Uzito mkubwa na kitambi

Jinsi ya kufanya mwili wako kuwa mashine inayounguza mafuta

Kwa mwenendo mzuri wa maisha utakayo ishi nayo unaweza kuubadili mwili wako kuanzia leo kuwa mashine inayo unguza mafuta bila hata kuwa unahangaika kutumia bidhaa za kupunguza uzito zenye gharama kubwa.

Watu wengi wamekuwa wakitumia bidhaa mbalimbali za kupunguza uzito lakini baada ya muda flani uzito unakuja kuongezeka kwa kasi sana na kurudia hali yako ya mwanzo. Hivyo hii inaonesha kuwa mbali na matumizi ya bidhaa hizo za kupunguza uzito uwe na elimu hii ambayo itakusaidia maishani mwako daima.

FIKRA POTOFU  1

Watu wengi tunajua na tunashauriwa na baadhi ya vyakula vimeainisha kiwango cha sukari (kalori) ambazo unatakiwa utumie kwa siku moja. Basi watu wengi wamekuwa wakijitahidi kuhesabu na kujinyima kiwango kingi cha kalori kwa kutumia vyakula vyenye kiwango kidogo ili kuweza kuepukana na uzito mkubwa. Nimekuwa nikikutana na vinywaji vimeandikwa ‘ Kiwango maalumu cha kalori” na vyakula vingine vimeandikwa ” low fats” chakushangaza karibia vinywaji vingi vimeandikwa hivyo na watu wanajichunga sana kwani wanajua nini maana ya maneno hayo, LAKINI BADO SWALA LA UZITO MKUBWA NI CHANGAMOTO. Ina maana kuwa kuwa siri nyingine ambayo wewe unatakiwa kuijua kuhusu mwili wako ndipo uweze kulinda uzito wako kiafya.

Usemi huo ni mzuri kuwa tule vyakula vyenye mafuta kidogo na vyakula vyenye kiwango flani cha kalori, lakini usemi huo unatumika sana PALE VICHOCHEO VYA MIILI YETU VINAPOKUWA KATIKA USAWA (NORMAL RANGE) hapo ndipo mwili utakuwa katika utendaji wake kiuhalisia. Lakini kutokana na miili yetu imekuwa ikipata misuko suko mingi kiafya kuanzia kwenye vyakula tunavyokula,hewa tunayovuta na vyote tunavyoweka juu ya ngozi homoni  za kutumia mafuta zimevurugika na ule usemi wa mafuta kidogo na kalori chache upungue uzito hautatumika tena, Inatakiwa tushughurikie mwili uanze kuunguza mafuta pale vichocheo vyetu vinapokuwa vimevurugika na uzito unaongezeka kila siku.

“Tunapo zungumzia viwango vya homoni mwilini, vitu vingi vinaweza kusambaratisha homoni zako na kusababisha kupoteza uwezo wa mwili wako kuunguza mafuta mwilini, kama msongo wa mawazo,hasira nyingi,kiwango sahihi cha usingizi, mazoezi yako na mengineyo,Lakini  MLO SAHIHI ndio kiini pekee cha kukuwezesha kupungua uzito kwa  kuunguza mafuta,kwani kiwango cha homoni mwilini mwako kinategemea sana MLO SAHIHI KIAFYA.

Kitendo cha watu wengi kuhesabu kiasi cha kalori kinaweza kukufanya ukafurahia kupungua kwa kilo mwanzoni na ukafurahia zoezi hilo, LAKINI kimwenendo wa mwili wako zoezi hilo halitaendelea hivyo hivyo milele mwili baadae hubadili mtazamo na hii ndio sababu watu wengi ambao ni wazuri sana wa kuhesabu kalori wanazotumia kwa siku huishia kutoona matokeo baada ya muda flani.

FIKRA POTOFU 2: UZITO NI WAKURITHI

Watu wengi tumekuwa tukikutana na maelezo mengi sana kuhusu kurithi kwa magonjwa kutoka kwa wazazi wetu kupitia Genes (vibeba taarifa) au DNA.

>Ukipata kisukari, utaambiwa umeridhi DNA za kisukari kwa wazazi wako kama kilikuwepo

>Ukipata Kansa utaambiwa umeridhi Gene au DNA za kisukari kutoka kwa wazazi wako

>Ukipata Shinikizo la damu na uzito mkubwa utaambiwa umeridhi kutoka kwa wazazi wako.

IMEKUWA NI KURITHI GENES,KURITHI GENES,KURITHI GENES kila ugonjwa na watu tunafurahia kutamkiwa kurithi huku na kutofikiria zaidi namna gani unaweza kuikinga familia yako na vizazi vyako.

Hebu soma hiki kitu

“Ukweli ni kwamba VINA SABA (DNA)/GENES hazijawahi kubadilika takribani miaka 40,000 hadi sasa. Lakini umekuwa ukiona ongezeko kubwa la magonjwa kama kisukari,shinikizo la damu,uzito mkubwa anavyo endelea kushambulia binadamu hadi sasa. Swali la kujiuliza kama tumerithi magonjwa haya mbona enzi hizo hakukuwa na magonjwa mengi kiasi hiki na watu wengi wenye matatizo kama haya? Kwa nini sasa unaendelea kuzilaumu GENES au DNA za urithi kila siku? Tafuta chanzo kuanzia leo”

NOTE: Ni asilimia 0.01% ya magonjwa yanayofikirika kuwa ni magonjwa yakurithi na miongoni mwa hayo UZITO MKUBWA SIO MIONGONI MWAO. Tafakari! Hivyo fikra potofu kuwa uzito ni wakurithi unakukosesha uwezo mpana na kubaini tatizo kwa kutafuta taarifa Zaidi za tatizo lako.

“ The best way to lose weight is to Get healthy” Hivyo basi lishe sahihi ni muhimu na nguzo kubwa sana katika safari yako kiafya.

Ni kweli inaweza kuwa genes/DNA za urithi zina mchango kiasi katika kukufanya uzito uwe mkubwa lakini sio kwa mtizamo wako.

Uzito mkubwa unasababishwa na kuishi maisha ambayo yanapingana na uhalisia wa mazingira ya seli za mwili zilivyo tengenezwa kufanya kazi katika uhalisia flani. Hivyo basi chochote unachoweka ndani ya kinywa chako kinaenda kubadili uhalisia wa mwili wako kufanya kazi na hatimaye kuishia kupata madhara mbalimbali ya kiafya.

KWA NINI UNAKUWA NA KITAMBI AU NYAMA UZEMBE

Katika miili yetu kuna makundi makundi makuu mawili ya lishe

  1. MACRO –NUTRIENTS

Hizi ni molekyuli kubwa za lishe kama WANGA,PROTINI, MAFUTA NA POMBE. Mwili unapokuwa unahitaji nishati huanza kwanza kutumia wanga, na unapokuwa umepungukiwa wanga unatumia Mafuta( Fats) na mwisho hutumia Protein wakati kama hakuna vyanzo vingine vyote vya nishati

  1. MICRO-NUTRIENTS

Hizi ni molekyuli ndogo za lishe ambazo hujumuisha madini yote na vitamin zote. Madini kama zinc,selenium manganese, Chuma nk na vitamin kama vitamin A,B,C,D,E K nk

SABABU KUU MBILI KWA NINI UNAPATA KITAMBI

Baada ya kuona mchanganuo wa lishe kwa upana hebu sasa kabla sijasema sababu ya kwa nini uzito wako unaongezeka kila siku na hupati suluhisho.

“ Ukitaka kutibu tatizo lolote la magonjwa yanayosababishwa na lishe kuzidi,kupungua au usahihi wake basi angalia chimbuko la tatizo kuanzia kwenye molekyuli za chakula na seli za mwili zinavyofanya kazi, utalibaini tatizo na kulipatia ufumbuzi wa moja kwa moja ndicho ambacho nataka ujifunze leo”

SABABU YA KWANZA

Kukosa taalamu sahihi ya lishe kamili kwa mtu mwenye tatizo la uzito mkubwa au kitambi, kwani wengi tumekuwa tukitumia ushauri ambao sio sahihi na hatimaye kuishia kuongezeka uzito.

Ulaji wa kiwango kikubwa cha wanga ni chanzo kikubwa sana cha wewe uzito kuwa mkubwa kila kukicha

Kwani chakula cha wanga chote hubadilishwa kwenye damu na kuwa sukari (glucose) ili tuweze kupata nishati ya mwili kuendesha shughuli za mwili. Kadri kiwango cha wanga kinavyozidi kuwa kikubwa katika mlo wako, ndivyo kiwango kikubwa cha sukari kitakacho zalishwa kwenye mzunguko wa damu.

Miili yetu ina tabia ya kutokubali kupoteza  chanzo cha nishati ya mwili yani glucose hovyo hivyo baada ya kiwango kuwa kingi sana mwili unachovya maji kutoka kwenye kongosho yaitwayo Insulin. Maji haya ni homoni ambayo hutolewa kwa lengo la kuja kuhifadhi sukari kwa matumizi ya baadae (sio kupunguza sukari kama wengi tunavyojua) kupungua kwa sukari kwenye damu ni matokeo ya kazi ya insulin hili wengi hupotosha!

NAMNA GANI INSULIN INAPUNGUZA SUKARI?

Insulini inafanya kazi kubwa ya kubadili sukari iliyozidi kiwango kuwa mafuta kwa kiwango kikubwa na kuhifadhi mafuta haya katika sehemu za kuhifadhia mafuta kama kiunoni,kifuani,mgongoni,tumboni,kwenye mikono nk.

Hivyo basi homoni ya insulin ni homoni ambayo ningependa kusema ni FAT STORING HORMON

>Kadri kiwango cha wanga kinavyo ongezeka ndivyo kiwango cha sukari kinavyo ongezeka

>Kadri kiwango cha sukari kinavyo ongezeka ndivyo kiwango kikubwa cha insulin homoni kitatolewa kwenda kupunguza kiwango kwa kuhifadhi kwa matumizi ya baadae

>Kadri Kiwango kingi cha insulin kilivyo juu ndivyo kiwango kingi cha mafuta kitahifadhiwa sehemu maalumu kama kiunoni,tumboni,mikononi,mgongoni nk

Nazani umenielewa jinsi gani mwili wako unashugurika na kiwango kingi cha wanga mwilini mwako!

MASWALI YA KUJULIZA

SWALI NO 1. Je ulaji wa nafaka ambayo haijakobolewa kunapunguza kiwango cha sukari inayozalishwa kwenye damu baada ya wanga kutumika kutengeneza glucose kwenye damu? Jibu ni Hapana!

SWALI NO 2. Je kama kwenye nafaka ambayo haijakobolewa kina kiwango kingi cha fiber ( Nyuzi), jiulize hizo nyuzi zinapunguza kiwango cha sukari kitakacho tengenezwa baada ya kiwango flani cha wanga kutumika? Hapana! Kwani moja ya kazi kubwa ya fibers kwenye kupunguza uzito ni kupunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula na kukufanya ukae muda wote unajisikia umeshiba! Lakini kumbuka kuna aina zingine za vyakula vyenye fibers nyingi ambavyo vinakiwango kidogo sana cha wanga! Kwa nini hufukirii hilo?

Watu wengi wanaopenda kula kiwango kikubwa cha wanga na vyakula vingine vya wanga na sukari vilivyo andaliwa viwandani kama mikate,biskuti,chokoleti na vinywaji vyenye sukari,vionjo,rangi na kemikali za kuhifadhia vinywaji vyakula vinavyokuja  wana matatizo yafuatayo.

  1. Wote ni wanene kupita kiasi
  2. Wote muda mwili hujisikia wachovu( kusinzia hovyo)
  3. Hawawezi kufuata mpangilio wa mlo (over eating)
  4. Matunda na mboga mboga haziwezi kuwakatia kiu ya njaa
  5. Wanafikiria kachumbali ya matunda na mboga za kijani sio chakula sahihi kwao wao wanahitaji kula chakula kizito kuweza kushinda bila njaa
  6. Muda mwingi hujisikia wenye njaa na hupenda kula sana vitu vitamu vitamu na hawawezi kujizuia wanaona kama mateso

UNAJITAMBUAJE WEWE UMEATHIRIWA NA KIWANGO KINGI CHA WANGA?

Unaweza kufanya zoezi hili hata ukiwa nyumbani kwako, chukua mchemsho wa samaki (protein), kachumbari ya mboga za majani ( Asparagus,cauliflower, spinach, kabeji,sukumawiki)  na Tango pembeni kata kata. Baada ya muda mchache tu utajiskia kama vile hujala chochote kabisa! Pole kama umekumbwa na tatizo hilo, na hongera kama hujakuta tatizo hilo endelea kupata mlo sahihi kwa kutumia elimu hii.

SABABU YA PILI: kwanini una uzito mkubwa na kitambo

Moja ya sababu kubwa watu wengi wamekuwa wakifanya mazoezi mengi katika gymes mbalimbali na wamekuwa wakijitahidi kufanya mazoezi mengi na kuishia kuumia viungo vya mwili bila kiu yao ya kupunguza uzito kukatika. Hii ni kwa sababu ya upungufu wa madini na vitamin mwilini mwako.

Madini kama manganese na selenium yanafanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha shughuli za mwili zinafanyika katika kiwango kinachostahiki. Hivyo basi endapo kuna upungufu wa madini kama haya pamoja na baadhi ya vitamin muhimu mwili wako hauwezi hata kuunguza mafuta katika kiwango kinachotakiwa maana shughuli zote zinakuwa zinafanyika katika kiwango cha chini sana.

KWA NINI INAWEZEKANA UNA UPUNGUFU WA MADINI NA VITAMIN KWA SABABU YA UZITO MKUBWA

Nimeongelea kuhusu vyakula vya wanga jinsi gani vinavyo athiri utendaji kazi wa mwili wako endapo unapokuwa unatumia wanga katika kiwango kikbwa sana kupita kiasi. Kiwango kikubwa cha madini na vitamin kinapatikana katika matunda na mboga za kijani. Sasa watu wengi wenye uzito mkubwa nimeeleza kuwa kiu yao huwa haikatwi na vyakula kama matunda na mboga za majani wengi hupenda kusema kuwa wanastahili chakula kizito kuweza kuhimili miili yao hadi kesho ( Ndio maana atatumia viazi vya kukaanga na soda pembeni amejitahidi sana juisi iliyotengenezwa masaa kumi yaliyopita sio fresh imemaliza vitamin zote kwani vitamin huwa zina athiriwa kiurahisi sana na joto na mwanga hivyo juisi ya tiba inahitaji uhifadhi maalumu kama usipoinywa pale pale baada ya kuitengeneza)

Hivyo basi nadhani umeona kwa nini uzito wako unazidi kuongezeka bila sababu kwa sababu tu ya kukosa vitamin na madini mwilini mwako bila hiari yako ni kwa sababu homoni zako zimevurugika kwa sababu ya ulaji mbovu zinakulazimu kupenda vyakula flani ambavyo vinazidi kupeleka afya yako pabaya.

Basi ningependa kukomea hapa kwa siku ya leo, bali kitu ambacho unatakiwa ujifunze ni kwamba tupunguze kiwango cha wanga katika sahani unayo weka mezani kwako, asilimia 75 ziwe mboga za kijani,protini,fats na matunda na asilimia 15 iwe wanga. Pia tuache kuogopa neno FATS (MAFUTA) kwani hili neno kila mtu huwa ananiambia sasa hivi ,Mshauri nimeacha kabisa mafuta. Napenda tu niendele kuwapongeza wote mnaendelea kufuatilia Makala zangu, hebu endelea kuwakaribisha watu wengine waweze kutufuatilia katika jukwaa letu la afya.

Chati nasi whatsapp kwa namba 0678626254

Share and Enjoy !

Shares
Shares