Mwongozo wa Elimination diet

elimination diet

Elimination diet (EDI)

Kama unapata aleji mara kwa mara unapokula vyakula, ama unahisi ngozi kututumka na kuvimba, chakula hakisagwi vizuri tumboni. Unapata choo kigumu ama kukosa choo kwa muda mrefu na hujui unafanyaje ili kuzifukuza dalili hizi. Basi lishe hii ninayoiita EDI yani elimination diet itakufaa.

EDI ni aina ya lishe ambayo inakutaka kuondoa baadhi ya vyakula ulivyozoea kula katika mlo wako ambayo ndio chanzo cha aleji na matatizo mengine ya tumbo kisha kufidia aina ingine ya vyakula taratibu taratibu wakati huo unafatilia mwili unapokeaje aina hiyo ya chakula.

Lengo la aina hii ya lishe ni kugundua hasa ni aina ipi ya vyakula ndo chanzo cha matatizo yako kwenye mfumo wa chakula na matatizo mengine ya kiafya. Pale inapofikia unaumwa na ukienda hospitali unaambiwa hakuna tatizo, wakati tayari unapata dalili mbaya.

Dalili mbaya

Dalili hizi zitatazokusukuma uanze kutumia lishe hii ya EDI ni kama

Vyakula gani vya kufutilia mbali kwenye lishe yako ya EDI na kwa muda gani??

Vyakula hivi ni pamoja na

  • Vyakula vya ngano
  • Maziwa yaliyosindikwa kiwandani mazao yake
  • Bidhaa za Soy
  • Sukari iliyosafishwa ama inayoongezwa kiwandani
  • Pombe
  • Mayai kwa baadhi ya watu
  • Vyakula na vinywaji vyote vilivyosindikwa
  • Mafuta ya alizeti, canola , pamba na margarine

Lishe hii huchukua kuanzia week 3 mpaka week sita. Mpaka kufikia muda huu mwili utakuwa umepona na hautatutumka ama kukataa tena chakula.

Dalili gani mbaya ambazo zinakuhitaji uanze kufatilia Elimination Diet

Aleji ya chakula ni matokeo ya kinga ya mwili kukataa aina fulani ya protini iliyopo kwenye chakula. Pale unapokula aina husika ya protini mwili huitikia kwa kupambana na chaula husika kwa kutoa dalili kama kuvimba, kutokwa vipele, kuhema kwa shida na maumivu kwenye mfumo wa chakula hasa tumbo.

Kwahivo utakubaliana nami kwamba kujua na kuondoa vileta aleji (allergies) ni muhimu kwa afya yako. Mwili unapokataa chakula unafanya kinga ya mwili kupambana na aina husika ya chakula na hivo kupelekea mpaka tishu za karibu kuathirika.
Athari za kwenye tishu zinaweza kuletekeza dalili kama

  • Ganzi isiyopona
  • Kuvimba kwa maungio (arthritis)
  • Mwili kukosa virutubisho muhimu kutokana na kubagua vyakula
  • Msongo wa mawazo na kubadilika kwa mood
  • Pumu ya ngozi
  • Magonjwa ya kinga kushambulia tishu za mwili (autoimmune disoders)
  • Mishipa ya damu kuwa migumu (atheroscleros) na hivo kupelekea magonjwa ya moyo
  • Magonjwa ya neva na kupungua kwa uwezo wa kujifunza na kufanya maamuzi
  • Kukosa usingizi (insomnia)
  • Uzito mkubwa na kitambi
  • Maumivu ya kichwa na kupata maruerue
  • Maumivu ya misuli na .
  • Matatizo ya figo

Jinsi ya kuanza Elimination Diet

Hatua za kufuata kwenye Elimination diet

1.Hatua ya kwanza: Acha kula vyakula ambavyo vinasababisha aleji ( tazama list pale juu ) . Vyakula hivi usitumie kwa muda wa week 3 mfululizo. Kuondoa vyakula hivi kwenye mlo wako inakusaidia kugundua kinachokutesa hasa ni kipi.

2.Hatua ya pili: Wakati unaepuka vyakula hivi hakikisha unakuwa makini kwa kusoma lebel inayowekwa kwenye vyakula. Hasa vya kununua sokoni au supermaket. Soma kuhusu viambata (ingradients ) za vyakula husika kucheki kama vimeongezewa vileta aleji.

3. Hatua ya tatu: Baada ya ya week 3,(tutaita kipindi hiki reintroduction phase) anza kula na moja ya chakula kati ya vile usivyotakiwa kutumia pale juu, kula kila siku ikiwezekana kisha angalia na dalili unazopata. Orodhesha dalili za tofauti ulizoziona kati ya kipindi cha elimintion phase na reintroduction phase.

4.Hatua ya nne:Kama utaona dalili mbaya zimejirudia haraka pale tu ulipurudia kutumia chakula husika basi tayari utakuwa umempata mbaya wako. Unaweza kuhakiki kuwa chakula hiki siyo salam kwako kwa kukiacha kukitumia tena na kucheki mabadiliko ya mwili. Utaona hili zoezi ni la kujaribu jaribu, lakini haitakiwi kuchukua zaidi ya week 4 maka 6 kugundua aina ya chakula kibaya na kuamua kukiondoa kabisa kwenye mlo wako.

Vyakula vya kujumuisha kwenye mlo wako.

Kwenye lishe yako ya Elimination Diet jitahidi walau asilimia 40 ya sahani yako iwe ni mboga za majani (pika kidogo sana), asilima 30 iwe ni protini , asilimia 20 iwe ni vyakula vyenye mafuta mazuri na 30 iwe ni matunda na wanga. Vyakula vingine vya kuongeza kwenye lishe yako ni pamoja na

  • Supu ya mifupa (bone broth)
  • Maziwa asili ya mtindi
  • Nazi pamoja na bidhaa zake kama maziwa ya nazi,unga wa nazi na mafuta ya nazi
  • Vyakula vya protini kutoka kwenye vyanzo asili
  • Vyakula vyenye mafuta mazuri kama maparachichi
  • Mafuta ya olive

Muhimu: Asilimia kubwa ya sahani yako iwe ni mboga za majani na kiwango kidogo cha matunda. Mboga nzuri za majani pendelea zaidi zile za kijani kilichokolea, kabeji, cauliflower, broccoli,celery, uyoga na matango.

Namna Elimination diet inavifanya Kazi.

Asilimia 70 ya kinga ya mwili ipo kwenye mfumo wa chakula. Hili ni muhimu kulifahamu na hasa kuanzia mdomoni mpaka kwenye haja kubwa (Gut). Kwahivo mfumo wa chakula pamoja na ubongo vinafanya kazi kwa ukaribu sana. Kila muda tunapoweka kitu flani mdomoni taarifa husafiri mpaka kwenye ubongo na kisha kutafsiriwa juu ya chakula husika.

Kwenye mfumo wa chakula kuna visafirisha taarifa(neurotransmitters) . Kazi yake ni kusafirisha taarifa kwenda kwenye ubongo na kisha ubungo huitikia kwa kutoa kemikali za kuchakata/kusaga chakula, homoni na pia kuamrisha mwili kukataa kile chakula kwa konyeza dalili za kututumka na kuvimba.

Kwahivo mawasiliano haya haya yanayofanikisha kujua muda gani una njaa na muda gani umeshiba ndio yanatumika kutoa viashiria juu ya aleji, na madhara ya chakula kilichoingia mwilini. Endapo mwili utagundua chakula ulichokula kina shida basi utaitikia kwa kinga ya mwili kuanza kuapambana na kile chakula na hivyo kupelekea tishu za karibu kuathirika na kuvimba (inflammation).

Kumbuka kwamba wakati unaendelea na Elimination Diet utaacha kula baadhi ya vyakula kwa amuda wa mwezi mmoja. Kisha utarudisha tena kile chakula kwenye mlo wako kukijaribisha. Kama mwili utakikataa basi itakulazima kuacha kabisa kutumia chakula husika. Lengo ni kuhakisha mwili haupati shida tena.

Share and Enjoy !

Shares
Shares