Kizazi kuinama (retroveted uterus)

Kizazi kuinama.

Je umewahi kusikia kuhusu kizazi kuinama?, pengine ndugu , rafiki ama mke wako amefanyiwa vipimo na kugundulika kwamba kizazi chaje kimeinama. Leo nitakupa tafsiri nzuri ya kuinama kwa kizazi na jinsi gani inavoathiri afya ya uzazi kwa mwanamke.

Kuinama kwa kizazi kwa majina mengine ya kitaalamu tunaweza kuita tilted uterus,retroflexed uterus, retroveted uterus au backward uterus ni namna mfuko wa mimba unapovutika kuelekea nyuma zaidi ya mlango wa kizazi badala ya kuvutika kuelekea mbele.

Ili uweze kunielewa vizuri angalia picha hapa chini. Picha ya kushoto inaonesha kizazi (uterus) cha kawaida na kinaonekana kimepinda kuelekea upande wa mlango wa kizazi. Picha ya kulia ndio inaonesha kizazi kuinama kuelekea nyuma zaidi.

kizazi kuinama

Dalili Anazopata Mwanamke Mwenye Kizazi Kilichoinama

Kumbuka siyo lazima kupata dalili zote kwa pamoja. Kama unapata dalili zisizo za kawaida ni vizuri kufika hospitali ili kufanya vipimo ukaanza tiba mapema. Sasa baada ya kuona dalili tuangalie uhusiano kati ya kizazi kuinama na afya ya uzazi.

Nini Kinasababisha Kizazi kuinama?

Mfuko wa mimba ambacho ndio kizazi tunachozungumzia ni sehemu tupu ambayo inajiweka katika eneo la chini ya nyonga za mwanamke. Kazi yake ni kuhifadhi kichanga baada ya urutubishaji kufanyika. Kizazi cha mwanamke kinaweza kuinama kutokana na sababu mbalimbali kama

  • Kulegea kwa misuli ya nyonga: Mwanamke akishafikia kukoma hedhi au baada ya kujifungua, misuli inayosapoti tumbo la uzazi hulegea na hivo kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma kama picha pale juu inavooensha.
  • Kupanuka kwa kizazi kutokana na ujauzito, ama vimbe mbalimbali kama fibroids au vimbe ambazo ni saratani (tumor) zinaweza kusababisha kuinama kwa kizazi.
  • Makovu ama msuguano kwenye nyonga
    Mfuko wa mimba ama kizazi kinaweza kupata makovu kutokana na hali mbalimbali mfano , maambukizi kama PID, uvimbe(endometriosis) ama makovu kutokana na upasuaji uliowahi kufanyiwa kwa kipindi cha nyuma. Makovu haya yanaweza kufanya kizazi kuvutika kuelekea nyuma na kuinama.

Kizazi Kuinama na Uwezo wa Kushika Ujauzito.

Kuinama kwa kizazi inaweza kupelekea ugumu wa kushika ujauzito Lakini athari hii siyo ya moja kwa moja. Madaktari wanatakiwa kuhakikisha hakuna sababu ingine inayopelekea usishike ujauzito ndipo hii iwe sababu ya mwisho. Kuwa na kizazi kilichoinama siyo sababu ya mimba kutokukua vizuri, bali kuwa na ujauzito yaweza kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma.

Kizazi Kuinama na Tendo la Ndoa

Maumivu wakati wa tendo la ndoa ni tatizo linaloondoa furaha kwa wanawake. Bado hakuna sababu ya moja kwa moja inayopelekea maumivu haya kwa wanawake wenye kizazi kilichoinama. Japo baadhi ya nadharia zinasema kwamba maumivu yanaweza kutokana na namna uume unavoingia na kukandamiza mlango wa kizazi.

Tishu laini zinazosapoti kizazi zinaweza kutenguliwa na hivo kupelekea maumivu wakati wa tendo. Ni muhimu kwa wapenzi kuzungumza kuhusu staili gani ya kufanya tendo ambayo haimuumizi mwanamke.

Vipimo Kugundua kama Kizazi chako Kimeinama.

Pelvic examination husaidia kugundua kizazi kilichoinama. Daktari ataingiza vidole viwili kwenye uke, kisha mkono mwingine kuweka kwenye tumbo na kusuka taratibu kuelekea kwenye vidole vya ndani ili kuupata mfuko wa mimba, hii itasaidia kujua shape, size na uelekeo wa kizazi.

Wanawake wanaoapata maumivu wakati wa tendo la ndoa na dalili zingine za kizazi kuinama kama nilivoorodhesha pale juu wanatakiwa kumwona daktari haraka. Dallili hizi zinaweza kuashiria pia tatizo lingine baya la kiafya, ndiomaana kuna umuhimu wa kugundua mapema ili uanze kutibu mapema.

Tiba Kupitia Mazoezi

Wakati mwingine daktari wako anaweza kubadili ukaaji wa kizazi bila kufanyiwa upasuaji. Kwa maana hiyo utajitaji kufuata utaratibu wa mazoezi ambayo hulenga kukaza misuli inayoshikilia kizazi. Mfano wa mazoezi hayo ni Kegels. Mazoezi mengine yanajumuisha

Knee chest

pelvic exercise

Lala kwenye sakafu (unaweza kutanguliza kipande cha nguo). Mikono ikiwa imeshika kichwa, kunja goti mpaka ikaribie kugusana na kifua, fanya kama picha inaoeleza hapa chini. Tulia katika hali hiyo kwa sekunde 20 mpaka 30 kisha pumzika. Rudia zoezi husika mara 10 mapak 15 kwa kubadilisha miguu

Pelvic contractions

Mazoezi haya yanalenga kuimarisha misuli ya nyonga nakukaza misuli ya uke. Jinsi ya kufanya zoezi hili lala kwenye floor huku mikono yako ikiwa imenyooka kuelekea kwenye miguu. Taratibu nyanyuka eneo la katikati na makalio kuelekea juu kama picha inavoonesha hapa chini. Tulia hivo hivo kwa sekende 30 kisha pumzika, rudia zoezi hili mara 10 mpaka 15 kwa ssoma iku.

Share and Enjoy !

Shares
Shares