Mwongozo wa Ketogenic Diet-Suluhisho la magonjwa ya lishe

ketogenic diet
ketogenic diet

Maelezo ya utangulizi kuhusu ketogenic diet.

Wagonjwa wengi wa saratani, kisukari, uzito mkubwa  na kitambi wametoa mrejesho chanya baada ya kuanza kutumia ketogenic diet. Ambayo inataka kuondoa vyakula vya wanga na sukari kwenye mlo wako na kisha kula zaidi vyakula vya mafuta na protini kiasi

Seli za binadamu kikawaida zinaweza kubadilika kutoka kwenye kutumia sukari kama chanzo kikubwa cha nishati na kuanza kutumia ketone bodies, kitu ambacho seli za saratani haziwezi. Ulaji wa vyakula vya mafuta siyo hatari kwa afya yako kama ambavyo inaaminishwa bali ni rafiki mkubwa .

Tafadhali kumbuka kwamba kurekebisha lishe ndio silaha yako namba moja katika kupambana na saratani kisukari, uzito mkubwa  na kitambi . Vyakula vilivyosindikwa na vinywaji vya viwandani siyo sehemu ya ketogenic diet na unatakiwa kuviepuka katika safari yako ya kutibu magonjwa ya lishe

Ketogenic diet ni kitu gani?

Ketogenic diet ni lishe inayojumuisha ulaji wa vyakula vya mafuta kwa wingi na protini na kuondoa vyakula vya wanga na sukari. Lengo hapa ikiwa ni kubadili mwenendo wa mwili badala ya kutumia sukari kama chanzo cha nishati utumie mafuta yaliyohifadhiwa mwili kama chanzo cha nishati .

Kwa upande mwingine kwa wagonjwa wa saratani, kuzuia  ukuaji wa seli za saratani kwa kuzinyima chakula au mbolea yake. Seli za saratani hukua zaidi kwa sukari. Na ikiwa umekula wanga nao hubadilishwa kuwa sukari na hivyo kuongeza zaidi kiwango cha sukari mwilini.

Lishe hii siyo tu kwa wagonjwa wa saratani bali ni muhimu pia katika kupambana na kisukari na magonjwa mengine ya lishe kama uzito mkubwa na kitambi, kuvurugika kwa homoni na presha. Ni lishe ambayo itakusaidia pia kuchoma mafuta yaliyohifadhiwa mwilini na hivo kuweka uzito wako sawa kwa kubadilisha mwili kuwa mashine iunguzayo mafuta.

Ni kwa Jinsi gani Ketogenic Diet inaminya Ukuaji wa Seli za Saratani?

Kikawaida seli za mwili hutumia sukari aina ya glucose kama chanzo cha nishati. Pale tunapokula wanga nao hubadilishwa kuwa gulucose kisha shuguli za kikemikali kuendelea mpaka kuzalisha nishati inayotumika kwa shuguli mbalimbali za mwili. Seli za saratani pia nazo hutumia sukari kama mbolea kuweza kukua na kusambaa maeneo mbalimbali ya mwili..

Pale mwili wako unapokosa sukari basi seli hubadilika na kuanza kutumia ketone bodies ambazo ni matokeo ya kuvunjwavunjwa kwa mafuta ili kuzalisha nishati. Habari njema ni kwamba seli za saratani haziwezi kubadilika na kutumia ketone bodies na hapo ndipo penye tumaini la kutibu na kupona saratani yako.

Vipi kuhusu vyakula vya protini?

Kwa mgonjwa wa saratani tunashauri uamuzi mzuri ni kubadili wanga kwa vyakula vyenye mafuta mazuri na kupunguza matumizi ya protini zenye ubora. Mgonjwa anashauriwa kutumia siyo zaidi ya gramu 50 kwa siku za vyakula vya protini ili kufidia mahitaji ya mwili

Ni kiasi gani cha Wanga unaweza kutumia ukiwa kwenye Ketogenic diet??

Pale unapoanza safari yako ya kupambana na magonjwa ya lishe kama saratani kisukari, uzito mkubwa  na kitambi nashauri kufuata mtiririko huu

  • 70% ya mlo wako iwe ni mafuta mazuri
  • 25% ya chakula iwe ni protini na mbogamboga na
  • 5% ya chakula iwe wanga

Hii itakusaidia kuubadili mwili kutoka kutumia wanga kama chanzo cha nishati na kuanza kutumia ketone bodies ambazo zinazalishwa kutoka kwenye vyekula vya mafuta.

Jinsi ya kuanza lishe yako ya Ketogenic Diet.

Hatua ya kwanza yaweza kuwa ngumu pengine kutokana na kwamba ulishazoea kula zaidi vyakula vya sukari na wanga.  Lakini kabla sijakuandikia list ya vyakula kwenye hii ketogenic diet ni vizuri kwanza ukajitathmini unachokula kwa sasa na kutupitilia mbali vyakula vyote ambavyo sio rafiki kwa afya yako. Ni vizuri kufagia kwanza jiko lako kabla kuanza ketogenic diet.

Hii ikimaanisha kwamba unatakiwa kufagia vyakula vya sukari,nafaka, wanga, na vyakula pamoja na vinywaji vyote vilivyosindikwa. Manake vyakula vyote ambavyo havipo kwenye list ya ketogenic diet vinatakiwa kutupiliwa mbali  mpaka pale afya yako itakapotengemaa. Hapa chini nimeweka baadhi ya vyakula unayotakiwa kuepuka kwenye lishe yako.

  • Vinywaji vilivyosindikwa mfano soda
  • Vyakula vyote vilivyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye makopo
  • Maziwa ya kiwandani
  • Chips na vyakula vilivyochemshwa kwenye mafuta kwa muda mrefu
  • Mafuta ya alizeti,canola
  • Vyakula vilivyoongezwa ladha na sukari.
  • Vyakula vilivyofungwa na kuhifadhiwa kwa muda mrefu visiharibike.

Vyakula halisi vya Mafuta mazuri unavyotakiwa kutumia

Unaokuja kwenye swala la ketogenic diet kumbuka kwamba unatakiwa kutumia kiasi kidogo tu cha protein. Na pia wanga inatakiwa kuwa kidogo zaidi huku vyakula vya mafuta mazuri vikiwa vingi kwenye sahani yako.

Vyakula vya mafuta mazuri.

Kama nilivoeleza hapo mwanzo kwamba lishe yako kubwa karibu 70% inatakiwa kuwa ni mafuta.  Ili kuanza safari yako hapa chini nimekuweka list ya vyakula vya mafuta ambavyo utatumia

  1. Mafuta ya kupikia ya nazi
  2. Maziwa kutoka kwa wanaya waliofugwa kwa kula nyasi siyo nafaka.
  3. Parachichi
  4. Chai ya cacao
  5. Nyama
  6. Mayai ya kienyeji
  7. Karanga na jamii za karanga mbichi
  8. Mbegu kama za maboga (unaweza kutumia unga wake pia)
  9. Mafuta ya kupikia ya mizeituni (olive oil)
  10. Omega 3 kutoka kwenye Samaki
  11. Nazi

Vyakula Vya Protini

Kiwango cha protini unachotakiwa kutumia kwa mgonjwa mwenye  saratani, kisukari, uzito mkubwa  na kitambi ni chini ya gramu 50 kwa siku. Hii itasaidia kufidia mahitaji ya kila siku ya mwili katika kujenga misuli. Vyanzo vikuu vya protini ni kama nyama nyekundu kama ya ngombe na nguruwe na nyama ya kuku. Kujua ni kiwango gani cha protini umekula kwenye chakula chako fuata mtiririko huu.

  • Nyama nyekundu kama ya ngombe, mbuzi, kondoo, nguruwe na kuku kwa kiwango cha ujazo wa mkono zina kiasi cha gramu 6 mpaka 9 za protini.
  • Yai moja la kuku wa kienyeji lina ujazo wa gramu 6 mpaka 8 za protini.
  • Mbegu na karanga ujazo wa kikombe kidogo cha chai zina gramu 4 mpaka 8 za protini
  • Maharage yaliyopikwa ujazo kwa kikombe yana gramu 7 mpaka 8 za protini

Kwa ujumla chakula chochote cha protini unachokula basi hakikisha  mazao yake yametokana na wanayama waliofugwa kwa kula nyasi.

Mbogamboga

Mbogamboga zinaleta mchango mkubwa sana kwenye kupambana na saratani kwasababu zina kiwango kidogo sana cha wanga na zina nyuzinyuzi/fibers kwa wingi ambazo zina faida kubwa kiafya. Fibers zimegawanyika katikamakundi makubwa matatu.

Soluble fibers: hii ni aina ya nyuzinyuzi kutoka kwenye vyakula na husaidia mwili kuhisi umeshiba mda mrefu na kukuzuia kula kila mara. Husaidia pia kupunguza uchakataji wa wanga na hivo kupunguza kupanda kwa sukari kwenye damu.

Insoluble fibers: Hupatikana zaidi kwenye mbogamboga, aina hii husaidia kuongeza ukubwa wa kinyesi chako na hivo kusaidia utoaji wa taka hiyo kiurahisi. Husaidia pia kupunguza matatizo kama tumbo kujaa gesi, na kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu.

Digestive-resistant starch: Aina hii ya kambakamba au nyuzinyuzi husaidia kuongeza bacteria wazuri kwenye tumbo lako ambao ni muhimu katika kinga na usagaji wa chakula.

Vifuatavyo Ni Vyanzo Vya Mbogamboga

  • Nyanya
  • Uyoga mweupe
  • Vauliflower
  • Asparagus
  • Broccoli na
  • Spinach

Napendekeza tumia zaidi mboga za hapo juu kwasababu zina kiasi kidogo zaidi cha wanga. Mbogamboga kama viazi vitamu, viazi mviringo, corn vina wanga nyingi na yatakiwa kuviepuka.

Karanga

Karanga  na jamii zake kama walnut, husaidia kuongeza kiwango cha omega 3 ndani ya mwili na madini ya manganese. Karanga pia ni chanzo kizuri cha mafuta.

Matunda

Japo matunda ni mazuri kwa afya yako lakini katika safari hii ya kupambana na sukari yatakiwa kuepuka matunda mengi kutokana na kwamba ya kiwango kikubwa cha sukari. Matunda haya ni kama ndizi, apple,zabibu maembe, na  mananasi. Baadhi ya matunda yenye uchachu kama limau strawberries unaweza kutumia kuongeza ladha kwenye mlo wako .

Vinywaji

Kwa upande wa vinywaji kuna uwanja mkubwa unaweza kuchagua. Lengo ni kutokukubana uwe na uhuru wa kula vyakula vingi lakini visivyo na shida kiafya. Kinywaji cha kwanza ni maji safi na salama. Kinywaji kingine juisi ya nazi au maziwa ya nazi, pamoja na green tea.

Jitahidi kukaa mbali na vinywaji vyenye sukari kama soda na vinywaji vingine vilivyosindikwa. Kutokana na kwamba vitaharibu mpangilio wa kubadilika kwa seli kutoka kuunguza sukari hadi kutumia ketone bodies kama chanzo cha nishati.

Vionjo vya Kuongeza Ladha

Vionjo ni muhimu katika kungeza ladha ya chakula chako, vitamin na viondoa sumu. Kwa nyongeza vionjo vingi vina kiwango kidogo cha wanga. Hakikisha unatumia vionjo fresh baadhi ya vionjo vinavyouzwa madukani vikiwa viekaushwa na kusagwa vinakuwa vimepungua nguvu. List ya vionjo ni kama

  • Pilipili, hoho
  • Turmeric au manjano
  • Mdalasini
  • Majani ya basili
  • Tangawizi na
  • Chilli powder

Kwa maelezo ya hapo juu sasa unaweza ukaandaa ketogenic diet yako mwenyewe kwa kuzingatia sheria hapo juu bila kukufunga. Hapa chini nimekupa mpangilio na mfano kwa muundo wa ketogenic diet.

Siku ya Kwanza Kwenye Ketogenic Diet Unaweza kufuata utaratibu huu.

Breakfast.

Unapoamka unaweza kuwa unajiskia kushiba kama ndivyo usile chakula kizito badala yake tumia kinywaji chako chenye maji kwa wingi ambacho umezoea. Kama unahisi una njaa basi kula mayai mawili, yalipikwa kwa mafuta ya nazi.

Lunch

Chakula cha mchana unaweza kula saladi yako uliyotengeneza kwa mchanganyiko wa mboga nilizoelezea pale juu ujazo hata vikombe vi3 pamoja na parachichi moja. Ukatumia na kipande cha nyama. Kinywaji chako kwenye glasi ukachanganya na apple cider vinegar.

Dinner

Chakula cha usiku ni muhimu kikaliwa masaa matatu kabla ya kulala. Chakula hiki cha usiku kinatakiwa kiwe na kiwango kidogo cha protini , kiwango cha mbogamboga  kilichopikwa kwa mafuta ya olive au mafuta ya nazi. Hakikisha pia mlo wa usiku ni mwepesi kuliko wa mchana na asubuhi.

Snacks

Vyakula vya kutafuna muda wote mwingine unaweza kutumia karanga mfano almond, na siyo chips zilizokaushwa, unaweza kutumia pia parachichi.

Maswali Unayoweza Kujiuliza mara kwa mara kuhusu Ketogenic diet

Je Popcorn ni ketogenic?

Kama ndo unataka kuanza lishe yako ya ketogenic katika kupambana na saratani, waweza kujiuliza je hizi popcorn ambazo watu hutafuna kila mara ni nzuri kwa afya yako? Ukweli ni kwamba kikombe kimoja kidogo cha popcorn kina ujazo wa gramu 6 za wanga. Kwa wagonjwa wangu kutokana na kwamba yatakiwa kiwango cha wanga kiwe kidogo zaidi.

Nashauri usitumie kabisa popcorn, by the way zaidi ya kiwango cha wanga kilichopo kuna kemikali hatarishi pia zinazozalishwa kutokana na nature ya uuandaaji wa popcorn zenyewe. Sumu ambazo zitarudisha nyuma uwezo wa mwili kupambana na saratani.

Je tambi Naweza kula ?

Kiasi kidogo za tambi kwenye kikombe ni sawa na gramu 7 za wanga ndani yake. Sasa ebu angalia katika mtiriko wetu wa lishe ya saratani tumesema wanga iwe chini ya 20% kwenye sahani yako. Manake unapokula tambi tayari umezidi kiwango cha wanga unachotakiwa kula kwa siku ambapo ni gramu 5 pekee.

Je asali ni Ketogenic

Asali mbichi tunafahamu kwamba ni nzuri kiafya kama kupambana na bacteria na kuimarisha kinga ya mwili. Japo kwa upande mwingine haitakuwa salama kwako kutokana na kwamba imejaa sukari nyingi aina ya fructose. Kumbuka sukari inaharibu ule utaratibu wa seli kutumia mafuta kama chanzo cha nishati na siyo sukari. Nashauri kwa sasa wakati unapambana kuweka sawa afya yako usitumie asali.

Je Maziwa ya almond yanafaa

Maziwa ya almond ni mbadala mzuri kwa maziwa ya kawaida kwenye ketogenic diet. Tafiti pia zinasema kwamba viambata hai vilivyoo kwenye maziwa haya husadia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Kama unataka kutumia maziwa ya almond basi hakikisha unatengeneza ya kwako nyumbani usinunue yaliyotengenezwa kiwandani.

Je Nyanya ni Ketogenic.

Gramu 100 za nyanya ambazo ni kama 1 ya 10 ya kilo moja ya nyanya ina gramu 3.8 za wanga. Kwahivo unaruhusiwa kuongeza tunda hili kwenye lishe yako ya ketogenicc diet. Lakini kumbuka kupika nyanya zako ili kuongeza uwezo wa kiambata cha lycopene ambacho ndicho hupambana na saratani.

Tabia zingine za Kimaisha Zitakazokusaidia Kupambana na Magonjwa ya Lishe

  1. Vitamin D

Tafiti nyingi zimeeleza uhusiano katia ya saratani na upungufu wa vitamin D. Unaweza kupunguza hatari ya kuenea kwa saratani kwa kuhakikisha unapata mwanga wa kutosha wa jua la asubuhi kila siku.

  1. Kupata usingizi wa kutosha
    Hapa kwenye usingizi tunaongelea masaa ya kutosha na muda pia wa kwenda kitandani. masaa mazuri ya kulala ni kati ya saa 4 usiku mpaka saa 12 asubuhi , kwhivo hakikisha unalala masaa 8 kati ya saa 4 mpaka 12 asbuhi
  2. Msongo wa mawazo.
    Hakikisha unacontrol msongo wa mawazo
  3. Mazoezi ya mwili
    Namna mojawapo ya mazoezi yanavopunguza hatari ya kusambaa kwa saratani ni kwa kupunguza kupanda kwa kiwango cha insulini kwenyedamu nahivo kupunguza mazingira ya upatikanaji wa sukari ambao ni chanzo na mbolea ya seli za saratani. Mazoezi pia huongeza usafirishaji kwa seli za kinga ndani ya mwili, kinga yako ndio mpambanaji wa kwanza wa magonjwa kama saratani.

 Maelezo ya mwisho

Baada ya maelezo mengi ya hapo juu naamini sasa utakuwa na uwezo wa kutengeneza keto diet yako ukiwa nyumbani kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nyumbani kwako. Kama una mashaka na chakula unachotaka kuandaa basi usiache kuniuliza kwanza kabla ya kutumia.

Kumbuka pia ili kutimiza lengo la nutritional ketosis yaani kubadili mwenendo wa seli kutoka kutumia sukari mpaka kutumia mafuta kama chanzo cha nishati unatakiwa kupunguza matumizi ya wanga hadi gramu 50 kwa siku.

Matokeo yanaweza kuanza kuonekana ndani ya  mwezi wa kwanza kwa mabadiliko ya mwili. Utaanza kwanza kupoteza mafuta yaliyohifadhiwa mwilini na kuanza kupungua uzito wako taratibu. Unaweza kupata dalili zisizo za kawaida kama tumbo kujaa gesi, kupata kiu ya vyakula vya sukari, mkojo mwingi na kukosa nguvu ndani ya siku 30 za mwanzo. Lakini baadae mwili ukishazoea utakaa sawa usihofu. Usiache kushare makala hii na wenzako.

Share and Enjoy !

Shares
Shares