Tatizo la meno kutoboka au dental cavity kwa kitaalamu ni hali ya jino kuwa na shimo. Shimo kwenye jino huanza taratibu na huendelea kupanuka kama jino halitatibiwa mapema. Ni kutokana na kwamba kufanyika kwa shimo kwenye jino huwa haina maumivu kwenye kipindi cha awali inakuwa vigumu kujua kama tatizo lipo, ndio maana tunashauri kuonana na Daktari wa meno kila baada ya miezi mtatu akufanyie vipimo.
Pamoja na kwamba tayari umepata shimo kwenye jino na jino lako linaoza, fahamu kwamba kuna hatua unaweza kuchukua kuzuia hali hii isiendelee
Dalili za Meno Kutoboka
Dalili za meno kuwa na mashimo huwa inategemea na ukubwa wa tatizo la meno kuoza. dalili hizi ni kama
- Meno kupata ganzi
- Maumivu ya meno
- Uwepo wa shimo kwenye jino
- Utando mweusi kwenye meno
Nini Kinachangia Meno Kutoboka na Kuoza
Kutokana na maeleo ya Dr, Eddward Mellanby kuna vitu vinne vikuu ambavyo huchangia kwa meno kutoboka na kuoza
- Upungufu wa vitamini kwenye lishe (A, D, E na hasa vitamin D)
- Matumizi makubwa ya vyakula vyenye tindikali
- Upungufu wa madini kama (calcium, magnesium na phosphorus)
- Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari iliyosindkwa
Kila mtu na bakteria kwenye mdomo. Bakteria hawa hubadili mabaki ya vyakula mdomono kuwa tindikali. Na tindikali hii huanza kumomonyoa jino na kuruusu bakteria kushambuliza jino.Ndio maana tunashauri kusafisha meno kila baada ya kula au walau amara mbili kwa siku ili kuondoa mazingira ya bacteria wabaya kumea.
Makundi ya Watu waliopo kwenye Hatari zaidi ya Meno Kutoboka
- Watu wenye matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari na tindikali kwa wingi
- Uchafu wa kinywa kama kutopiga brush vizuri
- Watu wenye kukosa hamu ya kula na
- Wagonjwa wa kiungulia ambapo asidi ya tumbo hurudi mpaka mdomoni.
Meno ambayo hutoboka zaidi ni yake ya mwisho yani magego. Meno haya yana uvungu na eneo pana kiasi kwamba linakamata kiurahisi mabaki ya vyakula.Meno haya ya magego hayasafishwi vizuri kutokana na ugumu wa kuyafikia ndio maaa yanakuwa kwenye hatari zaidi ya kuoza.
Hatua 4 za kufuata uzuia Meno kutoboka
Sasa na tuchambue zile sababu kuu nne ambazo zinachangia meno kutoboka na na hatua asili za kuchukua kulinda meno yako yasiendelee kuoza.
1.Epuka Sukari
Sukari ndio sababu namba 1 ya kutoboka kwa meno yako na pia ni chanzo cha magonjwa mengine mengi kama uzito mkubwa, kitambi, na kuvurugika kwa homoni.
Anza na kupambana na ulevi wa sukari, kwa kukaa mbali na vitu pmoja na soda na vyakula vya ngano. Tumia majani ya stevi kama kionjo cha kuongeza utamu kwenye kinywaji chako. Tumia pia asali mbichi kwa kiwango cha kati.
2.Tumia mazao ya maziwa na Vyakula vyenye virutubishi kwa wingi
Maziwa asili yana kiwango kikubwa cha vitamin na madini ambayo huimarisha afya ya meno. Ni muhimu kutumia maziwa asili walau mara mbili kwa week. Maziwa yana Calcium, Vitamin K2, Vitamin D3, magnesium na phosphorus. Mpangilio wa vyakula uwe kama huu
- Vyakula vya wanyama kama supu ya mifupa, nyama na mayai
- Mbogamboga kama spinach na mboga zenye kijani kilichokolea
- Matunda kipande kimoja kila sikuVitamin D kutoka kwenye jua, nusu saa kila siku.
- Vyakula vyenye mafuta mazuri kama mafuta ya nazi, nazi, parachichi, mafuta ya zeituni na samaki
- Karanga, mbegu na maharage
- Kutokula vyakula vilivyosindkwa, na fast food
3.Jaribu Coconut Oil Pulling
Njia hii iliyoanza kutumika kwa karne nyingi ili kusafisha kinywa na kuzuia meno kutoboka. Njia hii imekuwa ikitukuzwa sana katika uwezo wake wa kusafisha kinywa kwa kuweka mafuta mdomoni na kuyazungusha kisha kutema baada ya dakika 20.
Mafuta yana uwezo wa kuvuta na kunasa uchafu na vimelea wabaya waliopo mdomoni.
Soma vizuri hapa kuelewa kuhusu coconut oil pulling.
4. Punguza matumizi ya vyakula vinavyoongeza tindikali kama wanga uliokobolewa na kusafishwa, soda, juusi zilizosindikwa na pipi.
Maelezo ya mwisho
Matumizi ya mouth wash inaweza kuwa isiwe suluhisho la kudumu kwa kunuka mdomo au kuzuia meno yasioeze, mara nyingine mouthwash huongeza kunuka kwa mdomo, badala yake nashauri tumia njia asili na hakikisha unamwona daktari wa meno kila baada ya miezi mitatu.
Kuondoa maumivu ja jino lilotoboka tumia Peppermint
Ni mafuta asili yaliyozalishwa nchini Pakistan. Yanasaidia kuondoa kabisa maumivu ya jino, na pia kuangamiza bakteria wabaya kwenye meno. Ni uhakika ukitumia tiba yetu hii ndani ya masaa mawili maumivu yanaisha na hayajirudii.