Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama Tendo la ndoa

Je ni Salama Kufanya Mapenzi kipindi cha Hedhi?

period

Kikawaida kipindi cha hedhi kinatokea mara moja ndani ya mwezi. Kama huna changamoto ingine ya kiafya, basi hakuna haja ya kuogopa kufanya mapenzi kwenye kipindi hiki. Japo panaweza kuwa na uchafu kutokana na damu inayotoka, lakini kiafya hakuna madhara na badala yake kuna faida kwa mwanamke. Soma zaidi kufahamu faida za kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke wakati wa hedhi.

Faida za Kufanya Tendo la Ndoa Kipindi cha Hedhi

  1. Kupungua kwa maumimu ya misuli ya tumbo na nyonga : Mwanamke anapofika kileleni kwa kutoshelezwa kimapenzi husaidia kupunguza maumivu kwenye nyonga na misuli. Kufika kileleni kunasaidia misuli kusinyaa na hivo kuondoa maumivu. Tendo la ndoa pia husaidia kutoa kichocheo na endorphims ambacho kinakufanya ujiskie vizuri.
  2. Kupunguza siku za hedhi Kufanya mapenzi kipindi cha hedhi kunaweza kusaidia kupunguza siku za kutokwa hedhi. Hii inawafaa zaidi wanaopata hedhi zaidi ya siku 4. Kutanuka kwa misuli ya kizazi kunasaidia kusukuma damu kwa wingi na haraka na hivo kufupisha siku za hedhi.
  3. Kuongezeka kwa hamu ya tendo Baadhi ya wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa wanaweza kutumia kipindi cha hedhi kufaidi tendo hili. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa hamu ya kufanya mapenzi kwenye kipindi cha hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni.
  4. Damu ya hedhi kama kilainishi Kipindi cha hedhi damu inayotoka inaweza kutumika kama kilainishi ili kupunguza maumivu.
  5. Kupunguza maumivu ya kichwa:Karibu nusu ya wanawake hupata maumivu ya kichwa kipindi cha hedhi. Kushiriki tendo kutakusaidia kupunguza maumivu haya.

Je kuna Madhara yoyote Kufanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi?

Kufanya mapenzi kipindi cha hedhi kunaweza kuleta madhara ya kawaida ya kimazingira, mfano kuchafua mashuka na mwili pia kutapakaa damu. Lakini pia unaweza kuathirika kisaikologia hasa kama wewe ni mwoga wa kuangalia damu. Hatari nyingine ni kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa na homa ya ini. Hii ni kwa sbabau virusi wanaishi kwenye damu. Kama unaamua kufanya mapenzi kipindi cha hedhi basi hakikisha unatumia kondomu.

Je Naweza Kupata Ujauzito Kufanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi?

Inawezekana kabisa kushika ujauzito wakati wa hedhi. Kwahivo kama hujapanga kushika mimba kumbuka kutumia kondomu muda wote. Kila mwanamke ana mzunguko tofauti wa hedhi, na pia mpangilio unaweza kubadilika ushike mimba kwenye kipindi ambacho hukupangilia. Wanawake wenye mzunguko mfupi wa siku 22 wapo kwenye hatari zaidi ya kushika mimba kipindi cha hedhi. Kumbuka mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ndani ya kizazi kwa siku 5 mpaka 7, kwaivo kama una mzunguko wa siku 22 na yai kutolewa baada ya hedhi, kuna uwezekano mimba ikatungwa.

Dondoo zingine Muhimu Unapofanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi.

  • Ongea na mpenzi wako jinsi unavojiskia unapofanya mapenzi kipindi hiki cha hedhi. Kuwa muwazi na mweleze kama hujiskii vizuri.
  • Tumia taulo nyeusi au kitambaa cha pamba cheusi kutandika kwenye godoro ili kufyonza damu.
  • Andaa kitambaa chenya maji au wipes pembeni ya kitanda ili kujisafisha baada ya kumaliza tendo
  • Ongea na mpenzi wako kuvaa kondomu kabla ya tendo kupunguza hatari ya kupata maambukizi.
  • Jaribu staili tofauti kufanya mapenzi ili kupata inayokufaa ambayo haisababishi maumivu.

Bofya makala inayofuata:Je naweza kushika mimba nikisex kwenye hedhi?

Share and Enjoy !

Shares
Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Dalili za Kukoma Hedhi(Menopause)

kukoma hedhi (menopause)
Menopause

Hatua 7 za Kupunguza Makali ya Menopause.

Kukoma hedhi au menopause huanza katika ya umri wa miaka 40 mpaka 50. Wakati wa kipindi hiki wanawake hupata dalili zisizo za kawaida ambazo hazikuwepo awali. Dalili hizi ni pamoja na joto la mwili kuongezeka, kupata jasho jingi hasa wakati wa usiku, kujiskia vibaya na uchovu, kukosa hamu ya tendo na maumivu wakati wa tendo.

Kwa kuongezea ni kwamba wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya mifupa kama kumomonyoka kwa mifupa, kuongezeka uzito, magonjwa ya moyo na kisukari.

Tambua kwamba Menopasue/kukoma hedhi siyo ugonjwa

Kama tulivoona hapo juu pale mwili wa mwanamke unapokoma kutengeneza homoni za estrogen na progesterone ndipo hedhi yako itakoma. Wanasayansi huenda mbali zaidi na kuwaanzishia wahanga wa tatizo hili program ya kurudisha homoni hizi kwa kuwawekea homoni zilizotengenezwa maabara.

Kitendo hiki hufahamika zaidi kama hormone replacement therapy. Njia hii inatazama ishu ya kukoma hedhi kama ugonjwa wakati ni suala la kawaida kabisa linalomkuta kila mwanamke. Ukweli ni kwamba kitu chochote kilichotengenezwa kwa mkono wa binadamu hakitafanya kazi sawa na kitu kilitengenezwa halisi kwa ajili ya kazi fulani kwenye mwili. Ndio maana madhara ya kuwekewa homoni hizi ni makubwa zaidi.

Njia 7 asili za kutumia kupunguza makali ya menopause.

1.Kutumia vyakula vyenye madini ya Calcium na Vitamin D kwa wingi

Mabadiliko ya homoni wakati wa menopause huweza kusababisha kudhoofika kwa mifupa. Madini ya Calcium na vitamin D husaidia kuimarisha mifupa na kupunguza hatari ya kuchanika kwa nyonga. Unaweza kupata madini ya Calcium kwa kutumia vyakula kama maziwa. Mboga kama spinach na maharage.

Mwanga wa jua ni chanzo kizuri cha Vitamin D, hivo hakikisha kila siku unapata walau nusu saa ya kukaa juani. Kama huna muda wa kukaa juani au kukosa muda mzuri wa kuandaa chakula chako pengine kutokana na aina ya shuguli unayofanya basi hakikisha unatumia virutubishi ambavyo vipo kwenye mfumo wa vidonge ili kuongeza Madini ya Calcium na Vitamin D.

2.Kurekebisha uzito wako

Kuongezeka uzito ni changamoto inayowapata wanawake wengi wanapokoma hedhi. Hii ni kutokana na mabadiliko ya homoni, uzee na mabadiliko ya vinasaba.

Kuongezeka kwa mafuta hasa eneo la tumbo inaongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kisukari. Kwa kuongezea ni kwamba wanawake wenye uzito mkubwa dalili za menopause zinakuwa kali zaidi ukilinganisha na wale wenye uzito mdogo.

3.Epuka vyakula vinavyoongeza hatari kama

Vyakula vilivyosindikwa: vyakula vingi vilivyosindikwa kiwandani huongezwa sukari, vionjo vya kuongeza ladha na kemikali nyingine kulinda kisiharibike (preservatives). Pia vyakula vingi vya namna hii vimejaa wanga ambayo ni adui kwa mwanmke aliyekoma hedhi.

Mafuta ya kula yaliyosafishwa kama mafuta ya kupikia ya alizeti badala yake tumia mafuta ya nazi au olive kupikia. Pombe: ambayo huongeza hatari ya kuongezeka uzito na Vinywaji kama soda ambavyo huchangia katika kudhoofisha mifupa, na matatizo ya meno.

4.Punguza na udhibiti msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo usipodhibitwa ni chanzo cha kuvurugika kwa homoni na hivo kukufanya uwe mlevi wa vyakula vya sukari na wanga. Kukosa usingizi na kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa. Baadhi ya njia nzuri za kudhibiti msongo wa mawazo ni kama mazoezi, aromatherapy (kuvuta hewa ya mafuta mfano mafuta ya lavender), kutumia muda mwingi kwenye maeneo yaliyotulia, kuongea na uwapendao na kusali.

5.Weka ratiba ya kufanya mazoezi

Maozezi ni muhimu sana kwa mwanamke kama unataka kupunguza dalili mbaya zinazojitokeza wakati wa kukoma hedhi. Baadhi ya dalili hizi ambazo utadhibiti kwa mazoezi ni kama kuongezeka uzito, kukosa usingizi, misuli kupungua na msongo wa mawazo. Napendekeza kutumia walau dakika 10 mpaka 30 kwa siku kufanya mazoezi .

6.Pata muda mrefu wa kulala

Tafiti zinasema kwamba msongo wa mawazo pamoja na kukosa usingizi ni chanzo cha kupungua kwa kinga ya mwili, kupungua kwa ufanisi kwenye shughuli zako na kuongezeka uzito na kitambi. Ili kuruhusu mwili wako kurekebika kutokana na mawazo hakikisha unapata muda wa masaa 7 mapak 9 ya kulala kila usiku.

7.Jenga mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka

Tengeneza mtandao wa marafiki wazuri ambao utashauriana nao mambo ya kujenga na siyo mambo mabaya. Mahusiano mazuri yatakufanya mwili uwe mtumivu na kuepuka msongo wa mawazo

Soy power ni Muhimu kutumika kwa Wanawake waliokoma hedhi ana wanaokaribia kukoma.

soy power kwa menopause
soy power

Faida za soy power

  • Kuongeza uzalishaji wa uteute ukeni ili ufurahie tendo
  • Kuimarisha hamu ya tendo la ndoa
  • Kuondoa dalili mbaya kama uchovu na kutokwa jasho jingi usiku
  • Kuimrisha afya ya mifupa na usingizi mnono pamoja na
  • Kuimarisha ngozi yako

Soy power ni Tsh 90,000/= tu. Itakufanya ufurahie tendo kama vile ulipokuwa binti.

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai.

Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata huduma

Bofya makala inayofata: Kwanini uke wako ni mkavu sana na hufurahii tendo

Share and Enjoy !

Shares
Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Mambo ya kufahamu Kuhusu bikira.

Mambo 10 Muhimu ya kufahamu kwa Mwanamke  kabla hujaamua kupoteza Bikira yako.

bikira

1.Tafsiri ya bikira inatofautiana kwa kila mtu.

Jambo la kwanza kufahamu kwa wewe mwanamke mwenye bikira ni kwamba maana ya bikira inatofautiana inategemea na mtu husika kwa mfano. Wengine bikira humaanisha kutoingiliwa kingono kwa mwanamke. wengine humaanisha kutojihisha na mapenzi kwa namna yoyote either njia ya uke au mdomo (oral sex).

Kwa vyovyote ambavyo unaweza kuelezea bikira basi yapaswa kufahamu kwamba una maamumuzi ya kupanga lini uvunje bikira yako. Na pia kumbuka kwamba siyo kitu kibaya kuvunja bikira maana inakufungulia mwonekano mpya wa maisha ya kuanza kujihusisha na ngono ambapo mwanzo haikuwa hivo.

2.Utando laini kwenye bikira yako haupasuki kwa ngono pekee.

Naamini kama wewe ni bikira ama hujawahi kujihusisha na vitendo vya ngono basi umewahi kusikia kuhusu utando laini unaoziba uke. Kwamba utando huu hupasuka wakati uume unapoingia kwenye uke kwa mara ya kwanza.

Ukweli ni kwamba tishu hii haipasuki wakati wa tendo pekee bali hata kwenye shuguli zingine za kawaida kama mazoezi na kazi nzito. Kwahivo usipate mawazo pale ambapo hujaona damu ikitoka wakati unafanya tendo la ndoa kwa mara ya kwanza.

3.Mwili hautabadilika baada ya kupoteza bikira yako

Baada ya kufanya ngono kwa mara ya kwanza basi kumbuka mwili wako hautabadilika kwahivo usipate hofu. Japo kutawepo na mabadiliko kidogo ya kisaikolojia kwa upande wa hisia za kimapenzi kama

  • Mashavu ya uke kuongezeka
  • Wakati fulani kasi ya kupumua kuongezeka
  • Ngozi kuwa ya moto
  • Kupata jasho sana

Kumbuka dalili hizi ni za muda mfupi tu kutokanana na hisia za kimapenzi unazokuwa nazo kwa wakati husika na zitapotea baada ya muda flani.

4.Huwezi kutambulika na watu kwamba umetoka kufanya ngono

Baada ya kumaliza kufanya ngono aidha kwa mara ya kwanza kutokana na kwamba siyo kawaida yako basi unaweza kuwa na hofu labda watu watajua kwamba umepoteza bikira yako kwa kukutazama machoni. Jibu ni hapana, watu hawawezi kukujua kwenye macho kwamba umepoteza bikira yako labda uwaambie, kwa maana ingine hakuna mtu atajua kwamba wewe sio bikira tena.

5.Kufanya tendo haitakuwa kama vile unavyoangalia kwenye tv ama  picha za X

Wanawake wenye bikira hufikiri kwamba siku ya kwanza wanapoanza ngono basi ufanyaji wake utakuwa kama kwenye TV wanavyoangalia au video za ngono hapana. Kila mmoja hufanya tendo hili kwa namna yake. Kwahivo usidangaywe na vido unazoona kwenye mtandao ama kwenye TV. mengi huwa ni maigizo.

6.Tendo lako la kwanza hutafurahia lakini halitakuumiza.

Ni kawaida kwa mwanamke kutofurahia tendo pale anapofanya kwa mara ya kwanza. Msuguano hutokea pale uume unapoingia kwenye uke wako kwa mara ya kwanza na inaweza kukupelekea kutojiskia vizuri. Kama ukipata maumivu wa tendo la kwanza basi ni wazi kwamba hukuandaliwa vizuri ama uke wako ni mkavu hauna majimaji. Kama maumivu yakiwa ya mara kwa mara inaweza kuwa una uvimbe kwenye kizazi na unatakiwa kumwona dacktari.

7.Utahitaji kuandaliwa kabla ya tendo na uke wako utaloa

Kwa mwanamke pale unavonja bikira fahamu kwamba kwenye kila tendo utakalofanya baada ya hapo uke wako utalowa majimaji ambayo kazi yake ni kulainisha njia ili uume upite kiurahisi. Na pia fahamu kwamba utahitaji kuandaliwa kwanza kabla ya kufanya ngono.

8.Magonjwa ya zinaa huambukizwa kupitia aina yoyote ya ngono

Kwasababu tayari umeanza kujihusisha na vitendo vya ngono basi fahamu kwamba unaweza kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa endapo hutakuwa mwangalifu kwenye mahusiano yako. Magonjwa ya zinaa husambaa kwa aina yoyote ya ngono iwe kupitia uke, njia ya haja kubwa, au ngono kwa mdomo. Inashauriwa kutumia kondom kwa kila tendo ili kujikinga na maambukizi haya.

9.Unaweza usifike kileleni siku ya kwanza

Naamini umekuwa ulisoma na kuambiwa na wenzako kuhusu swala la kufika au kutofika kileleni. Kitendo ni hali ya mwanamke kutosheka kimapenzi baada ya tendo la ndoa.

Kutokana na kwamba siku ya kwanza utakuwa na woga na pia kuhisi maumivu wakati wa tendo, hutaweza kufurahia ngono kwahivoo hutaonja ile ladha ya kutosheka kimapenzi ama kufika kileleni. Lakini usohofu maana kadri unavoshiriki zaidi ngono ndivyo utakavokuwa mzoefu na utaweza kujua mbinu mbalimbali za kimapenzi. Fahamu pia kadri unavorelax na kuweka akili itulie ndipo itarahisisha kufika kwako kileleni.

10.Kama hukufurahia tendo siku ya kwanza, unaweza kufanya vizuri siku zijazo.

Bofya makala inayofuata: Chanzo cha uke mdogo na kupungua kina cha uke

Share and Enjoy !

Shares
Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Nini kinasababisha maumivu ukeni?

maumivu ukeni
maumivu ukeni

Uke ni njia inayopitisha mbegu za kiume kutoka kweye uume kwenda kwenye mji wa mimba. Kupata maumivu ukeni huchangiwa na sababu za kisaikologia ama uwepo wa maambukizi fulani. Kupata tiba ya mapema kwa tatizo lako la uke ni njia nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupata athari zaidi kwa hapo baadae

Dalili za Kupata Maumivu Ukeni

Maumivu ukeni yanatofautiana kwa kutegemea chanzo cha tatizo dalili hizi ni kama ifuatavyo

  • Kupata hali ya kuunguza
  • kuwasha sana ambapo ukijikuna unapata raha
  • Kupata maelengelenge na
  • Maumivuu wakati wa tendo la ndoa

Kama maumivu yako yanatokana na maambukizi eidha ya bacteria ama fangasi basi inaweza kuambatana na kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali.

Nini Kinasababisha Maumivu Ukeni

Visababishi vikubwa vya maumivu ukeni ni maambukizi ya magonjwa ya

  • Fangasi
  • Gonorrhea na
  • Chlamydia

Visababishi vingine ni pamoja na

  • Madhara ya kiafya yaliyotokana na tatizo la kuzaliwa na upasuaji
  • Saratani ya mlango wa kizazi
  • Ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen (huwapata zaidi waliokoma hedhi)

Makundi yaliopo kwenye hatari kupata maumivu ukeni

  • Wanawake wote wapo kwenye hatari ya kupata maumivu ukeni;
    Tatizo la maumivu ya uke huwapata karibu kila mwanamke katika point flani ya maisha yao.
  • Matatizo baadhi ya kiafya huongeza hatari ya kupata maumivu ya uke. mfano mabadiliko ya homoni kutokana na kujifungua, kukoma hedhi au upasuaji wa kuondoa kizazi huongeza hatari ya kupata maumivu makali ukeni.
  • Matumizi ya baadhi ya dawa pia kwa muda mrefu yanaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ukeni
    Wanawake walioenda umri wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana na kukoma hedhi ambapo utengenezaji wa ute unaolainisha uke hupungua kwa kasi.

Vipimo Namna ya kugundua Tatizo kwenye uke.

Kama unapata maumivu ya uke mara kwa mara, weka mihadi uonane na dactari ili akufanyie uchunguzi kujua chanzo cha tatizo lako. Dactari atachukua historia yako ya kuumwa, anaweza kufanya uchunguzi wa kutumia mikono na macho(physical examination) ama uchunguzi zaidi wa maabara kama itatakiwa hivo.

Ukiwa na swali tuandikie kwa Whatsapp no 0678626254

Share and Enjoy !

Shares
Shares