Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Nini kinasababisha maumivu ukeni?

maumivu ukeni
maumivu ukeni

Uke ni njia inayopitisha mbegu za kiume kutoka kweye uume kwenda kwenye mji wa mimba. Kupata maumivu ukeni huchangiwa na sababu za kisaikologia ama uwepo wa maambukizi fulani. Kupata tiba ya mapema kwa tatizo lako la uke ni njia nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupata athari zaidi kwa hapo baadae

Dalili za Kupata Maumivu Ukeni

Maumivu ukeni yanatofautiana kwa kutegemea chanzo cha tatizo dalili hizi ni kama ifuatavyo

  • Kupata hali ya kuunguza
  • kuwasha sana ambapo ukijikuna unapata raha
  • Kupata maelengelenge na
  • Maumivuu wakati wa tendo la ndoa

Kama maumivu yako yanatokana na maambukizi eidha ya bacteria ama fangasi basi inaweza kuambatana na kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali.

Nini Kinasababisha Maumivu Ukeni

Visababishi vikubwa vya maumivu ukeni ni maambukizi ya magonjwa ya

  • Fangasi
  • Gonorrhea na
  • Chlamydia

Visababishi vingine ni pamoja na

  • Madhara ya kiafya yaliyotokana na tatizo la kuzaliwa na upasuaji
  • Saratani ya mlango wa kizazi
  • Ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen (huwapata zaidi waliokoma hedhi)

Makundi yaliopo kwenye hatari kupata maumivu ukeni

  • Wanawake wote wapo kwenye hatari ya kupata maumivu ukeni;
    Tatizo la maumivu ya uke huwapata karibu kila mwanamke katika point flani ya maisha yao.
  • Matatizo baadhi ya kiafya huongeza hatari ya kupata maumivu ya uke. mfano mabadiliko ya homoni kutokana na kujifungua, kukoma hedhi au upasuaji wa kuondoa kizazi huongeza hatari ya kupata maumivu makali ukeni.
  • Matumizi ya baadhi ya dawa pia kwa muda mrefu yanaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ukeni
    Wanawake walioenda umri wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana na kukoma hedhi ambapo utengenezaji wa ute unaolainisha uke hupungua kwa kasi.

Vipimo Namna ya kugundua Tatizo kwenye uke.

Kama unapata maumivu ya uke mara kwa mara, weka mihadi uonane na dactari ili akufanyie uchunguzi kujua chanzo cha tatizo lako. Dactari atachukua historia yako ya kuumwa, anaweza kufanya uchunguzi wa kutumia mikono na macho(physical examination) ama uchunguzi zaidi wa maabara kama itatakiwa hivo.

Ukiwa na swali tuandikie kwa Whatsapp no 0678626254

Share and Enjoy !

Shares
Shares