Maambukizi kwenye njia ya uzazi(PID)

Maelezo Ya Utangulizi Kuhusu PID

Maambukizi kwenye njia ya uzazi au kwa kifupi PID, ni mambukizi ya bacteria yanayoathiri sana wanawake kwenye mfumo wa uzazi. Na kuweza kuleta athari katika sehemu zozote kwenye njia ya uzazi. Moja ya madhara ya PID  ambayo wanawake hupata ni kuzuba kwa mirija ya uzazi na hivo kuutoweza kushika mimba yaani ugumba.

Tafiti zinasema kati ya wanawake nane waliowahi kuugua PID basi mmoja wao atakutana na shida kupata mimba kwa siku za hapo baadae. Huku wale wanaofanikiwa kupata ujauzito basi hupata matatizo pia ikiwemo mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati.

Nini kinasababisha PID??

Wataalamu wa afya wanaamini kwamba magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa ipasavyo hasahasa gonorrhea na chlamydia yanaongoza kwa kusababisha PID. Japo kuna baadhi ya wanawake wanaugua PID pasipo magonjwa ya zinaa hasa wale waliotoa mimba. Pengine kutokana na maambukizi ya kawaida ya bacteria(bacteria vaginosis)

Nini Maana Ya Pelvic Inflammatory Disease(PID)

PID
Athri za PID kwenye kizazi

Maana halisi ya PID ni hali ya kututumka, kuvimba au kucharuka kwa sehemu ya njia ya uzazi kwa mwanamke kunakosababishwa na athari ya bakteria, fungus au hata virusi kwenye kizazi. Sehemu hizi zinazoathiriwa ni kama mirija ya uzazi na mifuko ya mayai yani ovary.

PID inaweza kusambaa

Maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID) yana tabia ya kusambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Ndio maana kuna umuhimu wa kutibu tatizo hili mapema. Maambukizi haya yanaweza kusambaa kutoka kwenye uke mpaka sehemu zingine za uzazi wa mwanamke kama mirija ya uzazi, mifuko ya mayai(ovari) na kwenye shingo ya kizazi(cervix).

Maambukuzi haya yanaweza kusababisha makovu kwenye mirija ya uzazi na kupelekea kupata ectopic pregnancy . Ectopic ni mimba iliyotungwa na kushindwa kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa mimba(uterus) kutokana na majeraha kwenye mirija.

Je mtu aliyetoa mimba anaweza kuugua PID?

Jibu ni ndio, endapo umetoa mimba unakuwa kwenye hatari kubwa ya kuugua PID. Hii ni kutokana na mazingira ya uke kuvurugika na hivo kurhusu bakteria kusambaa mpaka eneo la uzazi. PID kwa mwanamke alieytoa mimba endapo haitatibiwa yaweza kupelekea mirija kuziba na hivo ukashindwa kushika mimba siku za mbele. Unatakiwa kusafisha kizazi kupitia vidonge vya UCP ama ukasafishwa hospitali kwa vyuma.

Dalili Za PID

Dalili za PID zinatofautiana kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa baadhi ya wanawake dalili huwa mbaya na kwa wengine dalili huwa za kawaida. Wakati mwingine wanawake hukaa na ugonjwa kwa muda mrefu bila kujua kutokana na kuchanganya dalili na magonjwa mengine. Zifuatazo ni dalili zinazojotokeza zaidi kwa wanawake wengi.

  • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuwa upande mmmoja au pande zote kulia na kushoto
  • Sehemu za uke kuwa na ulaini sana
  • Kupata maumivu wakati watendo la ndoa wakati mwingine kupelekea kuvuja damu wakati na baada ya tendo la ngono na hivo kukosa tena hamu ya tendo la ndoa
  • Kuvurugika kwa hedhi
  • Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida hasa yenye rangi ya njano na kijani
  • Maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa choo
  • Kupata dalili za homa kama kizunguzungu, mwili kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula na uchovu mwingi.

Madhara Yanayosababishwa Na Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi(PID)

Maambukizi kwenye njia ya uzazi husababisha athari kubwa sana kwa mwanamke. Kama tulivoona pale juu PID inaweza kusababisha ugumba na mimba kujishikiza mahali pasipo sahihi(ectopic pregnancy).

Kadiri unavoumwa zaidi PID ndivyo hatari ya kupata ugumba inavoongezeka. Mimba kutokea nje ya mfuko wa mimba ni ishu kubwa ya kiafya na inahitaji uangalizi mkubwa wa kidaktari ili kuzuia kuvuja kwa damu na hatimae kupelekea kifo kwa mama. Madhara mengine ya PID ni

  • Kupata majeraha kwenye mirija ya uzazi, majeraha yanaweza kutokea nje ama ndani, tatizo hili linaweza kuwa gumu kutibika na hutokea tu pale ambapo maambukizi hayakutibiwa kwa muda mrefu zaidi.
  • Kuziba na kujaa maji kwa mrija ya uzazi(hydrosalpinx kutokana na majeraha ya tishu zake
  • Maumivu ya tumbo ya muda mrefu husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwanamke kutofurahisa unyumba.
  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata matatizo mengine wakati wa ujauzito na kujifungua.

Kama tulivokwisha kusoma kwamba PID huletekezwa kwa kiasi kikubwa na magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa vizuri (sexual transmitted diseases). Kwa hivo basi ni muhimu kufahamu dalili za magonjwa ya zinaa ambayo ni common sana kwenye jamii yetu kama gonorrhea-kisonono na chlamydia. Ugonjwa wa Chylamidia ni ugonjwa wa zinaa unaowaathiri wake kwa wanaume na husambazwa kupitia uke, njia ya haja kubwa na pia ngono ya mdomo.

Magonjwa ya ngono yayonasababisha PID yana dalili karibu sawa na PID. Dalili za magonjwa ya zinaa ni kama

  • Kutokwa na uchafu kupita kiasi ukeni, wenye rangi ya njano na kijani na unaonuka kwenye.
  • Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa na kutoa haja kubwa
  • Kwa baadhi ya watu hupata maumivu mahala pa haja kubwa na kutokwa na uchafu

Tabia Hatarishi Zinazopelekea Uugue PID.

Kwa kiasi kikubwa wanawake waliopo chini ya umri wa miaka 35 wanaathirika zaidi na maambukizi kwenye njia za uzazi. Hii ni kutokana na kwamba wanajihusisha zaidi na ngono. Tumeona hapo juu kwamba kutokutibiwa vyema kwa maradhi ya gonorrhea na chlamydia ndio chanzo kikubwa cha PID.

Achilia mbali sababu hii, baadhi ya bacteria wengine wanaweza pia kusababisha PID. Bacteria wengine wanaweza kuambukizwa wakati wa tendo la ngono au wakati wa kujifungua, au kwenye kitendo cha utoaji mimba na kisha wakajificha kwenye njia ya uzazi wakaanza kukua taratibu na kusambaa. Baadhi ya bacteria ambao wamegundulia kusababisha PID ni hawa wafuatao

  • Chlamydia trachomatis
  • Neisseria gonorrheae
  • Mycoplasma genitalium

Mazingira Na Sababu Hatarishi Zinaongeza Uwezekano Wa Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID)

  • Kundi la wanawake wenye umri kati ya miaka 25 mpaka 35
  • Kufanya ngono bila kinga
  • Wanawake waliowahi kuugua PID huko nyuma ama kupata maambukizi mengine ya bacteria kwenye njia ya uzazi.
  • Kusafishwa kizazi mara kwa mara na matumizi ya kemikali kujisafisha ukeni, kitendo ambacho kinaharibu bacteria wazuri na kusababisha ukuaji wa bacteria wabaya na fangus
  • Matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kupanga uzazi
  • Kuugua UTI mara kwa mara, na wanawake waliwahi kutoa mimba wapo kwenye hatari zaidi ya kupata PID
  • Uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya.
Hatua 4 Zifuatazo Zitakusaidia  Kuzuia Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID) Na Magonjwa Ya Zinaa
  1. Fanya ngono salama kwa kutumia kinga na kuishi na mpenzi mmoja mwaminifu.
    Hii ni hatua muhimu ya kwanza na ya uhakika zaidi katika kuzuia kupata PID. Kama ukichagua kuwa na wapenzi wengi basi hakikisha unavaa condom kwa kila tendo. Kama una mpenzi mmoja na kati yenu kuna ambaye kaugua basi hakikisheni mnaacha kufanya ngono mpaka pale mtakapotibiwa mkapona kabisa.
  2. Hakikisha unafanya vipimo kwa magonjwa ya zinaa na kuyatibu haraka iwezekanavyo
    Wataalamu wa afya wanashauri kwamba watu walioko chini ya miaka ishirini na tano wafanye vipimo kila mwaka kwa magonjwa ya zinaa kama chlamydia. Wanawake wenye wapenzi wengi wanatakiwa kuonana na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake(gynecologist) kwa vipimo kugundua uwepo wa vimelea vya magonjwa ya zinaa. Ni muhimu kufanya vipimo mapema na kutibu mapema ugonjwa, kwa maneno mazuri ni kwamba kadiri unavochelewa kutibu magonjwa ya zinaa ndivyo unaongeza hatari zaidi ya kupata athari kubwa kwenye uzazi.
  3. Jikinge na maradhi ya bacteria na maambukizi mengine

Baadhi ya njia unazoweza kutumika kuzuia kutokea kwa maambukizi ni

  • Tumia sabuni zisizo na harufu kali(mild soap) kujisafisha- kuosha uke kwa kutumia sabuni zenye harufu kali na kemikali hufanya tishu za uke kututumka, kuharibu uwiano wa bacteria kenye uke na pia kupunguza tindikali iliyopo mpaka kupelekea kuongezeka kwa uchafu unaotolewa
  • Ukiwa kwenye hedhi tumia pedi zisizo na kemikali, pedi za asili zisizo na harufu kali. Hii itasaidia kuzuia ukuaji wa bacteria kwenye uke.
  • Hakikisha unaimarisha kinga yako ya mwili : unapokuwa na kinga imara basi unajikinga dhidi ya kushambuliwa na magonjwa ya zinaa. Unaweza kutembelea stoo yetu kwa kubonyeza hapa ili upate virutubisho vya kuimarisha kinga yako.
  1. Epuka kujisafisha mara kwa mara ukeni. Kujisafisha kupita kiasi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bacteria kwenye uke(normal flora). Baadhi ya wanawake wanadhani kujisafisha sana husaidia kuondoa mambukizi, lakini ukweli ni kwamba uke umeumbw na uwezo wa kujisafisha wenyewe. Kwahiyo unapotumia kemikali na spray kujisafisha unaua bacteria wazuri na kuongeza athari na ahatari ya kupata maambukizi.

Zingatia haya

Endapo utagundua kwamba unapata dalili za magonjwa ya zinaa kama tulivoelekeza hapo juu mfano maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu wakati wa kujamiiana, maumivu wakati wa kukojoa, hedhi kuvurugika, mamumivu makali wakati wa hedhi, na mengine, basi hakikisha unamuona Dactari mapema kwa ajili ya vipimo. Kama unashiriki ngono na mwenzi wako pia inashauriwa wote mpate vipimo na kutibiwa vizuri.

Muhimu kwa Wagonjwa wa PID

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, maambukizi ya bacteria na hedhi kuvurugika. Tunashauri atumie uterus cleansing pill pamoja na Lukol kusafisha kizazi na kutibu maambukizi. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama , harufu mbaya ukeni, muwasho, fangasi, PID na maambukizi ya bakteria. Na Lukol ipo kwenye mfumo wa vidonge 60 vya kumeza kwa week mbili.

Vidonge vya ucp vinatumika kwa wiki moja. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24,unaweka tena kidonge kingine. Na dawa ingine ya lukol unatumia kwa kumeza 2×2 kwa week mbili.

Gharama ni Tsh 125,000/= kwa dawa zote mbili.

Kumbuka haya kabla ya kutumia UCP

UCP haifai kutumiwa na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi na pia ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata Tiba

Share and Enjoy !

Shares
Shares