Figo ni viungo vyenye umbo la maharage, ambavyo vina ukubwa unaokarbiana na ngumi yako. Kila binadamu ana figo mbili ambazo zimehifadhiwa chini ya mbavu. Figo ni viungo muhimu sana katika kuchuja vimiminika na kutoa mahi yaliyozidi kwenye mwili. Uwepo wa mawe kwenye figo huleta maumivu makali sana wakati wa kukojoa.
Waliowahi kuugua tatizo hili watakweleza vizuri jinsi wanavoteseka. Tatizo la mawe kwenye figo linaweza kukufanya ushindwe kuendelea na kazi zako. Kwahiyo kuna ulazima wa kutibu tatizo mapema si tu kwa ajili ya kuepusha maumivu bali pia kupunguza hatari ya kufeli kwa figo.
Fahamu kwamba haupo peke yako
Mawe ya figo (kidney stones) ni moja ya matatizo la mfumo wa mkojo linalowatokea watu wengi sana. Inakadiriwa kwamba mtu mmoja kati ya kumi atapata tatizo la mawe kwenye figo katika kipindi flani cha maisha yake. Najua umekuwa unawaza jinsi gani upate tiba bila kupata matumaini ndio maana tumeandika makala hii kwa uchambuzi na weledi wa hali ya juu kukupa majibu kwa maswali yako yote.
Mawe kwenye figo ni kitu gani hasa?
Ni vijimawe vidogovidogo sana ambavyo hufanyika ndani ya figo yako. Mawe haya hutokana na muunganiko wa madini na taka mbalimbali ambazo ni matokeo ya kuchujwa kwa mkojo.
Mawe ya Figo Kukwama Kwenye Mirija
Vijimawe hivi vinaweza kukwama kwenye mirija ya kutoa mkojo wakati wa kukojoa na kusababisha kibofu kujaa mkojo kupita kiasi na kuanza kuuma. Kabla damu haijapita katika figo, huwa imebeba maji na taka taka nyingi sana (urea)
Lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini. Masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwemo pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili (ureters)kuelekea kwenye kibofu ( urinary bladder) na kisha kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo (urethra).
Mawe ya Figo ni Mkusanyiko wa Kemikali
Mkusanyiko wa kemikali hizi (chemical crystals), wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga.
Kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe (nephrone) au kwenye mirija yakupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu (ureter). Hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.
Kwa watu wengi tatizo la mawe kwenye figo halileti athari baada ya mawe haya kutolewa kwa njia ya mkojo. Lakini kwa wengine mawe yanapokuwa makubwa ndipo shida huanza.
Mawe kwenye figo husababisha kufeli kwa figo ambalo ni tatizo linalotishia uhai wa mtu kama hutapata tiba mapema. Kama unaanza kupata dalili za mawe kwenye figo basi makala hii itakufundisha hatua kwa hatua namna gani utibu tatizo hili ukiwa nyumbani kwako.
Nitajuaje Kama Tayari Nina Mawe Kwenye Figo?
Kujua kama tayari una shida ya mawe ya figo tazama uwepo wa dalili hizi
- Maumivu makali chini ya mbavu zako, maumivu haya huja na kuondoka kila baada ya dakika 10 mapaka 15 hasa kila unapoenda kukojoa na yanaweza kutofatiana ukali wake.
- Maumivu chini ya mgongo ambayo yanaweza kusambaa mpaka kwenye nyonga
- Kupata mkojo unaotoa harufu kali na wenye damu
- Kujiskia kukojoa kila muda kuliko kawaida wakati mwingine unaweza kwenda haja lakini usitoe mkojo.
- Kupata Maumivu wakati wa usagaji wa chakula tumboni, kutapika na kupata kizunguzungu
- Homa kali
Wakati mwingine uwepo wa mawe ndani ya figo hauleti maumivu mpaka pale tatizo linapokuwa kubwa na mawe makubwa kuanza kupita ili kutolewa nje.
Watu wenye hatari zaidi ya Kuugua
Makundi yafuatayo wapo kwenye hatari zaidi ya kupata mawe kwenye figo ukilinganisha na wengine.
- Wanaume wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanawake (sababu zake zikiwa bado hazijajulikana)
- Watu wenye umri wa makamo kuanzia miaka 30 mpaka 50
- Wamarekani weupe wako kwenye hatari zaidi kuliko wamarekani weusi
- Wanaotumia madawa kwa mda mrefu
- Waliowahi kuugua magonjwa maka gout, UTI, na matatizo ya tezi ya thyroid na
- Watu wasiofanya mazoezi, shughuli zao nyingi wanakuwa wamekaa
Hatua Tano Za Kutibu Mawe Kwenye Figo
Kwa watu wengi kitendo cha kutoa jiwe kwenye figo kupitia mkojo kinaweza kuchukua mpaka siku 5 huku ikiambatana na maumivu makali.
Lakini habari njema ni kwamba kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kuharakisha utolewaji wa mawe kwenye figo na kuzuia mawe kurudi rivasi kwenye figo yako. Japo katika mazingira baadhi itakulazimu kufanyiwa upasuaji ili kuondoa mawe yaliyokwama kwenye figo.
Hatua Ya Kwanza: Kunywa Maji Ya Kutosha Kila Mara Kama Moja Ya Tiba Ya Mawe Kwenye Figo.
Kutokunywa maji ya kutosha kunakuweka katika hatari kubwa ya kupata mawe kwenye figo hasahasa kama wewe siyo mtu wa mzoezi, unatumia sana vinywaji vyenye sukari kwa wingi na unaishi katika mazingira ya joto sana.
Hatua Ya Pili :Kula Chakula Chenye Virutubisho Vya Kutosha.
Ulaji wa vyakula visivyo na kambakamba/fibers kwa wingi na viondoa sumu, vyakula vyenye mafuta mazuri nap rotini kiasi, unakuweka katika hatari zaidi ya kupata mawe kwenye figo. Ulaji pia wa vyakula vyenye chumvi kwa wingi na protni kupita kiasi huongeza kiwango cha ammonia kwenye mwili. Hapa chini ni mtiririko wa vyakula sahihi vya kutumia
- Vyakula vyenye kambakamba/fibers kwa wingi: kwenye mlo wako wek vyakula vingi vyenye kambakamba au nyuzinyuzi mfano karanga, nafaka isiyokobolewa, maharage, mboga za majani, na mbegu. Parachichi, broccoli, apple na viazi vitamu
- Mbogamboga za kijani na matunda :tafiti zinasema kwamba watumiaji wa vyakula vya majani kwa wingi kuliko nyma wapo kwenye hatari ndogo zaidi kupata mawe kwenye figo ukilinganisha na walaji wa nyama zilizosindikwa na kuhifadiwa kwenye vifungashio.
- Vyakula vyenye vitamin E kwa wingi.(ama unaweza kutembelea stoo yetu kupata kirutubisho hiki. : vyakula vyenye vitamn E kwa wingi ni kama mafuta ya mizeituni, almonds, parachichi, na zabibu. Vitamin E ni kiondoa sumu kwenye mwili na hivo inasaidia mwili uweze kutoa sumu za oxalates ambazo ndio chanzo cha mawe kwenye figo
- Vyakua vyenye magnesium na potassium kwa wingi: hii itasaidi kubalance uwepo wa madini ya calcium kwenye mwili, kwahiyo hakikisha unaongeza kweye mlo wako mbogamboga za kijani, matikiti, parachichi na ndizi.
Hatua Ya Tatu Epuka Vyakula Ambavyo Vinakufanya Upate Mawe Kwenye Figo.
Vyakula vyenye sukari: tafiti zinasema kwamba matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari kwa wingi huongeza ukubwa wa tatizo, kwahiyo hakikisha unapunguza matumizi snaks na vinywaji unavyotumia hasa soda.
Nafaka zilizosindikwa na kusafishwa sana: bidhaa hizi ni kama unga wa ngano, ugali na mikate.
Nyama zilizosindikwa: nyama zilizosindikwa husababisha mwili kutoa calcium nyingi n hivo kuongezeka kwa hatari yam awe kutengenezwa kwenye figo.
Pombe na vyakula vyenye caffeine: vyakula na vinywaji vyenye caffeine na pombe hupunguza maji kwa kiasi kikubwa kwenye mwili na hivo kuharakisha kufanyika kwa mawe kwenye figo.
Hatua ya nne: Weka Ratiba Ya Kufanya Mazoezi Mara Tatu Kwa Week,ni Tiba Nzuri Ya Mawe Kwenye Figo
Mazoezi hasa yake ya kutumia nishati nyingi na mazoezi mbalimbali ya kupunguza unene ni mazuri katika kujenga mifupa. Kwa upande mwingine maisha ya kizembe bila kufanya mazoezi yanaongeza utolewaji wa calcium, na kama tulivotangulia kusoma hapo juu calcium nyingi kwenye figo ndio inatengeneza mawe zaidi ndani ya figo.
Hatua ya tano:Tumia virutubisho mbalimbali
- Magnesium: unaweza kutumia vidonge vyenye Milgram walau 250 mara mbili kwa siku.
- Vitamin B: vitamin B husaidia kupunguza kujikusanya kwa Calcium na Oxalates ambapo hupelekea mawe kwenye figo. Unaweza kuchukua vidonge vya vitamin B complex na kumeza milligram 50 kila siku.
- Virutubisho vya kuondoa sumu
- Jusi ya aloe vera hupunguza kufanyika kwa mawe. Kunywa walau robo kikombe kidogo kwa siku
- Unaweza kutembelea stoo yetu ya virutubisho ambapo utaanza program yako ya kusafisha mawe kweye figo ndani ya siku 30.