Goiter

Umewahi kuugua goiter au kumfahamu mtu mwenye goiter? Kama bado basi dalili mojawapo inayojionesha ni uvimbe mkubwa kwenye sehemu ya mbele ya shingo kwa kiswahili tunaita rovu. Uvimbe huu unaweza kuwa wa size tofauti tofauti na inaweza kumpata mtu wa rika lolote, kuanzia watoto mpaka wazee.

Japo kama wewe ni mwanamke una miaka zaidi ya 40 basi kwa bahati mbaya una hatari kubwa ya kuugua Goiter.
Kuna aina nyingi za ugonjwa wa Goiter lakini kwa ujumla ni ile hali ya uvimbe kwenye shingo kutokana na kukua kwa tezi ya thairodi.

Goiter kwa watu baadhi inaweza kuisha yenyewe pasipo uhitaji wa dawa lakini kuna kipindi inaweza kuwa ni tatizo sugu linaloashiria kuna shida kubwa kwenye tezi za Thairodi. Kazi ya tezi za Thairodi ni kuzalisha homoni ama vichocheo kwa ajili ya shughuli za kimwili. Sasa inapotokea uzalishaji ni mdogo ama uzalishaji ni miubwa kupita kiasi ama kuna upungufu wa madini ya iodine ndipo tatizo la Goiter huanza.

ugonjwa wa goiter

Goiter Ni Nini

Bilashaka utakuwa umepata maelezo ya awali pale juu kuhusu goiter lakini tuendelee kuchimba zaidi tupate maana zaidi ya goiter. Taasisi ya Thairodi ya nchini Marekani inaeleza goiter kama ‘ukuaji usio kawaida wa tezi ya thairodi. Hali inayotokea baada ya uzalishaji wa homoni kwenye tezi kuongezeka kupita kiasi (hypothyroidism) ama kuwa chini kupita kiasi (hyperthyroidsm) ama mwili umepungukiwa madini ya Iodine.

Nini maana ya tezi ya Thairodi na ipi kazi yake? Tezi ya thairodi ni kiungo chenye umbo la kipepeo-angalia picha hapa chini.

Tezi ya thairodi

Kiungo hichi kipo kwenye shingo chini ya koromeo la sauti. kazi kuu ya Tezi hii ni kuzalisha homoni za triiodothronine (T3) na thyroxine (T4), ambazo kw apamoja hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu na kazi mbalimbali za mwili. Goiter hotokea endapo T3 na T4 ni kidogo sana ama ni nyingi kupita kiasi.

Dalili za Goiter

  • Kupanuka kwa tezi ya thairodi ambay huonekana kama uvimbeuliotuna kwenye shingo
  • Kujiskia hali ya kukaza kwenye koo
  • Kupata ugumu kwenye kumeza kikohozi
  • kupata ugumu kwenye kupumua sauti kuwa rafu na kukwangua

Kwa wagonjwa wachache goiter inaweza kuweka presha kubwa kwenye koo la chakula na hewa na hivo kuleta ugumu kwenye kupumua na kumeza chakula hasa vyakula vigumu, wakati mwingine huleta maumivu makali.

Zifuatazo Nni Tabia Na Mazingira Hatarishi Yanayoongeza Hatari Ya Kupata Goiter.

  • Upungufu wa madini ya iodine kwenye lishe.
  • Wanawake wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanaume
  • Umri: hatari ya kupata goiter inaongezeka kwa wenye umri wa kuanzia miaka 40.
  • Historia ya mgonjwa- kama familia yako ina historia ya magonjwa ya Autoimmune (magonjwa ya kinga kushambulia tishu za mwili)
    wajawazito na wanawake waliokoma hedhi
  • Matumizi ya baadhi ya dawa kama dawa za virusi, na magonjwa ya moyo huongeza hatari ya kuugua goiter
  • Mionzi: hatari ya kuugua inaongezeka kama uliwahi kufanyiwa tiba kupitia mionzi kwenye shingo ama eneo la kifua.

Goiter Inatokeaje

Kwa ujumla goiter hufanyika pale tezi ya thairodi inaposhindwa kutengeneza homoni za kutosha kukidhi mahitaji ya mwili. Kutokana na upungufu huu tezi ya thairodi inatumia nguvu kubwa kujaribu kufidia uhitaji huu wa homoni kwenye mwili kwa kukua zaidi na zaidi.

Aina ya pili ya goiter ambayo huwatokea watu wengi zaidi ni kutokana na upungufu wa madini ya iodine. Pale panapotokea upungufu wa iodine basi tezi yako ya thairodi huvimba na kutuna ili kufyonza kwa kasi zaidi kiasi cha iodine na kufidia upungufu huu. Tatizo hili lilipoanza kuwa kubwa ndipo utengenezaji wa chumvi zenye madini ya iodone ukaanza.

Tiba Ya Kisasa Ya Goiter

Matibabu ya hospitali kwa goiter hutegemea na dalili anazozipata mgonjwa, ukubwa wa uvimbe wake na kisababishi. Daktari anaweza kuweka muda wa uangalizi kama uvimbe wako ni mdogo sana na tezi yako ya thairodi inafanya kazi vizuri kabisa, hivo uvimbe wa namna hii unaweza kupotea baada ya muda mfupi.

Tiba ya hormone replacement therapy: ni tiba maarufu sana kwa goiter iliyosababishwa na ufanyaji kazi mkubwa kupita kiasi au ufanyaji kazi mdogo wa tezi ya thairodi.

Radioactive iodine: Mgonjwa hupatiwa madini ya iodine kwa mdomo, madini haya yanaenda kuvunjavunja seli za tezi na kuzipunguza.
upasuaji wa kutoa sehemu ya tezi au yote, hii ni pale goiter yako inapokua kubwa mpaka kukufanya kushindwa kupumua. Baada ya kufanywa upasuaji mgonjwa atahitaji kutumia homoni za kutengenezwa maabara kila siku kwa maisha yote. Kwa uvimbe mkubwa sana, madaktari wanaweza kuchukua kiasi kidogo cha nyama kwenye uvimbe wa goiter ili kuchunguza kama kuna saratani.

Tiba Asili Kwa Tatizo La Goiter

  1.  Iodine
    kundi kubwa la watu wanaweza kuwa hawatumii kiwango stahiki cha madini ya iodine. kwa watu wengi chanzo kikuu cha madini ya iodine ni kwenye chumvi ya dukani, huku kwa bahati mbaya ni kwamba chumvi nyingi zinazotengenezwa viwandani hazina kiwango cha kutosha cha madini ya iodine. Matumizi ya vyakula vyenye iodine kwa wingi ni silaha kubwa ya kuepuka tatizo hili. baadhi ya vyakula vyenye iodine kwa wingi ni kama yogurt, mayai, samaki na nyanya.
  2. Kula mlo wenye virutubisho na madini mengi.
    ukosefu wa madini a Zinc, manganese na vitamin A, inaelezwa kuwa na mchango kwenye goiter, pamoja na upungufu wa protini. Upungufu wa virutubishi hivi hupelekea mwili kushindwa kuvyonza iodine nyingi kutoka kwenye chakula. Tembelea stoo yetu kupata huduma hii ya virutubisho vya madini
  3. Kama chanzo cha goiter ni kushuka kwa ufanisi tezi ya thairodi (hypothyroidsm): Hypothyroidsm ini kushuka kwa uzalishaji wa homoni kwenye tezi ya thyrodi. kama hiki nicho chanzo chako cha kupata goiter basi unaweza kurekebisha haya kwenye chakula kwa kutumia kwa wingi vyakula vifuatavyo
    • Mafuta ya nazi na nazi
    • Vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi
    • Supu ya mifupa
    • Maji safi na salama ya kunywa
    • Matunda na mboga za majani

Kwa upande mwingine hivi ni vyakula vya kuepuka kula

  • Vyakula vya sukari
  • Vyakula vya ngano
  • Bidhaa za maziwa na maziwa yaliyochakatwa sana kiwandani
  • Unga uliosafishwa kupita kiasi kiwandani

4. Kama Tezi yako ya thairodi inafanya kazi kupita kiasi (Hyperthyroidsm)
Vyakula hivi ni muhimu kutumia.

  • Juisi ya kijani: juisi ya mbogamboga
    kama kale, spinach zina virutubishi vingi sana, hakikisha unaosha mboga kwa vinegar na maji kabla hujaweka kwenye blender yako kutengeneza juisi.
  • Vyakula asili visivyokobolewa: pendelea zaidi kula vyakula asili ambavyo havipitia kiwandani
  • Tangawizi: husaidia kuimarisha kinga ya mwili
    Supu ya mifupa: supu ya mifupa inaharakisha utoaji sumu mwilini, na kutibu magonjwa ya tumbo kiwemo leaky gut

Tahadhari za kuchukua kwa Wagonjwa wa Goiter

Muda wowote unapoona kuna dalili za goiter kwenye shingo basi hakikisha unafika hospitali kupata huduma ya matibabu haraka. Uvimbe unaweza kuashiria uwepo wa matatizo mengine kama kuvuja kwa ndani ya mwili, athari kwenye kinga ya mwili ama uwepo wa saratani kwenye shingo.

Share and Enjoy !

Shares
Shares