Kujaa Maji na Kuziba kwa Mirija ya Uzazi

kuziba kwa mirija ya uzazi
kizazi

Hydrosalpinx ni kitendo cha kuziba kwa mirija ya uzazi au kujaa maji kwa mirija (fallopian tubes) kutokana na kuwepo kwa majimaji katika mirija hii. Kuziba kwa mirija kunazuia yai kusafiri kutoka kwenye mifuko ya mayai (ovari) mpaka kwenye mfuko wa mimba (uterus).

Hydrosalpinx (kuziba kwa mirija ya uzazi) husababishwa na nini?

Kwa kiasi kikubwa wataalamu wanasema tatizo hili linatokea endapo mgonjwa aliwahi kuugua magonjwa yoyote  katika njia ya uzazi au magonjwa ya ngono. Vyanzo vingine ni uvimbe kwenye kizazi kutokana na kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba.

Kama mgonjwa aliwahi kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi kwa kipindi cha nyuma. Upasuaji ukapeleka majeraha kwenye mirija ya uzazi basi hupelekea kupata tatizo hili la kuziba mirija. Endelea kusoma zaidi makala yetu kupata ufahamu wa tatizo hili ambalo linaweza kuzuia mwanamke kupata ujauzito na hatimaye ugumba.

Jinsi gani kuziba kwa mirija inavosababisha ugumba

Tunafahamu kwamba ili mwanamke apate mimba basi ni lazima yai ambalo lipo tayari yaani limeshapevuka litoke kwenye ovari kisha lisafiri hadi kwenye  mirija ya uzazi ndipo lipate kurutubishwa na mbegu ya kiume.

Ovari ndicho kiwanda cha mwanamke cha kutengeneza mayai. Kitendo hichi cha urutubishaji hutokea siku ya 14 kwenye mzunguko wa hedhi. Kwahivo kama mrija umeziba manake yai halitaweza kusafiri na urutubishaji hautafanyika hivo mimba haitaweza kutungwa.

Swali: vipi kama mrija mmoja umeziba na mwingine uko vizuri je kuna uwezekano wa kushika mimba?

Kuna mrija miwli ya uzazi, mrija mmoja kutoka kwenye kila mfuko wa mayai(ovari). Hivo kila mwezi mfuko mmoja wa mayai hutoa yai moja ili liweze kurutubishwa na mbegu ya kiume. Na mara chache hutokea mifuko yote kutoa yai moja ndani ya mwezi mmoja.

Hivo ni wazi kwamba kama mrija mmoja umeziba na mwingine upo vizuri basi yai litasafiri vizuri na urutubishaji utafanyika na  mimba itatungwa. Lakini athari zingine zaa mrija wa kwanza kuziba itaendelea kuwepo.

Wanasayansi wamebaini kwamba kuziba kwa mrija mmoja kunaweza kusababisha kutiririsha maji kuelekea kwenye mfuko wa mimba na hivo kuathiri kiumbe kipya.

Matibabu yanayopatikana kwa kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kuna aina nyingi za matibabu yanayotolewa kwa kuziba kwa mrija ya uzazi katika mahospitali. Daktari wako anatakiwa akupe maelezo ya kina ni tiba gani inafaa zaidi kutokana na tatizo lako. Tiba hizi ni kama inavoelezwa hapa chini

1.Tiba ya Kuondoa mrija ulioathorika

Madaktari wanaweza kupendekeza kufanya upasuaji na hivo kuondoa mrija ulioziba ama kujaa maji. Kitaalamu tiba hii huitwa laparoscopic salpingectomy. Njia hii huweza kuhatarisha ufanyaji kazi wa ovari kwa kukosa damu kutokana na kwamba mrija wote hukatwa na kuondolewa kabisa.

2.Tiba ya kunyonya maji yaliyoziba mirija(sclerotherapy)

Tiba hii hufanyika kwa ultrasound na yaweza kuwa tiba salama  zaidi kuliko kukata mrija wa uzazi. Katika tiba hii tube nyembamba huingizwa kwenye mrija ulioathirika na hivo kunyonya maji yaliyopo.

3.Tiba ya upasuaji mdogo kwenye mrija

Upasuaji huu hulenga eneo husika kwenye mrija wa uzazi. Hivo eneo hili hupasuliwa na maji kusafishwa na kisha kushonwa tena ili kuzuia maji maji kuvia kwenye mfuko wa mimba ama uterus.

Muhimu kwa Wagonjwa wa Kuziba kwa Mirija Ya uzazi

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya mirija ya uzazi kujaa maji na kuziba, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 4 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama kuziba kwa mirija ya uzazi, fangasi na PID.

uterus cleansing pills

Vidonge hivi vinatumika kwa wiki moja. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24 unaweka tena kidonge kingine. Kulingna ana ukubwa wa tatizo tunaweza kupendekeza utumie dozi mbili.

Gharama ni Tsh 100,000/= Kwa dozi moja

Ushuhuda wa mgonjwa alieyepona kupitia UCP

Makundi yasiyotakiwa kutumia UCP

Dawa haitumiki kwa wanawake bikira na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi, ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Ofisi zetu zipo Mwembechai Plaza, Magomeni Mwembechai,
Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata Tiba ili uwe shuhuda wetu

Share and Enjoy !

Shares
Shares