Categories
Dondoo za afya Tendo la ndoa

Nini kinasababisha Mwanamke Kushindwa kufika Kileleni

Orgasmic dysfunction/mwanamke kushindwa kufika kileleni ni hali ya kutifikia raha ya tendo la ndoa. Hali hii inaweza kutokea hata kama mwanamke ameandaliwa vizuri na hisia zake zimeamshwa kufanya mapenzi. Hali hii ya kutofika kileleni inaweza kutokea kwa watu wote mwanamke na wanamume, japo inawapata zaidi wanawake.

Mwanamke Kufika kileleni kupoje

Inawezekana kabisa hujui kufika kileleni ikoje, au pengine hujawahi kufika kileleni hata mara moja katika maisha yako. Usishtue sana, kwasbabu kuna wanawake wana umri wa miaka 40 na hawajawahi kufurahia utamu wa kufika kileleni. Kufika kileleni (orgasm) ni kiwango cha juu cha hisia ambazo mtu anapata pale anapofanya tendo la ndoa. Mguso wa hisia wakati wa kufanya mapenzi hufanya mwili kutoa kemikali ambazo zinakufanya ujiskie raha ya hali ya huu zaidi pale unapokuwa kitandani na mwenzi wako.

Wanawake wengi sana hawajawahi kufika kileleni na kuonja raha ya kufanya tendo la ndoa, japo wengine wamepata na watoto, lakini bado hawajawahi kuona raha ya kufikia mshindo. Nimekuwa nikipokea kesi nyingi za wakina mama kwa tatizo la kutofika kileleni na ndio maana nimeleta makala hii iwe msaada kwako. Endelea kusoma

Nini Kinasababisha Mwanamke Kushindwa kufika Kileleni

Hili ni swali ambalo wengi hujiuliza kwanini jirani yako anafurahia mapenzi lakini kwako tendo la ndoa ni karaha, na pengine unafanya kwa kumridhisha tu mwenzi wako. Ili kujua chanzo cha tatizo lako inatakiwa ufatiliaji wa karibu. Sababu mbalimbali za kimwili, kuhisia au kisaikologia zinaweza kufanya mwanamke kushindwa kufika kileleni. Sababu hizi hatarishi ni kama

  • Umri mkubwa
  • Magonjwa kama kisukari
  • Mgonjwa kuwa na historia ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi
  • Matumizi ya vidonge kwa ajili ya sonona
  • Imani za kidini au kikabila
  • Woga wakati wa kufanya mapenzi
  • Kuhisi kama mwenye makosa kwenye kufanya mapenzi
  • Historia ya kunyanyaswa kingono mfano kubakwa
  • Msongo wa mawazo
  • Kushindwa kutambua thamani yako mfano kuhisi kama huna thamani mbele ya mwenzi wako na jamii kwa ujumla
  • Matatizo kwenye mahusiano na
  • Kuvurugika kwa homoni

Chukua muda utafakari na kujichunguza kwa upande wako nini chanzo kati ya hivi nilivoeleza. Wakati mwingine siyo lazima iwe ni sababu moja tu inayopelekea ushindwe kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa. Yaweza kuwa ni muunganiko wa sababu zaidi ya mbili.

Mwanamke Kushindwa kufika kileleni kunagawanyika katika makundi ma4

  • Primary anorgasmia: Hali ya kutowahi kabisa kufika kileleni hata mara moja
  • Secondary anorgasmia: Kushindwa kufika kileleni japo siku za nyuma uliwahi kufurahia
  • Situational anorgasmia: Hali ya kufika kilelni kwenye matukio flani flani tu, mfano ukifanya ngono kupitia mdomo(oral sex) ama ukipiga punyeto.
  • General anorgasmia: Ni hali ya kutofika kileleni kwenye mwzingira ypyote yale, hata kama utaandaliwa vizuri na kupata msisimuko wa kihisia.

Matibabu kwa Mwanamke Kushindwa Kufika Kileleni

Matibabu ya tatizo hili yanatofautiana kwa kulingana na chanzo chake. Tiba hizi zinaweza kujumuisha

Ushauri kwa wapenzi ni tiba kubwa sana. Mshauri wa mambo ya mahusioano atawasaidia wanandoa kusuluhisha migogoro yao kama ipo. Kwa kesi zingine itahitajika mwanamke kuanza kutumia vidonge ili kurekebisha homoni zake. Baadhi ya virutubisho asili kama soy power na cordyceps vinaweza kutumika ili kumsaidia mwanamke afikie kilele na akafurahia tendo la ndoa.

Watu wanalichukuliaje tatizo hili la Mwanamke kushindwa kufika Kileleni

Mwanamke kushindwa kufika kileleni inaweza kuwa ni tatizo la kuleta mawazo na hata kutishia kuvunjika kwa mahusiano. Wanaume wengi huwalaumu wake zao kwamba wana michepuko ndio maana hawatosheki, jambo ambalo siyo kweli.

Kama wewe ni mwanamke ambaye unapitia tatizo hili tambua kwamba haupo peke ako. Kila siku wanawake zaidi ya 20 hunitafuta kuhitaji tiba ya changamoto hii. Na pia fahamu kwamba inawezekana kutibu tatizo hili na ukafurahia tendo la ndoa. Usiendelee kuficha tatizo na kuigiza kwamba halipo huku unateseka kisaikolojia. Cha muhimu ni kufahamu tu chanzo cha tatizo lako. Unaweza kufika hospitali ukaonana na daktari wako akakupa mwongozo jinsi ya kupata tiba. Ama unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja.

Tuandikie kwa whatsapp no – 0678626254 ili upate tiba asili kwa sh 150,000/= uanze kufurahia utamu wa kufika kileleni.

Bofya makala inayofuata: Kwanini unakuwa mkavu sana ukeni+tiba

Share and Enjoy !

Shares
Shares