Baridi Yabisi

Ugonjwa wa Baridi Yabisi (Arthritis)

maumivu ya baridi yabisi
maumivu ya baridi yabisi

Baridi yabisi ni moja ya magonjwa kwenye kundi la (autoimmune diseases) magonjwa yanayotokana na kinga ya mwili kushambulia tishu za mwili na kupekelea tishu hizi kututumka na kuvimba.Tatizo hili huathiri maeneo ya maungo na kuletekeza maumivu makali yasiyokwisha, kuvimba kwa joint na kusababisha ugumu kukunja viungo. Changamoto inaweza kuwa kubwa pale mpambano kwenye joint (inflammation) unapokuwa mkubwa na baadae maumivu hupungua.

Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ni muhimu kurekebisha lishe na mtindo wa maisha kama ambavyo nitaelekeza hapa chini ili kupunguza makali ya ugonjwa. Ugonjwa wa baridi yabisi kama usipochukuliwa hatua za haraka kuudhibiti unaweza kusababisha matatizo makubwa kama kuharibika kwa maungio, neva na athari kwenye mishipa ya damu.

Baridi yabisi husababishwa na muunganiko wa sababu ikiwemo lishe, vinasaba, mtindo wa maisha, vichocheo pamoja na kinga ya mwili.Tafiti zinasema kwamba kwa mgonjwa anayeanza tiba mapema hupata nafuu zaidi na kuepuka madhara ya baridi yabisi. Pamoja na dawa za hospitali wataalamu wa tiba asili tunashauri mgonjwa azingatie zaidi lishe na mazoezi ili kupunguza maumivu.

Dalili za Mgonjwa Mwenye Baridi Yabisi.

Dalili za baridi yabisi hutokana na kupotea kwa utando mweupe uliopo mwishoni mwa mfupa (cartilage). Utando ambao hupunguza msuguano kati ya mfupa na mfupa. Kuvimba kwa tishu zinazozunguka jointi na kukaza kwa joint. Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ute uliopo kati ya mfupa na mfupa hupungua na kufanya mifupa kusagana. Dalili kuu za mgonjwa mwenye baridi yabisi ni

  • Maumivu ya joint-Kuvimba kwa tishu zinazozunguka maungio ya mifupa husababisha maumivu makali kwa mgonjwa. Jointi zinazoathirika zaidi ni kwenye mikono, enka, vidole vya miguuni na kwenye magoti.
  • Ngozi ya joints kuwa nyekundu, laini na inayochoma kama vile imeungua moto.
  • Maumivu na kushindwa kusonga mbele baada ya kuamka asubuhi, hali hii huchukua dakika 30 na baaade mgonjwa anaweza kuendelea kutembea.
  • Mwili kufa ganzi na maumivu ya misuli
  • Kupata ugumu kwenye kutembea, kushika kitu, kufanya mazoezi na kupanda ngazi.
  • Kwa baadhi ya wagonjwa hupoteza hamu ya kula na kupata homa za muda mfupi.

Madhara gani ya Muda Mrefu Anaweza Kupata Mtu Mwenye Baridi Yabisi.

Kwa baadhi ya wagonjwa wenye baridi yabisi hupata madhara ya kiafya ya muda mrefu mwilini. Tafiti zimebaini matatizo haya huzaliwa na uwepo wa arthritis.

  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.
  • Maumivu ya kifua, pumzi kukata na kushindwa kupumua kutokana na athari kwenye mapafu.
  • Maumivu ya kichwa yasiyoisha.
  • Matatizo ya figo na kujikusanya kwa maji mwilini
  • Maumivu na kudhoofika kwa mifupa
  • Kuishiwa damu na kupata ganzi
  • Kuota vinyama vidogo vidogo kuzunguka eneo la maungio ambavyo huongeza ukali wa maumivu

Nini Kinasababisha Uugue Baridi Yabisi

Kama nilivoeleza mwanzo ugonjwa huu ni moja ya kundi la magonjwa ya autoimmune. Kumanisha kwamba ugonjwa unaletekezwa na mazingira ambayo husababisha kinga yako ya mwili ishambulie kimakosa tishu zinazozunguka maungio ya mifupa.

Swali la msingi ni kwanini kinga ya mwili ishambulie tishu kimakosa? Mpambano kwenye tishu inaweza kuletekezwa na vihatarishi vifuatavyo

  • Kuzorota kwa afya ya mfumo wa chakula
    Lishe mbaya na vyakula vinavyoleta alegi (vyakula vinavyoletekeza mpambano kama vyakula vilivyosndikwa, sukari na vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta)
  • Uzito mkubwa na kitambi hasa kwa watu chini ya umri wa miaka 55
    Mazingira yenye sumu ambayo yanaathiri mwili na kuvuruga mpangilio wa homoni, ndomana tunashauri utumie Detox Care Package yetu kutoa sumu kwanza kabla hujaanza tiba nyingine.
  • Kushuka kwa utendaji wa kinga ya mwili kutokana na athari za kiafya na
  • Uvutaji wa sigara

Tiba Asili na Jinsi ya Kukabiliana na Tatizo la Baridi Yabisi.

Kwa kutumia virutubisho ukiwa nyumbani.

Mara nyingi madactari wanapogundua una baridi yabisi, watakwandikia vidonge ambavyo ni antiinfammatory na pain killers kwa ajili ya kupunguza mpambano na maumivu kwa muda mfupi. Tatizo la tiba hii ni ya muda mfupi na mgonjwa hurejea katika hali ya mateso akishamaliza kuvitumia.

Ndio maana nashauri kulenga chanzo cha tatizo lako na kutumia njia asili kutibu uginjwa wako. Zifuatazo ni hatua salama unazoweza kuchukua ukiwa nyumbani kwako ili upunguze makali ya ugonjwa na kutibu.

Hatua ya kwanza: Tumia Lishe inayosaidia kupunguza kuvimba na kututumka kwa tishu (Anti-inflammatory Diet)

Wataalamu wa lishe wanashauri matumizi lishe sahihi katika kupunguza kuvimba kwa tishu kutokana na kushambuliwa na kinga ya mwili. Lishe hii inajumuisha vyakula vyenye mafuta mazuri kama mafuta ya kupikia ya nazi,mizeituni, mboga za majani, supu ya mifupa, vyakula vyenye omega 3 kwa wingi kama walanut (lozi) na samaki wa kina kirefu.

Ni muhimu pia kuepuka vyakula vinavyoongeza kuvimba kwa tishu za kwenye maungio, vyakula vya ngano, sukari, vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta,  na vyakula vyote vilivyosindikwa.

Hatua ya pili: Kufanya mazoezi mara kwa mara

Najua unapata maumivu makali kwenye maungio kutokana na ugonjwa wa baridi yabisi. Lakini ni muhimu kushugulisha mwili wako ili kupunguza athari ya tatizo. Ndio maana unapolala ukaamuka asubuhi unapata ugumu kutembea na kuendelea. Hakikisha unafanya mazoezi mepesi kila siku wakati huo unazingatia sheria zingine nitakazofafanua.

Hatua ya tatu: Punguza msongo wa mawazo na Hakikisha unapata usingizi wa kutosha

Kupata usingizi wa kutosha kila siku kuanzia masaa 8 na kupunguza msongo wa mawazo inasaidia joint kujitibu vizuri. Msongo wa mawazo unafanya tatizo kuwa baya zaidi na kukuongezea dalili zingine mbaya kama maumivu ya misuli, kushuka kwa kinga, kushambuliwa na magonjwa, na uzito kuongezeka kupita kiasi.

Hatua ya 4: Tumia njia za asili ili kupunguza maumivu ya jointi. Njia hizi ni kama

  • kufanya masaji kwenye eneo lililoathirika kwa kutumia mafuta ya eucalyptus.
  • Weka kipande cha barafu kwenye eneo ya maungio yya mifupa

Jaribu pia tiba yetu asili Kupitia Dawa Asili za Joint Health na Omega 3 fish oil.

.

Gharama ya Tiba ni Tsh 175,000/= dozi ya mwezi mmoja, ofisi yetu ni hapa Mwembechai Magomeni. Tuandikie kwa whatsapp no 0678626254 kupata dawa

Share and Enjoy !

Shares

One reply on “Baridi Yabisi”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shares