Categories
Dondoo za afya

Maumivu makali wakati wa Kukojoa

Maumivu Makali Wakati wa Kukojoa

maumivu makali wakati wa kukojoa

Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa kitaalamu inaitwa Dysuria. Kitendo hichi huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume. Maumivu haya mara nyingi hutokana na maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) au maambukizi ya magonjwa ya zinaa(STD), lakini pia maumivu haya yanaweza kuashiria tatizo kubwa la kiafya kama saratani au kisukari.

Dalili Mbaya ni kama

  • Kukojoa kwa shida
  • Kujisikia hali ya kuchomachoma wakati wa kukojoa
  • Muwasho wakati na baada ya kukojoa
  • Mkojo kuwa na rangi ya mawingu
  • Kupata mkojo wenye chembechembe za damu (hematuria), kwa kesi hii ni muhimu kumwona daktari mapema ili ufanyiwe vipimo kugundua chanzo.

Chanzo cha Maumivu Makali Wakati wa Kukojoa

  • Maaambukizi ya bakteria
  • Maaambukizi kwenye njia ya mkojo(UTI)
  • Kuvimba kwa tishu za ndani za mrija kwa kutolea mkojo
  • Kufanya ngono iliyo rafu
  • Kuosha uke mara kwa mara
  • Matumizi ya njia za kupanga uzazi hasa za kuweka ukeni
  • Matumizi ya sabuni kuosha ukeni
  • Magonjwa ya tezi dume
  • Saratani
  • Matatizo kwenye figo mfano mawe ya figo
  • Lishe
  • Tiba ya Chemotherapy radiotherapy kwa ajili ya saratani
  • Vimbe kwenye utumbo mdogo
  • Matatizo kwenye kibofu cha mkojo

Kwa watoto mamumivu haya (Dysuria) yanaweza kutokana na kitendo cha mkojo kurudi kutoka kwenye kibofu kwenda kwenye figo kutokana na kuwepo kwa jeraha au kizuizi kwenye njia ya kutolea mkojo

Makundi yaliyo Katika Hatari zaidi ya Kupata Dysuria

  • Wanawake
  • Wanawake wajawazito
  • Wagonjwa wa kisukari
  • Kukua kwa tezi dume
  • Kuwa na matatizo kwenye kibofu cha mkojo
  • Kufanya ngono bila kutumia kinga, unakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya zinaa.

Tiba asili ukiwa nyumbani kwa Tatizo la Maumivu Makali Wakati wa Kukojoa

  1. Kunywa maji ya kutosha
    Kunywa maji mengi kunasaidia kusatoa nje sumu na taka na hivo kupunguza mamumivu wakati wa kukojoa. hakikisha kila unapopata kiu kunywa maji na siyo soda.
  2. Mafuta ya karafuu
    mafuta ya karafuu yanafahamika kwa kupambana na vimelea wbaya na fangasi na pia kuimarisha kinga ya mwili. Mafuta ya karafuu yasitumike zaidi ya week mbili kama unameza.
  3. Vitamin C
    Ni muhimu kula kwa wingi vyakula vyenye vitamin C pale unapohitaji kuimarisha kinga ya mwili kupambana na maambukizi. Vyakula hivi ni kama machungwa, strawberries, papai, mananasi,mapera, maembe na mboga za broccoli.
  4. Kula vyakula vinavyosaidia kuongeza bakteria wazuri tumbo. Vyakula hivi ni kama maziwa mtindi.

Angalizo

Kama tatizo lako la mamumivu wakati wa kukojoa limetokana na magonjw aya zinaa, ni muhimu kwa mwanamke mwenye maambukizi haya kumaliza dozi vizuri ili kuzuia hatari ya kuwa mgumba na maatizo mengine ya uzazi.
Kama tatizo lako limesababishwa na UTI ni muhimu kutibu kwanza ugonjwa husika. Kama usipotibu UTI vizuri inaweza kusababisha matatizo kwenye figo.

Ukiwa na swali tuandikie kwa Whatsapp no 0678626254

Bofya kusoma makala inayofuata:Chanzo cha Uume mdogo/kibamia

Share and Enjoy !

Shares

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shares