Je ni salama Kujamba? au inategemea na Harufu?
Wengi wetu lazima tumeshapitia hali ya kujamba sana kupita kiasi na kutukosesha raha. Japo kujamba ni kawaida na kila mtu anajamba kila siku, kuna watu wengine wanapata shida ya tumbo kujaa gesi na hivo kutoa gesi chafu mara kwa mara kuliko kawaida. Kitaalamu tatizo hili huitwa flatulence.
Ushuzi ni kitu gani
Ushuzi (fart) hutokana na gesi inayozalishwa tumboni kutokana na hewa tunayovuta na matokeo ya usagaji wa chakula tumboni. Kwahivo kutokea kwa ushuzi inaweza kutofautiana kwa kila mtu kutokana na mazingira na hali yake ya mwili.
Kama ambavyo umewahi kujishuhudia mwenyewe kuna wakati unajamba ushuzi wenye harufu mbaya. Wakati mwingine hakuna harufu, ama unaweza kujamba kwa sauti au pasiwe na sauti.
Mtu mzima mwenye afya anajamba mara 14 mpaka 18 kwa siku. Wakati mwingine anajamba hata bila kujijua kwasabau hakuna harufu au sauti.
Kwahivo unapotaka kuchambua hali ya afya yako ni muhimu zaidi kutazama harufu ya ushuzi na dalili zingine unazopata baada ya kujamba.
Je kuna jambo lolote la Kuhofia kuhusu Kujamba kwako?
Inaweza kuwa ndio au hapana,kwasababu wakati mwingine inategemea na aina ya chakula ulichokula. Mfano ukila vyakula vyenye kambakamba kwa wingi(high-fiber diet) na vyakula asili utapata ushuzi wa kawaida.
Lakini unapojamba kila mara kupita kiasi na ikiambatana na dalili zingine inaweza kuwa ni kiashiria kwamba kuna tatizo kwenye mfumo wako wa chakula. Tatizo hili laweza kuwa ni mabadiliko ya mazingira ya ndani ya tumbo (microbiome), kutokana na kukua kwa bakteria wabaya au fangasi.
Kilichopo kwenye Ushuzi
Fahamu kwamba ushuzi unatengenezwa kwa gesi, na gesi gesi kuu ni Nitrogen. Ambapo watafiti wanasema inachangia kwa asilimia 20 mpaka 90 ya gesi chafu inayotoka wakati umejamba.
Gesi zingine zinazounda ushuzi ni kama carbon dioxide ambayo huchangia asilimia 10 mpaka 30, oxygen ambayo huchangia aslimia 10, methane ambayo inachangia asilimia 10 na gesi ya hydrogen inachangia asilimia 10 mpaka 50.
Muunganiko wa gesi hizi ndio unaofanya harufu mbaya ya ushuzi kwasababu baadhi ya gesi zina kemikali ya sulphur ambayo ndio kiambata kinachotoa harufu. Sulphur hupatikana pia kwenye vyakula kama mayai na mboga kama kabeji.
Kwanini kuna utofauti wa asilimia za gesi zinazounda ushuzi na harufu?
Hii ni kwasababu hali ya ushuzi inatofautiana kwa mtu na mtu kutokana ni kiasi cha hewa aliyobugia, chakula alichokula na hali ya umeng’enyaji wa chakula tumboni.
Unaweza kushangaa ni kwanini unajamba lakini hakuna harufu mbaya inayotoka. Kiambata cha sulphur ndicho hufanya harufu kuwa mbaya zaidi ya kunuka. Asilimia moja tu ya sulphur inaweza kuleta harufu mbaya kwenye ushuzi. Kwahiyo kama aina ya chakula ulichokula kinategeneza sulphur kwa wingi basi ushuzi wako utakuwa unanuka.
Nini hasa kinasababisha Kujamba
Unaweza kuwa unajiuliza nini hasa hupelekea kujikusanya kwa gesi ambayo baadae unaitoa kwa njia ya kujamba. Japo visababishi vya ushuzi vinaweza kutofautiana kwa mtu na mtu lakini gesi inayotolewa ni ile ile haitofautiani.
Gesi iliyojikusanya tumboni hupita kwenye utumbo mdogo na baadae kutolewa nje kama unavyotoa haja kubwa. Wakati mwingine utoaji wa gesi hii unaweza kuambatana na maumivu hali inayoashiria pengine kuna chakula ulichokula kina tatizo. Au hakijachakatwa vizuri na hivo kuchacha.
Tatizo lingine kujaa gesi tumbo kikawaida huambatana na kujamba.
Baadhi ya sababu kwanini gesi inajikusanya tumboni mwako na kukupelekea kujamba ni pamoja na
- Kumeza hewa (aerophagia): Hii inamaanisha kumeza hewa pasipo matarajio ambayo inajikusanya tumbo na kisha unaitoa kwa njia ya kujamba au kwikwi. Sababu mojawapo kwanini unabugia hewa tumboni ni kwasababu unakula chakula haraka au kutotafuna chakula vizuri kabla ya kukimeza. Kwahivo kama unaona wewe ni mtu wa kula haraka , jaribu kurekebisha tabia hii, tafuna taratibu ili usimeze hewa pamoja na chakula.
- Kukusanyika kwa hewa chafu: Kujamba ushuzi unaonuka maranyingi hutokana na gesi inayozalishwa na bacteria waliopo kweye utumbo mpana baada ya uchafu ambayo haujafozwa kuchacha.
- Mabadiliko ya mazingira ya ndani kwenye mfumo wa chakula (microflora): Fahamu kwamba katika mfumo wote wa chakula kuanzia mdomoni, kwenye koo, tumboni, mpaka kwenye utumbo kuna bacteria wazuri na wale wabaya. Bacteria wazuri wanasaidia katika uchaataji wa chakula na pia kama kinga dhidi ya athari za bacteria wabaya. sasa inapotokea bacteria wabaya wamakuwa wengi kuzidi wale wazuri ndipo utaanza kupata matatizo kama gesi tumboni na chakula kutosagwa.
- Constipation(Kupata choo kigumu na kukosa choo kwa muda mrefu: Inaweza kusababisha mkusanyiko wa gesi chafu na kukupelekea kujamba sana kwasababu ukiwa na tatizo hili kasi ya mmen’genyo wa chakula inapungua.
Kwanini watu wengi wanajamba kwa sauti na wengine wanajamba polepole na harufu ni mbaya zaidi?
Hii yaweza kusababishwa na mpangilio wa misuli ya utumbo mpana na eneo la haja kubwa. Baadhi ya misuli inakusaidia kubana ushuzi na kuutoa taratibu pasipo sauti. Kama kila mara ukijamba sauti ni kubwa basi fahamu kwamba misuli ya eneo la haja kubwa(sphincter muscles) imelegea kiasi kiasi cha kuruhusu hewa kutoka bila ridhaa yako.
Je kujamba kuna Faida yoyote kwako? au kuna Madhara?
Kujamba ni kitu cha kawaida na moja ya njia ya mwili kutoa hewa chafu, kama vile tunavyopumua kutoa nje carbondioxide. Kwahivo kama unajamba usihisi kama ni jambo baya la kupambana nalo. Maana wakati mwingine kujamba kunaweza kuwa ni ulinzi na kwama tumbo lako linafanya kazi vizuri.
Vyakula vyenye kambakamba mfano matunda, mboga za majani, viazi, magimbi, uwele na ugali wa dona husababisha gesi kwenye mfumo wako. Lakini bado vyakula hivo vinatoa mbolea kwa bactetia wazuri kukua ambao watakukinga dhidi ya magonjwa kam saratani ya utumbo, kisukari, uzito mkubwa na kitambi na magonjwa ya moyo.
Kwa upande mwingine ni kwamba kama unajamba sana kupita kiasi, inaweza kuashiria kuna tatizo la tumbo matatizo haya ni kama
- Mwili kukataa aina fulani ya chakula(Food intolerance)
- Kutoboka kwa kuta za utumbo mwembamba(leay gut syndrome) na kusababisha sumu na vimelea kuingia kwenye mzunguko wa damu.
- Kukua kwa vimelea kwenye utumbo/small intestinal bacteria overgrowth(SIBO).
Utajuaje kama kujamba kwako si kwa kawaida
Cheki kama kujamba kwako kunaambatana na dalili hizi ndipo uchukue hatua. Dalili hizi ni kama
- Kukosa nguvu na uchovu
- Ngozi kucharuka na kupata rashes au chunusi
- Aleji mfano kutokwa machozi na koo kuwasha
- Kuharisha na kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
- Kupata mkojo wenye damu au kinyesi chenye damu
- Mumivu kwenye kwapa na katikati ya paja na viungo vya uzazi na
- Mabadiliko ya joto la mwili, uzito, usingizi na mpangilio wa hedhi
Namna gani Upunguze Kujamba kupita kiasi
Haya ni matamanio ya kila mmoja wetu ili kupunguza aibu ya kujamba mara kwa mara pengine ukiwa na kundi la watu. Kitu cha kwanza kubadilisha ni lishe yako. Tumbo lako laweza kuwa linapata shida ya kuchakata aina flani ya vyakula au tumbo kuhifadhi zaidi sulphur, fangasi na bacteria.
Zoezi hili ni la kuajaribu maana watakiwa kufatilia ni aina gani ya chakula inakufanya kujamba sana, na siyo kila chakula kinaleta gesi kwa kila mtu. Baadhi ya vyakula vya kutizama zaidi ni kama
- Maharage: Maharage ni chakula kikubwa ksababisha gesi kulio vingine. Ni kwasababu vimejaa aina ya wanga inayoitwa polysaccharides, ambayo inachacha kiurahisi inapoingia tumboni. Huhitaji kuacha kabisa kula maharage, ila fanya kuloweka kwenye maji usiku mmoja kabla ya kuyapika ili kupunza gesi inayozalishwa.
- Maziwa na bidha za maziwa: kushindwa kumeng’enya maziwa (lactose intolerance) ni tatizo kubwa na linawapata watu wengi. Hii ni kwa bidhaa zote za maziwa. Bidhaa za maizwa zina aina ya sukari zinazouwa galactose na glucose amabazo ni ngumu kuchakatwa kiasi cha kupelekea gesi tumboni.
- Mboga zenye sulphur: Mbona mboga zenye sulphur kwa wingi kama kundi la cruiferous, hapa kuna kabeji, broccoli na caulifolower huletekeza gesi kuliko mboga zozote zingine kwasabau zina kambakamba kwa wingi zaidi. Zinapopikwa gesi inapungua kiasi kuliko kuliwa mbichi.
- Vyakula vilivyosindikwa ma kusafishwa(artificial, processed foods): Baadhi ya vyakula vya viwandani vyenye mafuta mabaya vinaweza kuwa vigumu kuchakatwa na hivo kupelekea gesi tumboni. Lenga kula vyakula asili na kutumia mafuta mazuri kama ya nazi na oilve kama kiungo cha kupikia. Kadiri unavokula vyakula asili nivyo unarahisishia kazi tumbo kusaga chakula vizuri.
Badili Mtindo wa Maisha ili Kupunguza Tatizo la Kujamba kwa
- Kufuta kwenye lishe yako vyakula ambavyo siyo rafiki.
- Tumia virutubishi (probiotics) ambavyo vitasaidia kurudia bacteria wazuri tumboni. Vyakula hivi ni kama maziwa asili ya mtindi na sprulina.
- Weka vionjo kwenye lishe yako: Vionjo hivi husaidia kuimarisha usagaji wa chakula na kuua vimelea wabaya tumboni. Vionjo hivi ni kama manjano(tumeric), tangawizi, mdalasini na pilipili.
- Fanya mazoezi na kunywa maji ya kutosha: Vyote hivi kwa pamoja vitakusaidia kutoa uchafu nje ya mwili na kusafirisha virutubishi ndani ya mwili. Mazoezi ya squats ni muhimu zaidi.
Tiba asili ya hakika ili upone kujambajamba ovyo
Kama una tatizo la kujamba sana. Muhimu tukupatie Chai tiba ya intestine Cleansing na vidonge vya gasex utumie pamoja. Itakusaidia kusafisha tumbo na kurekebisha mazingira ya mfumo wa chakula.
Dozi hii yenye chai tiba+Gasex ni Tsh 85,000/= tu kwa dawa zote mbili. Tuandikie kwa whatsapp no 0678626254 kuanza tiba.