Saratani ya koo la chakula (esophageal cancer)
Nini maana ya Saratani ya koo?
Koo au esophagus ni bomba lenye misuli ambayo kazi yake ni kupitisha chakula kutoka mdomoni kuelekea tumboni. Saratani ya koo hutokea baada ya seli zisizo za kawaida (tumor) kuanza kukua pasipo mpangilio kwenye ukuta wa koo. Seli hizi zinavyoendelea kukua, huanza kuathiri tishu na misuli ya koo.
Aina za Saratani ya Koo la chakula
Kuna aina mbili za saratani ya koo la chakula ambazo ni
Squamous cell carcinoma: Ni aina ya saratani ambayo huathiri zaidi eneo la juu la koo la chakula. Na huathiri seli za eneo ja juu la koo.
Adenocarcinoma ambayo hutokea pale saratani inapoanza kuathiri seli za glanduar ambazo huusika na uzalishaji wa majimaji(mucus), maji ambayo hulainisha koo na kukukinga dhidi ya athari za vimelea. Aia hii ya saratani huathiri zaidi eneo la chini la koo.
Dalili za Saratani ya Koo la Chakula
Mara nyingi saratani ya koo inaweza isioneshe dalili mbaya kwenye kipindi cha awali, lakini kadiri saratani inavosambaa ndipo utaanza kupata dalili hizi
- Kupungua uzito kwa kasi
- Kiungulia
- Maumivu na ugumu kwenye kumeza chakula
- Kutapika
- Chakula kurudi juu
- Maumivu ya kifua
- Kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula
- Kikohozi kisichoisha na
- Kukosa nguvu mara kwa mara
Nini kinsababisha Saratani ya Koo la Chakula?
Kama ilivo kwa saratani zingine kisababishi hasa cha saratani ya koo bado hakijulikani. Inaaminika kwamba saratani hii ni matokeo ya mabadiliko ya gene (chembechembe ndogo sana kwenye seli zinahusika na urithishwaji) wa sifa mbalimbali. Mabadiliko haya yasio ya kawaida huitwa mutation na hutokea kwenye vinasaba vya seli za koo la chakula.
Makundi ya watu waliopo kwenye Hatari ya Kupata Saratani ya Koo
Wataalamu wa afya wanaamini kwamba kututumka (irritation) kwa koo mara kwa mara huchangia kutokea kwa saratani. Baadhi ya tabia na hali zinazochangia kututumka kwa tishu za koo ni kama
- Uvutaji wa sigara
- Matumizi ya pombe kali kupita kiasi
- Kuwa na tatizo la kiungulia kwa mda mrefu
- Uzito mkubwa
- Matumizi hafifu ya mboga na matunda
- Wagonjwa wenye tatizo la achalasia ambapo misuli ya chini ya koo inalegea na hivo kuruhusu tindikali kutoka tumboni kupanda juu kwenye koo.
- Wanaume wanakuwa kwenye hatari zaidi kupata saratani ya koo kuliko wanawake
- Wenye umri zaidi ya miaka 45 wapo kwenye hatari zaidi kuliko watu wa umri mdogo.
Vipimo Vinavyofanyika ili Kugundua uwepo wa Saratani ya Koo.
Njia ya kwanza: Endoscopy: ambapo kifaa chenye camera iliyowekwa kwenye tyubu inaingizwa ndani kupitia mdomo ili daktari aweze kutazama mwonekano wa koo lako na kugundua kama kuna tishu zimekua kupita kiasi.
Njia ya pili: Barium meal/barium swallow; ambapo daktari atakupa mchanganyiko wa kemikali unaoitwa barium. Kipimo hichi cha X-ray humuwezesha daktari kutazama ukurta wa koo la chakula na hivo kugundua kama kuna ukuaji wa seli usio wa kawaida.
Njia ya tatu: Biopsy; Njia hii inajumuisha kutolewa kwa nyama ndogo kwenye koo kw akutumia kifaa cha endoscope na kupelekwa maabara ili kufanyiwa vipimo.
Njia ya nne: CT scan au MRI; vipimo hivi hutumika kujua kama saratani yako koo imesambaa kwa kiasi gani kwenye viungo vingine vya mwili.
Matibabu ya Saratani ya Koo
Kutokana na vipimo Daktari anaweza kupendekeza moja ya tiba hizi kuzuia uvimbe wa saratani usiendelee kukua ili uweze kuondolewa kiurahisi kupitia upsuaji.
Upasuaji
Upasuaji hufanyika kama saratani ipo kwenye hatua za awali haijasambaa. Upasuaji hulenga kuondoa vimbe za saratani na kisha nyama za tumboni na utumbo mpana hutumika kufidia eneo la koo lililoondolewa.
Chemotherapy
Chemotherapy ni tiba inayojumisha matumizi ya dawa ili kupambana na seli za saratani. Tiba hii ya chemotherapy inaweza kutumika kabla au baada ya upasuaji, na inaweza kutumiwa pamoja na tiba ya mionzi-radiotherapy.
Tiba ya Chemotherapy huambatana na madhara(side effects) yafuatayo.
- Nywele kunyonyoka
- Kupata kichefuchefu
- Kuwa
- Mwili kukosa nguvu
- Maumivu na
- Ganzi
Tiba ya mionzi (Radiotherapy)
Tiba hii inajumuisha matumizi ya miale katika kuua seli za saratani. Mionzi hii inaweza kupigwa nje ya mwili au ndani kwenye kiuongo kilichoathirika.
Tiba hii ya mionzi mara nyingi hutumika pamoja na chemotherapy. matokeo hasi ya tiba ya miozni ni pamoja na
- Kuungua kwa ngozi
- Kupata maumivu wakati wa kumeza
- Mwili kukosa nguvu
- Mumivu ya vidonda kwenye ukuta wa koo
MUHIMU KUJUA
Fahamu kwamba utapata dalili zisizo za kawaida wakati unaendelea na tiba ya mionzi au chemotherapy mpaka utakapomaliza tiba. Dalili hizi mbaya ni pamoja na kupungua kwa njia ya koo na hivo kupata ugumu kwenye kumeza chakula au kinywaji.
Namna ya kujizuia usipate saratani ya koo
Ni muhimu kuhakikisha unaepuka vihatarishi ambavyo hupelekea saratani ya koo ikiwa ni pamoja na
- Kuacha uvutaji wa sigara na kutafuna tumbaku
- Kupunguza matumizi ya pombe
- Kuweka sawa uzito wako kwa kutumia virutubisho
- Kutumia lishe yenye vitamin na madini kwa wingi.
Muhimu Kwa Wagonjwa wa Saratani
- Kwa mgonjwa wa saratani hakikisha unapitia makala hii inayoelezea kuhusu mpango wa lishe ya kutumia wakati huo unaendelea na tiba ya hospitali.
- Nashauri pia kutumia virutubisho vya, Ginseng, Spirulina, Cordyceps, Chitosan na Ganoderma ambavyo vitakusaidia, kupunguza makali ya chemotherapy na tiba ya mionzi, na kupambana na seli za saratani. Nimepata shuhuda nyingi zaidi kwa wagonjwa wanaotumia tiba ya hospitali na hivi virutubisho kwa pamoja kupata matokeo mazuri zaidi kwa haraka kuliko wanaotumia aina moja tu ya tiba.