Mawe ya Mfuko wa Nyongo, Maelezo, Ushauri na Tiba Asili

mawe ya ini

Nyongo ni kitu gani?

Ni muhimu kufahamu kwanza kazi ya nyongo na inazalishwa vipi. Nyongo ni kimiminika ambacho hzualishwa na ini. Bilashaka umeshaona wakati ukichinja kuku ama mbuzi, tunakata kifuko cha nyongo na kuitupa kwa vile ikipasuka ni chungu sana inaweza kuharibu nyama.

Sasa nyongo inapozalishwa na ini huhifadiwa kwenye mfuko unaoitwa gallbladder, na nyongo hutumika hasa kurahisisha usagaji wa vyakula vya mafuta. Kwahivo utaona hapa kwamba mfuko wa nyongo umeunganika na sehemu ya tumbo na ni muhimu sana katika uchakataji wa chakula.

Mawe ya Nyongo/Gallstones ni Kitu Gani?

Mawe ya nyongo ni vitu vigumu vinavyopatikana kwenye mfuko wa nyongo unaoitwa gallbladder, kazi ya mfuko huu ikiwa ni kuhifadhi nyongo iliyozalishwa na ini. Mawe haya ya nyongo kitaalamu huitwa gallstones au cholelithiasis. Yanafanyika kwa muunganiko wa chembechembe za mafuta, madini ya calcium na chembechembe zingine zinazopatikana kwenye nyongo.


Chembechembe hizi zinapoungana hufanya vitu vigumu ambayo vinakwama kwenye mfuko wa nyongo na kuletekeza matatizo makubwa kama maumivu chini ya mgongo, tumbo kujaa gesi, kutapika na chakula kutosagwa vizuri tumboni. Kikawaida mfuko wa nyongo unahifadhi kimiminika ambacho ndio nyongo yenyewe na pale inapotokea mawe ama vitu vigumu vikafanyika kwenye mfuko huu basi dalili zake huwa mbaya na dhahiri kwavile ni kitu kigeni kwenye eneo hilo la mwili.

Dalili Za kuonesha una Mawe ya Nyongo ni Kama

  • Maumivu ya tumbo na kujiskia kutapika
  • Kuvurugika kwa tumbo baada ya kula vyakula hasa vyenye mafuta
  • Maumivu makali juu ya tumbo kulia yanyokuja kwa haraka na kuisha baada ya nusu saa.
  • Maumivu chini na nyuma ya bega la kulia

Madhara ya Mawe ya nyongo

Mawe ya nyongo yanaweza yasilete shida kubwa kwa baadhi ya wagonjwa , na kwa wengine inaweza kuwa shida zaidi mpaka kupelekea kufanyiwa upasuaji hata kuondolewa mfuko wote wa nyongo. Kama unahisi una dalili za mawe haya tafadhali nenda hospitali. Daktari anaweza kukufanyia utrasound ama x-ray kugundua uwepo wa tatizo

Makundi gani ya watu yapo kwenye hatari zaidi ya kupata mawe ya Nyongo; Makundi haya ni pamoja na

  • Wanawake
  • Watu wenye umri zaidi ya miaka 40
  • Wenye uzito mkubwa na kitambi (hasa wenye nyama uzembe nyingi kwenye eneo la tumbo)
  • wanaopata lishe duni
  • Wanaopoteza uzito mkubwa kwa haraka sana kwa kujinyima kula
  • wajawazito
  • Wagonjwa wa kisukari
  • Familia yenye historia ya kuugua mawe ya ini
  • Wasiofanya mazoezi ya viungo na
  • Wenye upungufu wa mafuta mazuri mwilini(good HDL)

Uhusiano kati ya Mawe ya Mfuko wa Nyongo na Homoni ya Estrogen

Tafiti zinasema kwamba mawe ya nyongo yanachangiwa zaidi na kupanda kwa homoni ya estrogen mwilini. Na ndio maana inawatokea zaidi wanawake wajawazito au wanaotumia zaidi uzazi wa mpango. Na pia homoni hii ndio sababu kwanini wanawake huugua zaidi kulinganisha na wanaume kutokana na kwamba homoni ya estrogen ni nyingi zaidi kwa wanawake.

Kama hufahamu ni kwamba homoni hii ndio inachangia zaidi uanamke. Kwa maana ya ukuaji wa matiti, nyonga kupanuka na makalio pia.
Homoni ya estrogen inaweza kuongeza kiwango cha mafuta(cholesterol) kwenye nyongo na pia kupunguza kasi ya usafirishaji ndani ya kifuko cha nyongo na hivo kupelekea mawe ya nyongo.

Mtindo wa maisha ni chanzo cha Kuongezeka Kwa homoni ya Estrogen

Kutokana na ongezeko la matumizi ya vitu mbalimbali vinayovuruga homoni ukianzia kwenye urembo, dawa za usafi, kemikali zinazoongezwa kwenye maji ya kunywa, na kwenye vyakula na vinywaji vilivyosindikwa kwa miaka ya hivi karibuni tatizo limeongezeka zaidi.
Kemikali hizi zinaleta matokeo kama homoni ya estrogen na hivo kufanya uchakataji wa mafuta mwilini kuwa mgumu na nyama uzembe kugoma kuisha mwilini.

Matumizi ya dawa mbalimbali zenye estrogen yanaweza kuchangia mawe ya nyongo, mfano dawa kupanga uzazi na dawa za kurekebisha homoni. Dawa za kupunguza cholesterol pia huchangia mawe ya nyongo kwasababu hufanya ini litoe cholesterol nyngi sana na kuimwaga kwenye nyongo ili yaweze kuvunjwavunjwa.

Hatari ya tatizo la Mawe ya Nyongo

Inaaminika kwamba watu wengi wanatembea wakiwa wana changamoto ya mawe ya nyongo pasipo wao kujua. Dalili za mawe ya mfuko wa nyongo zinatofautiana kwa ila mtu kwa ukubwa wa tatizo na muda wa dalili kutokea. Baadhi ya wagonjwa wanaweza kutoonesha dalili zozote kabisa wakati wagonjwa wengine wakipata dalili haraka kama maumivu makali.

Watu wengi dalili hujionesha usiku pale mawe yanapoziba njia ya nyingi kupita kitaalamu inaitwa gallstone attack. Na wengine wanaweza kugundua wana tatizo pale ambapo daktari alikuw akifanya kipimo kwa changamoto ingine ya kiafya mfano CT scan.

Kama tatizo lisipotibiwa mapema mawe ya kifuko cha nyongo yanaweza kusababisha matatizo makubwa hata kupasuka kwa mfuko wa nyingo. Na ndio maana kwa kiasi kikubwa matibabu yake hupelekea upasuaji kuondoa kabisa kifuko cha nyongo.

Hatua Tano za Kutibu Mawe ya Mfuko wa Nyongo

  1. Rekebisha uzito wako
    Uzito mkubwa na kitambi ni kihatarishi kikubwa cha kuugua mawe ya nyongo na hasa kwa wanawake. Tafiti zinasema kwamba watu wenye uzito mkubwa ana kitambi wanazalisha kiwango kikubwa cha mafuta kwenye maini yao na hivo kupelekea mafuta haya kusukumwa zaidi kwenye kifuko cha nyongo hadi kusababisha mawe ya nyongo. Tafiti pia zinasema kwamba watu wenye mafuta mengi yanayozunguka viungo vya mwili na eneo la tumbo wako hatarini zaidi kuugua mawe ya nyongo.
    Hakikisha unapata lishe vizuri unaweza kusoma mpango lishe wetu kupungua uzito kwa kubofya hapa, na pia ukaweka ratiba ya kufanya mazoezi ya viungo.
  2. Usitumie njia hatarishi za kupunguza uzito haraka ndani ya muda mfupi. Tumefahamu kwamba uzito mkubwa na kitambi ni kihatarishi kikubwa cha kupata mawe ya nyongo, lakini pia kupunguza uzito haraka haraka pengine kwa kumeza vidonge siyo salama. Tafiti zinasema kwamba kupungua zaidi ya kilo moja ya ndani ya week moja inakuweka hatarini zaidi kupata mawe ya ini. Inashauri kwamba walau upungue nusu kilo katika week ama kilo 2 au 3 kwa mwezi mmoja.
  3. Shugulisha mwili wako usikae kizembe
    Watu wanaofanya mazoezi na kushugulisha miili yao wanapunguza sana hatari ya kuugua mawe ya ini. Kufanya mazoezi pia kutakusaidia kupunguza uzito mkubwa pasipo kuathiri mwili na pia kurekebisha shinikizo la damu. Ushauri mzuri ni kutnega walau nusu saa mpaka lisaa kufanya mazoezi kila siku.
  4. Tumia aina ya vyakula vya kuimarisha afya ya ini na Mfuko wa nyongo:Vyakula hivi kwa ujumla tunaviita anti-inflammatory diet.Kumbuka kwamba lishe yako ndio mchawi wako mkubwa kwenye afya ya mwili, unaweza kujiwekea utarjiri wa afya ama pia ukabomoa afya yako kupitia tu lishe. Jaribu kula zaidi vyakula vyenye kambakmba kwa wingi na visivyokobolewa(high fiber foods) kama mboga zote za majani, matunda/mbegumbegu, maharage na jamii ya karanga na kunde.
  5. Epuka vyakula vilivyosindikwa maana vingi vmesafishwa sana na kupunguzwa kambakamba na pia vimewekwa sukari nyingi .
  6. Kwenye vyakula vya mafuta pendelea zaidi kutumia mafuta salama ambayo yanachakatwa na mwili kiurahisi , mfano mafuta ya samaki, mafuta ya nazi na olive. Mafuta ya nazi ni mazuri zaidi kwani yanaundwa na aina ya mafuta yakiitwa medium chain fatty acids (MCFAs) ambayo husagwa na mwili kwa urahisi zaidi. Mbegu zenye mafuta kama chia na mbegu za maboga
  7. Kuwa Mwangalifu kwenye matumizi ya Kupanga uzazi
    Njia nyingi za kisasa kupanga uzazi zinavuruga homoni na kuongeza kiwango cha estrogen na hivo kupelekea uzalishaji na uhifadhi mkubwa wa mafuta.Zungumza na daktari wako akwelekeze njia salama za kupanga uzazi ambazo hazivurugi mpangilio wa homoni.

Tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254 kuanza Tiba kwa Tsh 165,000/=

Share and Enjoy !

Shares
Shares