Hatua Tano za kutibu Ganzi iliyotokana na Kisukari

ganzi ya mikono
ganzi ya mikono

Kisukari Kinavyosababisha Ganzi ya mikono na Miguu

Tatizo la ganzi kwenye mikono na miguu kwa kitaalamu peripheral neuropathy hutokea baada ya neva (seli zinazosafirisha taarifa) kukujeruhiwa. Kisukari ni ugonjwa mkubwa unaosababisha ganzi hii kwenye mikono na miguu. Japo siyo kila mgonjwa kisukari atapata dalili za ganzi, lakini wagonjwa wengi karibu asilimia 70 hupatwa na dalili hizi. Kwahivo kitaalamu ganzi inayotokana na sukari na kuathiri neva za kwenye miguu na mikono huitwa diabetic peripheral neuropathy.
Ganzi hii kwa mgonjwa wa kiasukari hutokea baada ya sukari kujeruhi neva za taarifa zilizopo kwenye miguu na mikono, na hivo kupelekea kudhoofika kwa uwezo wa mishipa midogo kusafirisha hewa safi ya oxygen kwenye damu.

Dalili za Mgonjwa wa Ganzi iliyotokana na Kisukari

ganzi ya miguu

Baadhi ya dalili za awali kwa mgonjwa wa kisukari mwenye ganzi ni pamoja na

  • Kupoteza uwezo wa kuhisi maumivu au joto
  • Kujiskia hali ya kuungua, na kutingishika kwa miguu na mikono
  • Kupata hisia kali zaidi unaposhika kitu
  • Kupungua kwa uwezo wa kubalansi mwili
  • Vidonda vikubwa miguuni na matatizo ya mifupa na joints

Dalili hizi zinaweza kuwa mbaya inapofika usiku. Kama tatizo lisipotibiwa mapema basi huweza kusababisha kudhoofika kwa misuli na maungio kama kwenye enka, ambapo hubadili hata namna mtu anavotembea. Kumbuka kama kidonda kisipopona haraka kwenye mkono au mguu kutokana na kisukari, basi hupelekea kiungo kukatwa.
Kwa bahati nzuri ni kwamba unaweza kurekebisha mtindo wa maisha na ukazuia kutokea kwa hali hii mbaya. Endelea kusoma ujifunze hatua tano za kutibu ganzi hii inayoletekezwa na kisukari

Hatua ya kwanza. Kurekebisha Kiwango cha Sukari kwenye Damu:

Kurekebisha sukari kwenye damu ni hatua muhimu na ya kwanza kuifanya ili kuzuia athari kwenye neva, mishipa ya damu, macho, ngozi na kwenye viungo vingine vya mwili. Na njia nzuri katika kurekbisha sukari ni kuhakikisha unapima kila siku, kula lishe nzuri, mazoezi ya viungo na kumwona daktari mara kwa mara ili kujua kama unahitaji kuanzishiwa dawa za kisukari.

Hatua ya pili: Fuatilia lishe Bora

Unachotakiwa kufahamu kwa wewe mgonjwa wa kisukari ni kwamba lishe yako ina machango mkubwa katika kudhibiti dalili mbaya za kisukari kama ganzi. Kiujumla lishe yako ilenge katika vyakula vya asili, punguza wanga na sukari, na vinywaji vya sukari kama soda.
Najua itakuwa ngumu kuacha soda kwa mara moja maana tayari ilishatengeneza ulevi ndani yako, ili utimize lengo fanya hivi, badala ya soda, kunywa green tea mfano kuding tea na pine pollen tea ambazo unaweza kuzipata Jumia.
Kula vyakula vyenye mafuta mazuri badala ya wanga na sukari, punguza manunuzi ya vyakula vya kwenye pakiti, weka ratiba ya kujipikia chakula chako nyumbani.

Tumia pia vyakula vyenye kambakamba kwa wingi ambavyo vimejaa virutubishi kama

  • Mboga za majani na matunda halisi
  • Samaki wana mafuta ya omega 3 ambayo husaidia kupunguza mafuta mabaya mwilini (triglycerides)
  • Vyakula vya mafuta: mafuta ya nazi, maziwa ya nazi, mafuta ya zeituni, na parachichi
  • Protini: Kutoka kwenye nyama na kuku waliofugwa kienyeji
  • Unaweza pia kutumia majani ya stevia kama kionjo badala ya sukari.

Hatua ya tatu. Weka ratiba ya Kufanya Mazoezi

Kufanya mazoezi mara kwa mara ni njia moja rahisi ya kupambana na dalili za kisukari, kuweka uzito sawa,kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu, kurekebisha shinikizo la damu na kuimarisha utimamu wa mwili.
Tenga muda wa dakika 30 kwa siku kufanya mazoezi, unaweza kuanza na mazoezi mepesi kama kuogelea, kutembea na kukimbia au kuruka kamba.
Mazoezi ya viungo yana faida zingine nyingi ikiwemo kupunguza mafuta mabaya kwenye mishipa ya damu, kupunguza msongo wa mawazo na kuimarisha misuli.

Hatua ya nne. Ni kuepuka Mazingira yenye Kemikali Hatarishi na kuacha kuvuta Sigara.

Wagonjwa wenye ganzi wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua magonjwa ya figo kama mawe ya figo ndio maana ni muhimu kuepuka mazingira yenye sumu ili kupunguza mzigo kwenye figo kuchuja hizo sumu. Punguza kukaa kwenye mazingira yenye kemikali za kuulia wadudu, matumizi ya bidhaa za urembo, kumeza dawa pasipo ulazima, pombe na kuvuta sigara.
Kama unashindwa kuacha sigara unaweza kutumia kirutubisho cha anti addiction kitakusaidia kukata hamu ya sigara.

Hatua ya tano: Kupambana na Msongo wa Mawazo

Msongo wa mawazo ni kichocheo cha tishu za mwili kuvimba na kututumka (inflammation) na kuongeza makali ya dalili mbaya za kisukari ikiwemo ganzi. Kufanya mazoezi, tahajudi (meditation), kutumia mda mwingi kwenye maeneo yenye asili(nature) kama kwenye misitu, baharini na kuwa karibu na familia vyote hivi ni njia nzuri za kupambana na msongo wa mawazo.

Maelezo ya Mwisho

kwa mgonjwa mwenye shida ya ganzi namshauri mara kwa mara kufanya vipimo na kujua maendeleo ya tatizo lako. Na pia usimeze dawa kwa kununua famasi pasipo maelekezo ya daktari.

Nashauri pia kutumia virutubisho asili kama chitosan, fish oil, joint health basalm tea na compound marrow powder ambavyo vitakusaidia kutoa sumu, kurekebisha sukari na kuimarisha neva ambazo zimeathirika na sukari nyingi kwenye damu.

Share and Enjoy !

Shares
Shares