Kuvurugika kwa homoni za kike ni chanzo cha ugumba

kuvurugika kwa homoni za kike

Kuvurugika kwa homoni za kike ni suala pana linalojumuisha vyanzo vingi, kama mtindo wa Maisha (lifestyle), umri kwenda, sababu za kimazingira kama msongo wa mawazo. Sababu zote hizi zinaathiri uzalishaji na ufanyaji kazi wa vichocheo ama homoni zako.

Napenda niseme tu kwamba moja ya sababu kubwa iliyonigusa kuandika elimu hii juu ya kuvurugika kwa homoni za kike ni ukubwa wa tatizo. Kwani tatizo hili limekuwa ni tatizo ambalo kila mwanamke analo na wengi wao wametumia kila mbinu ya kuondoa tatizo na wameshindwa.

Je ugumba unatibika? hili ni swali linaloulizwa zaidi na wenye tatizo. Basi leo utapata ufumbuzi juu ya chanzo cha tatizo hili na namna gani uweze kutatua ukiwa nyumbani kwako kupitia virutubisho na dawa ya asili ya ugumba .

Mambo Yanayoashiria Kwamba Una Tatizo Kwenye Homoni Zako Za Kike

 1. Kuwa na hedhi ya muda mrefu Zaidi ya siku 7 unatumia Zaidi ya pedi 2
 2. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana
 3. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na kichefu chefu,kuharisha
 4. Kuwa na hedhi iliyojaa woga mkubwa sana
 5. Hedhi kuvurugika, Unaweza kuingia mara tatu kwa mwezi mmoja, mara mbili au unaweza usipate kabisa hata miezi 6 hadi mwaka.
 6. Kuwa na ndevu sehemu za usoni,kifuani nyingi kupita kiasi
 7. Kuwa na kitambi cha tumbo la chini
 8. Ugumba na Kukosa mtoto kwa muda mrefu
 9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa ama  lenye kuambatana na maumivu makali
 10. Mwili kuwa unauma sana hasa misuli bila sababu ya msingi, kuumwa sana na kichwa bila sababu ya msingi.

Nimekuwa nikitafutwa na wakina mama wengi sana na wamekuwa wakinisimulia jinsi gani wamesumbuka na kutatua tatizo hilo . Kusema kweli huwa ni watu ambao napenda kuwaweka katika makundi yafuatayo halafu wewe utajitambua upo kundi lipi.

 1. Kundi la kwanza ni wale ambao ndio tatizo nimeanza kuwaandama na hivyo wanajaribu kutafuta njia nyepesi za kuondoa tatizo kabla hawajafikia zile njia ngumu za hospitali za kuliondoa tatizo. Wanawake wengi huwa ni woga sana wa kuguza uzazi wao hasa pale inapotokea hajaolewa na hajapata mtoto hivyo ikitokea ana tatizo kama hilo wengi huwa wanakuwa makini kutojishirikisha na njia hatarishi. Afya yako ni hazina yako wewe ndiye mwenye mamlaka wa kuruhusu tiba flani itekelezeke au hapana.
 2. Kundi la pili ni wale watu ambao wametumia kila mbinu za kutatua matatizo kwa kuanzia ngazi za juu lakini hawapata suluhisho. Sasa anaanza kutafuta suluhisho kwa upande wa pili ili aone kama na  huko pia atafanikisha kuifikisha afya yake mahali stahiki. Hawa huwa wamesumbuka kwa wataalamu mbalimbali lakini hawajakata tamaa.
 3. Kundi la tatu ni wale watu waliotumia njia zote bila mafanikio na hadi wametamkiwa na washauri wao hapo hutaweza kufikia malengo, shusha pumzi yako ipokee hali yako maisha yaendelee. Hawa ni watu ambao wanaishi katika msongo wa mawazo mkubwa sana ambao sitamani hata kuelezea mpendwa. Siri kubwa ambayo nakumegea ni kwamba  Hukuzaliwa na matatizo hayo  Ulikuwa mwenye afya tele na mwenye kufurahia hedhi yako.

Mwanamke huwezi kuwa na Amani kama hedhi yako ina kasoro,kwani hio ndio nyota njema katika maisha yako kiafya ya kila siku ni jukumu letu kuhakikisha inarudi katika misingi ya mwanzo na ufurahie hedhi yako.

Nina Imani kwamba umetumia njia nyingi sana, na kama ndio umehitimisha na umekata tamaa basi napenda nikushauri kwamba ili uweze kunielewa vizuri katika haya machache hakikisha  Unatupilia mbali yote ambayo ulishauliwa kuyafanya na hayajakupa matunda  yote unayojua kichwani mwako inawezekana kabisa hayana faida yoyote na inaweza kuwa ni chanzo moja wapo cha kukuzuia wewe kurudiaa afya yako njema. Hebu kuwa kama hujui kitu ili elimu hii ianze marekebisho ya afya yako.

Hukuzaliwa na kitambi,hukuzaliwa na ndevu,hukuzaliwa na maumivu makali kiasi hicho ya hedhi na hukuzaliwa ukiwa na mtu mwenye mateso kuhusu afya yako ya hedhi sasa hizi ndizo njia rahisi ya kuondoa tatizo kwani inawezekana wewe ndiye kisababishi kikubwa cha lishe mbovu inayokuuguza kila siku.

UGONJWA WA POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME

Mwanamke huwa ana viwanda viwili vya kuzalisha mayai kila mwezi yaani kwa lugha nyingine ni Ovari ya kushoto na Ovari ya kulia. Ndani ya ovary ya mwanamke kuna mayai ambayo hayajakomaa kwa lugha ya kilatini huitwa Follice cells ,hizi ndizo hukomazwa kila mwezi na kutupatia yai ambalo linatakiwa lipatiwe urutibishaji endapo itakutana na mbegu ya kiume.

Sasa inapotokea hizo follicle cells zimekomaa vizuri kwenye ovary na zinatakiwa zipasuke zitoe mayai bahati mbaya kabisa Kitendo hicho kinashindikana hivyo hizo follicles ambazo zimeshindwa kupasuka na kutoa yai zinabaki na umbo kama Zabibu zilizo kwenye kikonyo chake mwonekano wake kwa kitaalamu zinafananishwa na kitu kiitwacho Cyst kwa sababu zipo nyingi tunatumia neno la kitalamu Polycystic. Na hii hali huambatana na dalili nyingi ambazo zinauvuruga mwili wako kwa sababu ya ovary zako kutengeneza cyst nyingi  Polycystic  kwa pamoja dalili hizo tunaziita Syndrome neno hili humaanisha Mkusanyiko wa dalili nyingi.

Kwa hio basi kitendo cha ovary zako kushindwa kutoa mayai kama kawaida na hatimaye kutengeneza polycysts nyingi kwenye ovary inakupelekea unapata ugonjwa wa  Polycystic Ovarian syndrome. Ovary yako inaonekana kama zabibu ambazo hazijatolewa kwenye kikonyo chake zilivyokusanyika (ambazo kwa jina rahisi daktari wako anaweza kukwambie ni uvimbe kwenye kizazi lakini kiusahihi ni vimbe kwenye mifuko ya mayai)

Neno cyst ni kitu chenye uwazi kwa ndani na kimezungushiwa ukuta mwembamba na laini (Membrane). Na mle ndani kunaweza kukaa damu,usaha,maji nk. Lakini kwa upande wa mwanamke hizo follicles nyingi ambazo zimekomaa na zimeshindwa kutoa mayai zinafanishwa na Cysts  lakini jina halisi ilitakiwa kuwa POLYFOLLICULAR SYNDROME,  kwa sababu follicles nyingi katika ovary zimeshindwa kutoa mayai na zinaonesha mwonekano kama  Cysts

Nini Kinapelekea Unapata Ugonjwa Huu Wa Polycystic Ovarian Syndrome?

 1. Kuongezeka kwa homoni za kiume zinajulikana kama  Androgens ambazo ni Testosterone. Kwa kawaida mwanamke huwa ana kiwango kidogo sana cha homoni hii ya kiume Testosterone  Homoni inayomfanya mwanaume aonekane mwanaume kuongezeka kwa homoni hii inampelekea mwanamke kuonesha dalili za kuongezeka kwa dalili za kiume kwa mwanamke kama kuota ndevu kidevuni,chunusi sugu na pia kuongezeka uzito kupita kiasi na kitambi pia.

Homoni hizi zinatengenezwa na Ovary za mwanamke na tezi ya adrenali baada ya kupata msukumo kutoka kwenye homoni iitwayo insulin. Kwa hio basi watu wenye kiwango kikubwa cha insulin wapo hatarini kupata ugonjwa huu wa Polycystic Ovarian Syndrome(PCOS)  na ndio maana watu wengi wenye PCOS ukubwani huwa ni ishara moja wapo unaelekea kupata ugonjwa wa kisukari maana yake upo hatua za mwanzo yaani  Pre diabetic ambapo hatua ambayo kwa nchi zinazo endelea tunaweza kukubaini kwa kutumia dalili zinazo unazo na sio kwa kipimo maana kiwango cha sukari huwa kipo sawia kabisa lakini unakuta insulin ipo juu changamoto inakuja hatuna vifaa vya kupita kiwango cha insulin kwenye damu. Hivyo basi njia rahisi ya kukubaini haraka kama upo hatua za mwanzo ni kuangalia dalili gani ulizo nazo.

Mbali na nywele sehemu za kidevu kuonekana,chunusi sugu, uso wenye mafuta mengi sana kupita kiasi,shingo kuwa nyeusi sana na sehemu zingine kama kwapa na kwenye mikunjo sehemu za siri kwa kitaalamu inaitwa  Acanthosis Nigricans pia hata kupata viotea shingoni yaani  Skin Tags  pia ni dalili kuwa kiwango cha insulin kipo juu na upo  Pre diabetic  na endapo ukiamua kurudisha afya yako upya unaweza kabisa. Zote hizo ni dalili moja wako kwa wananwake wanaosumbuka na PCOS.

Hebu sasa tujiulize swali moja kubwa! Kumbe homoni ya Testosterone inapokuwa katika kiwango cha juu kupita kiwango maalumu kwa wanawake inampelekea mtu kupata Polycystic Ovarian Syndrome(PCOS!) Na hii homoni kuongezeka kwake ni pale insulin inapo enda kuamuru Tezi ya Ovary na Adrenali kutoa homoni za Kiume kwa wingi kupita kiasi.

Swali: Kama ndivyo hivyo swali la kujiuliza sasa kwa nini wagonjwa wenye PCOS wapo hatarini kupata kisukari

JIBU: Wagonjwa wenye PCOS wapo hatarini kupata ugonjwa wa kisukari maana wote huwa wana kiwango kikubwa cha insulin kupita kiasi kwenye damu kama ishara ya  Insulin resistance kwa lugha nyingine  Insulin Tolerance  yaani seli za miili yao huwa haziwezi kubaini uwepo wa insulin kwenye damu na hivyo insulin huwa haifanyi kazi yake ipasavyo. Na hii hali ya seli za mwili kutoweza kubaini uwepo wa insulin kwenye damu inasababisha sukari katika damu kutofanyiwa kazi na hatimaye sukari inaanza kupanda na kukupelekea kupata kisukari  Hali ya sukari kwenye damu kuwa katika kiwango cha juu muda wote kwenye damu kiwango hiki kingi cha insulin ndicho kimekuwa kichochezi kikubwa kwa wana wake wengi kuugua ugonjwa huu!

Swali: Nini kinasababisha insulin kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ipasavyo

Neno  Insulin resistance  limekuwa likitafsiriwa tofauti sana na watu wengi hasa washauri wa afya. Lakini tafsiri mbaya kabisa ambayo hata wewe unayo hapo ni kwamba insulin inaposhindwa kufanya kazi maana yake mafuta mabaya yameziba kwenye kipikea insulin  Insulin receptor  na hatimaye insulin haiwezi tena kufanya kazi. Huu ni Uongo kabisa tena ulio wazi!

Ili uweze kunielewa vizuri nakupa tafakari nzuri hapa kama mbili ili uje unielewe vizuri.

 1. Nadhani kila mtu anajua jiji la Dar es salaam lilivyo na joto kali kupita hali ya hewa ya mikoa mingine yote. Mtu ambaye ni mkazi wa mwanza ukimleta jijini lazima atasumbuka sana kuzoea joto hili. Na ndio maana sasa baada ya kukaa miezi kama 6 anakuta amezoea mazingira haya anaona kama hakuna utofauti kabisa. Maana yake mwili wako umezoea mazingira  You have Tolerated the hot climatic condition  neno kuzoea naweza kusema ni sawa na kulipa maana ya  Tolerance au Resistance
 2. Pia chukulia mfano mlevi wa pombe kali kama  Dompo  mwanzo alikuwa nakunywa chupa mbili na analewa sana hadi kuendesha gari hawezi. Lakini kadri muda unavyo enda atajikuta anapiga pombe hizo chupa mbili hata halewi chochote kabisa. Maana yake zile chupa mbili zimemzoea haziwezi tena kufanya kazi yake  Kumlewesha  kama zamani. Hivyo kwa lugha nyingine hizo chupa mbili za dompo mwili wako ume  Tolerate au Umepata  Resistance dozi inatakiwa iongozwe ili ulewe Zaidi.
 3. Mfano wa mwili ni pale unapo ambiwa na washauri wa afya usitumie antibiotic hovyo hovyo maana wale wadudu watazoea hizo dawa na hatimaye isiwe rahisi kuwatibu kwa dawa hizo ndio maana tunaambiwa tupime kwanza kabla ya kunywa dawa ili kupunguza matumizi ya dawa hovyo na kusababisha dawa zingine kutokuwa na uwezo wa kuangamiza vimelea.

Haya nahitimisha kwamba kitu kinacho sababisha  Tolerance au Resistance  ni kile kile . mfano yule ambaye alisema dar kuna joto sasa joto lile lile amelizoea. Aliyesema pombe mbili nalewa sasa pombe ileile haiwezi kumlewesha, na dawa kutofanya kazi yake kisababishi ni matumizi ya madawa hovyo.

Hivyo basi hata kongosho la binadamu linapomwaga maji ya insulin kwa kutumia seli zake aina ya beta moja kwa moja kwenye damu. Kadri linavyozidi kuongeza kiwango chake kingi katika damu ndivyo itafikia hatua seli za mwili zinapata  Insulin Tolerance  yaani hio insulin haiwezi tena kufanya kazi yake ipasavyo.Hivyo kisababishi cha insulin resistance au Tolerance ni insulin yenyewe.

Ulaji wa vyakula vya wanga kupindukia na vyakula vyenye sukari rahisi vinasababisha kiwango cha insulin kumwagwa kwa wingi kupita kiasi na hatimaye kupelekea insulin kuwa katika kiwango cha juu muda wote na mwishowe insulin inakuwa haiwezi tena kufanya kazi yake.

Kwa hio basi chanzo kikubwa cha insulin kuwa katika kiwango cha juu kupita kiasi ni ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi. Na tafiti zinaonesha kwamba vyakula vya wanga  na sukari vinaongoza kupandisha kiwango cha insulin mwilini mwako,ikifuatiwa na vyakula vya protini na vyakula vya mafuta vimeonesha havina madhara kabisa ya kuongeza insulin katika damu baada ya kula. Ukitaka kuifanya insulin ifanye kazi ni kupunguza vitu vinavyo ongeza kiwango cha insulin.

Hii ndio maana wagonjwa wengi wenye PCOS wanapewa dawa kama Metformin dawa za kuongeza utendaji kazi wa insulin yaani inaondoa  Insulin resistance  lakini hilo sio suluhisho la kudumu katika maisha yako na suluhisho pekee ni kuhakikisha vitu vinavyopandisha insulin vinaepukwa na utashangaa maajabu yake.

Hivyo basi napenda kusema kwamba jiko lako linaweza kuwa linakuuguza kabisa na ni wakati sasa wa kusafisha jiko lako na vyakula ambavyo uliambiwa ni adui yako hebu kuanzia leo view rafiki yako mpendwa, vyakula kama Nafaka yaani mahindi,mtama,ulezi nk,viazi,Ngano aina yoyote vinywaji vyote vyenye sukari, pombe aina zote ,Epuka tambi , hivi ndivyo vinavyokuuguza hata kama unatumia dawa ndio maana hupati mwafaka. Safisha jiko lako sasaa!

Kula vyakula kama samaki,karanga,ufuta,alizeti,korosho,almonds,Nyama aina yoyote,mayai nk kwani ni vyakula sana kwako na tiba kwako ndani ya muda mfupi sana.

 1. Ugonjwa huu ni wakurithi kwa asilimia ndogo sana

Napenda tu kukuambia kuwa ugonjwa huu wa PCOS ni ugonjwa wa lishe ambayo haizingatii kanuni na masharti ya tiba. Watu tukiongea lishe mbovu anajua ni ile hali ya kula vyakula vya mafuta,kula sana,kunywa pombe na kutofanya mazoezi! Najua unawaza hayo maana umepotokavyakutosha umejaribu kuyaepuka hayo na bado unaendelea kuugua kila siku. Tizama sana kwa kina vyakula ambavyo vinavuruga homoni za mwili wako na hatimaye kukuletea ugonjwa huu. Na nimeeleza kwa kina namna gani vyakula vya wanga vinavyo tuletea ugonjwa wa PCOS na suluhisho lake.

Hivyo bas unapotaka kusema huu ugonjwa ni wakurithi hakikisha umeondoa visababishi vingine vyote vya ugonjwa huo kwa kitaalamu tunasema  Genetic factor should be the diagnosis of Exclusion huwa nasema kila siku huwezi kuniambia kwenu kuna watu wenye ndevu na wewe basi umerithi ndefu kutoka kwa bibi yako sio kweli! Maana yake mmerithishana mapishi mabovu yasiyozingatia afya ya uzazi wako. Hivyo neno kurithi huwa sipendi kulisikia linakukuficha kifikra katika maradhi na unashindwa kulitafutia suluhisho ukiwa mwenye nguvu tele.

Nini Madhara ya Kuvurugika Kwa Homoni Hizi Kwa Mwili Wa Mwanamke

Sayansi ya homoni  Endocrinology  naifananisha na vitabu kumi ambavyo nimevipanga kwa wima kwenye meza, ikitokea nimekisukuma kitabu kimoja kikaangukia kitabu cha pili yake vitabu vyote kumi vitaanguka kwa kufuata mlolongo ule ule. Hii namaanisha kwamba homoni moja ikitoka katika misingi yake homoni zingine pia zinavurugika kwa kiwango kikubwa sana na ndio maana watu wenye Polycystic Ovarian Syndrome huwa wana dalili Zaidi ya moja kwani ugonjwa huu unahusisha mvurugiko wa homoni nyingi sana. Kumbuka usihofu sasa tiba ya ugonjwa huu ni lishe hata wewe unaweza kuanza leo kuhakikisha unasawazisha homoni zako zote zirudi katika misingi.

Zifuatazo ni baadhi ya homoni ambazo huvurugika mwilini mwako na mwisho wake unapata PCOS.

 1. Kiwango cha Estrogen huongezeka kupita kiasi.Hii inasababishwa na insulin kuisisimua ovary kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na hii inapelekea kiwango cha homoni hii kuwa juu kwenye damu. Madhara ya homoni hii kuwa katika kiwango kikubwa katika mwili wako inaweza kukupelekea ukuta wa kizazi kujengeka na kuwa mnene kupita kiasi  Endometrial hyperplasia  na hatimaye unaweza kuwa hatarini kupata kansa ya kizazi. Na hii ndio sababu kubwa ya kupata hedhi nzito kupita kiasi yenye mabonge ya damu sana, kwa sababu kazi kubwa ya estrogen ni kukufanya wewe uonekane  mwanamke  na ndio homoni ambayo inajenga ukuta wa kizazi kila mwezi ili kama mimba ikitungwa mtoto aje ajishikize kwenye ukuta imara. Lakini inapotokea kiwango chake ni kukubwa ukuta mnene utajengwa kila mwezi na inapokuwa mimba haijatungwa ukuta utabomolewa na kama ni mnene damu nyingi sana zitatoka hali hii tunaita  Polymenorrhea  ukiona dalili hizo fika hospitali maana kuna hatari kubwa ya kuishiwa damu.
 2. Follicle Stimulating Hormon(FSH)  inashuka kiwango

Hii ni homoni inayotolewa na upande wa mbele wa tezi ya  Pituitary  kwenye ubongo baada ya kupata taarifa kutoka kwenye hypothalamus. Homoni hii kazi yake kubwa huwa inakomaza mayai kwenye ovary za mwanamke. Sasa kiwango hiki kinaonekana kuwa katika kiwango kidogo sana kwa mwanamke mwenye PCOS kwa sababu kiwango kingi cha estrogen kwenye damu kinapeleka taarifa kwenye ubongo kwamba homoni zipo zinajitosheleza (Negative feedback inhibition) na hatimaye ubongo hautatoa taarifa yoyote ya kutengenezwa kwa FSH. Na hii ndio sababu kubwa ya ugumba kwa wanawake wenye PCOS kwani kama hii homoni ipo katika kiwango cha chini hakuna yai lolote litakomazwa.

 1. Homoni ya luteinizing (LH)

Homoni hii kwa wagonjwa wa Polycystic Ovarian Syndrome(PCOS) huwa ipo pia katika kiwango cha kawaida au chini na hivyo basi inakuwa haiwezi tena kufanya kazi yake ipasavyo. Kazi kubwa ya Luteinizing homon ni kuishinikiza ovary itoe mayai kila mwezi yale yaliyo komaa. Sasa kama haifanyi kazi yake hakuna kitakacho timia katika zoezi zima la mayai kuja kwenye mirija ya uzazi kwa kurutubishwa.

Jinsi Ya Kubaini Kama Una Polycystic Ovarian Syndrome

Napenda tuweze kubaini ugonjwa huu kwako kwa kushirikiana na wewe mpendwa,lakini wanasayansi hawakutaka kila mtu aje na tafsiri yake kwa ugonjwa huu, tunatumia  ROTTERDAM CRITERIA  Huu ni mwongozo wa kuweza kubaini mwanamke kama ana ugonjwa huu au hapana ambao una vitengo 3 vikubwa:

 1. Dalili za magonjwa ya uzazi zote ambazo nimezitaja hapo juu. Kama unazo basi moja wapo kuzihusisha
 2. Kipimo cha damu na kwenda kuangalia homoni za Estrogen,Testosterone,FSH,LH na Insulin
 3. Kipimo cha mionzi ya tumbo (Abdominal Ultrasound)-Ikinonesha ovary ina cyst nyingi (Polyfollicular ovary)

Endapo ukiangukia katika vitengo kuanzia viwili au vitatu basi kuna uwezekano mkubwa kuwa una ugonjwa wa POLYFOLLICULAR SYNDROME (PCOS).

Makundi Ya Watu Wenye Polycystic Ovarian Syndrome

Hebu tizama makundi haya matatu maana kila mtu ambaye amekuwa akinitafuta huwa anapenda sana  nitoe ufafanuzi kuhusu ugonjwa huu, basi leo nimeamua kukupa mchanganuo mwepesi kabisa uelewe kwa kina kama ifuatavyo:

 1. Kundi la kwanza ni mwanamke amepima amekutwa ovary zake zina  Poycysts ,hapati hedhi mara kwa mara yaani hedhi yake mbovu na ana dalili za homoni za  kiume (Nimezitaja juu)
 2. Kundi la pili ni mwanamke mwenye ovary zenye  Polycysts  ana dalili za homoni za kiume lakini Mzunguko wake upo vizuri ( Hawa wapo wengi sana, ana ndevu, na ukipiga picha ya tumbo unakutana na ovary ina cysts) na ukimwambia una tatizo anakwambia ndevu za urithi,weusi huu shingoni ni wa urithi unaanza kutafuta dawa za kuondoa weusi za kupaka. Dawa ni lishe tu unapona!
 3. Kundi jingine ni mwanamke mwenye ovary zenye  polycysts ,hana dalili za homoni za kiume lakini mzunguko mbovu sana ( Huyu hana ndevu, hana dalili zozote za kiume lakini hedhi yake inamtia mawazo kila mwezi)
 4. Kundi la mwisho ni wale ovary zao zipo vizuri kabisa  Ikipimwa naambiwa hakuna cysts kabisa Lakini ana dalili za homoni za kiume na mzunguko mbovu na yenye yenye kuambatana na maumivu makali sana kupita kiasi. ( Hawa pia wengi sana kwani husema mimi sina PCOS kabisa nilipima anashindwa kujua Rotterdam criteria imeweka makundi 4 baada ya uchunguzi)

Tiba Asili kupitia vidonge vya Evecare

evecare

Dawa ni asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili.

Baada ya kutumia evecare tegemea kupata matokeo haya

 • Homoni kubalansi
 • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
 • Hedhi yako kuwa nyepesi ya kawaida
 • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa na
 • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

Angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge feki vya evecare , tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Bei ya Evecare ni elfu sabini na tano tu 75,000/= Wasiliana nasi kwa whatsapp namba 0678626254 kuanza tiba.

Bofya Makala inayofuata:Tambua siku za hatari za kushika mimba haraka

Share and Enjoy !

Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shares