Categories
Dondoo za afya

Ganzi kwenye mikono ya miguu

ganzi
ganzi ya miguu

Maelezo ya utanguzi

Mwili umeenea vibeba taarifa ambavyo ni seli huitwa neva. Seli hizi za neva husafirisha taarifa kutoka eneo la mwili kwenda kwenye ubongo ili taarifa husika kutafsiriwa. Mfano unatembea kisha ghafla ukakanyaga kaa la moto, taarifa hizo husafirishwa haraka kwenda kwenye ubongo kupitia neva na kisha ubongo kutuma mrejesho kwamba ulichokanyaga ni moto.
Sasa inapotokea neva hizi za viungo vya pembezoni mwa mwili yani kwenye mikono na miguu kutofanya kazi ndipo mtu huanza kupata ganzi na wakati mwingine maumivu. Hapo unaweza kushika kitu na usijue kama umeshika kitu ama ukahisi maumivu wakati hakuna kitu kinachokuumiza

Nini Maana ya Peripherial Neuropathy?

Peripheral neophathy ni ugonjwa unaotokea pale neva za kwenye maeneo ya pembezoni mwa mwili hasa miguu na mikono kushindwa kufanya kazi kutokana na kupata majeraha. Kujeruhiwa kwa neva kunasababisha mwili kutumwa kwa taarifa ya maumivu wakati hakuna maumivu, au kutotuma taaria ya maumivu wakati kuna kitu kinachokuumiza. Neva hizi zinaweza kujeruhiwa kutokanana na

 • Ajali
 • Kuumwa magonjwa
 • Kupata maambukizi
 • Au kurithi

Dalili za Tatizo la Ganzi kwenye Miguu na Mikono.

 • Kutetemeka kwa mikono na miguu
 • Kupata hisia kama umevaa kitu cha kubana kwenye mikono au miguu
 • Kuangusha vitu mara kwa mara kutoka kwenye mikono
 • Ngozi kuwa nyembamba
 • Kushuka kwa shinikizo la damu
 • Kupungua uweo wa tendo la ndoa hasa kwa wanaume
 • Tumbo kujaa gesi na kukosa choo
 • Kuharisha na
 • Kutokwa na jasho jingi

Nini Kinachosababisha Ganzi kwenye Miguu na Mikono?

Watu ambao familia zao zina historia ya kuugua tatizo hili wapo kwenye hatari kubwa ya wao kuugua pia tatizo kutokana na kurithi vinasaba. Sababu zingine ni kama

Magonjwa

Kisukari ni ugonjwa unaoongoza kwa kuathiri neva za fahamu na kisha kupelekea mwili kuwa na ganzi kwenye mikono au miguu. Kisukari husababisha kujeruhiwa kwa neva kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kutodhibitiwa. Magonjwa mengine yanayoweza kujeruhi neva za fahamu na hivo kupelekea ganzi miguuni na mikononi ni pamoja na
Magonjwa ya figo ambapo figo zisipofanya kazi vizuri hupelekea kiwango kikubwa cha sumu kujikusanya mwilini na kuathiri neva
Kupungua uwezo wa tezi ya thyroid (hypothyroidsm) kunakopeleka mwili kuhifadhi maji kwenye eneo linalozunguka neva
Upungufu wa vitamin E, B-1, B-6 and B-12 ambazo ni vitamini muhimu katika kuimarisha afya ya neva.

Ajali

Ajali ni moja ya sababu kubwa inayopelekea kuathirika kwa neva. Ajali hizi ni pamoja na ajali za magari, kuanguka au kuvunjika kwa viungo.

Pombe na Sumu

Pombe hupelekea kuchelewa kwa taarifa zinazosafirishwa na kuleta athari kwenye neva. Watumiaji wa pombe waliokithiri wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua ganzi kwenye miguu na mikono.
Watu wanaofanya kazi kwenye maeneo ya sumu na kemikali mfano sumu za kuulia wadudu,wanaweza kuugua tatizo hili la kupata ganzi ya mikono na miguu.

Maambukizi na Magonjwa ya Kinga

Baadhi ya bateria na virusi wanaweza kushambulia neva. Wagonjwa wa Ukimwi pamoja na wagonjwa wa tetekuwanga na mkanda wa jeshi wapo kwenye hatari ya kuugua tatizo hili la ganzi,

Matumizi ya Dawa kwa muda mrefu

Matumizi ya baadhi ya dawa yanaweza kusababisha kuathirika kwa neva. Hii ni pamoja na

 • Dawa za kutibu kifafa
 • Antibiotics
 • Baadhi ya dawa kwa ajili ya presha na
 • Dawa kwa ajili ya saratani

Nini cha kufanya kwa Mgonjwa wa ganzi

Moja ni kurekebisha tabia na mazingira yanayosababisha kama kisukari, ulevi na mazingira yenye kemikali

Mazingira, tabia na Makundi yaliyopo kwenye Hatari zaidi kuugua Ganzi

 • Kisukari
 • Matumizi ya pombe kwa muda mrefu
 • Kupungukiwa na Vitamin hasa Vitamin B
 • Wagonjwa Ukimwi, mkanda wa jeshi na tetekuwanga
 • Magonjwa ya kinga kushambulia tishu (autoimmune diseases)
 • Kuwa na magonjwa ya figo, ini na tezi ya thyroid
 • Familia zenye historia ya kuugua ganzi.

Zingatia maisha ya kiafya kama; kula lishe yenye matunda, mboga ili kuimarisha afya ya neva. Tumia vyakula veynye vitamin B-12 kwa wingi kama nyama, samaki, mayai

Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara. Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara 4 kwa week nusu saa kwa siku.

Epuka mazingira yanayoweza kujeruhi neva kama . Kufanya kazi kwenye mazingira yenye kemikali kwa muda mrefu, kuvuta sigara na matumizi ya pombe kupita kiasi.

Tiba asili Kupitia Mafuta ya Eucalyptus

Mafuta ya eucalyptus yamekuwa yakitumika kwa zaidi ya miaka 5000 kutibu changamoto mbalimbali hasa na misuli na maungio. Huhitaji tena kuagiza nje ya nchi, tumefanya utafiti na kukuletea mafuta haya asili, yasiyochakachuliwa na salama zaidi.

Kutibu maumivu ya misuli na joints chovya kiasi kidogo cha mafuta yetu haya ya eucalyptus kisha pakaa taratibu kwenye ngozi na ufanye masaji kwa dakika 5 mpaka 10, fanya hivo mara mbili kwa siku.

Gharama za mafuta ni Tsh 40,000/= Ofisi tupo Mwembechai Magomeni, Tuandikie whatsapp kwa namba 0678626254 kuanza tiba

Share and Enjoy !

Shares
Shares