Nini kinapelekea kuharisha?

kuharisha
kuharisha

Kuharisha ni moja ya matatizo makubwa ya mfumo wa chakula ambapo mgonjwa hutoa kinyesi chenye maji mengi zaidi kuliko kawaida. Kama wewe au mtoto wako unapatwa na tatizo hili basi naamni kabisa swali la kwanza ambalo utajiuliza ni jinsi gani uweze kutibu tatizo hili na ufunge kuharisha kwa haraka.

Aina za kuhara

Kuharisha kumegawanyika katika aina mbili, acute diarrhea na chronic diarrhea. Acute diarrhea ni kuharisha kwa kawaida inaweza kuchukua wiki moja ama wiki mbili ikaisha. Chronic diarrhea huchukua zaidi ya week mbili ni ni hatari zaidi.

Habari njema ni kwamba kuharisha kwa muda mfupi ni kinga moja nzuri sana dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kiafya. Japo inaleta usumbufu sana lakini ni kitu rafiki wa afya yako. Kuharisha kwa muda mfupi kunasaidia kutoa uchafu kwenye mfumo wa chakula ambavyo vingeleta maradhi kwa hapo baadae.

Kuharisha kusiko kawaida

Kwa upande wa pili dalili za kuharisha kusiko kawaida yaaani chronic diarrhea huwa tofauti sana na ile ya kawaida. Dallili hizi zinaweza kuja na kuondoka kulingana mwenendo wa lishe yako na mtindo wa maisha.

Tunaposema mwenendo wa maisha tuanamaanisha jinsi gani unadeal na vitu kama msongo wa mawazo na hali ya kinga ya mwili. Tafiti zinasema kwamba asilimia 3 ya watu wanougua kuharisha kusiko kawaida ni wale wanaosafiri zaidi kuelekea kwenye nchi zinazoendelea.

Kuharisha kwa muda mfupi (acute diarrhea) kunaweza kutibika kwa haraka bila kutumia vidonge.

Nini husababisha kuharisha

Kuharisha ni matokeo ya mwili kukataa kitu kibaya kilichoingia ndani ya mwili. Vitu hivi vinaweza kuwa ni sumu, au athari za ugonjwa fulani kwenye mfumo wako wa chakula. Baadhi ya vimelea vinavyosababisha kuharisha ni kama virusi na bacteria.

Moja ya hatari inayotokana na kuharisha ni kwamba inakufanya kuishiwa maji mengi na kupata homa kali. Hii ni kwasababu kuharisha kunapoteza madini mengi ikiwemo madini ya sodium kwenye mwili na maji .

Zifuatazo ni dalili za kuarisha

 • Kwenda choo zaidi ya mara 4 kwa siku
 • Kupata kinyesi chenye maji mengi
 • Maumivu ya tumbo na wakati mwingine tumbo kujaa na kuhisi umeshiba mda mwingi
 • Kupata kizunguzungu na kutapika
 • Kukosa hamu ya kula na wakati mwingine ama kupata shida kula chakula cha kutosha.
 • Kuongezeka kwa kiu kutokana na kupoteza maji mengi
 • Mwili kuwa mchovu na akili kutofanya kazi vizuri

Unapolenga kutibu tatizo la kuharisha na kuzuia kuharisha kusiko kawaida kwa baadae inabidi kuangalia chanzo cha tatizo. Kuharisha kunaweza kuwa kwa namna nyingi, mfano kuharisha kutokana na mwili kukosa maji mengi, au athari ya ugonjwa ama sumu kwenye chakula. Watoto na wazee wanaweza kupata kuharisha  kutokana na mwili kushindwa kuchakata baadhi ya vyakula, msongo wa mawazo na  kutokunywa  maji ya kutosha.

Mazingira na tabia hatarishi zinazopelekea mtu kuharisha.

 • Maambukizi ya bacteria: Maambukizi haya yanaweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka kwenye chakula kilichoathirika.
 • Alegi ya vyakula mbalimbali kama maziwa. Baadhi ya watu hawana uwezo wa kumeng’enya sukari aina ya lactose ambayo inapatikana kwenye maziwa.
 • Kunywa maji yenye bacteria ama vimelea vya ugonjwa
 • Kula chakula chenye sumu au vimelea wa aina fulani
 • Kuishiwa maji kwenye mwili kwa mtu kutokunywa maji ya kutosha au kutapika
 • Mwili kushindwa kumeng’enya chakula vizuri
 • Kula kupita kiasi na unywaji wa viywaji vingi
 • Kula zaidi matunda yasioiva au yalioiva kupita kiasi
 • Matumizi makubwa ya vyakula vyenye grisi au utonvu mwingi na kupelekea kushindwa kuchakatwa tumboni
 • Matumizi makubwa ya pombe na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa ambavyo hunyonya sana maji mwilini
 • Matumizi ya vidonge vya kupunguza acid tumbo(anticids) hupelekea choo kuwa kilaini kupita kiasi.

Nini husababisha kuharisha kwa watoto na vichanga?

 • Alegi au mzio kwa vyakula mfano mayai, maziwa, na karanga. Unaweza kusoma zaidi makala ya alegi kwa kubonyeza hapa
 • Kuharisha kutokana na mwili wa mtoto kukataa maziwa baada ya mama kula aina fulani ya chakula.
 • Mtoto kutokunywa maji ya kutosha au kunyweshwa kupita kiasi vinywaji vya majimaji mfano juisi na maziwa
 • Maambukizi ya bacteria kutokana na mtoto kugusa maeneo machafu, na
 • Matumizi ya dawa kwa mtoto ambayo hupelekea kuvurugika kwa mazingira ya tumboni yanayopelekea kubadilika kwa mfumo wa usagaji chakula.

Kumbuka kwamba ni kawaida kwa watoto kuwa na choo kilaini kuliko mtu mzima. Ongea na daktari wako kama utaona hali ya tofauti kama

 • kupata choo mara kwa mara,
 • mtoto kulia bila machozi,
 • mdomo kuwa mkavu,
 • macho kuingia ndani zaidi na kuishiwa maji,
 • harufu isiyo ya kawaida kwenye choo, homa,
 • kupoteza hamu ya kula na pia
 • kama ukiona damu kwenye kinyesi.

Jinsi ya kuzuia kuharisha.

Hatua tatu za kuzuia kuharisha ukiwa nyumbani kwako.

 1. Hatua ya kwanza kula vyakula laini ambavyo ni rahisi kuchakatwa na mwili, vyakula gani unakula ukiwa unaharisha? Ifuatayo ni list ya vyakula kwa mgonjwa wa kuhara.
  • Kula chakula kidogo: kadiri unavyokula chakula kingi zaidi ndipo inakuwa ngumu kwa mwili kusaga na kuchakata chakula tumboni. Kwa hiyo unapokuwa unaharisha kula kiasi kidogo cha chakula ili kurahisisha mfumumo wa chakula kusaga chakula haraka
  • Kula vyakula kama ndizi, epo, na nafaka ambazo hazijakobolewa , vyakula hivi husagawa haraka tumboni na vitakupatia vyuzinyuzi au kambakamba za kutosha.
  • Matunda na mboga za majani kwa wingi: hivi huchangia nyuzinyuzi au fibers na maji
  • Asali mbichi na tangawizi- tumia mchanganyiko wa asali na tangawizi kwenye maji ya moto kwenye kikombe husaidia kutuliza kuharisha .kwa upande wa pili hivi ni vyakula ambavyo hutakiwi kutumia wakati unaharisha
   • Maziwa yaliyosindikwa: maziwa haya yaweza kushindwa kuchakatwa na tumbo na hivo kuongeza kuharisha
   • Vyakula vyovyote vinavyoleta mzio au alegi hutakiwi kuvitumia
   • Vyakula vya mafuta vilivyosindikwa na kuhifadhiwa
   • Pombe na vinywaji vyenye caffeine
   • Vyakula vyenye sukari kwa wingi hasa iliyoongezwa kiwandani
 1. Mbili: Hakikisha unakunywa maji ya kutosha:
  kunywa maji mengi ni kitu cha lazima kutokana na kwamba maji mengi hupotea pale unapoharisha. Hii itakusaidia pia kupunguza zile athari zinazotokana na kuharisha kama uchovu,. Chai tiba kama vile, kuding tea na  chai ya tangawizi ni nzuri zaidi, husaidia kusafisha tumbo lako.
 2. Hatua ya tatu: pata mda mwingi wa kupumzika: Unapokuwa na tatizo la kuhara basi hakikisha unapumzika zaidi na kupunguza kazi ngumu kama mazoezi

Namna ya kuzuia kuharisha kwa mtoto mdogo

Watoto wadogo kama tulivoona wapo hatarini zaidi kupatwa na tatizo hili la kuhara kutokana na alegi ma kuumwa kiurahisi. Maana kinga yao ya mwili inakuwa bado haijakomaa.

Inakadiriwa kwamba silimia 3 ya watoto wana alegi ya protein ambayo hupatikana kwenye maziwa. Wengine hupata alegi kwa protini ambayo huongezwa kwenye formula za vyakula vya viwandani.

Utagundua kuwa mwanao ama alegi na protini kama utaona kuharisha kunakoambatana na kutapika na kupata malengelenge kwenye Ngozi. Unaweza kujaribu njia hizi kwa mtoto anayeharisha ili kuzuia hali hiyo.

Bofya kusoma kuhusu: kubanwa kifua na kukosa pumzi

Share and Enjoy !

Shares
Shares