Nini Kinasababisha Kujamba Wakati wa Tendo la Ndoa?

kujamba wakati wa tendo la ndoa

Kwa mwanamke unaweza kujihisi vibaya pale unaposikia sauti ya kujamba wakati wa tendo la ndoa. Ukweli ni kwamba hii huwatokea watu wengi na ni kawaida.
Uchakataji wa chakula huendelea hata wakati wa kufanya ngono. Hali yako ya kujamba wakati wa tendo la ndoa inategemea na aina ya chakula ulichoku;a, muda uliokula na mara ya mwisho umepata haja kubwa.

Kwanini Watu Hujamba Wakati wa Tendo la Ndoa?

Kwa wanawake kujamba kunaweza kusababishwa na msuguano kati ya uke na uume wakati wa tendo. Presha inayozalishwa kutokana na msuguano huu hupelekea pia mgandamizo kwenye eneo la mkundu ambapo lipo karibu na uke, na hivo kupelekea gesi kutoka nje. Kujamba wakati wa tendo la ndoa inaweza kutokea kwa staili yoyote ya tendo na pia muda wowote.
Baadhi ya watu kujamba hutokea zaidi pale wanapofikia kileleni, pale misuli ya mwili inaposinyaa ndipo gesi chafu inaweza kutoka nje.

Kujamba kwa Wajawazito Wakati wa Tendo la Ndoa.

Kitendo hiki huongezeka zaidi kwa wanawake wakiwa wajawazito.
Mabadiliko ya homoni yanayotokea kwenye kipindi cha ujauzito husababisha mrundikano wa gesi tumboni. Homoni ya progesterone huwa juu zaidi kipindi cha ujauzito. homoni hii hupelekea kusinyaa kwa misuli na kupungua kwa kasi ya uchakataji chakula na hivo kuzalisha gesi nyingi tumboni.
Wajawazito pia hupata kichefuchefu na hivo kushindwa kula vizuri, hali inayochangia uzalishaji wa gesi nyingi tumboni. Kwa kesi hiyo inatakiwa kudhibiti kwanza hamu ya kula ili kuweka sawa usagaji wa chakula tumboni.

Namna ya Kuzuia Kujamba Wakati wa Tendo la Ndoa

Kujamba wakati wa tendo la ndoa inaweza kuwa siyo tatizo hasa kama inatokea mara chache. Lakini kama ni tatizo linalojirudia kila unapofanya tendo la ndoa basi hakikisha unaonana na Dakatari kupata ushauri na vipimo kujua chanzo cha tatizo lako.
Kama kuna changamoto kwenye viungo vya mwili moaka kupelekea hali hiyo, unaweza kufanya mabadiliko yafuatayo kwenye mtindo wa maisha

  • Jiwekee mazoea kupata choo kabla ya kufanya tendo la ndoa
  • Punguza matumizi ya vyakula vinavyozalisha gesi
  • Punguza matumizi ya vinywaji kama soda na vyakula vya ngano.
  • Unapokula, kula taratibu ili kuvunjavunja chakula vizuri kabla ya kumeza.
  • Epuka kuvuta sigara: uvutaji sigara huchangia kumeza hewa na hivo kupelekea gesi tumboni.
  • Fanya mazoezi mara kwa mara, kusaidia kutoa gesi tumbo. Hasa mazoezi ya squats.

Je kujamba Ukeni ni Kawaida?

Wanawake wanaweza kutoa gesi kupitia uke wakati wa tendo la ndoa. Uke ni kiungo chenye tishu na mikunjo mingi, siyo kwamba ni bomba lililonyooka. Kwahivo mikunjo hii inaweza kuhifadhi gesi. Mara nyingi gesi kwenye uke hutolewa pale mwanamke anapofikia kileleni kwasababu misuli ya uke husinyaa.

Gesi hii hutoa sauti kama vile ya kujamba, lakini inatoka ukeni. Wakati mwingi kujamba kupitia uke kunaweza kutokea wakati mwanamke akifanya mazoezi.
Wanawake wengi hujsikia aibu kutokana na kitendo hiki pangine kwasabbau ya mila na taratibu za jamii. Fahamu kwamba ni jambo la kawaida, ongea na mwenza wako ili uwe huru endapo kitendo hiki kitatokea, unaweza pia kucheka ili kuonesha kwamba ni jambo la kawaida.

Maelezo ya Mwisho

Ni ngumu kuzuia moja kwa moja kujamba wakati wa tendo la ndoa. Lakini unaweza kupunguza tatizo kwa kubadili mtindo wa maisha kwa kufata maelekzo pale juu. Weka ratiba ya kufanya mazoezi kila siku au walau mara tatu kwa week. Punguza maumizi ya vyakula na vinywaji vilivyosindikwa. Amua kutumia zaidi vyakula asili unachopika nyumbani.
Kama tatizo ni kubwa sana hakikisha unafika hospitali kufanya vipimo, ama fika ofsini kwetu kupata virutubisho vya kusafisha tumbo na kurekebisha mfumo wa chakula.

Kwa ushauri wasiliana nasi whatsapp kwa namba 0678626254.

Soma makala inayofuata:Harufu ya shombo la samaki ukeni na suluhisho lake

Share and Enjoy !

Shares
Shares