kukoma hedhi (menopause), elimu na virutubisho.

 
mawazo ya kukoma hedhi

Kukoma hedhi au kwa kitaalamu menopause ni hali ya kawaida inayomtokea kila mwanamke. inatokea pale kupata hedhi kunapofikia kikomo na hivo uwezo wa kupata mimba au ujauzito kushuka na kukoma kabisa. Hatua hii hutokea pale mwanamke anapofikisha umri wa miaka 50 na kuendelea.

Kwa wanawake wengine hali hii hutokea pia kabla ya hapo kuanzia miaka 40. Na inaweza kutokea kutokana na ushauri wa madactari ama kufanyiwa upasuaji mdogo. Mfano mifuko ya mayai(ovaries) na mfuko wa mimba (uterus) inapoondolewa  kutokana na athari ya magonjwa mbalimbali kama saratani.

Pale mwanamke anapofikia umri wa kukoma hedhi basi huanza kuona dalili zifuatazo

  • Joto kupanda mara kwa mara na kupata jasho jingi
  • Ukavu kwenye uke
  • Kubadilika badilika kwa mpangilio wa hedhi
  • Kuongezeka uzito na
  • Msongo wa mawazo na kubadilika kwa mood yako.

Kuna njia nyingi za namna ya kupambana na dalili mbaya za kukoma hedhi. Kuna njia za mda mrefu na njia za mda mfupi. Njia nzuri na kuepusha madhara yanayotokana na  kukoma hedhi ni kuekebisha lishe yako na kufanya mazoezi ya viungo. Kwa kuzingatia lishe waliyokula mababu zetu hapo zamani basi utapunguza madhara ya kukoma hedhi kama kuongezeka uzito na kutokwa na jasho jingi hasa kipindi cha usiku.

Tambua kwamba Menopasue/kukoma hedhi siyo ugonjwa

Kama tulivoona hapo juu pale mwili wa mwanamke unapokoma kutengeneza homoni za estrogen na progesterone ndipo hedhi yako itakoma. Wanasayansi huenda mbali zaidi na kuwaanzishia wahanga wa tatizo hili program ya kurudisha homoni hizi kwa kuwawekea homoni zilizotengenezwa maabara.

Kitendo hiki hufahamika zaidi kama hormone replacement therapy. Njia hii inatazama ishu ya kukoma hedhi kama ugonjwa wakati ni suala la kawaida kabisa linalomkuta kila mwanamke. Ukweli ni kwamba kitu chochote kilichotengenezwa kwa mkono wa binadamu hakitafanya kazi sawa na kitu kilitengenezwa halisi kwa ajili ya kazi fulani kwenye mwili. Ndio maana madhara ya kuwekewa homoni hizi ni makubwa zaidi.

Zifuatazo njia za asili unazoweza kutumia ili upunguze adha zinazotokana na kukoma hedhi.

Kwanza kabisa kama huna uhakika kama umeingia katika kipindi cha kukoma hedhi nenda hospitali. Mwambie daktari wako akufanyie kipimo cha FSH, kifupi cha follicle stimulating hormone. Kipimo hichi kinagundua iwapo tezi ya pituitary inaonesha kama ovari zako hazifanyi kazi inavotakiwa na hivo kuna uzalishaji mkubwa wa FSH.

Kama uliwahi kufanyiwa upasuaji wa kufunga kizazi basi huna haja ya kufanya hiki kipimo. Kwa sababu tayari wewe umeshakoma hedhi na uzalishaji wa FSH utakuwa juu zaidi. Pale FSH inapokuwa nyingi basi kuna uhakika mkubwa kwamba tayari umeanza kukoma hedhi. Kisha baada ya hapo utaingia kipindi cha post-menopause. Ni pale ambapo utakoma kupata hedhi mfululizo kwa mwaka mzima.

Kumbuka mwanzo tumesema menopause siyo ugonjwa na kitu cha kawaida, lakini matokeo yake unaweza kuyabadili kwa kurekebisha lishe na mtindo wako wa maisha na ukafurahia Maisha yako.

Tumia virutubisho/supliments kama

Virutubisho vya mafuta ya samaki(fish oil) yenye Omega 3 , vyenye ubora wa hali ya juu, kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.

Zinc supliments

Kwa wanawake, Madini ya Zinc yanahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri.

Soy power

Vidonge hivi vilivyotengenezwa kiasili kwa kutumia viambata vya mimea ya Glycine, Radiz Paeoniae Alba Eztractum na Ganoderma husaidia: kuongeza ufanyaji kazi wa mfuko wa mayai (ovaries), kuzuia Saratani ya matiti na kuimarisha afya ya mifupa kwa wanawake waliokoma hedhi.(menopause).

2.Hakikisha mlo wako unakuwa na kiasi sawa cha vyakula vya mafuta yale mazuri, kwa wingi ikifuatiwa na protini na kisha matumizi ya wanga na sukari kwa kiasi kidogo sana

3.Epuka matumizi ya vyakula na vinywaji vilivyosindikwa maana huongeza kiasi cha homoni ya estrogen.

4.Hakikisha unakuwa na ratiba nzuri ya kufanya mazoeziili kurekebisha kiwango cha insulin na hivo kusaidia kubalansi kiwango cha estrogen.

5.Pata vitamin D ya kutosha, miili yetu ina uwezo wakutengeneza vitamin D kutoka kwenye mwanga wa jua, hivo hakikisha kila siku unapata mwanga wa jua walau nusu saa mpaka saa 1 ili kuuwezesha mwili kutengeneza Vitamin D ya kutosha. Tafiti zinaonesha kuwa Vitamin D husaidia kupunguza athari za zinazotokana na kukoma hedhi kama kutokwa na jasho jingi usiku bial kumeza vidonge.

6.Kupunguza uzito husaidia kurekebisha na kupunguza athari za menopause kama kubadilika kwa joto la mwili: Tafiti zinasema kwamba wanawake wanaopunguza uzito ama walio kwenye program za kupunguza uzito wana uafadhali katibu 33% zaidi ya kupunguza athari za menopause kuliko wanawake wengine. Kutokana na kwamba swala la kupunguza uzito huchukua muda mrefu nashauri ujijengee tabia ya kurekisha uzito wako kabla hujafikia kipindi cha menopause.

Hitimisho

Ni matumaini yetu kwamba utaanza kurekebisha sasa mtindo wako wa maisha ikiwemo lishe , ili uweze kupunguza athari za kukoma hedhi. Kwa ushauri huduma ya virutubisho na maswali,

Wasiliana nasi kupata dawa ili kutibu maudhi ya kukosa hedhi kama maumivu kwenye tendo, ukavu ukeni na kukosa hamu ya tendo kwa gharama ya Tsh 150,000/= tu

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata dawa kwa Tsh 150,000/= tu

Share and Enjoy !

Shares
Shares