halisi ya nazi na juisi ya mboga badala ya kunywa soda na juisi zilizojazwa sukari na kemikali.
Punguza msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo hudhoofisha kinga ya mwili na kupelekea kusambaa sana kwa ugonjwa wa homa ya ini. Ruhusu mwili wako kupumzika usifanye kazi ngumu sana hasa ukiwa umechoka na huna nguvu za kutosha. Jaribu baadhi ya njia asili za kupunguza msongo wa mawazo kama kutembea nje umbali kiasi, tumia pia mafuta ya lavender kwa kupuliza katika eneo la kazi au nyumbani.
- Kutoa sumu mwilini
- Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya mishipa midogo ya ini na kuimaarisha utendaji wa ini
- Kuimarisha kinga na kudumaza virusi vya homa ya ini
- Kupunguza kasi ya kuharibika kwa ini (liver cirrhosis) kunakochangiwa na ini kuwa na mafuta, hepatitis na utumiaji wa pombe
- Kuzuia uharibifu wa ini kutokana na kemikali, metali nzito, madawa, sumu ndani ya chakula na uchafu mwingine.