Kwanini unakoroma usingizini

kukoroma usingizini
kukoroma usingizini

Kukoroma usingizini ni jambo linaowatokea watu wengi kwenye jamii yetu na linaathiri kundi kubwa sana la watu. Tatizo hili likionekana kuwakumba zaidi wanaume kuliko wanawake. Pia watu wenye uzito mkubwa na kitambi wanaathirika zaidi na tatizo hili la kukoroma huku ukubwa wa tatizo ukiongezeka zaidi pale mtu anavozeeka.

Kama umewahi kulala kitanda kimoja na mtu anayekoroma basi utakuwa shahidi juu ya adha na usumbufu unaotokea. Hali hii huwakumba zaidi wanandoa pale mmoja wao mke au mume anapokuwa na tatizo la kukoroma. Kumbuka ukiwa na tatizo hili basi si tu unaleta usumbufu kwa wanakuzunguka bali unaathiri hata afya yako. Hivo ni muhimu kutafuta huduma ya kiafya mapema

Kukoroma usingizini husababishwa na nini?

Kukoroma hutokea pale hewa inapokwama kupita kwenye mirija midogo ya kupitisha hewa kati ya mdomo na pua. Sababu mbalimbali zinweza kukwamisha hewa kupita vizuri kama

  • Kuziba kwa mirija ya hewa kutokana na mtu kuwa na alegi kwa mazingira fulani mfano kipindi cha baridi au joto, ama kipindi cha upepo mkali.
  • Kulegea kwa misuli ya koo na ulimi: Tabia kama unywaji wa pombe kupita kiasi na matumizi ya dawa za kuimarisha usingizi husababisha usingizi mzito na kuongezeka kwa hali hii, kadiri umri unavoenda pia huletekeza kuchoka kwa misuli ya koo na ulimi na hivo kuongezeka kwa hali ya kukoroma.
  • Mrundikano wa tishu za koo: Uzito mkubwa ni sababu ya kurundikana kwa nyama kwenye koo, watoto pia wenye tonsil kubwa hukoroma zaidi wakati wa usiku.
  • Urefu wa tishu laini (uvula) iliyopo nyuma ya mdomo:
  • kurefuka kwa tishi hizi husababisha kuziba kwa njia za hewa zinazounganisha mdomo na pua na hivo kusababisha mtu kukoroma usingizini.
  • Kukosa usingizi kwa mda mrefu husababisha hali hii ya kukoroma kutokana na kulegea kwa misuli ya koo.
  • Namna ya kulala pia inachangia kuongeza tatizo la kukoroma mfano kulala kifudifudi.

Makundi yafuatayo yapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la kukoroma usingizini

  • Wanaume wapo kwenye hatari Zaidi kupatwa na tatizo hiki ukilinganisha na wanawake
  • Wenye uzito mkubwa na kitambi
  • Watu wenye njia nyembamba za kupitisha hewa kwenye pua
  • Watumiaji wa pombe:
  • kama wewe ni mtumiaji wa pombe na unakoroma usingizini basi hii ni hapa ndipo pa kuanzia, acha pombe.
  • Kama familia yenu ina historia ya kupatwa na tatizo hili na matatizo mengine ya upumuaji basi utakuwa kwenye hatari Zaidi ya kupata tatizo la kukoroma.

Madhara gani ya kiafya hupatikana kwa kukoroma usingizini

Tabia ya kukoroma usingizini mara kwa mara yaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya endapo ikizoeleka, athari kubwa ikiwa ni kushindwa kupumua ambayo huletekeza

  • Kuharibu usingizi na mtu kulazimika kushtuka mara kwa mara anapokuwa usingizini
  • Mgandamizo mkubwa kwenye moyo, kukosekana kwa hewa mara kwa mara kutokana na kuziba kwa njia za kupitisha hewa safi husababisha presha kubwa kwenye moyo na hivo kupelekea kutanuka kwa moyo na hivo kuongeza hatari ya kupata shambulizi la moyo na stroke.
  • Kuharibu mzunguko wa usingizi na hivo kukufanya mda mwingi umechoka na kushindwa kufocus kwenye shuguli zako, mfano yaweza kusababisha ajali.
  • Kutokana na kutopata usingizi wa kutosha usiku muhanga wa tatizo hili hulazimika kusinzia ovyo mchana na kushindwa kufanya kazi zake ipasavyo.
  • Kukoroma pia ni chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi, kutokana na mwenza mmoja kushindwa kuvumilia .

Nini cha kufanya ili kutibu tatizo la kuoroma usingizini.

Zifuatazo ni njia salama unazoweza kutumia ukiwa nyumbani mwako ili kuondoa usumbufu huu.

  1. Toa ulimi nje kadiri uwezavyo kwa nguvu ukiwa umenyoka, kisha jaribu kugusa pua yako inapoishia kwa chini. Kisha fanya kama unakunja kulia na pia kushoto, rudia zoezi hili kwa haraka zaidi mara 10.
  2. Zoezi la pili pinda ulimi wako kuelekea ndani kwenye koo. Hakikisha unakunja vya kutosha mpaka unyoke kuelekea ndani ya koo kama vile unataka kugusa sehemu ya chini ya meno ya juu. Rudia zoezi hili mara 15 kila siku.
  3. Zoezi la tatu: fungua mdomo kwa nguvu kadiri uwezavyo kisha piga kelele ya ahhhhhhhhhhh* kwa muda wa sekunde 20.tudia zoezi hili mara moja.
  4. Zoezi la 4: mdomo wako ukiwa umefunga vuta na kutoa hewa kupitia pua, fanya zoezi hili kwa kurudia mara 4 kwa pumzi 5, huku ukipumzika kwa sekunde 2 kwa kila pumzi unayovuta.

Kama una tatizo la kukoroma ama ndugu au mpenzi wako, basi tunashauri jaribu mazoezi haya kama tulivoelekeza kila siku mpaka tatizo litakapoisha ama kupungua kwa kiasi kikubwa. Kama tatizo litazidi kuwa kubwa ama kutoisha basi hakikisha unaonana na dactari wako kwa ushauri na matibabu zaidi.

Bofya kusoma makala inayofuata: Kinachopelekea uume mdogo ama kibamia

Share and Enjoy !

Shares
Shares