Kifua kikuu

Maelezo ya utangulizi kuhusu ugonjwa wa Kifua kikuu (TB)

kifua kikuu
TB

Kifua kikuu ama Tb ni ugonjwa hatari unaoua watu wengi duniani kwa sasa. Ukweli ni kwamba karibu watu bilioni 1.7 duniani kote wanaumwa ugonjwa wa TB, ni karibu robo ya idadi ya watu duniani. Ukirudi nyuma karne ya 20, Tb ilikuwa ni kisababishi namba moja cha vifo duniani.

Lakini mpaka sasa ugonjwa umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na maendeleo na utegenezwaji wa antibiotics, japo unatakiwa kutumia dozi kwa muda mrefu wa miezi 6 mpaka 9.

Tb ni nini

TB ni kifupi cha maneno Tuberclosis. Tuberculosis ni ugonjwa unosababishwa na bacteria wanaoitwa Mycobacterium tuberculosis . Ni ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya hewa unaoshambulia zaidi mapafu. TB pia inaweza kushambulia sehemu zingine za mwili kama ubongo, figo  na uti wa mgongo.

Aina za kifua kikuu(TB)

Kuna aina kuu mbili za ugonjwa wa TB, latent tuberculosis( maambukizi yasiyojinesha) na active tuberculosis(maambukizi yanayojionesha). Maambukizi yasiojinesha maana yake una bakteria wa TB ndani ya mwili lakini hawajaleta madhara na pia huwezi kupata dalili za kuumwa TB na pia huwezi kumwambukiza mtu mwingine kama una latent TB.

Japo kuna uwezekano wa maambukizi yasiyojinesha kubadilika kuwa  TB inayojionesha (active Tuberclosis) na ikaleta madhara. Ndiomaana ni muhimu kufanya vipimo mara kwa mara vya kifua kikuu kama unajua umenza kukohoa kupita kiasi ama umejichanganya kwenye maeneo hatarishi.

Mazingira hatarishi yanayopelekea kupata maambukizi ya kifua kikuu(TB).

Sasa tuangalie namna gani mtu anapata hawa bacteria wa tuberculosis mpaka anaanza kuumwa. Ugonjwa wa kifua kikuu(TB) husambazwa zaidi kwa njia ya hewa kutoka mtu mmoja anayeumwa kwenda kwa mtu mwingine mzima. Mtu anayeumwa TB anaweza kusambaza hawa bacteria pale anapokohoa, kucheka, kupiga miayo, kuongea na hata kupiga chafya. Kwa watu wenye kinga ya mwili imara wanaweza kuvuta hewa yenye bacteria hawa na wasiumwe maana kinga yao itapambana na bacteria hawa.

Dalili za kifua kikuu(TB)

Kwa kiasi kikubwa dalili za mtu mwenye maambukizi ya TB zinafanana sana na dalili za maambukizi mengine ya mapafu.ni kama zifuatazo.

  • Kukohoa kwa muda mrefu zaidi ya mara tatu kwa week
  • Kupata maumivu ya kifua
  • Mwili kuwa mchovu mara nyingi
  • Kupungua kwa uzito kupita kiasi
  • Kukosa hamu ya kula
  • Kutokwa na jasho jingi
  • Kukohoa kikohozi chenye damu

Dalili za TB zinaweza kutofautiana kulingana na mahali pa mwili ambapo maambukizi yametokea. Mfano kama maambukizi yametokea kwenye figo basi utaona dalili ya damu kwenye mkojo. Au kama umepata maambukizi kwenye uti wa mgongo basi utapata dalili kama maumivu ya mgongo wa chini(back pain)

Visababishi vya kifua kikuu na mazingira hatarishi

Visababishi vya TB vipo wazi na vinaeleweka vizuri. Lakini kwa ujumla tuweza kusema kwamba kisababishi ni kimoja tu. Maambukizi ya kifua kikuu(TB) husafiri kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Pale ambapo watu hawa wakikaribiana na mgonjwa akapiga chafya, kukohoa, kuongea ama kucheka, tayari bacteria wa mycobacterium tuberculosis wanampata mtu mzima wa afya.

Habari njema ni kwamba kuugua TB ni kitu minatokea mara chache sana. Siyo kwa sababu wagonjwa ni wachache kiasi cha kushindwa kusambaza hawa bacteria, hapana. Ni kwasababu tunavuta bacteria lakini kinga zetu ziko imara na inaweza kupambana na bacteria hawa. Lakini pia kwa mgonjwa wa kifua kikuu(TB) akishaanza dozi inachukua siku 14 kwa mgonjwa kutoweza kumwambukiza mtu mzima wa afya.

Hatari ya kuugua kifua kikuu inaongezeka unapokuwa kwenye mazingira haya

  • Kama umetumia muda mrefu na umekaa karibu na mtu mwenye maambukizi
  • Kama afya yako imezorota na hupati huduma ya kiafya
  • Wanaofanya kazi kwenye vituo vya afya ambapo kuna wagojwa wengi wa kifua kikuu na sehemu zenye watu wengi kama jela.
  • Watu wenye magonjwa kama ukimwi wako kwenye hatari zaidi
  • Wanaovuta sigara na wanywaji wa pombe
  • Watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wazee
  • Wenye matatizo mbalimbali ya kiafya ama waliowahi kuugua magonjwa kama kisukari na nimonia
  • Wagonjwa wa kifua kikuu ambao hawakutibiwa vizuri siku za nyuma.

Hatua 5 za kuzuia na kutibu dalili za TB

Kwa mjibu wa chuo kikuu cha Maryland kitengo cha tiba, na shirika la afya duniani, ugonjwa wa TB ama kifua kikuu haitakiwi kutibiwa kwa kutumia tiba asili pekee. Ili kutibu kifua kikuu vizuri na ukafanikiwa untakiwa kutumia dawa za hospitali pamoja na dawa asili kama umeridhia. Ifuatayo ni list ya virutubisho ambavyo unaweza kuvitumia kwa pamoja  na dawa za hospitali

Vitamin D

Tafiti mbalimbali zinaonesha kwamba Vitamn D husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia maambukizi ya kifua kikuu. Kumbe Vitamin D inauongezea mwili nguvu kupambana na maambukizi haya ya TB kwa kuua bakteria wanaosababisha.

Chanzo kikubwa cha mwili kupata TB ni kupata mwanga wa jua wa kutosha kila siku. Lakini kama una upungufu basi hakikisha unatumia virutubisho asili ambavyo vina ubora ili kuongeza vitamin D.

Mafuta yaeucalyptus

Titi zinasema kwamba kuvuta hewa ya mafuta ya eucalpyptus kunasaidia kuzuia kusambaa kwa maambukizi kwenda kwa mtu mwingine, na pia husaidia kudhoofisha bacteria kwa mgonjwa husika na kupunguza makali ya ugonjwa.

Matumizi ya mimea tiba na virutubisho kama propolis na Cordyceps

Muunganiko Clear lung na Cordyceps na imeonyesha kufanya kazi vizuri dhidi ya vizazi vya bakteria ambavyo vimekuwa sugu kwa tiba ya antibiotics za kemikali. Maeneo ya kutumia tiba hii ni mapana sana. Yanajumuisha kifua kikuu, kuvimba kwa koo, sinus congestion, mafua na kikohozi sugu.

Ushauri kwa mgonjwa wa TB

  • Epuka vyakula vyote ambavyo vinakupa mzio au aleji
  • Tumia vyakula vyenye vitamin B kwa wingi na madini ya chuma kama parachichi, mbogamboga za kijani, maini, almond na matunda
  • Tumia kwa wingi vyakula na matunda ambavyo ni viondoa sumu kama mboga za kabeji, machungwa, na green tea.
  • Epuka kula vyakula vilivyosindikwa viwandani na kuongezwa ladha kama mikate na mchele na tambi
  • Epuka kutumiavyakula na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa, pombe na tumbaku

Maelezo ya hitimisho na tahadhari kwa ugonjwa wa kifua kikuu

Ugonjwa wa TB ama kifua kikuu bado ni ugonjwa hatari sana kama tulivosoma kwenye makala hapo juu. Ni muhimu kuchukua tahadhari ili kujiepusha na maambukizi ya TB. Pia ni jambo la msingi kufanya vipimo mara kwa mara ili kudhibiti tatizo mapema. Hakikisha pia unamuuliza mtumishi wa afya au daktari wako kuhusu ugonjwa huu ili akupe maelezo ya kina. Tiba ya kifua kikuu inapatikana bure hospital zote Tanzania.

Tiba yetu asili inagarimu Tsh 165,000/=

Muhimu: Kabla ya kuanza tiba zetu, hakikisha uwe umeanzishiwa tiba hospitali.

Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 kupata dawa zetu za mimea.

Share and Enjoy !

Shares
Shares