Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama Tendo la ndoa

Je ni Salama Kufanya Mapenzi kipindi cha Hedhi?

period

Kikawaida kipindi cha hedhi kinatokea mara moja ndani ya mwezi. Kama huna changamoto ingine ya kiafya, basi hakuna haja ya kuogopa kufanya mapenzi kwenye kipindi hiki. Japo panaweza kuwa na uchafu kutokana na damu inayotoka, lakini kiafya hakuna madhara na badala yake kuna faida kwa mwanamke. Soma zaidi kufahamu faida za kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke wakati wa hedhi.

Faida za Kufanya Tendo la Ndoa Kipindi cha Hedhi

  1. Kupungua kwa maumimu ya misuli ya tumbo na nyonga : Mwanamke anapofika kileleni kwa kutoshelezwa kimapenzi husaidia kupunguza maumivu kwenye nyonga na misuli. Kufika kileleni kunasaidia misuli kusinyaa na hivo kuondoa maumivu. Tendo la ndoa pia husaidia kutoa kichocheo na endorphims ambacho kinakufanya ujiskie vizuri.
  2. Kupunguza siku za hedhi Kufanya mapenzi kipindi cha hedhi kunaweza kusaidia kupunguza siku za kutokwa hedhi. Hii inawafaa zaidi wanaopata hedhi zaidi ya siku 4. Kutanuka kwa misuli ya kizazi kunasaidia kusukuma damu kwa wingi na haraka na hivo kufupisha siku za hedhi.
  3. Kuongezeka kwa hamu ya tendo Baadhi ya wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa wanaweza kutumia kipindi cha hedhi kufaidi tendo hili. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa hamu ya kufanya mapenzi kwenye kipindi cha hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni.
  4. Damu ya hedhi kama kilainishi Kipindi cha hedhi damu inayotoka inaweza kutumika kama kilainishi ili kupunguza maumivu.
  5. Kupunguza maumivu ya kichwa:Karibu nusu ya wanawake hupata maumivu ya kichwa kipindi cha hedhi. Kushiriki tendo kutakusaidia kupunguza maumivu haya.

Je kuna Madhara yoyote Kufanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi?

Kufanya mapenzi kipindi cha hedhi kunaweza kuleta madhara ya kawaida ya kimazingira, mfano kuchafua mashuka na mwili pia kutapakaa damu. Lakini pia unaweza kuathirika kisaikologia hasa kama wewe ni mwoga wa kuangalia damu. Hatari nyingine ni kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa na homa ya ini. Hii ni kwa sbabau virusi wanaishi kwenye damu. Kama unaamua kufanya mapenzi kipindi cha hedhi basi hakikisha unatumia kondomu.

Je Naweza Kupata Ujauzito Kufanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi?

Inawezekana kabisa kushika ujauzito wakati wa hedhi. Kwahivo kama hujapanga kushika mimba kumbuka kutumia kondomu muda wote. Kila mwanamke ana mzunguko tofauti wa hedhi, na pia mpangilio unaweza kubadilika ushike mimba kwenye kipindi ambacho hukupangilia. Wanawake wenye mzunguko mfupi wa siku 22 wapo kwenye hatari zaidi ya kushika mimba kipindi cha hedhi. Kumbuka mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ndani ya kizazi kwa siku 5 mpaka 7, kwaivo kama una mzunguko wa siku 22 na yai kutolewa baada ya hedhi, kuna uwezekano mimba ikatungwa.

Dondoo zingine Muhimu Unapofanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi.

  • Ongea na mpenzi wako jinsi unavojiskia unapofanya mapenzi kipindi hiki cha hedhi. Kuwa muwazi na mweleze kama hujiskii vizuri.
  • Tumia taulo nyeusi au kitambaa cha pamba cheusi kutandika kwenye godoro ili kufyonza damu.
  • Andaa kitambaa chenya maji au wipes pembeni ya kitanda ili kujisafisha baada ya kumaliza tendo
  • Ongea na mpenzi wako kuvaa kondomu kabla ya tendo kupunguza hatari ya kupata maambukizi.
  • Jaribu staili tofauti kufanya mapenzi ili kupata inayokufaa ambayo haisababishi maumivu.

Bofya makala inayofuata:Je naweza kushika mimba nikisex kwenye hedhi?

Share and Enjoy !

Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shares