Hatua 5 za kuondoa weusi kwenye mapaja na kwapa

weusi kwenye mapaja na kwapa
weusi kwenye kwapa

Nimekuwa nikipokea maswali mengi sana kwa wadada wengi wakihitaji msaada wa tatizo na weusi kwenye mapaja na kwapa. Wakitaka kujua hasa nini kisababishi baada ya kutumia vipodozi vingi vya kujichua na kuchubua bila mafanikio.

Nimeamua kuleta makala hii ili kujibu maswali ya watu wengi na kutoa msaada kwani wadada na wamama wengi wamepoteza urembo na mvuto wao na hawajui namna sahihi ya kurudia hali nzuri ya zamani.

Athari ya kisaikolojia

Kuwa na weusi kwenye mapaja na sehemu zingine za mwili ni hali inayoathiri kisaikologia na kuleta msongo wa mawazo. Kwani hali hio inakunyima uhuru wa mavazi na kujiachia unapokuwa na mwenza wako. Ndio maaana wanawake wengi wamekuwa wakijaribu njia nyingi sana bila mafanikio. Hasa unapofikia hadi kutumia kemikali kali ambazo zinakuongezea tatizo kuwa sugu zaidi.

Basi usiwaze na huna haja ya kukosa uhuru tena katika maisha yako kwa tatizo hili ambalo unaweza kulitatua ukiwa nyumbani kwako bila kutumia vipodozi na dawa zenye kemikali.

Kabla ya yote tuangalie visababishi vya tatizo hili kuanzia vitu vidogo vidogo hadi vitu vikubwa.

Chanzo cha weusi kwenye mapaja, kwapa na sehemu za mwili

1.Msuguano kati ya sehemu mbili kwa muda mrefu.

Hii ni hali ambayo inawatokea sana watu ambao unakuta viungo vyao vimekaribiana sana hasa mapaja na husuguana. Wengine hupelekea kupata maumivu makali sana na kuwapelekea kutumia nguo ndefu za ndani kupunguza msuguano huo.

2.Unene kupita kiasi

Pia hii ni hali ambayo huwatokea watu wa namna hii baadhi, kwa sababu ya uzito kuongezeka bila sababu na kupelekea sehemu hizo kuwa na msuguano mkali sana.

3.Matumizi mabaya ya deodorant spray

Watu wengi wanaotumia deodorant spray hasa zenye aluminium salt zinaziba vitundo vya ngozi ambavyo hutoa uchafu na jasho. Hi inapelekea ngozi yako kutopumua vizuri na hatimaye kuidhuru ngozi yako. Weusi wa namna hii unapatikana sana katika  kwapa kutokana na watu wengi kujipulizia spray ili kukata harufu ya jasho.

4. Matumizi ya vipodozi vikali.

Watu wamekuwa wakisumbuka kwa hali na mali kuondoa weusi kwenye kwapa na wamekuwa wakijitahidi kwa namna yoyote kuondoa adha hii lakini sasa matumizi ya vipodozi vikali vinaweza kuharibu sana na kuongeza tatizo kwa kuangamiza [melanocytes] ambazo ndizo seli zinazotengeneza melanin kiini kinachoipa ngozi rangi yake kiuhalisia na kinachozuia athari za miale mikali ya jua.

  1. Vichocheo kuvurugika
    Watu wengi wenye vichocheo vilivyo vurugika/hormonal imbalance unaweza ukawatambua kwa dalili hii ya weusi kwenye kwapa. Na wengi wapo katika kundi hili, unakuta ana ndevu,kwapa nyeusi na mapaja meusi na hadi kupelekea shingo nyeusi sana, pia kwa wanawake wenye mvurugiko wa homoni wengi ni wagumba na pia  wana tatizo la uvimbe kwenye mayai(ovarian cyst). Kumbuka homoni imbalance inatokea kwa wote mwanaume hata mwanamke. Hivyo ukitaka kushinda tatizo hili hakikisha unarekebisha vichocheo vyako kwanza.
  2. Ugonjwa wa polycystic ovarian syndrome [PCOS]
    Huu ni ugonjwa unaoathiri ovary za mwanamke. Utakutana na mwanamke analalamika mzunguko mbovu, maumivu makali wakati wa hedhi na wengine watakwambia kuwa anajaribu kutafuta mtoto bila mafanikio.
    Wagonjwa wengi wenye PCOS ni wahanga wa tatizo hili, hivyo wagonjwa wa namna hii wanapofika ofsini kwanza tunawapatia virutubisho ana mbili kwa ajili ya kubalance homoni zao na ushauri namna ya kupangilia lishe.
  3. Ugonjwa wa kisukari.
    Kuna watu maelfu ambao tayari wamegundulika na kisukari aina ya pili tayari tunawaita ni DIABETIC lakini pia kuna wale ambao bado wapo ktk safari ya kuangukia ktk kundi hilo endapo wasipo jihadhari na kulinda afya zao hawa tunawaita  [PRE DIABETIC]
    Tofauti kati ya Diabetic na Pre diabetic ni kwamba mtu ambaye ni diabetic sukari huwa ipo juu na insulin pia huwa ipo juu ambapo pre diabetes wao sukari huwa ipo kawaida kabisa lakini ukipima insulin ipo juu, na wana dalili zingine tunaziita kwa pamoja metabolic syndromes kamma nilivozitaja hapo juu [weusi sugu sehemu nyingi] belly fats ama [ Nyama uzembe] ndio maana ni vigumu sana kumbaini mtu mwenye pre diabetes kwa kutumia Glucometer[kipimo cha sukari] hadi pale utakapo tumia Insulin Sensitivity test [kipimo cha kuangalia wingi wa insulin].

Kiwango kingi cha insulin kwenye damu kwa muda mrefu kinachotolewa na kongosho kuja kusawazisha kiwango cha sukari kinasababisha seli za melanocytes kufanya kazi kupita kiwango stahiki na hatimaye kusababisha hyperpigmentation [Weusi kwenye ngozi].

ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO UNAWEZA KUTUMIA KUONDOA TATIZO

  1. Pata ushauri kwa mtaalamu wa afya.
    Hii itakusaidia kubaini nini hasa chanzo chake na ataanza kukutibu kulingana na tatizo lako baada ya kujua hasa kisababishi ni nini, unaweza kutembelea ofisi zetu hapa Machinga Complex Karume Dar kwa ushauri zaidi.
  2. Badili mwenendo Maisha yako katika lishe na mazoezi.
    Hakikisha lishe yako unapunguza wanga nzito hasa nafaka, wali nk pia punguza vyakula vyenye sukari na vionjo vya kemikali kama soda, badala yake tumia zaidi vyakula vyenye mafuta, vitamins na protini kama nyama, parachichi, samaki,nazi, mboga za majani na karanga.
    Pia punguza kula gluten nyingi ambayo ni kiambata kinachopatkana kwenye  vyakula vingi vya ngano .Jitahidi kula sana matunda yenye vitamin C kwa wingi, A kwa wingi E kwa wingi, mboga za majani nk.
  1. Majani ya Aloevera.
    Chukua utomvu wa jani la Aloevera pale pale unapokata.
    Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu/moto  Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka. Unaweza pia kutumia vidonge vya aloe vera vinavyapatikana kwenye stoo yetu.
    Utafurahia jinsi gani mmea huu ulivyo na maajabu katika ngozi yako kwani ngozi mpya itatengezwa haraka sana na jinsi gani ilivyo mashuhuri kama strong natural antibiotics kwenye ngozi yako, ambapo ofsini  kwetu tunatumia vidonge vyake kuwahudumia wenye vidonda vya tumbo na matatizo ya uvimbe na wagonjwa wetu huleta mrejesho mzuri sana.
  2. Yogurt
    Kuna maajabu makubwa sana na yogurt kwani imekuwa ikitumika km natural bleaching agent kutokana na kiini chake [ingredient] lactic asidi pamoja na zinc yenye uwezo mkubwa wa kuzuia kuharibika kwa ngozi kutokana na jasho jingi sehemu za mapaja,shingoni na kwapa.

-Chukua yogurt paka sehemu husika kisha fanya massage [sugua] halafu acha kwa dk 10-15 na baada ya hapo osha na maji ya uvugu vugu.

Pia unaweza kuchukua yogurt kijiko kimoja cha chai  ukachanganya na kipande cha limao kisha paka na sugua sehemu husika rudia mara 3-4 kwa wiki.

  1. LIMAO
    Limao ina uasili wa ASIDI ambao unafanya itumike kama Natural bleaching agent cha ngozi yako ambayo imeharibika.
    Pia limao ina kiwango kingi cha vitamin C kinachosaidia seli za ngozi yako kuzalishwa upya na kasi ya ajabu.

Chukua pamba na chovya kwenye juisi ya limao kisha paka sehemu husika kisha acha kwa dk 20 baada ya hapo osha na maji masafi.
Rudia zoezi hili mara 3 hadi 4 kwa wiki moja.

Note: Epuka kutumia juisi ya limao endapo ni muda mfupi umemaliza kunyoa na umejikata sehemu nyeti.

  1. TANGO
    Hii pia imekuwa ikishika nafasi kubwa kama ni natural bleaching agent ya ngozi.
    Inauwezo mkubwa wa kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kurudisha mpya haraka sana. Na hatimaye kufanya mapaja yako kuwa meupe na sehemu zingine.

Chukua kipande cha tango au juisi yake sugua sehemu husika kwa dk 10 hadi 15. Kisha acha angalau dk 10 tena baada ya hapo osha kwa maji ya uvugu vugu.

Pia unaweza kuchukua juisi ya tango,changanya na binzari [unga wake uliosaga] na limao kisha fanya hivyo hivyo.
Fanya zoezi hili mara mbili kwa siku.

Tiba Salama Kupitia Mafuta ya Lavender

lavender oil

Haya ni mafuta ambayo yamekuwa na umaarufu mkubwa wa kulainisha ngozi na kuifanya yenye kupendeza. Pia inaondoa sumu zote kwenye ngozi na kuwezesha ngozi kurudisha seli zilizokufa haraka sana.

Huhitaji tena kuagiza nje ya nchi, tumefanya utafiti na kukuletea mafuta asili yasiyochakachuliwa, yatakayo kupa matokeo ndani ya week moja ya matumizi.

Gharama ya mafuta ni Tsh 40,000/= kwa dozi ya week mbili

Tuandikie kwa whatsapp namba 0746672914 upate tiba hii

Bofya kusoma kuhusu: Vyakula na mazoezi ya Kuongeza ukubwa wa makalio

Share and Enjoy !

Shares
Shares