Maumivu ya mabega, mgongo na shingo

Asilimia 47 ya watu wanaofanya kazi wanapata maumivu ya mabega katika kipindi flani cha maisha, hasa wanaofanya kazi kwenye ofisi ambapo wanahitaji kusogeza vitu mara kwa mara kama kwenye saluni, waendesha mitambo, wakulima, washona nguo nk.
Tatizo hili kitaalmu linaitwa thoracic outlet syndrome(TOS). Ongezeko la wangonjwa wa mabega, kifua na mikono kwa miaka ya hivi karibuni imechangiwa na mabadiliko ya mtindo wa maisha, mfano kutumia mda mwingi kukaa kwenye kiti na kutofanya mazoezi.

Kwa upande mwingine TOS inaweza kuwaathiri hata watu wanaofanya kazi za mtindo wa kurudia rudia matumizi ya kiungo cha mwili mfano waendesha baiskeli, wajenzi, wanyanyua mizigo nk. Kundi hili la wafanyakazi wapo kwenye hatari zaidi ya kupata dalili hizi kama mikono kupata ganzi na kutetemeka, mikono kukosa nguvu, shingo kuwa ngumu na maumivu kwenye bega.
Nini kinaweza kufanyika kutibu dalili hizi? kubadli mtindo wa maisha, aina flani za mikao na mazoezi ya mara kwa mara yatasaidia kutibu dalili hizi za maumivu ya mabega, mikono na shingo.

Thoracic Outlet Syndrome ni nini

Thoracic outlet syndrome(TOC) ni neno pana linalowakilisha dalili zote unazopata baada ya mgandamizo wa neva za eneo la juu la mwili hasa kwenye shingo, kifua, mabega na mikono.(Fahamu kwamba neva ni seli za mwili ambazo husafirisha taarifa kwenda kwenye ubongo ili kutambua kitu husika) mfano unapokanyaga moto, neva ndio hupeleka taarifa na kisha ubongo kutafsiri kwamba ni kitu gani hicho.
Mgandamizo huu unatokea katika eneo la juu la mgongo, mahali kwapa, kifua na shingo vinapounganika. Tazama picha hapa chini

Kinachosababisha Maumivu ya Mabega na Tabia Hatarishi

Watafiti wanakubaliana kwamba Maumivu haya ni kutokana na mgandamizo wa neva zinazoendelea kutoka eneo linalounganisha mkono na na bega na kifua. Neva hizi zinaweza kujeruhiwa kutokana na ukaaji mbaya, tendo la kurudiarudia kupitia mkono nk. Sababu zinazopelekea mgandamizo na hatimae kutokea kwa maumivu ya mabega, mikono na kifua ni pamoja na

 • Historia ya kupata ajali kwenye eneo la shingo, mikono na vidole
 • Ukaji mbovu unaopelekea presha kubwa kwenye neva hasa kichwa kuinama kwa mbele tazama picha hapa chini.
 • Kufanya kazi za kurudia rudia
 • Kuzaliwa na mapungufu kwenye mpangilio wa viungo
 • Uvimbe kwenye bega ambao unapelekea mgandamizo kwenye neva na
 • Ujauzito

Makundi gani yapo kwenye Hatari zaidi ya Kupata Maumivu ya Mabega, Shingo na Mikono?

 • Wanawake wanaathiriwa zaidi kuliko wanaume
 • Watu wa umri kati ya miaka 20 mpaka 50
 • Kuishi maisha ya kizembe, kama kutofaya mazoezi na kutumia mda mwingi ukiwa umekaa.
 • Wanamichezo wanaotuumia kiungo cha mkono kwa tendo la kurudiarudia mfano kuogelea, martial arts, mielek nk.
 • Wenye msongo wa mawazo kupita kiasi
 • Wenye uzito mkubwa na kitambi
 • Watu wenye historia ya kuugua kisukari, ganzi kwenye mikono na miguu, na matatizo mengine ya neva
 • Wavutaji wa sigara na walevi kuindukia
 • Mtumiz ya dawa za aleji, saratani, vidonge vya kupanga uazi na vidonge vya kupunguza msongo wa mawazo.

Aina 8 za Mazoezi na Mikao ya Kutibu Maumivu ya Mabega, Shingo na Mikono

Hapa chini ni maelezo ya aina fulani za mazoezi na mikao itakayokusaidia kutibu tatizo lako la maumivu ya mgongo. Hakikisha unafanya mazoezi haya taratibu na kwa uangalifu ili usiumize mwili na kusababisha maumivu zaidi.
Lengo letu ni kufanyisha mazoezi eneo la juu la mwili kwenye mabega ili kutanua kifua na maeneo yenye mgandamizo. Kila mkao tumia sekunde 30 mpaka dakika 1, kisha jiachie taratibu pumzika sekunde 10 endelea na mkao mwingine.

1.Back of Neck Stretch

Ukiwa umekaa, shika magoti kwa mikono isha taratibu peleka shingo yako nyuma na mbele huku ukiwa unavuta hewa.

2.Side of Neck Stretch


Ukiwa umekaa kwenye kiti,shika eneo la nyuma ya kichwa, kisha peleka shingo kulia na kushoto.

3.Chest Stretch

Nyoosha mikono ya mbele ukiwa umekaa kwenye kiti. Kisha fanya zoezi la kutumbukiza kichwa katikati ya mikono.

4.Shoulder Stretch

Ukiwa umekaa kwenye kiti, kutanisha mikono yako kwa juu ya kichwa, fanya kama unasukuma kuelekea juu.

5.Pectoralis Stretch

Ukiwa katika eneo la kona ya nyumba, wakati huo umesimama ,nyanyua mikono yote shikilia eneo la ukuta kwa dakika 1.

6.Rowning Exercise

Ukiwa umekaa kwenye kiti au puto la mazoezi, weka kamba yako ya mazoezi inayovutika kwenye miguu kisha vuta kwa mikono yote kwa kumakimilisha walau mizunguko 20.

7.Mid-trap Exercise

Ukiwa umelalia kwa tumbo mto mwembamba laini huku mikono na miguu ikiwa imenyooka, fanya zoezi la kunyanyua mguu wa kushoto na mkono wa kulia kwa mara moja seti 10 kisha badili nyanyua mkono wa kulia na mguu wa kusho kwa wakati mmoja seti 10 pia.

8.Flys

Ukiwa umesimama, nyanyua vyuma vyako vya mazoezi(dumbbells). Tumia vyuma vidogo vya kilo 5 mpaka 15 kulingana na uwezo wako wa kumudu. Nyanyua kwa pamoja kutoka kwenye eneo la paja mpaka kichwa. Rudia seti 15 mpaka 20.Unaweza pia kubadilisha zoezi hili ukafanya ukiwa umekaa kwenye kiti.

Nini ufanye ili Usipatwe na maumivu ya Mabega, shingo na Mikono

 1. Rekebisha Eneo lako la Kazi
  Kama unatumia mda mwingi ukiwa umekaa, anza leo kurekebisha mahali pa kazi, kwa kurekebisha mkao unaokuletekezea maumivu. Ukaaji mbaya unapunguza mzunguko wa damu kwenye mikono na hivo kusababisha maumivu. Unaweza kutumia meza ndefu inayokufanya usimame wakati unaendelea na kazi zako.
  Unapokaa kwenye kiti hakikisha shingo inanyooka na usiiname kwa mbele.
 2. Jipe mda Mrefu wa Kupumzika
  Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yak0, lakini kufanya mazoezi kupita kiasi inaweza kupelekea mauivu ya mabega, shingo na mikono. hasa kama hupati mda wa kupumzika kati ya zoezi na zoezi. Jipe mda wa siku mbili kama unafanya mazoezi makali sana ili kuruhusu mwili kurudi katika hali ya zamani.
 3. Punguza au ondoa vitu vinavyofanya mwili kututumka(inflammation);kama kuacha kuvuta sigara na matumizi makubwa ya pombe, ondoa vyakula vinavyoongeza mpambano wa tishu na kinga ndani ya mwili kama mafuta yalisindikwa, wanga iliyosafishwa, sukari iliyoongezwa kiwandani na viongeza ladha visivyo asili kwenye chakula.
 4. Cheki matumizi yako ya dawa
  Kama unatumia dawa zozote ambazo zinapunguza mzunguko wa damu inaweza kuwa ndio sababu ya tatizo lako. Ongea na Daktari anayekuhudumia akupe njia zingine mbadala.

Makala inayofuata:Hatua za Kubana Uke uliolegea

Share and Enjoy !

Shares
Shares