Chanzo Cha mimba Kuharibika

Mimba kuharibika mara kwa mara
mjamzito

Mimba kuharibika au miscarriage ni kitendo cha kupoteza kichanga kwa mama mjamzito kabla ya muda wa kujifungua kuwadia. Mara nyingi hutokea ndani ya miezi mitatu ya mwanzo baada ya kushika ujauzito. sababu za  mimba kutoka zinatofautiana kwa kila mwanamke. Zifuatazo ni dalili kwamba mimba yako imeharibika

Dalili za Mimba Kuharibika.

Kwa kutegemea na hatua ya ujauzito wako, dalili hutofautiana . Wakati mwingine hujitokeza haraka pengine kabla hujajua kama una ujauzito tayari mimba inakuwa imeharibika. Dalili hizi ni pamoja na

 • maumivu ya mgongo
 • kuvuja damu ukeni
 • kutoka kwa tishu za mabongemabonge katika uke
 • misuli kukaza na
 • maumivu makali ya tumbo

Hakikisha unaongea na daktari haraka iwezekanavyo unapoanza kuona dalili kama hizi. Kumbuka inawezekana kabisa kupata dalili hizi lakini mimba yako ikawa salama. Lakini ni muhimu kwa dactari kujiridhisha kama uko salama.

Namna 5 za Mimba Kuharibika na Kutoka.

Kuna aina namna nyingi za mimba kuharibika. Kwa Kutegemeana na sababu ya mimba yako kutoka mapema pamoja na hatua ya ukuaji wa mimba aina hizi zinaweza kuainishwa kama ifuatavyo

 • Blighted ovum: ni pale yai lililorutubishwa linajipandikiza kwenye ukuta wa uterus lakini mimba haikui na kupelekea kuharibika.
 • Complete miscarriage: ni pale kiumbe kilichotungwa kinatolewa nje ya mfuko wa mimba. Inaweza kusababisha damu kuvuja
 • Missed miscarriage: Ni pale kiumbe kidogo kufariki tumboni pasipo kupata viashiria vyovyote
 • Reccurent miscarriage: ni pale mimba zako zinapotoka mfululizo mara 3 au zaidi ndani ya miei mitatu ya kwanza
 • Ectopic miscarriage: Mimba kujishikiza mahali pengine hasa kwenye mirija ya uzazi badala ya mji wa mimba na kupelekea kutoka kwa mimba
 • Threatened miscarriage: Ni pale mjamzito anaanza kupata dalili za kutokwa na damu ukeni na maumivu yanayoashiria kuharibika kwa mimba.

Nini hasa Kinasababisha Mimba Kuharibika Na Kutoka Kabla ya Wakati?

Wakati wa ujauzito mwili hupeleka virutubisho na homoni kwenye kiumbe kinachokua. Hivi vyote husaidia kiumbe kuwa na afya njema na kukua vizuri. Mimba nyingi zinazoharibika ndani ya miezi mitatu ya kwanza ni kutokana na kiumbe kudumaa. Kuna sababu nyingi zinapelekea Mimba kuharibika mapema kama ifuatavyo.

Vinasaba

Karibu 50% ya mimba zinazotoka kabla ya wakati ni kutokana na makosa kwenye vinasaba. Makosa yanaweza kufanyika pale seli za kiumbe zinapogawanyika. au inaweza kutokana na majeraha kwenye mbegu ya kiume au yai la mwanamke.

Matatizo ya Kiafya

Matatizo ya kiafya pamoja na mtindo wa maisha unaweza kuletekeza mimba kutoka, hasa kwenye kipindi cha miezi mitatu ya pili (second trimester). Kumbuka mazoezi ya mwili na kushiriki ngono haiwezi kusababisha mimba kutoka. Mazingira yafuatayo yanaweza kuhataraisha mimba yako

 • lishe mbaya inayokosa virutubisho  vingi
 • matumizi ya pombe, madawa na sigara
 • matatizo kwenye tezi ya thairodi ambayo hayajatibiwa
 • maambukizi kwenye njia ya uzazi
 • msongo wa mawazo
 • uzito mkubwa na kitambi
 • matatizo kwenye mlango wa kizazi (cervical incompetence)
 • kulegea kwa mfuko wa mimba
 • shinikizo la damu kuwa juu zaidi
 • kutumia chakula chenye sumu na
 • matumizi ya dawa pasipo ushauri wa Dactari

Jinsi ya Kuzuia Mimba Kuharibika

Kwa kiasi kikubwa mimba kuharibika inaweza kuepushwa japo siyo kila mazingira mfano kama tatizo limetokana na vinasaba. Zifuatazo ni sheria za kiafya za kuzuingatia ili kupunguza hatari ya mimba kutoka.

 • Usitumie pombe, madawa, na kuvuta sigara wakati wa ujauzito
 • Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha ukuaji wa kichanga tumboni
 • Jikinge na maambukizi kwenye njia ya uzazi kwa kunawa mikono kwa maji safi na kutoambatana na watu wanaoumwa
 • Usitumie vyakula na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa wakati wa ujauzito
 • Kula mlo mzuri wa vitamin ili kuimarisha ukuaji wa kichanga

Nini cha kufanya pale Ujauzito Unapoharibika na Kutoka.

Baaada ya mimba kutoka mwili huanza kurudi katika hali ya kawaida taratibu taratibu. Kuimarika haraka kwa mwili kunategemea mimba yako ilikuwa na umri gani kabla haijatoka. Baada ya mimba kutoka unaweza kupata dalili hizi

Mwili utaanza kupata tena hedhi baada ya week 3 mpaka 6 baada ya mimba kutoka. Ni vizuri kujipa mda wa kupumzisha mwili na ukapata usaidizi wa kifikra na hisia ili kuondokana na msongo wa mawazo.

Kushika Mimba tena Baada ya Mimba ya Awali Kuharibika.

Kabla hujaamua kushika ujauzito mwingine ni vizuri kuhakikisha mwili uko sawa na afya yako ni njema. Ukiwa na afya njema inapukupunguzia hatari ya mimba nyingine kuharibika.

Daktari inabidi akufanyie vipimo kadhaa ili kujua chanzo cha tatizo lako; Vipimo hivi vinajumuisha

 • Vipimo vya damu kuangalia kama una mvurugiko wa homoni
 • Kupima vinasaba
 • Kipimo cha mkojo na nyonga na
 • Kipimo cha utrasound

Unashauriwa kujipa mda wa kupumzika walau miezi 8 mpaka mwaka mmoja kabla hujaamua kushika ujauzito tena.

Kama umependa makala yetu hii basi usisite kutuandikia maoni yako.

Muhimu kwa Wanawake wenye Changamoto ya Mimba Kuharibika Mara kwa Mara

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya mimba kuharibika mara kwa mara kutokana na maambukizi ya fangasi, PID au UTI sugu na hedhi kuvurugika. Tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na kutibu maambukizi. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake.

uterus cleansing pills

Vidonge hivi vinatumika kwa wiki moja. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24,unaweka tena kidonge kingine.

Gharama ni Tsh 50,000/= kwa dozi ya week moja. Endapo mimba imeharibika ni kubwa, au ni mara ya pili mimba kuharbika tunashauri upate dozi kubwa ya Tsh 100,000/=

Angalizo Unapotumia UCP (uterus cleansing Pill)

UCP haifai kutumiwa na wajawazito na wanwake bikira. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi na pia ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata Huduma

Makala inayofuata: Madhara makubwa ya kutoa mimba(abortion)

Share and Enjoy !

Shares
Shares