Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Nini kinasababisha maumivu ukeni?

maumivu ukeni
maumivu ukeni

Uke ni njia inayopitisha mbegu za kiume kutoka kweye uume kwenda kwenye mji wa mimba. Kupata maumivu ukeni huchangiwa na sababu za kisaikologia ama uwepo wa maambukizi fulani. Kupata tiba ya mapema kwa tatizo lako la uke ni njia nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupata athari zaidi kwa hapo baadae

Dalili za Kupata Maumivu Ukeni

Maumivu ukeni yanatofautiana kwa kutegemea chanzo cha tatizo dalili hizi ni kama ifuatavyo

  • Kupata hali ya kuunguza
  • kuwasha sana ambapo ukijikuna unapata raha
  • Kupata maelengelenge na
  • Maumivuu wakati wa tendo la ndoa

Kama maumivu yako yanatokana na maambukizi eidha ya bacteria ama fangasi basi inaweza kuambatana na kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali.

Nini Kinasababisha Maumivu Ukeni

Visababishi vikubwa vya maumivu ukeni ni maambukizi ya magonjwa ya

  • Fangasi
  • Gonorrhea na
  • Chlamydia

Visababishi vingine ni pamoja na

  • Madhara ya kiafya yaliyotokana na tatizo la kuzaliwa na upasuaji
  • Saratani ya mlango wa kizazi
  • Ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen (huwapata zaidi waliokoma hedhi)

Makundi yaliopo kwenye hatari kupata maumivu ukeni

  • Wanawake wote wapo kwenye hatari ya kupata maumivu ukeni;
    Tatizo la maumivu ya uke huwapata karibu kila mwanamke katika point flani ya maisha yao.
  • Matatizo baadhi ya kiafya huongeza hatari ya kupata maumivu ya uke. mfano mabadiliko ya homoni kutokana na kujifungua, kukoma hedhi au upasuaji wa kuondoa kizazi huongeza hatari ya kupata maumivu makali ukeni.
  • Matumizi ya baadhi ya dawa pia kwa muda mrefu yanaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ukeni
    Wanawake walioenda umri wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana na kukoma hedhi ambapo utengenezaji wa ute unaolainisha uke hupungua kwa kasi.

Vipimo Namna ya kugundua Tatizo kwenye uke.

Kama unapata maumivu ya uke mara kwa mara, weka mihadi uonane na dactari ili akufanyie uchunguzi kujua chanzo cha tatizo lako. Dactari atachukua historia yako ya kuumwa, anaweza kufanya uchunguzi wa kutumia mikono na macho(physical examination) ama uchunguzi zaidi wa maabara kama itatakiwa hivo.

Ukiwa na swali tuandikie kwa Whatsapp no 0678626254

Share and Enjoy !

Shares
Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Muwasho ukeni

Muwasho Ukeni

muwasho ukeni

Muwasho ukeni na hali ya kuungua kwa uke mithili ya moto ni tatizo linalowaumiza sana wanawake na kuleta usumbufu mkubwa. dalili hizi zinaweza kuwa ni matokeo ya tatizo kubwa la kiafya ndio maana kuna umuhimu wa kumwona dactari mapema pale unapoona hali imezidi kuwa mbaya. Kwenye makala yetu ya leo tutajifunza

  • Nini husababisha Muwasho ukeni, kuchomachoma na kuvimba
  • Namna tatizo linavotibiwa na
  • Tiba ya nyumbani unayoweza kutumia kupunguza makali ya tatizo na kuzuia

Nini Husababisha Muwasho ukeni kuchomachoma na kuvimba

Kuna sababu nyingi zinazopelekea muwasho ukeni ambazo ni pamoja na

Maambukizi ya bacteria ukeni (bacterial vaginosis)

Maambukizi ya bacteria ukeni ni moja ya maambukizi yanayowatokea mara kwa mara wanawake. Wengi wanaoathirika ni wale wanaojihusisha na ngono zaidi, wenye kinga dhaifu na wajawazito. Watafiti wanasema kinachosababisha Bacterial vaginosisi ni kuvurugika kwa uwiano wa viumbe kwenye mazingira ya uke (vaginal microflora) ambayo inahusisha uwepo wa bacteria na fangasi pia.
Kuvurugika huku kwa mazingira ya uke kunaweza kuletekekezwa na sababu nyingi ikiwemo, kudhoofika kwa kinga ya mwili na mabadiliko ya pH- kikawaida uke una tindikali zaidi 3.8-4.2 ni kawaida na pH zaidi ya 4.5 siyo salama kwa afya ya uke.

Vipimo kwa tatizo la Muwasho ukeni

Mara nyingi tatizo ua kuwasha ukeni huisha ndani ya siku chache baada ya kuanza. Kama tatizo litaendelea na dalili kuwa kali zaidi wek apointment uonane na dactari kupata vipimo na tiba. Dactari atafanya pelvic examnation ambapo atangalia dalili anazopata mgonjwa kwenye via vya uzazi (eneo la nje la uke, mfuko wa mimba, mlango wa kizazi, mirija ya uzazi, kibofu cha mkojo na mifuko ya mayai, ) Daktari pia anaweza kuchukua sampuli ya uchafu unaotoka na kuufanyia vipimo ili kugundua chanzo cha tatizo.

Kwa hivo tiba ya tatizo hili la kuwasha kwa uke itategemea na chanzo ama ugonjwa unaosababisha kama ugonjwa ni

  • Maambukizi ya bacteria (Bacterial vagoniosis): mgonjwa hupewa antibitics na antiparastis ili kuua vimelea vya ugonjwa
  • Yeast infection (candidiasis): mgonjwa hupewa daw za kuua fangasi, antifungal ambazo humeza na zingine kuweka ukeni.
  • Menopause: kama chanzo ni kukoma hedhi basi mgonjwaanaweza kupata dawa na virutubisho vya kuongeza uzalishaji wa homoni ya estrogen.

Ushauri wa Kufuata na Tiba Mbadala kama Unapata Shida ya Muwasho Ukeni.

Zifuatazo ni hatua za kuchuka ili kuzuia na kutibu muwasho ukeni.

  • Epuka kuvaa pedi, kutumia cream na spray zenye harufu kali tabia hizi zinaharibu mazingira ya ukeni na kutoa mwanya wa fangasi na bacteria kukua.
  • Tumia maji na sabuni zisizo na kemikali kujisafisha ukeni na usioshe uke zaidi ya mara moja kwa siku.
  • Siku zote unapojisafisha ukeni ama ehemu ya haja kubwa basi jifute kuanzia mbele kwenda nyuma. Kufanya hizi inazuia kusambaa kwa bacteria walioko mkunduni kwenda ukeni.
  • Vaa nguo za ndani za pamba ambazo huruhusu hewa kupita na kukausha unyevu ambao ni mbolea kwa fangasi na bacteria wabaya.
  • Epuka kufanya douching
  • Kwa watoto wadogo, wabadilishiwe diepers zao mara kwa mara
  • Tumia condom ili kujikinga na magonjwa ya zinaa
  • Usifanye ngono mpaka pale uatakapopona ugonjwa unaosababisha upate muwasho ukeni.
  • Onana na Daktari haraka pale unapoona dalili zisizo za kawaida kama kutokwa na uchafu unaonuka mfululizo, kuwasha kwa uke, kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya nyonga na mabadiliko kwenye hedhi.

Muhimu kwa Tatizo la Muwasho ukeni

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya muwasho na harufu mbaya ukeni,hedhi kuvurugika, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na kutibu maambukizi.

Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge viwili vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama , harufu mbaya ukeni, muwasho, fangasi, PID na maambukizi ya bakteria.

vidonge vya kusafisha kizazi ucp

Vidonge hivi vinatumika kwa siku 7. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika siku 1,unaweka tena kidonge kingine. Gharama ni sh 50,000/= kwa dozi moja. Muhimu mgonjwa atumie dozi mbili.

Angalizo Unapotumia Uterus Cleansing Pill

UCP haifai kutumiwa na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi na pia ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

ANGALIZO

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata huduma

Share and Enjoy !

Shares
Categories
wanawake

Jinsi ya kuondoa michirizi na mikunjokunjo kwenye ngozi

mikunjo kwenye mapaja na michirizi
michirizi

Michirizi na mikunjokunjo kwenye ngozi ya mapaja, tumbo na kwenye mikono ni tatizo linalowatesa zaidi wanawake. Kwani wengi wanahangaika ili kuondokana na tatizo hili bila mafanikio. Pamoja na kutumia vipodozi na cream mbalimbali bado tatizo halijaisha.

Tatizo linapelekea wadada kuona aibu, kushindwa kujiachia na kutovaa nguo wanazozitaka kwa kuogopa mikunjo kuonekana.  Makala yangu ya leo itaangalia tatizo kwa upana wake na kukupa mpangilio wa lishe. Pamoja na njia za asili za kutibu tatizo lako ili ufurahie urembo wako wa mwili Karibu.

Cellulite ni kitu gani?

Cellulite ni mwonekano wa mikunjokunjo na mistari kwenye ngozi ya mwili. Mistari hii hutokea zaidi kwenye eneo la tumbo, chini ya mikono, kwenye mapaja na matako. Cellulite hutokea zaidi kadiri umri unavoenda. Baadhi ya vitu vinavyoletekeza mikunjokunjo kwenye ngozi ni pamoja na kuvurugika kwa homoni, pamoja na kutokufanya mazoezi.

Wanawake wanapata zaidi Michirizi kuliko Wanaume

Tatizo hili huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume ambapo kutokana na unene. Unene kupita kiasi hupelekea leya ya ndani yenye mafuta (fat globules) kuwa na msuguano na tishu za ngozi na hivo kupelekea mikunjokunjo na michirizi kwenye ngozi.

Tafiti zinasema kwamba asilimia 80 ya wanawake wana tatizo hili la cellulite ambapo wengi wanalipata kadiri wanavozeeka kwa ngozi kupungua uwezo wa kuvutika na kusababisha nyama kuanguka na kuleta mikunjokunjo.

Kuwa na michirizi siyo tatizo kiafya ndio maana wengi huliacha kama lilivyo bila kushughulika nalo. Lakini kama wewe ni mwanamke unayependa urembo na unapenda kujiachia maeneo kama beach na sehemu za wazi basi hiki kitakuwa kikwazo sana. Maana utaogopa kuonekana na watu kwamba ngozi yako ina kasoro ndio maana nimeandika makala hii ikusaidie.

Nini kinasababisha Mikunjokunjo Kwenye Ngozi-Cellulite

Mazingira hatarishi na sababu zinazochangia upate mikunjokunjo na michirizi kwenye ngozi ni pamoja na

  • Lishe mbovu
  • Mwili kubakiza maji tumboni (fluid retention ambapo wakati mwingie hupelekea tumbo kujaa gesi)
  • Damu kutozunguka vizuri
  • Udhaivu wa tishu zenye  Collagen na kuepelekea kujikunja kiurahisi
  • Mabadiliko ya homoni
  • Mwili kukosa mazoezi na kutoshugulika
  • Msongo wa mawazo kupita kiasi ambao hupunguza uzazlishaji wa collagen: collagen ni kiungo kilichosheni protini ambacho kinatengeneza shape na tishu za ngozi. hivo kufanya ngozi ya mtu kuonekana bado changa.
  • Historia ya magonjwa mfano magonjwa ya autoimmune, kisukari, watu wanaovuta sigara na wenye alegi/mzio.

Sasa umejifunza jinsi sababu za kimaisha zinavoharibu mwonekano wa ngozi yako na tayari umejua chanzo cha tatizo lako kuwa ni kwenye lishe. Ni wazi sasa kwamba dawa na cream za kupata kwenye ngozi au mikanda ya kuvaa ili upunguze michirizi siyo suluhisho salama na la kudumu. Bali unatakiwa kubadili mtindo wa maisha  kwenye lishe na kuweka ratiba ya mazoezi.

Tiba Asili ili Kuondoa Michirizi na Mikunjokunjo kwenye Ngozi Yako

Hizi ni njia zangu 5 zitakazokusaidia kuondoa shida ya michirizi.
Angalizo: Kama wewe unataka njia za haraka haraka basi hutazipata hapa. Maana ninaelekeza namna ya kubadili mtindo wa maisha ili uepuke tatizo miaka yote. 

1.Kula Lishe Bora

Kama tulivosoma pale juu kuna uhusiano mkubwa kati ya uzito mkubwa na kitambi na kupata mikunjokunjo. Hivo punguza vyakula vya wanga na sukari na kula zaidi vyakula vya mafuta kama nyama, parachichi, nazi namafuta ya nazi, samaki nk. weka ratiba ya kupunguza unene wako uliopitiliza kwa kufanya mazoezi na kushugulisha mwili wako.

Baadhi ya vyakula vingine  vya kutumia kwa wingi kwenye safari yako ya kuondoa mikunjokunjo kwenye ngozi ni kama

2.Tumia Collagen ya Kutosha

Kama tulivojifunza mwanzoni ni kwamba Tishu za ngozi zimetengenezwa kwa protini za Collagen. Kwahiyo kama ngozi yako ipo imara basi utapunguza uwezekano wakupata mikunjokunjo. Collagen ni protini inayopatikana kwa wingi kwenye ngozi na husaidia kuvutika na kufanya ngozi kuwa hai na laini. Chanzo kizuri cha Collagen ni kunywa supu ya mifupa (bone broth) . Supu ya mifupa ina amino acid kwa wingi ambazo hutengeneza collagen. Collagen iliyopo kwenye Supu ya mifupa  husaidia kuimarisha tishu za ngozi na kuondoa tatizo la cellulite.

3.Tumia virutubisho

Vya kuondoa mikunjokunjo kwenye ngozi na michirizi (anti-cellulite Suppliments): unaweza kufika ofsini kwetu ukatumia virutubisho kama Royal gel na sipiriluna vikakusaidia kupambana na tatizo lako bila kikwazo.

4.Fanya mazoezi kila mara

Mazoezi ni njia nzuri sana pale unapotaka kupunguza uzito, tumeona pale juu athari za uzito mkubwa na kitambi kwenye kupata mikunjokunjo, pamoja na kula lishe nzuri ni muhimu sasa uweke ratiba ya kufanya mazoezi walau mara tatu kwa week.

5.Tumia mafuta asili ya nazi kwenye kutibu ngozi yako.

Unaweza kutumia mafuta halisi ya nazi kwa kupaka kwenye ngozi yako baada ya kuoga. Kumbuka cream za madukani zinaweza kuwa ghali na hatari kwa afya yako kwa maana zina kemikali na metali nzito ambazo ni sumu kwa afya ya ngozi.

Maelezo ya Mwisho pale Unapopambana na Cellulite

  • Cellulite ni mwonekano wa mikunjokunjo kwenye ngozi na hii ni kutokana na kusuguana kwa leya ya mafuta na tishu za ngozi
  • Sababu zinazopelekea upate mikunjokunjo kwenye ngozi ni pamoja na uzito mkubwa, lishe mbaya, kubakiza maji ama mwili kukosa kabisa maji, matatizo kwenye usafirishaji mwilini na udhaifu wa tishu zenye collagen kwenye ngozi
  • Kupunguza uzito, kula vyakula asili vyenye kambakamba na kufanya mazoezi ,  husaidia kupunguza sana tatizo la cellulite.

Tuandikie kwa namba 0746672914 .Kwa maswali na maoni yako au unataka kufika ofsini uonane nami nikupe ushauri namna ya kuondokana na tatizo la mikunjokunjo kwenye mapaja na ngozi

Mafuta ya lavender

Mafuta ya lavender au mrujuani ni moja ya mafuta yanayotumika zaidi kwenye kundi la (essential oil) lakini faida zake ziligunduliwa kwa zaidi ya miaka 2500 iliyopita katika kutibu magonjwa na matatizo ya ngozi.

Matumizi ya mafuta ya lavenda kwa kupakaa kwenye ngozi huzuia na kuondoa chunusi na matatizo mengine ya ngozi kama madoa, michirizi, mikunjokunjo na pia kupunguza kasi ya kuzeeka kwa ngozi.

Mafuta ya levender yamekuwa adimu sana kutokana na uwezo wake mkubwa kupambana na matatizo ya ngozi. Fika ofsini hapa Magomeni Mwembechai upate mafuta haya ambayo ni original na asili. Gharama ya mafuta ni sh 40,000/=

Tuandikie kwa Whatsapp no 0678626254 kupata dawa kwa sh 40,000/=

Bofya makala inayofuata:Hedhi kutoka muda mrefu bila kukoma

Share and Enjoy !

Shares
Categories
Afya ya mwanamke na uzazi salama

Kulegea kwa uke

Je Inawezekana Kutibu Kulegea Kwa Uke?

kulegea kwa uke

Kulegea kwa uke ni moja ya mada inayowakuna sana wakina mama na wakina dada . Wengi hupendelea zaidi kuwa na uke uliobana ili kuwafurahisha wenza wao. Kuna nadharia dhana potofu nyingi sana kuhusu suala la uke wengine huamini kwamba uke unatakiwa kupoteza hali ya kutanuka na kusinyaa na kuwa mkubwa miaka yote.

Uke ni kiungo chenye lastiki, maana yake kinaweza kunanuka ili kuruhusu kutoka mfano mtoto na vitu kuingia yani uume. Lakini haitachukua muda mrefu kwa uke kusinyaa na kurudi katika hali ya kawaida.

Misuli ya uke

Uke hutanuka, kulegelea  na kuongezeka ukubwa kiasi fulani kadiri umri unavoongezeka na unavozaa zaidi. Sasa endelea kusoma makala yetu hii ili ufahamu vyema uke wako pamoja na fikra potofu kuhusu uke.

Nataka nikwambie kulegea kwa uke ni dhana mbaya ambayo inatumika kuwadhalilisha wanawake. Inawatokea zaidi hasa pale wanapoachana na wanaume zao. Wanaume hutumia hiki kama kigezo na silaha ya kuwadhalilisha wanawake kwamba wana uke mpana na wenye maji (bwawa) kitendo ambacho siyo kizuri.

Dhana potofu ni kwamba mwanamke mwenye kulegea kwa uke amekutana kimapenzi na wanaume wengi. Ukweli ni kwamba haijalishi umekutana na wanaume wangapi uke ni lastiki unaweza kutanuka na kusinyaa na ukaendelea kuwa kwenye ubora wake kama kawaida.

Uke mkavu yaweza kushiria ugonjwa

Ni muhimu kufahamu kwamba kuwa na uke uliokaza sana inaweza kuashiria una tatizo la kiafya. Hasa pale unapoingiliwa na kupata maumivu makali pamoja na kwamba mwenza wako amekuandaa vizuri. Mwili wa mwanamke unaposisimka misuli ya uke inalegea ili kuruhusu uume kupenya vizuri.

Kama misuli ya uke bado imekaza basi itakufanya upate maumivu makali sana na hutofurahia na kumaliza tendo la ndoa. Kama tatizo la maumivu ya uke yataendelea basi weka apointment na daktari wa magonjwa ya wanawake ili upate vipimo na ushauri zaidi maana unaweza kuwa na matatizo yafuatayo.

Hujaandaliwa vizuri na uke wako haujalainika inavotakiwa

Mwili wa mwanamke unaposisimuliwa basi huweza kutoa majimaji ya asili ambayo hulaishisha uke. Hivo hakikisha mwenza wako anakuaanda vizuri kabla ya kukuingilia. Kama una tatizo la kupata majimaji kidogo haijalishi umeandaliwa kiasi gani basi bofya hapa kutembelea stoo yetu kuagiza virutubisho ili ufurahie tendo la ndoa.

Maambukizi au ugonjwa

Maambukizi hasa ya kupitia ngono ni chanzo cha kupata maumivu wakati wa tendo. Maambukizi haya yanaweza kuwa ya fangasi au bakteria

Ajali na Msongo wa mawazo kupita kiasi.

Ajali kwenye maeneo ya nyonga na mfumo wa uzazi kwa ujumla inaweza kusababisha maumivu makali wakati wa tendo la ndoa na kukaza kwa uke. Hivo hakikisha umepona vizuri kabla hujaanza kushiriki ngono

Tatizo la Viginismus

Vaginismus ni tatizo la uke ambapo misuli ya uke inaweza kukaza pasipo hiyari ya mwanamke na hivo kuzuia uume kupenya. Wanawake wachache sana hukubwa na tatizo hili yaweza kuwa mmoja kati ya wanawake 500. Tatizo hili linaweza kuletekezwa na hofu na msongo wa mawazo. Dactari anaweza kutumia tiba zaidi ya moja katika kutatua shida hii ikiwemo kuongea na mgonjwa na kumshauri ama kutumia vifaa vya kutanua uke.

Ubora wa Uke Unabadilika Kadiri ya Muda na Umri

Fahamu kwamba vitu viwili vikubwa vinavyoathiri ubora na uwezo wa kunanuka na kusinyaa kwa uke ni umri na mara ngapi umezaa watoto. Kufanya ngono mara kwa mara na kubadilisha wanaume siyo tatizo na haviathiri uke wako.

Kadiri unavozaa zaidi ndivyo misuli ya uke huchoka na kulegea. Wanawake waliozaa zaidi ya mara moja huchoka zaidi. Umri pia kadiri unavosonga ndivyo uke huchoka zaidi hatakama uliwahi kujifunguaama laa.

Kulegea Kwa Uke Kutokana na Umri

Unapofikia umri kuanzia miaka ya 40 utaanza kuona mabadiliko. Hii ni kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen pale unapokaribia kukoma hedhi (menopause). Utaanza kupata dalili kama

  • Uke kusinyaa na  kuwa mdogo
  • Kukauka kwa uke
  • Kupungua kwa tindikali kwenye uke
  • Uwezo wa kutanuka kupungua

Kulegea kwa Uke Kutokana na Kuzaa

Ni kawaida kwa uke kulegea na kupungua ubora wake baada ya kujifungua. Hii inatokana na misuli ya uke kunanuka sana ili kuruhusu mtoto kupita. Baada ya kujifungua utagundua kwamba uke umebadilika kuliko ulivyokuwa mwanzo. Usipate shaka maana hii ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke lakini isichukue muda mrefu.

Maana uke unatakiwa urudi katika ubora wake baada ya miezi kadhaa. Japo haitarudi 100% kama shape ya mwanzo. Kama umejifungua mara nyingi zaidi basi uke utakuwa umetanuka zaidi na kupoteza lastiki yake kwa kiasi kikubwa. Najua hii ni habari mbaya kwa wengi lakini usipate shaka nitakuelekeza mazoezi ya kufanya pamoja na virutubisho vya kutumia ili kukaza uke na   kurudi kama zamani.

Jinsi ya Kukaza Misuli ya Uke Iliyolegea Kupitia Mazoezi ya Nyonga

Mazoezi ya nyonga ni njia nzuri na salama ya kukaza misuli ya uke inayoitwa(pelvic floor muscles). Misuli hii inasaidia kuweka sapoti kwenye

  • Kibofu cha mkojo
  • Kwenye eneo la haja kubwa
  • Utumbo mdogo na
  • Mfuko wa mimba (uterus)

Misuli ya pelvic floor inapolegea kutokana na umri kwenda ama kuzaa: basi utaanza kupata dalili kama

  • Kuponyoka kwa mkojo pasipo na hiyari yako
  • Kujiskia hali ya kukojoa mara kwa mara
  • Kupata maumivu ya nyonga na
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa

Mazoezi ya pelvic floor yanaweza kukusaidia kwa kesi za kurudisha ubora wa uke, lakini kama unashindwa kudhibiti mkojo mara kwa mara na kuvuja basi hakikisha unapata vipimo maana yaweza kuwa una shida ingine kubwa ya kiafya. Najua sasa unahamu ya kusikia kuhusu mazoezi haya basi na tuanze kuyachambua

Kegel Exercise

Kwanza unatakiwa kufahamu kuhusu misuli inayohusika katika kukusaidia kwenye safari yako ya kukaza uke. Fanya zoezi hili wakati unakojoa bana mkojo katikati.Ukifanikiwa zoezi hili basi tayari umetambua misuli yako ya kuitumia katika zoezi linalofuata, malizia kutoa mkojo iliobaki baada ya hapo fuata maelekezo haya

  1. Tafuta mahali pazuri pa kufanyia zoezi ukiwa nyumbani kwako, sehemu ambayo unaweza kulala chali ili tuanze zoezi
  2. Kumbuka misuli uliyokaza pale ulipokuwa unakojoa, basi tumia misuli hiyo hiyo.
  3. Kaza misuli yako kwa sekunde 5, kisha relax kwa sekunde 5 zingine
  4. Rudia zoezi hili mpaka awamu 5 kwa wakati mmoja unakaza unaachia

Kadiri unavoendelea na kulizoea zoezi hil basi ongeza muda wa kufanya zoezi hadi sekunde 10 kutoka sekunde 5 za awali. Hakikisha usitumie misuli ya tako, tumia misuli ya ndani ya uke na nyonga (pelvic floor muscles). Kwa matokeo mazuri zaidi fanya seti 3 za mazoezi ya kegel mara 5 mpaka 10 kwa siku.

Pelvic Tilt Exercise

Mazoezi ya kegel

Kukaza uke kwa kutumia zoezi hili fuata maelekezo haya

  1.  Lala chali kwenye floo  kisha mikono inyooshe chini
  2. Vuta tumbo kuelekea ndani kwa kubinuka kuelekea juu, unapofanya hivi sehemu ya mgongo itakuwa flati
  3. Endelea kukaza tumbo lako kwa sekende 4 bila kuachia
  4. Rudia hili zoezi mara 10 kwa kukaza na kuachia kila baada ya sekunde 4, ndani ya muda mmoja na urudie seti 5 ndani ya siku moja.

Jaribu Green health Uterus Cleansing Package Yetu.

Ni muunganiko wa virutubisho vya asili aina mbili zilizohifadhiwa katika mfumo wa vidonge 60. Vitakusaidia

  1. Kubalansi homoni za kike na kuimarisha ufanyaji kazi wa ovari
  2. Kuimarisha misuli ya uke na kujenga kuta za uke
  3. Kulainisha ngozi na kupunguza kasi ya uzee
  4. Kuzuia kutokea kwa saratani ya matiti
  5. Kuua bacteria wabaya na fangas (candidiasis) na kuimarisha kinga ya mwiliVirtubisho hivi vinawafaa zaidi wanawake
  • Wenye ute mdogo ukeni
  • Waliokoma hedhi
  • Wenye matatizo ya uke kusinyaa na kulegea
  • Wawagumba kutokana na kuvurugika kwa homoni na
  • Wanawake wanaotaka kuboresha afya zao

Muhimu kwa Wanawake wa tatizo la Kulegea kwa Uke

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya kulegea kwa uke na maambukizi ya bacteria ukeni tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na kuimarisha misuli ya uke. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama, kulegea kwa misuli ya uke, harufu mbaya ukeni, muwasho, fangasi na PID.

vidonge vya kusafisha kizazi na kuimarisha uke

Vidonge hivi vinatumika kwa siku 7. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika siku 1,unaweka tena kidonge kingine

Angalizo Wakati Unatumia Uterus cleansing Pills.

UCP haifai kutumiwa na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi na pia ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

Ofisi yetu ipo Mwembechai, Magomeni Dar eslaam.

Bei ya Ucp ni Tsh 50,000/ kwa dozi moja.Tunashauri utumie dozi mbili.
Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

Share and Enjoy !

Shares
Shares