Saratani ya utumbo mpana (colon cancer)

saratani ya utumbo mpana
saratani ya utumbo mpana

Saratani ya utumbo mpana kwa kitaalamu tunaita colon cancer au colorectal cancer. Ni moja ya saratani zinazosumbua zaidi baada ya saratani ya matiti na ile ya shingo ya kizazi. Takwimu zinaonesha kwamba tatizo linazidi kuongezeka siku hadi siku huku asilimia 5 tu ya wagonjwa wakiwa wamerithi tatizo hilo.

Tunaweza Kujikinga

Takwimu hizi zinatufahamisha kwamba kumbe tunaweza kujikinga kupata saratani ya utumbo mpana kwa kubadili lishe na mtindo wa maisha. Unaweza kujiuliza nitagunduaje kama tayari nina saratani ya utumbo mpana.

Dalili za mwanzo kabisa ni kama maumivu makali ya tumbo na kupata damu kwenye kinyesi, japo kuna magonjwa mengine yanaweza kusababisha dalili hizi ndio maana tunashauri uende hospitali mapema kupima kila upatapo dalili hizi.

Habari njema ni kwamba saratani ya utumbo mpana inaweza kutibika na kupona kabisa endapo utawahi mapema. Ukizingatia lishe na hatua tutakazoelekeza hapa basi ni lazima utapona. Endelea kufuatilia makala yetu mpaka mwisho kwa utulivu.

Ni maana ya Saratani ya Utumbo Mpana(colon cancer)

Ni aina mojawapo ya kansa ambayo inayothiri utumbo mpana na eneo ya mwisho la la utumbo mpana linaloitwa rectum. Pale saratani inakuwa imesambaa kwenye utumbo mpana na eneo la mwisho la utumbo mpana basi tunaita  ni colorectal cancer. Lakini ikiwa inapatikana kwenye utumbo mpana pekee tunaiita colon cancer au bowel cancer.

Ufahamu utumbo mpana

Maelezo ya hapa chini yatasaidia kukufungua macho na ufahamu wako kuhusu utumbo mpana

Utumbo mpana ama colon kwa jina lingine large intestine ni sehemu ya mmeng’enyo wa chakula inayopatikana baada ya utumbo mwembamba. Urefu wake ni mita karibu 1.5

Utumbo mpana umegawanyika katika maeneo kadhaa kama apendix, eneo la mwanzo, eneo la kati na eneo la mwisho.

Umetengenezwa kwa kuta mbili za tishu ambazo zinasaidia katika ufyonzaji wa virutubisho na maji na kisha uchafu kuhifadhiwa kwa mda kwenye sehemu ya rectum na kisha kutolewa nje kama kinyesi.

Saratani ya utumbo mpana huanza taratibu kwa vimbe ndogondogo zisizo saratani kuanza kujitengeneza kwenye utumbo na baadae kuanza kugeuka kuwa seli za saratani.

Dalili na Viashiria kwamba una Saratani ya Utumbo Mpana.

Unaweza kujiuliza je kuna maumivu ukiwa na saratani ya utumbo mpana? Baadhi ya watu wenye saratani ya utumbo mpana hupata dalili za maumivu kwenye tumbo. Kadiri tatizo linavokuwa la muda mrefu zaidi ndivyo ukali wa maumivu unavoongezeka zaidi. Dalili kuu za saratani ya utumbo mpana ni hizi.

  • Maumivu ya tumbo , tumbo kujaa gesi na mwili kutokuwa na usawa
  • Mabadiliko kwenye choo kama kuharisha na kupata choo kigumu ama kukosa choo kwa muda mrefu, dalili hizi zinaweza kuwa za muda mrefu
  • Kupata choo chenye damu ama choo cheusi na chenye nta
  • Mwili kuchoka sana
  • Kicheuchefu na kutapika
  • Kukosa hamu ya kula na mwili kupungua uzito kwa kasi
  • Mwili kuishiwa damu (anemia)
  • Macho na Ngozi kuwa ya manjano (jaundice)

Mazingira Hatarishi, Mitindo ya Maisha Inayoongeza Uwezekano wa Kupata Saratani ya Utumbo Mpana

  • Watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka ya 50 wapo kwenye hatari zaidi
  • Kula lishe mbovu hasa vyakula viliyosindikwa na kuchakatwa sana kiwandani, kama nyama za makopo, mafuta yaliyochemshwa sana kiwandani na kuwekewa hydrogen, vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta.
  • Uzito mkubwa na kitambi
  • Kuishi maisha ya kizembe pasipo na ratiba ya kufanya mazoezi na kushugulisha mwili
  • matumizi makubwa ya pombe hasa kwa watu wazima na wenye umri mkubwa
  • Uvutaji wa sigara na tumbaku
  • Wagonjwa waliowahi kuugua magonjwa ya mfumo wa chakula kwa kipindi cha nyuma
  • Watu wenye kisukari
  • Wanaofanya kazi kwenye maeneo yenye kemikali sababishi za kansa mfano kwenye mitambo ya mionzi na viwandani.

Hatua za Ukuaji wa Saratani ya Utumbo Mpana.

Kikawaida hatua za ukuaji wa saratani yeyote huwekwa katika makundi aidha kwa namba 0 mpaka 5, ikiwa 0 ni hatua ndogo zaidi na isiyo na makali  ama kwa herufi A, B, C na D. hii husaidia kujua seli za saratani zimekuwa na kusambaa kwa kiasi gani kwenye mwili ukilinganisha na seli za kawaida.

Zifuatazo ni hatua za ukuaji wa saratani ya utumbo mpana kwa maelezo ya Dr AXE wa nchini Marekani

Stage 0 (carcinoma in situ): hatua hii hugundulika endapo saratani haijakuwa na kusambaa zaidi kuvuka eneo la tishu za ndani za utumbo mpana(mucosa)

Stage 1: hatua ya kwanza inagundulika pale ambapo seli za saratani zinaanza kukua kusamba katika eneo moja ndani ya tishu za ndani. Tishu za saratani zinakuwa bado hazijakua kutoka nje ya ukuta wa utumbo mpana.

Stage 2: saratani imeanza kukua nje ya kuta za utumbo mpana lakini bado haijaanza kuathiri sehemu zingine za mwili kupitia kwenye damu.

Stage 3: saratani inasambaa mpaka kwenye lymph nodes, lymph nodes zipo kwenye mfumo unaoitwa lympatic system kazi ya mfumo ni kutoa sumu kwenye mwili na kuzuia magonjwa. Katika stage hii bado saratani haijaweza kusambaa kwenda kwenye viungo vingine vya mwili

Stage 4: saratani inakuwa imesambaa kwenye viungo vingine vya mwili na ndipo inakuwa ngumu kabisa kuitibu.

Matibabu ya Saratani ya utumbo mpana kwa Njia za Kisasa.

Matibabu ya saratani hutegemea hatua ya saratani ilipofikia, tiba hiyo inajumuisha

  • Kufanyiwa upasuaji, sehemu iliyoathirika inakatwa na kisha kuondolewa na kisha tishu nzima kuunganishwa.
  • Tiba ya mionzi (radiataion)
  • Tiba ya chemotherapy. Ambayo husaidia kuua seli za saratani na kuzuia kusambaa
  • Tiba za kuongeza kinga (immunotherapy) ambazo zinasaidia kuongeza uwezo wa mwili kupambana na seli za saratani.

Hatua sita za kuzuia na Kupambana na Saratani ya Utumbo Mpana.

1.Kula zaidi vyakula vya kuondoa sumu na vyenye nyuzinyuzi au kambakamba kwa wingi.

Hapa chini ni list ya vyakula vya kutumia kwa wingi.

  • Parachichi
  • Epo
  • Nazi na maziwa ya nazi
  • Viazi vitamu
  • Bamia
  • Karanga kama almonds na walnuts
  • Mafuta ya nazi na mizeituni
  • Chai ya kijani
  • Nyama kutoka kwa Wanyama waliokula majani
  • Tangawizi, tumeric
  • Kokoa na uyoga

2.Hakikisha unapunguza uzito

Kama una uzito mkubwa na kitambi basi hakikisha unafanyia kazi point hii maaana tayari upo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani. Unaweza kutembelea stoo yetu ya virutubisho vya kupunguza uzito kwa kubonyeza hapa

3.Fanya mazoezi ya kutosha na kushugulisha mwili wako

Watu wanaofanya mazoezi na kushugulisha miili yao wana ulinzi mkubwa dhidi ya saratani. Tafiti zinasema kwamba kufanya mazoezi kunapunguza karibu asilimia 40 mpaka 50 ya hatari ya kuugua saratani. Mazoezi huimarisha usafirishaji kwenye mwili na kuimarisha kinga ya mwili na pia kupunguza uwezekano wa kuugua kisukari

4.Punguza matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara

tafiti zinasema kwamba wanywaji wa pombe na wavuta sigara wapo kwenye htari zaidi ya kufa kutokana na saratani ya utumbo mpana ikilinganishwa na wasiovuta sigara na kuvuta pombe. Ongea na daktari wako akusaidie kukwelekeza njia sahihi za kuachana na tabia hizi hatarishi.

Hakikisha unatibu magonjwa ya mfumo wa chakula, kama kuharisha, na kukosa choo kwa muda mrefu: kwa kuzingatia kanuni hizi

5.Kunywa maji ya kutosha kwa siku ili kuzuia upungufu wa maji mwilini

6.Kula vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi

7.Punguza msongo wa mawazo

8.Tumia virutubisho na mimea tiba kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.

Unaweza kutembelea stoo yetu ya virutubisho vya kwa afya ya tumbo wagonjwa wetu wanafurahia zaidi (digestive care package) kwa kusafisha mfumo wa chakula na kutibu magonjwa kama bawasili, vidonda vya tumbo na constipation.

Jaribu Cancer Care Package yetu

Package yenye virutubisho na dawa asili aina tatu zilizofanyiwa utafiti na kuhifadhiwa kwenye mfumo wa vidonge ambazo zitakusaidia.

  • Kuimarisha kinga ya mwili a hivo kuzuia kutokea kwa saratani
  • Kupunguza madhara na dalili mbaya kama kutapika, maumivu, na uchovu kunakotokana na tiba ya Chemotherapy na Radiotherapy.
  • Kusaidia kutibu saratani pale ambapo virutubisho hivi vitatumika pamoja na dawa za hospitali
  • Kuzuia ukuaji wa seli za saratani na kusaidia uponaji haraka wa vidonda na
  • Kuongeza uzalishaji wa seli nyeupe za damu kwenye mwili ambazo hupambana na seli za saratani.
  • Unaweza kupata virutubisho hivi ofsini kwetu .

TAHADHARI KAMA TAYARI UNA SARATANI YA UTUMBO MPANA.

Kama unapata dalili za saratani kama tulivokwisha kusoma hapo juu badala ya kupaniki na kukosa matumaini ebu mtembelee dactari mapema. Dalili za saratani zinaweza kufanana na dalili za matatizo mengine kama bawasili na Crohns disease. Kwa hivo usipuuze dalili unazoziona, nenda hospitali mapema ili uanze tiba mapema.

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Huduma ya dawa zetu za mimea ni Tsh 270,000/=

Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata Huduma .

Share and Enjoy !

Shares
Shares