Faida 7 za Mafuta ya Lavender (Mrujuani)

lavender
mafuta ya lavender

Mafuta ya lavender au mrujuani ni moja ya mafuta yanayotumika zaidi kwenye kundi la (essential oil) lakini faida zake ziligunduliwa kwa zaidi ya miaka 2500 iliyopita. Kutokana na uwezo mkubwa kama kiondoa sumu na kupambana na bakteria mafuta haya ya lavenda yamewea kutumika kwa afya ya ngozi na pia kama tiba kwa karne nyingi sasa.

Hapo zamani wamisri walitumia mafuta ya lavender kama pafyum na pia kuhifadhia maiti zisiharibike (mummification), ambapo inasemekana kwamba harufu ya mafuta ya lavender iligundulika kuendelea kuwepo kwenye kaburi la farao kwa zaidi ya miaka elfu 3 tangu kufariki kwake.
Kwa upande mwingine warumi walitumia mafuta ya lavenda kwa ajili ya marashi ya kuogea, kupikia na kusafisha hewa. Kwenye biblia pia mafuta ya lavender inafahamika kwamba yalitumika kwenye kutibu na kutakasa. Kwa siku za hivi karibuni mafuta ya lavender yamekuwa yakitumika kwenye njia hizi

  • Kupunguza msongo wa mawazo (pasipo kumeza vidonge)
  • Kulinda mwili dhidi dalili mbaya za kisukari
  • Kuimarisha uwezo wa ubongo
  • Kuimarisha usingizi
  • Kurudisha ngozi nyororo na kuondoa chunusi
  • Kupunguza kasi ya uzee na
  • Kupunguza maumivu

Kutokana na faida nyingi zilizopo kwenye mafuta ya lavender, nashauri ununue uwe nayo nyumbani muda wote. Utafiti tayari umeshagundua uzuri wa mmea huu wa lavender.

Zifatazo ni Faida 7 za Kutumia Mafuta ya Lavender (mrujuani)

1.Kutibu Majeraha ya Moto na ya Kukatwa

Kutokana na uwezo wake wa kudhibiti ukuaji wa bakteria, mafuta la lavender yamekuwa yakitumika kuzuia maambuzi ya vimelea n magonjwa mbalimbali. Tafiti zinaonesha kwamba majeraha ya moto na kukatwa na kitu chenye ncha kali hupona haraka zaidi endapo utapaka mafuta ya lavenda.
Matumizi: kwa jeraha la kukatwa ama kuungua na moto changanya matone matano ya mafuta ya lavender na nusu kijiko cha mafuta ya nazi na upake kwenye eneo lililoathirika, unaweza kutumia pamba ama kidole kupakaa.

2.Kuimarisha Afya ya Ngozi na Ukuaji wa Nywele.

Matumizi ya mafuta ya lavenda kwa kupakaa kwenye ngozi huzuia chunusi na matatizo mengine ya ngozi kama madoa,michirizi na pia kupunguza kasi ya kuzeeka kwa ngozi.

Matumizi: kwa matumizi ya mafuta ya lavenda kwa afya ya ngozi, changanya matone kiasi pamoja na nusu kijiko cha mafuta ya nazi au jojoba na ufanye masaji kwa eneo husika la ngozi. Unaweza pia kupakaa mafuta ya lavender kwenye ngozi ya uso. Na kama ukikosa mafuta mengine basi tumia mafuta ya lavender pekee.

Tafiti pia zinaonesha kwamba mafuta ya lavender yakitumika pamoja na mafuta mengine kama rosemary yanapunguza tatizo la kunyonyoka kwa nywele(alopecia areata) kama yakipakaliwa kwenye ngozi ya kichwa kila siku.

3.Kupunguza Maumivu ya Kichwa

Kama wewe ni mmoja ya mamilioni ya watu wanaoteseka na maumivu ya kichwa kila siku, mafuta ya lavender yanaweza kuwa mwarobaini wako. Ni moja ya mafuta mazuri kutibu maumivu ya kichwa.
Matumizi; Changanya matone kidogo ya mafuta ya lavender pamoja na mafuta ya peppermint kisha sugua eneo ya nyuma ya shingo na eneo la juu ya masikio. Chukua pia mafuta kiasi vuta hewa yake.

4.Mafuta ya lavender yanaimarisha Usingizi mnono

Mafuta ya lavender ukilinganisha na dawa za kuleta usingizi haina madhara ya kiafya. itaimarisha utimamu wa mwili kwa ujumla.
Matumizi: Kutibu tatizo la kukosa usingizi na kuimarisha usingizi wako, chukua matone kidogo ya mafuta la lavenda pakaa kwenye mto wa kulalia, kwenye mashuka kabla ya kulala.
pia unaweza kumasaji eneo la nyuma ya shingo, kwenye kifua na eneo la juu la masikio.

5.Kutibu dalili mbaya za kisukari

Mwaka 2014 watafiti nchini tunisia waligundua kwamba mafuta ya lavender yanawaweza kupunguza dalili zifuatazo za mgonjwa wa kisukari
Kupanda kwa sukari kwenye damu
Kuongezeka kwa uzito
Kupungua kwa uwezo wa figo na ini
kwa wagonjwa wa kisukari pakaa mafuta ya lavender kwenye shingo na kwenye kifua. Pia vuta hewa yake .

6.Kupunguza maumivu ya mwili

Tafiti mbalimbali zimegundua kwamba mafuta ya lavender husadia kutibu maumivu ya mwili kama ikitumia ipasavyo. Tunaweza kuiita hii ni natural painkiller. Chukua mafuta yako kisha tumia kitambaa laini au pamba kusugua mahali penye maumivu.

7.Kuimarisha mood yako na Kupunguza Msongo wa Mawazo.

Kwa miaka ya hivi karibuni mafuta ya lavender yamekuwa ni kitu adimu na cha kuaminika zaidi kutokana na uwezo wake kukukinga dhidi ya matatizo ya neva.
Matumizi: kupunguza msongo wa mawazo na kutengeneza usingizi mzuri. Weka mafuta ya lavender kwenye kopo la kupuliza (diffuser) kisha pulizia kwenye chumba cha kulala. Unaweza kupuliza jioni katika eneo la kupumzika kabla ya kwenda kitandani, pia unaweza kupaka kwenye ngozi nyuma ya masikio na ukapaka kenye mto wa kulalia.

Mafuta mengi yaliyo sokoni yameongezwa viambata vingine na kupunguza uwezo wake. Hakikisha unapata mafuta ya lavender asili yasiyo na kemikali na kutoka kwenye chanzo cha uhakika.

Usimeze tena vidonge vya famasi kuleta usingizi ama kuondoa msongo wa mawazo maana vina madhara makubwa, tumia mafuta haya halisi. Gharama za mafuta ya lavender ni sh 40,000/= elfu 40 tu kama utafika ofsini kwetu.

Tuandikie kwa whatsapp namba 0746672914 na Tembelea ofisi zetu zipo Mwembechai kupata lavender.

Share and Enjoy !

Shares
Shares