Categories
Dondoo za afya

Kwanini unaumwa kichwa bila kupona

Nini husababisha Maumivu ya kichwa?

Makala hii itakupa maelekezo jinsi gani uweze kugundua chanzo cha maumivu ya kichwa yanayokupata, hii itakusaidia kuamua njia sahihi ya kutibu tatizo lako pasipo kukimbilia kumeza vidonge vya kupunguza maumivu ambavyo vina madhara makubwa kama vikitumika kwa muda mrefu pasipo ushauri wa daktari.

Yafuatavyo ni Baadhi ya mazingira yanayopelekea upate Maumivu ya Kichwa

  1. Mwili Kupungukiwa na maji

    Watu hupata maumivu ya kichwa pale mwili unapopungukiwa na maji, kama unapata maumivu ya kichwa baada ya kutapika sana, kutokwa na jasho jingi au mafua ya muda mrefu ni wazi kwamba unahitaji kunywa maji mengi ili kuondoa tatizo lako.
    Kama ni mtu wa mazoezi sana na huna tabia ya kunywa maji ya kutosha mwili utapungukiwa na maji na ni lazima kichwa kitauma. Kwenye majira ya joto sana hupelekea mwili kutoa jasho jingi na kuishiwa maji. Kumbuka kwamba mwili unahitaji maji ya kutosha ili kuendesha shuguli za ndani.

  2. Mwanga wa simu, coumputer na vifaa mbalimbali

    Kuangalia TV kwa muda mrefu ama matumizi makubwa aya simu yanafanya misuli ya macho kukaza na hatimaye kupelekea macho kuuma., vitu vingine vinavyopelekea kukaza kwa misuli ya macho ni kama  kutazama kitu kimoja ama upande mmoja kwa muda mrefu mfano unapoendesha gari na kusoma, Kukaa kwenye mazingira yenye mwanga mkali sana ama mwanga hafifu, mwili kuwa mchovu na ukavu wa macho.
    Kutatua changamoto hii ya kukaza kwa misuli ya macho hakikisha badili uelekeo wa mahali unapoangalia kila mbaada ya dakika 20. kama kuna kazi inakutaka utumie muda mwingi kuifatilia kwa macho basi hakikisha unabalansi na shughuli zingine ambazo zinahitaji pia matumizi ya macho.
    Hakikisha kifaa chako kama simu, computer ama televisheni kipo mbali kuanzia cm 30 , simu unapotumia iweke katika usawa wa chini kidogo na level ya macho. Kama tatizo ni kubwa ongea na dactari wako wa macho akushauri aina ya miwani ya kutumia ili kujikinga na miale ya mwanga.

  3. Vichocheo vya mwili (hormones)

    Kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen huchangia mabadiliko ya utoaji wa chemikali kwenye ubongo zinazochangia maumivu ya kichwa. Inatokea zaidi kwa wanawake wanapokuwa kwenye kipindi cha hedhi.
    Wanawake waliokoma hedhi ama wanaokaribia kukoma hedhi hupata pia maumivu ya kichwa kwa estrogen hupungua kwa kiasi kikubwa.
    Matumizi ya njia ya kuzuia mimba na tiba ya homoni za kutegenezwa maabara (hormone replacement therapy) huchangia kuongezeka ama kupungua kwa baadhi ya homoni na kisha kupata maumivu ya kichwa.
    Kwa wajawazito homoni ya estrogen huongezeka na kupelekea maumivu ya kichwa, baadhi ya wanawake maumivu haya huisha ndani ya kipindi kifupi, wengi hupata maumivu haya kwenye miezi ya kwanza ya mimba. baada ya kujifungua kiwango cha estrogen hushuka tena.

  4. Ukaaji wa mwili

    Ukaaji na ulalaji mbovu unapelekea presha kubwa eneo la juu nyuma ya mwili na kwenye mabega na hivo kupelekea maumivu ya kichwa. Maumivu unayoyapata baada ya kulala ama kukaa au kusimama kwa muda flani ni matokeo ya mwili kutobalansi.

  5. Kutoshugulisha mwili

    Mazoezi ya mwili ikiwemo kukimbia, kuendesha baiskeli, au squats husaidia mwili kutoa kemikali ambazo ni pain killer mfano endorfins. Watu wasiofanya mazoezi na wanaotumia muda mwingi wamekaa pasipo kushughulisha miili ni wahanga wa kuumwa kichwa. Hakikisha unaweza ratiba walau mara 3 kwa week kufanya mzoezi.

  6. Matumizi ya dawa

    Matumizi ya baadhi ya dawa ya kupunguza maumivu kwa muda mrefu badala yake huleta maumivu ya kichwa .Matumizi ya dawa ambazo zipo kwenye kundi la nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) husababisha tatizo kuwa baya zaidi.

  7. Msongo wa mawazo.

    Msongo wa mawazo hupelekea misuli yako kukaza na hivo kubadili namna ubongo unavotoa kemikali hadi kupelekea maumivu ya kichwa. kama wewe ni muhanga wa stress unaweza kusoma vzuri kuhusu namna sahihi za kudeal na msongo wa mawazo hapa.

  8. Kelele

    Kukaa kwenye mazingira yenye kelele nyingi kwa muda mrefu hisababisha kuumwa kichwa .

Njia gani utumie ili kupunguza maumivu ya kichwa kabla ya kumwona Dactari.

  • Tumia kipande cha barafu kwenye mfuko weka kwenye eneo la mbele la kichwa.
  • Kunywa maji ya kutosha walau glass 8 kwa siku
  • Fanya mazoezi madogo ya kutembea hasa kutembea peku kwenye mchanga wa bahari
  • Kaa mbali na eneo lenye kelele na mwanga mkubwa, tafuta eneo lililotulia

Ni muda gani unatakiwa kumwona dactari.

Endapo utapata dalili zifuatazo hakikisha unamwona dactari haraka

  • Maumivu ya muda mrefu pasipo kupata nafuu
  • Maumivu ya kichwa yanayoambatana na homa
  • Kupungua kwa uwezo wa kuona shingo kuwa ngumu
  • Kushindwa kutembea na tatizo kwenye kuongea
  • Kukosa nguvu ama kutetemeka kwa eneo moja la mwili
    Kumbuka ni muhimu kumwona dactari endapo dalili za kuumwa kichwa zitendelea zaidi pamoja na kwamba umetumia njia za kupunguza maumivu haya.

Tumia Mafuta ya lavender kutuliza kichwa

Mafuta ya lavender au mrujuani ni moja ya mafuta yanayotumika zaidi kwenye kundi la (essential oil) lakini faida zake ziligunduliwa kwa zaidi ya miaka 2500 iliyopita katika kutibu magonjwa kichwa na msongo wa mawazo.

Matumizi:Kutuliza kichwa kuuma pakaa matone kidogo eneo la masikio na pua, na pia dondosha matone mawili kwenye mto wa kulalia. Usimeze tena dawa za maumivu kwani zitakuletea magonjwa ya figo na ini bure. badala yake tumia haya mafuta ya asili.

Mafuta ya levender yamekuwa adimu sana kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutibu. Fika ofsini hapa Magomeni Mwembechai upate mafuta haya ambayo ni original na asili.

Gharama ya mafuta ni sh 40,000/= Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 kupata tiba

Share and Enjoy !

Shares
Shares