Muwasho Ukeni Baada ya Tendo la Ndoa.

muwasho ukeni
muwasho ukeni

Muwasho ukeni baada ya tendo la ndoa yaweza kukutokea katika kipindi flani wakati unashiriki tendo. Kupungua kwa ute unaolainisha uke kunaweza kusababisha msuguano na hivo kuleta muwasho . Kama hii ndio sababu basi unaweza kupumzika kufanya ngono wa muda kidogo kisha ukaendelea tena.

Je Shahawa Zinaweza Kuleta Muwasho Ukeni baada ya Tendo la Ndoa?

Aleji kwa mbegu za kiume ni tatizo linalotokea mara chache zaidi kwa kitaalamu huitwa seminal plasma hypersensitivity. Unaweza kupatwa na aleji pale unapofanya tendo la ndoa kwa mara ya kwanza, lakini pia inaweza kutokea unapofanya mapenzi na watu tofauti tofauti.
Sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo uke, mdomo na ngozi zinaweza kuathirika endapo zikigusana na mbegu za kiume. Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia dakika 10 ama nusu saa baada ya kugusana na mbegu. Dalili hizi ni kama

 • Muwasho
 • Ngozi kuwa nyekundu
 • Kuvimba
 • Maumivu na
 • Hali ya kuunguza

Ili kujua kama una aleji ya mbegu za kiume, jaribu kutumia condoms.

Ukavu kwenye Uke.

Ukavu kwenye uke ni sababu mojawapo ya kuletekeza muwasho baada ya tendo. Hali hii hutokea baada ya kupungua kwa majimaji yanayozalishwa na tezi kulainisha uke. Baadhi ya wanawake hutokea kuwa na uke mkavu. Matumizi ya sabuni na kemikali kuosha ukeni inaweza pia kusababisha ukavu.
Sababu kubwa inayofanya uke kuwa mkavu ni mabadiliko ya homoni yanayotokea hasa pale mwanamke anapojifungua, au baada ya kukoma hedhi.
Vitu vingine vinavyosababisha ukavu ukeni ni pamoja na

 • Mwanamke kutoandaliwa vizuri kabla ya tendo la ndoa
 • Matumizi ya baadhi ya dawa mfano vidonge vya kupanga uzazi, na vile vya kupunguza msongo wa mawazo
 • Pafyumu na sabuni
 • Baadhi ya magonjwa kama kisukari
 • Upasuaji wa kuondoa mifuko ya mayai

Kuvurugika kwa Mazingira ya Uke.

Tindikali ndani ya uke inatengeneza ulinzi dhidi ya fangasi na bakteria. Mabadiliko ya kiwango cha tindikali kwenye uke yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu mwingi kupita kiasi na pia maambukizi ya mara kwa mara. Dalili zingine kuonesha kuvurugika kwa mazingira ya uke ni pamoja na
Kupata harufu kali ukeni mfano wa harufu ya samaki
Hali ya kuungua wakati wa kukojoa.

Vitu vifuatanyo vinaweza kuvuruga mazingira ya uke

 • Kuflash uke mara kwa mara (douching)
 • Matumizi ya dawa hasa antibiotics amabzo zinaweza kuua pia bacteria wazuri.

Maambukizi

Maambukizi ukeni kama fangasi, na bakteria huletekeza muwasho kwenye uke. Maambukizi ya bakteria ukeni husababisha dalili zifuatazo.
Kubadilika kwa rangi na kiwango cha uchafu unaotoka ukeni
Maumivu na kujiskia hali ya kuungua wakati wa kukojoa
Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
Kutokwa damu kwenye siku zisizokuwa za hedhi na
Homa

Magonjwa ya Ngono (Sexual Transmmited Diseases)

Kuna magonjwa mengi ya kuambukiza kupitia njia ya ngono ambayo yanaweza kuletekeza muwasho ukeni kama

 • Trichomaniasis
 • Chlamydia
 • Gonorrrhea na
 • Genital Warts

Hakikisha unamwona daktari kama muwasho utaendelea kwa muda mrefu.

Chati nasi kwa whatsapp namba 0678626254 kupata ushauri na tiba

Share and Enjoy !

Shares
Shares