Kitunguu saumu ni dawa.

MAANDALIZI YA KITUNGUU SAUMU KIMA DAWA

Yaweza kuwa umewahi kupata vidokezo kwamba kitunguu swaumu chaweza kutibu baadhi ya magonjwa lakini bado huna uhakika kutokana na kutopata maelezo ya kina na uchambuzi makini utakaokufanya uamini na kuanza leo kutumia kitunguu saumu kama dawa yako, hakikika ukisoma maelezo haya basi hutakosa kitunguu saumu jikoni mwako maana maajabu yake ni makubwa, pengine utapunguza gharama kubwa kutununua dawa na waweza kujikinga pia na maradhi mbalimbali kwa kula kitunguu saumu tu.

Vitunguu saumu ni moja ya mmea wa maajabu kutokana na kuthibitika kwake kuponya magonjwa ya aina mbalimbali,. Kutafuna kipande kimoja kila siku kitakufanya usitembelee hospitali kwa muda mrefu zaidi, kumbuka afya yako sio dhamana ya dactari, wewe ndo mtu wa kwanza kulinda afya yako. Mmea huu unapatikana kwenye familia ya mimea ya allium ikiwa pamoja na vitunguu maji, kundi hili likisifika kwakuwa na harufu kali inayotokana na upatikanaji wa madini ya sulphur ndani yake.

Vitunguu Saumu Hupambana na Magonjwa zaidi ya 160 Ikiwemo Saratani/cancer.

Tafiti mbalimbali zimeonesha uwezo wa vitunguu saumu katika kupambana na magonjwa mengi zaidi ya 160 ambayo tunaweza kuyaweka katika makundi manne.

 1. Kundi la kwanza: kuzuia na kupunguza mpambano au mcharuko(inflammation), na hivyo kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya maumivu ya viungo.
 2. Kundi la pili: kuimarisha kinga ya mwili; na hivo kutibiti bacteria, fungasi, virusi, na mashambulizi mengine ya vimelea. Vitunguu saumu ni moja kati ya antibiotic asili yenye nguvu sana ikiweza kupambana hata na bacteria sugu (antibotic resistant Bacteria), na pia kiungo hiki kinaweza kupambana na minyoo na fangasi wa aina mbalimbali. Hii ni kutokana na viambata hai vilivyopo ndani yake kama tannins, saponins, phenols, flavonoids, na mafuta ya lazima kwa mwili.
 3. Kundi la tatu: kuimarisha afya ya moyo na mfumo wa mzunguko wa damu; na hivo kukukinga dhidi ya hatari ya kuganda kwa damu kwenye mishipa, kusawazisha presha ya damu na pia kuondoa mafuta mbaya kwenye mishipa ya damu.
 4. Kundi la nne: kupambana na aina zaidi ya 14 za kansa ikiwemo kansa ya ubongo, mapafu, matiti, tumbo na kansa ya kongosho. Tafiti mbalimbali zimeonesha wanawake wanaokula vitunguu saumu mara kwa mara pamoja na matunda na mbogamboga wanapunguza hatari ya kupata saratani ya utumbo mpana kwa 35%.

Vitunguu Saumu vina Viondoa sumu, Vitamins na Madini mengi kwa Afya ya Mwili .

Kama nlivosema mwanzo mimea hii ina maajabu mengi na ni vigumu kuelezea vyote, mimea hii imejaa madini ya manganese, calcium, phosphorus, selenium, na vitamini B6 na C. utafiti kutoka chuo Kikuu cha Tiba cha  Maryland marekani kinajumuisha matumizi na uwezo wa vitunguu saumu kwa kunukuu maneno haya

“……………vitunguu saumu husaidia kuzuia magonjwa ya moyo,ikiwemo atherosclerosis au kukakamaa kwa mishipa ya damu kunakoletekezwa na kuganda kwa mafuta mabaya na hivo kuzuia usafirishaji w damu), kusawzisha shinikizo la damu na kuimarisha kinga ya mwili.

 Ulaji wa vitunguu saumu marakwamara husaidia kukulinda dhidi ya saratani ama kansa mbalimbali.

Vitunguu saumu vimejaa viondoa sumu (antioxidant)  ambazo huondoa alkali huru(free radicals) kwenye mwili na hivo kusaidia kuzuia uharaibifu wa sumu hizi mwilini.” Mwisho wa kunukuu.

Jinsi ya Kuandaa na Kutumia Kitunguu Saumu

Hatua ya kwanza katika kutumia kitunguu saumu nia kutenganisha maganda yake na nyama yenyewe. Chukua kitunguu chako kisha kibangue na kutoa vipande vidogovidogo, baada ya hapo viweke kwenye kinu kidogo kisha vitindetaratibu kwa kutumia presha ndogo ya mikono, usitumie nguvu kubwa. Kisha anza kutoa maganda madogo madogo yaliyosalia kwenye vitunguu vyako,tayari vitunguu vyako vipo tayari kutumika, unaweza kutafuna vipande taratibu ama ukachanya kama kiungo kwenye chakula na juisi yako

 1. Kitunguu saumu na asali.

Mahitaji :chupa ya glasi na vitunguu saumu vilivyomenywa na kukatwa katwa.

Namna ya kuchanganya: weka vitunguu saumu vilivomenywa kwenye chupa yako ndogo ya glasi kisha  polepole mwaga  asali ya kwamba inajaza nyufa katikati ya fundo za kitunguu. Weka glasi kwenye sehemu ya joto yenye c 20c. Katika siku mbili hadi wiki nne, mwanga usichuje. Tumia katika muda wa miezi 3.

 1. Kitunguu Saumu dawa ya kikohozi

Maelekezo: Ponda kijiko cha chai cha kitunguu saumu katika kipimo hicho hicho cha       sukari au asali. Tumia mara mbili kwa siku kwa kikohozi.

ANGALIZO:

matumizi ya ya kitunguu saumu yanaweza kuingiliana na ufanyaji kazi wa dawa mbalimbali za hospitali, hivo kama unatumia dawa zifuatazo ama upo kwenye makundi haya basi hakikisha unamuuliza Daktari wako kabla hujaanza kutumia kitunguu saumu  kama dawa.

 • Isoniazid; hizi ni dawa zinazotumika kutibu maradhi ya kifua kikuu. Vitunguu saumu vyaweza kuingiliana na ufyonzaji wa dawa hii na hivo kupelekea dawa kutofanya kazi.
 • Vidonge vya kupanga uzazi , vitunguu saumu vyaweza kupunguza nguvu ya vidonge hivi.
 • Cyclosporine: dawa hizi hutumika kwa wagonjwa waliopandikiziwa kiungo mfano figo.
 • Dawa za HIV &AIDS, wagonjwa wa ukimwi wanatakiwa kuongea nawahudumu wao kabla ya kutumia kitunguu saumu ama virutubisho vyenye vitunguu saumu ndani yake.
 • Nonsteroidal anti-inflamatory drugs(NSAIDs), dawa hizi ni kama ibuprefen na naproxen zikitumiwa pamoja na kitunguu saumu huongeza kuvuja kwa damu.

Nini husababisha harufu kali mdomoni baada ya kula kitunguu saumu??

Najua hili ni swali la watu wengi, na imekuwa ikitusumbua sana kwamba pamojana virutubisho na madini muhimu yaliyopo kwenye kitunguu saumu lakini inakuwa ngumu kutafuna kwa kuhofia harufu kali. Hebu tufahamu harufu hii huletekezwa na nini na jinsi gani tuzaweza kuiondoa.

Pale unapotafuna kitunguu saumu, kemikali za kibaiologoa zilizoko kwenye mfumo wa chakula kwa ajili ya kuvunjavunja chakula kiweze kufyonzwa vizuri hubadilisha kiambata kilichopo kwenye kitunguu saumu kiitwacho Allin kuwa Allicin na kisha kuvunjwa zaidi kuwa Allyl Methyl Sulfide na hivo kusababisha harufu kali.. Njia rahisi ya kuepusha harufu hii kali nayo ni kunywa maziwa.

Tumia Kirutubisho Chetu Cha Garlic Oil Kwa Tsh 75,000/= Pekee.

Kirutubisho cha Kitunguu saumu

Kirutubisho hiki cha Garlic Oil ni cha asili kipo kwenye mfumo wa Vidonge, kimetengenezwa kwa kutumia Kitunguu saumu na mimea tiba ingine kitakusaidia

 1. Kuua bacteria, fangasi na vimelea wengine kwenye mwili. Hivo inafaa zaidi kwa wenye fangus sugu, H Pylori, Minyoo, vidonda vya tumbo na wenye maambukizi ya bacteria.
 2. Kupunguza mafuta mabaya (bad cholesterol), inafaa kwa wenye matatizo ya moyo na wanaotaka kupunguza uzito.
 3. Kulinda mfumo wa ubongo na kurekebisha presha ya mwili.
  • Fika ofsini kwetu Mwembechai Dar kupata huduma ya dawa na ushauri.

Endelea kufatilia makala zetu na kwa chochote tuandikie kwenye namba 0678626254

Share and Enjoy !

Shares
Shares