Categories
Dondoo za afya

Maumivu ya Kitovu Husababishwa na nini?

Chanzo Cha Maumivu ya Kitovu?

maumivu ya kitovu
maumivu ya kitovu

Maumivu ya kitovu yanaweza kuwa ya taratibu na ya muda mfupi ama yanaweza kuwa makali na yakachukua muda mrefu. Unaweza kupata maumivu haya kwenye kitovu chenyewe ama yakaendea kuelekea sehemu za tumbo zinazozunguka kitovu.

Napenda ufahamu kwamba maumivu ya kitovu hayatokani na kitovu chenyewe bali ni tatizo linaloanzia mbali, maumivu ya kitovu ni dalili tu ya tatizo kubwa ulilonalo ambalo ndio chnzo. maumivu haya yanaweza kutibika haraka kwa kumeza dawa ama kuhitajika upasuaji. Maumivu ya kitovu hutofautiana, wengine hupata maumivu ya mda mfupi na yanayokuja na kondoka na wengine hupata maumivu makali yanayovuta na kufanya tumbo kujaa.

Hakikisha unafatilia vizuri maumivu yako yatakusaidia kupata tiba sahihi pale unapomwelekeza daktari. Aina ya maumivu uliyonayo ndio yatamwongoza daktari kujua chanzo cha tatizo lako. na hivo kukupa tiba unayostahili.

Ukipata dalili hizi Zikiambataana na Maumivu ya Kitovu wahi Haraka Hospitali.

  • Kutapika damu
  • Maumivu bila kukoma kwa zaidi ya saa moja
  • Maumivu ya kifua
  • Kukosa pumzi ikiambatana na maumivu yanayosambaa kwenye shingo, mikono na taya.
  • Kupata choo chenye damu.

Nini Husababisha Maumivu ya Kitovu Yanayovuta

Kama unapata maumivu kitovu ya haraka na yanayovuta unaweza kuwa na henia. Yawezekana pia kupata maumivu kwenye eneo la via vya uzazi. Hernia au ngiri hutokana na kuongezeka kwa mgandamizo karibu na kitovu. Hernia inaweza kutibika kwa upasuaji.

Mazingira haya yanaweza kuongeza hatari ya kupata henia

  • Kulegea kwa kuta za tumbo
  • Unyanyuaji wa vitu vizito
  • Uzito mkubwa
  • Kikohozi cha muda mrefu

Nini kinasababisha Maumivu ya Kitovu pale Kinaposhikwa

Kwa mara nyingine henia inaweza kusababisha maumivu ya kitovu kila ukikishika. Matatizo kwenye mfumo wa chakula (Crohn disease) hupelekea pia maumivu haya na inaweza kuambatana na dalili kama

  • Kuharisha
  • Kupungua kwa uzito
  • Mwili kukosa nguvu
  • Kuhisi haja kila mara

Hakikisha unaweza mihadi kuonana na daktari kama dalili zitaendelea na kuwa mbaya zaidi.

Maumivu ya Kitovu Yanayoambatana na Tumbo Kujaa

Maumivu haya hutokana na tumbo kushindwa kusaga chakula vizuri na hivo kupelekea tumbo kujaa gesi au maji. Dalili zingine ambazo huambatana ni kama

  • Kujiskia umeshiba muda mwingi
  • Kujiskia ovyo baada ya kula
  • Kupata maumivu karibu na kitovu
  • Kichefuchefu

Sababu ingine ya tumbo kujaa inayoambatana na maumivu ya kitovu ni athari kwenye appendix. maumivu haya huanzia eneo la kitovu na kusambaa hadi kwenye eneo la kulia la tumbo.

Kama maumivu yataendelea zaidi ya masaa ma4, nenda hospitali uonane na daktari kupata matibabu. Vidonda vya tumbo ni sababu ingine ya tumbo kujaa na maumivu ya kitovu. Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kwa muda mrefu na athari ya bacteria ni chanzo kikubwa cha vidonda vya tumbo.

Ukiwa na vidonda vya tumbo unaweza kupata dalili zingine kama hizi

  • Kutapika na kizunguzungu
  • Kupungua kwa uzito kusiko kawaida
  • Tumbo kujaa
  • Kiungulia
  • Maumivu yanayokwamisha kula
  • Kupata choo cheusi
  • Maumivu ya tumbo yanayotulia baada ya kula au kunywa

Tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254 kupata ushauri

Bofya Kusoma kuhusu: Harufu ya shombo la samaki ukeni Tiba ya nyumbani

Share and Enjoy !

Shares
Shares