Bacteria wa H.Pylori husababisha vidonda vya tumbo.

Bacteria wa H.Pylori tumboni
H.pylori

Yawezekana umewahi kwenda hospitali ukisumbuliwa na dalili za vidonda vya tumbo na kufanyiwa vipimo kisha Daktari anakwambia una bacteria wanaoitwa H.pylori, kama bado basi usichukulie rahisi maana athari yake ni kubwa sana, maana baadhi ya athari zinazitokana na bacteria hawa huweza kusababisha saratani ya tumbo kama tatizo halitatibiwa vizuri haraka.  Tunashukuru kwa kuambatana nasi katika makala hii muhimu inayoendelea kubadilisha maisha ya watu kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo hasa vile sugu, endelea..

Maelezo yafuatayo tumeongelea nini hasa maana ya H.pylori, jinsi wanavoletekeza vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo, pamoja na tiba za asili za kuua bacteria hawa .Kunywa maji vuta pumzi kidogo kisha tuendelee kupata nondo hizi muhimu.

H.pylori ni nani?

Athari za H.Pylori

H. pylori ni kifupi na Helicobacter pylori ni aina ya bacteria ambayo huingia kwenye mwili na kujificha ndani ya mfumo wa chakula. Nikisema mfumo wa chakula hapa ieleweke kwamba ni kuanzia mdomoni unapobugia chakula chako mpaka kwenye puru ambapo unatoa kinyesi baada ya umeng’enyaji kufanyika, hivo kumbe bacteria hwa wanapatikana hata mdomoni na wanaweza kuambukizwa kwa mdomo pia. Sasa kutokana na bacteria hawa kuwa na uwezo wa kujishikiza kwenye kuta za tumbo bila kuathiriwa na tindikali inayomwagwa tumboni basi huweza kusababisha vidonda vya tumbo na saratani pia. Nafahamu kuwa uliwahi kuambiwa kwamba vidonda vya tumbo huletekezwa na tabia ya kutokula kwa wakati ama kukaa na njaa kwa mda mrefu ni kweli ila endelea kusoma makala hiiutajifunza ni kwann H.pylori.

Nini husababisha H.Pylori kuingia kwenye mfumo wa chakula?

Ukirudi mwanzo nmesema bacteria hawa hupatikana kwenye mfumo wa chakula, kuanzia mdomoni hadi kwenye puru, sasa nini kinapelekea mpaka hawa bacteria kumuingia mtu.Chanzo cha kupata bacteria huwa ni kupitia mdomo.  Bacteria hawa hupatikana kwa kiasi kikubwa kwenye maji, hivo kama maji unayokunywa hayajatibiwa ama kuchemshwa basi hatari ya kupata bacteria hawa ni kubwa zaidi, chakula pia unachokula kama kimepata maambukizi ya hawa bacteria basi ukila unameza na hawa bacteria, chanzo kingine ni kupitia ngono, najua kuna kundi kubwa la watu wanaopata maambukizi ya bacteria kupitia kufanya mapenzi kwa kunakohusisha midomo ikiwemo kunyonyana ndimi . Hivo hakikisha mpenzi wako yuko salama kabla hujamuamini manake utajiepusha si tu na H.Pylori bali pia na ugonjwa wa homa ya ini- Hepatatis B.

Vipimo vya namna ya kugundua H.Pylori

Kwa bahati nzuri hospitali zetu nyingi zinatoa huduma ya vipimo kwa gharama nafuu sana hivo kama unapata dalili ambazo nitazielezea hapo chini hakikisha unaenda hospitali kupata vipimo ili uwahi tiba mapema. Dalili hizi ni kama kujiskia tumbo limejaa mda wote hata kama umekula kidogo tu, kutapika na kupata kichefuchefu mara kwa mara, kushuka kwa uzito kwa kasi bila sababu ya msingi, mwili kuwa mzembe na kuchoka sana na maumivu makali ya tumbo, kiungulia, na kupoteza hamu ya chakula, kama tayari uliwahi kuugua vidonda vya tumbo hapo nyuma basi dactari ataangalia rekodi yako ya nyuma na kupendekeza matibabu yanayokufaa.

Tiba kwa H.Pylori

  • Kwenye tiba ya kisasa (conventional medicine) hatua ya kwanza Dactari wakoatakupatia dawa ya kwanza ni kwa ajili ya kuua hawa bacteria wa H.Pylori . hatua ya pili ni kutumia dawa kwa ajili ya kupunguza tindikali inayomwagwa kwenye kuta za tumbo, bada ya hapo itahitajika kufanya ufatiliaji juu ya mwenendo wa tatizo lako ili kuhakikisha kuwa linaisha kabisa.
  • Tiba asili ya H.Pylori (functional medicine); bacteria hawa wanapotibiwa mara kwa mara kupitia tiba ya kisasa zinazotolewa hospitali hufkia kipindi wanakuwa sugu yaani hawasikii dawa, nmekuwa nikipata kesi kama hizi wagonjwa wengi wanasumbuliwa na vidonda vya tumbo sugu ambavyo haviponi, vimechukua miaka mpaka mitano, mpaka wengine hupoteza tumaini. Basi unaweza kujaribu njia zingine za asili ambazo huweza kuua bacteria hawa. Njia za asili hulenga katika kuua bacteria wabaya tu na kaacha bacteria wazuri, kumbuka miili yetu imeumbwa na bacteria wazuri na wanahitajika ili kuweka msawazo.Kumbuka ni muhimu kufika hospitali kupata vipimo na ufatiliaji wa dactari juu ya tatizo lako. Tumia tiba asili kwa uangalifu na kwa kufata ushauri wa mtaalamu wa tiba asili, usinunue kila dawa mtaani zinaweza kuongeza tatizo badala ya kutibu.
  • wasiliana nasi kwa ushauri wa kiafya, huduma ya virutubisho na elimu ya mpangilio wa lishe ili kutibu matatizo mbalimbali ya kiafya. 
  • unaweza kujaribu DIGESTIVE CARE PACKAGE YETU ya siku 30 ambayo itakusaidia kusafisha mfumo wa chakula, na kuua bacteria wabaya.

Tiba zetu ni hakika na tunakuhakikishia kupona kwa 100%.
Gharama za dawa ni sh 150,000/=
Tupigie kwa namba 0678626254 au

Share and Enjoy !

0Shares
0 0